Weekend Story! Glory Be To God!

Weekend Story! Glory Be To God!

Return of Dee!

Nilisharudi Bongo mara nyingi tu, na kwa sasa nilikuwa nafanya biashara zangu kati ya Zambia, Congo na DSM. Na safari hii nilikuwa nimerdi kukaa mdaa kidogo maana mke wangu Pendo alikuwa na mimba ya kujifungua mda wowote. Sikuwa nime muoa rasmi bado, ni zile sogea tuishi, ila either way nilimheshimu sanaa Pendo. Sanaaaaa! Ni zaidi ya mke.

Na mara zote nikija ile short time nawasiliana na watu wa chache sanaa, wa muhimuuuu mnoo kwangu. Ishu za Sally nilikuwa nazipataaa zoote, sema sikutaka anione kwanza nikiwa bado sijafika napopatakaaa. Nikawa namfatilia low key ile tu kumuulizia kwa watu na nini kwa siri. Napata data zake zoote. Yupo na nani na ana nini. Mwisho nikasikia yupo na Msomaliiii na ni anampenda balaaa.

Ofcourse nikajua huyo msomali anapendwa kwasababu mi sipoooo. So its like a second position. Mimi kwa Sally i was number 1 and will forever be number 1. Hilo halitabadilikaaa kamwe, ni maishaaa tu. Then nikakumbukaaa what was i thinking, mtu nina mke, tena soon nitakuwa baba. I was ashamed by my self.

Mkutano na Sally niliupanga over and over kichwani kwangu. Nilipanga namna tofauti ambazo tungekutana face to face. Ila kwa bahati mbaya au nzuri ikatokea tu tumekutana ghaflaaaa. Na tulikutana hospital. Mimi nimempeleka mke wangu clinic na Sally akawa yupo Clinic ndo anatoka. Tukasalimiana fresh, za siku poa, poaaa. Nasikia upo Congo, ndio! Unfanya mishe gani nauza gypsum na tiles. Faida ikoje? Kila pc ni $2. Ooooh naweza kuja kujaribu. Karibu.

Nikamtambulisha Pendo maana yuko pembeni na kitumbo na nilitaka tu kumtoa roho Sally. Huyu my wife, nikamtambulisha na Sally kwa wife, wife alistukaaa kumuona Sally. Basi Sally akasema my Bf will be here anytime. Ameenda chooni, he is not well anaumwa. Nice to meet you, ngoja nikamtafute. Sawa, tukaachana.

Mda wa kutoka tukakutana tenaaa, actually mi na wife tulikua nyuma yao. Sikutakaaa kuaminiii. Msomali alikuwa anaumwaa, mdhaifuuu. So Sally akawa kama anampa maji, na kumpeti peti, Mshenzi anadekaaaa ni hatariiii. Roho ilinitokaaa. Sally anampenda yule mjingaaa. Maybe i am not her number one any more. Nikaamua to get a closer look.
Nikaenda mpaka pale, Sally akamtambulisha huyu ndo Dee. Akastukaa na nguvu zikamuishaaa kakaa kabisaaa. Wadudu waliongezekaaa mwilini. Na mimi nilistukaaa, nilijikaza tu. msomali ana genes nzuriiii. Kwanza mrefuuu, atakuwa na mashineee sio ya kitoto. Competition wa tough.

Mpaka mke wangu akaja kunifata. Sally akamwambia huyu Pendo, mkewe. mjinga akapata mpaka nafuuu ya kuinuka na kutembea kwa balance bila kuyumba yumba baada ya kuona mke ndo yule, mimba kubwa, nishaji nyoso mwenyewe. Sina pa kutokea zaidi ya kubakia mtazamaji tu. Kubabake. Kidogooo nimkanee Pendo basi tu nikakumbuka Sally ndo alisababisha mpaka nikaenda Congo. Na Pendo ndo alikuja kunitafutaaa maskini. Ila roho bado ikawa inaniumaaa.

Congo nimefika kule nikazulumiwa pesa zote. Nikataka kurudi, kuna mtu akanishauri komaa ulisome soko, ukija na pesa uta tusua. Nimeishi Congo kwa shida sanaa. Nikaanza kujenga network na watu wa hardware, nikawapanga kabisaa nawalete mzigo, nawaletea mzigo. Wakawa washanijua na kuniamini. Nilikaa mwaka nausoma mchezo na kutafuta masoko.

Siku sina hili wala lile nikaambiwa wewe ndo Desmond? Kuna mwamke ya Tanzania anatafuta wewe, jina yake ni Pendo. Natafuta kijana wa Tanzania, nimemkuta sokoni anauliza watu. Nikakimbilia sokoni. Kweli Pendo. Akanimbia nyumbani washakata tamaa. Yeye alipata mtu anataka kumuoa kabisaaa, sasa akasema asije kuolewa afu nikarudi. Ndo akasema aje anitafute, akinikosa ndo aolewe. Nikakaa nae kama wiki akarudi. Na mimi nikaja kurudi.

Ila tukawa tunawasiliana. Safari hii nikaja bongo kutafuta mtaji upyaaaa, nilikaa kama mwaka sio Dar lakini Mwanza. Nikapata, nikapakia gari mpaka Congo. Kidogo maslahi yakawepo. Nikajiongeza mpaka Zambia huko. Faida ipo kubwa. Maisha yakabadilika kabisaaa. Nikamfungulia na Pendo duka buguruni. Tukawa tuko njemaaa sanaaaa. Ila mda wote lazima nijue Sally yuko nani na je keshaolewa. Hili ndo lingenimaliza nguvu kweli kweli.

