Nimeenda Mogadishu, nikiwa naaminika kabisaa, na nilikuwa benet na Msomali Hussein mwanzo mpaka mwisho! Kabla sijamfahamu Hussein sikujua ni mtu wa namna gani, nilijua kama wasomali wenzie watu wasio eleweka. Ila baada ya kuwa boss wangu na kufanya nae kazi kwa ukaribu ndo nikamfahamu uzuri kwamba ni mtu mmoja poa sanaaa! Isingekuwa tunampenda mwanamke mmoja maybe we could have been Pals.
Wasomali ni watu wa mashaka mashaka sanaa. Hawa muamini mtu isipokuwa wao kwa wao wasomali wanaaminiana sanaa. Ila kwa msaada wa Hussein nikaweza kuishi kwa amani kabisaa. Na ku study security system yao, yoteee, nikatumaaa ripoti zangu ofisini, nikawapa recomendations kwamba wafanye hivi na vile.
Nikiwa najiaanda kwa safari wakasema ngoja uagize kabisaa hivo vifaa ufunge! Nataka kuwa na CIA yangu na FBI hapa Mogadishu. Advanced security systems zenyeweee. Nikawashauri wakatoa oda online China na kulipia online vikapakiliwa na kuja Mogadishu! Nikaanza kuvifunga vile vifaaa! Kipindi hiko Hussein hakuwepo
Nikiwa katika hatua za mwisho, siku hio nimelala usiku akaja binti mzuriiii sanaa, sanaa afu mdogo hana miaka 20 nawaambia, kavaa kimalayaaa malaya, akaanza kuvua nguooo sasa akili ilionijia huu ni mtegooo. Ni kambini tunalala hema moja wengi hata wa 5. Wale wasomali wakawa wananisemesha kisomali sasa siwaelewi! Ila wananipa ishara kula mzigooo huooo!
Akili ikawa haifanyi kazi vizuriii, kwamba ni zali tu la mentaliii au mtegoo huu nategewa kuniharibia kwa boss wangu!yule mwanamke ananionesha ishara twende kichakani, sasa nikasema huyu kule nambanaaa matiti mpaka aseme kama zali au soo! Afu nilikuwa na ukame kishenziii ila wasomali siwaweziiii! Afu wao wnapenda kula wanawake za watu ila wanawake zao wanavowabania kama wahindi.
Nikamfata kichakani, nikaamua kwanza nikate kiu, namna gani vipi baadae walau hata magoli ma 2 ma tatu ndo nimbanne matiti. Tumefika nashtukia nimeminywa pumbu, ule mminyo nikajua tu huyu mwanamke ni Comandoo tena wa hali ya juu. Nikawa mpoleee. Akasema listen carefully! Kesho kutwa asubuhi watakupotezaa! Sina uhakika watakuua vipi, ila ukikabidhi tu project you are a dead man! Hawawezi kukuacha utoke salama huku unajua kila kitu. Sasa basi kesho zua complexity kwenye system mpaka nitakapofanikisha kukuchomoa humu kwenye hili balaa ulilojiingiza.
Nikamuuliza who are you? Akasema haihusu. Ila jua wanajua wewe ni Interpol! Hata Hussein anajua. You think you played them while they played you and interpol all this while. They needed access ya kununua military china na kupata bypass interpol! Now mission is done wanakumaliza na wewe deal done.
Nikamuuliza Hussein anajua kivipi? Akasema anajua tangu akukute sebuleni kwake alikufatilia, unaenda kwake anakuchoraa tu, unamuomba kazi bado anakuchora tu! Mpaka yule mzee kaja Tz ni mipango tu. Unatega bomu wanakuchora tu. Inshort this opperation facked you up Doggy Style, actually it sodomized you.
Nilihisi malaria kaliii, kugundua niko on enemy lines, afu wamenizingiraa, team yangu nime i misslead! Pumbu nilizisikia mguuni siku hio. Nilipanic hatariii. Akaniambia buy time, naangalia jinsi ya kukuokoa hapa, dont trust anybody even Hussein, not anyone.
Nikawa nimelowaaa jashooo! Nikarudi usingizi ukanipaaa kabisaa kabisaa. Akili zinanienda race. Asubuhi nikabadilisha codes za system, nikamuita enginer wao na kumwambia kuna comlexity ajaribu kucheki. Akawa anahangaikaa na system. Mi nikawa napambana na hali yangu najiokoaje. Somalia mimi sio msomali nakimbilia wapiii! Niko out numbered. Chupi ilinibanaaa sanaaa. Nikawa namtegemea yule dada tu.
Hakuja siku 3. Engineer bado ana trouble shoot system imegoma. Wakasema wanawaleta wachina wa 2 from factory tuliponunua hizo systems. Watakuja ndani ya siku 3. In short i had 3 days to live. Nilianza kukondaaa. Mwili jumba ukaanza kuyeyukaaa.