Sababu ashanionaa nikawa sina sababu ya kujificha tena. Namba yake ninayooo miaka yote. Nikamuita Lunch tukumbukane kidogooo. Akajaaa. Tukakaaa mjini. Yani hata hanishobokei kabisaaa. Amekazaaa. Tukaongea biashara pale nikaondoka. Nikapata uhakika mmoja. Simooo kabisaaa sio moyoni wala kichwani. Kichwa chake kimejaa msomali mtupuuu. Nikaamua naanza kumtongoza upyaaaa ikibidi. Kwanini? Labda ndugu msomaji unisaidie wewe jibu juu ya hilo. Nina mke mzuriiii anajifungua mda wowote nakomaaa na michepukoo.

Nikawa na chat chat nae, anakaribia kusafiri, namshawishi tusafiri wote, huenda nikafikiriwa kupewa mzigo. Akagoma kwamba Hussein hatofurahiii sijui nini. Nikamtega unampenda sanaa Hussein? Akasema ndio, nikamtega kuliko mimi? Akajibu labda! Nilistukaaaa kama nimefumaniwaa.

Nikahisi labda Hussein kamrogaaa, maana wasomali nao watu wa shirki sanaaa. Wana pulizaa sanaa. Nikaamia kwenye business kumuuliza Hussein anafanya nini like what he is into? Akanijibu Mkeo anafanya nini? What is she into? Nikabadilisha topic. Kabisaaa! Nikaona no sweat ngoja nitumie direct method.

Nikamwambia nataka nirudi in my position! Kuwa bwana wako. Sawa niliondoka ila i want my rightful position back. Akauliza na Mkeo je? Atabakia position gani? Nikajibu yangu na mke wangu haya kuhusu, nitayamaliza mwenyewe, tuongeee mimi na wewe.

Nikastuka nimeliwa block. Mhhhh! Sikukubali nikatinga kwa bahariaaa. Akafurahi kunionaaa. Dee ma men, umerudiiii sijui niniii furaha kibao. Nikajifanya Sally sijawahi kumuona kabisaaa. Namwambia baharia nimekuja kuoa. Baharia akacheka akaniambia umechelewa kidogoo sahivi kuna wasomali. Nikajitia kustukaaa. Akaniambia ndo hivo.

Basi namtia ndimu, baharia how can you let her be with those peopleee. Sio watu waleee. Baharia yupo, ndo kampendaa, wamependanaa, he is actually nice ukimzoea. Kijana mzuri sanaa. Kila siku lazima asubuhi anipigie simu kujua nimeamkaje na jioni ajue nalalaje. Si unajua mi na Sally hatuna mahusiano mazuri kitambooo, ila toka msomali aje kuna mabadiliko makubwaaa sanaa. Sally anakuja na msomali, mda mwingine peke yake, we have healthy conversations sio kama zamani. Sally kakua. Sahivi ndo tumezoeana.

Mimi baharia binafsi yangu, Sally akisema anaolewa na yule baharia sina pingamizi. Hapo nikajua kura ya baharia nishaikosaaaa kabisaaa. Nilichokaaaa. Nikiwa hata sijachoka vizuri msomali akaingia mwenyeweeee. Akatusalimia pale, na kuzungumza na baharia kidogo. Baadae baharia akasema anaenda kunyosha mgongo uzeee. Tukabakia wawili.

I decided to cut the chase na kumwambia point black tu. Nimpe shingi ngapi apotelee alshabab huko asahau kuhusu Sally. Akachekaaa tu. Nikamwambia mwanangu niko serious. Lile goma langu afu design nalitaka tenaaa. Kama vipi aseme bei gani tumalizaneee. Akasema hataki pesaaa. Kwanini FREE P, Marioo, msingi kiuno mkubwaaa. Anakataa pesa kwa lipi? Akasema sio kila kitu kinanunuliwa na pesa. Pale kwa Sally habanduki.

Kuna siku kulikuwa na party kwa Lidya, Simpendi Lidya wala mambo yake, ila hii niliomba anialike, na alifurahi kunialikaaa mnooo, sikujua kwanini mpaka nimeenda kwenye party hio. Sally alikuja na yule msomali wake. wanapendanampaka wanatia hasiraaaa na kerooo. Hasa ukizingatia yule boya hanaa helaa, haja hustle Congo hata masaa 2 na anapendwa vile. Imagine mimi niliambiwa sina kituuu, na nikajitoa mhanga kwenda kote huku kutafuta hivo vitu, only to find kuna boya mwingine hana kitu kabisaa kabisaaa afu anapendwa ni hatariiii.

Nikawa nimekaa na Jolline, akaniambia mambo yaliozidi kunichefuaaa nafsi yangu kabisaaa. Hamuwezi amini Jolline kadataaa, kaisha kwa yule msomaliii. MOja haikai, mbili haisimamiii. Anampenda ni hatariiii. Roho inamchomokaaa. Ananiomba ushauri afanyajeee, anatesekaaaa na Sally shoga ake, alikuwa ana hope atamdump msomali ila haoni dalili na yeye ana miaka kama mi 5 hajawahi pendaaa wala kutamani mwanaume yoyote baada ya tukio la Mpemba kumkutaaa, ndo maana ni muhimu yeye kuwa na msomali.

Nikabaki najiuliza tu WHAT DO THEY SEE IN HIM?
 
Daah!natamani kuona msomali atakavyo nyolewa na Dee...ila kati ya msomali na Dee,Dee mwanaume mana anajua kutafuta sio yule marioo mjini msingi kiuno
 
Dadekiiiiiii

Men will always be men!

Yani Dee bado anataka kupasha kiporo kwa Sally?

Yani kaamua kushindana na msingi kiuno?

I didn't see this coming!

- KANA -
Hawara hapewi talaka mkuu,acha apashe kiporo tu haina makombo ile
 
Back
Top Bottom