Siku ya 2 yule dada akaja tenaa safari kajidisguise kma mwanaume, akaniambia kuna kapu chooni la kuwekea pedi za wanwake, niingie humo, watanitorosha humo! I have like 5 minutes. Now or never.
Nikazuga zuga nikaingia choo cha kike na kuingia hilo kapu na lina mi pedi kibaoo iliotumikaaa! Wakaja watu kulifunga na kufuli na kulibeba. Nikawa sijui naenda wapi wala natoka wapi. Nikawekwa kwenye gari kwa kuhisia, safari ikaanza. Mlinzi alitusimamisha njiani kataka kukagua akaambiwa hizi pedi akaacha tupite. Tukaenda mwendo mrefuuu sanaaa.
Mpaka nikalala humo na kuamka bado tu tunaenda nisikokujua. Baadae nikaja kitolewa. Kutok hivi najikuta niko kati kati ya jeshi la Somalia chini ya ulinzi mkali. Nikamshukuru Mungu sanaaa. Nikajua vile interpol nitapewa kinywaji, au chakula, na sehemu ya kupumzika. Nikashaanga naingizwa gerezani, pingu za mikono na miguu! Nikawa sielewiii what is what. Chumba cha giza tupuuu afu ni cha kukaa na kutambaa huwezi kusimama.
Nikaja kutolewa huko, nikapelekwa chumba cha mahojino. Nikamkuta yule dada sasa Comandoo na boss wake, wote wna nyota za juu. Nikapewa maji pale na waaknza kunihoji. Nikagoma mpaka niongee na HQ wa interpol! Wakacheka sanaa!
Wkaniambia hii ni Somalia, na as far as wanavojua wao i am a dead man, hakuna atakaekuja kunitafuta akanipataaa. Vita ya Alshababu ni vita ya ndani. Nianze kutiririsha mashairiii A to Z nilichofanya kule, ni drop na names, maybe wanaweza kuacha niishi.
Sasa nikawa sielewi muongo ni yupi kati ya kina Hussein au hawa. Nikawa sielewi ndugu msomajiii, sielewiiii. Najua nachezewa chezooo ila sijui na nani wala chezo linaendaje. Huenda hawa ndo wabaya au wale au wote sielewiii.
Nikaanza kuelezea uongo mtupuuu, mchoro wa uongooo, kwenye ukuta naweka mlango, kwenye dirisha naweka sealed mradi tu kuwapotezaa. Mwisho wakasema wanataka kuinfltrate ile ngome ya Alshabab na wamuue baba mkwe wa Hussein, a clean done job! Ila isjilikane kama ni waoa serikali ya Somalia ndo imeendesha hio operation wasingizie mataifa ya nje. In simple language wanisingizie mimi jumba bovu waache nahangaika na Alshabab!
Comandoo anaeenda kufanya hio kazi ni Rshida yule dada. Na idea twende makomandoo 15. Nikakataa kwamba 15 ni wengi sanaa kwa navoijua ile ngome nilivoiwekea ulinzi, max max twende wa 2 tu, mimi na Rashida baaaas!
Boss wao hakuridhika na hilo wazo kwamba naweza kumgeuka Rashida mda wowote. Nikamwambia sasa nikimgeukaa mimi nilivotoroka hivi wataniaminije na isitoshe kweli hawawezi kuacha niishi nikijua michoro yote ya pale. Mimi nitamsaidia Rashida kuumua yule mzee, akimbwela mbwela nitamuua mwenyewe ku buy time niweze kutoroka kurudi TZ kwa mke wangu na mwanangu.
Akajadili na Rashida mda mrefuuu sanaa, Rashida akamkomvice kwamba ananimuduuu na wamuamini kwa operation hii. Nikafungwa kitambaa na pingu tenaa kurudi huku. Njiani nawaza nitavompoteza Rashida kirahisi maana nimemchorea mchoro kanyaboya, akitaka kutorokea dirishani atakuta bonge la ukutaaa, akitaka kutoroke mlangoni atakuta kutala uhakikaa. Yaani hakunipa shida kabisaa. Shida mimi najiokoajeee.
Tumefika nikamwambia tuingilie sewage system. Tukaingia ndani hoii, tunanuka hatufai. Tuak revise mchoro kwa mara ingine tena, na kw roho ngumu nikamuhakikishia mchoro ndo huo huo. Akaanza kwenda mbele kumsaka yule babu. Nikachukua dakika 3 za ukimya kumuombea sala ya mwisho na kumsemea RIP beuty. Hizi kazi za kiume, ungepata bwana akakuoa leo usongekuwa mwisho wako. Mwanamke lake jiko.
Nikatoka pale na kutoka njr kabisaa kwenye giza, mi eneo nalijua nje ndani. Nikaona Rashida watamdaka sio mda, bora nimpore kamanda mmoja nguo, zikitokea tu chaos nachukua gari nasepaaa! Wakitulia sipooo. Nikwa naranda randa kwa tahadhariii kubwa. Wazo likanijia nimpore kamanda mkubwaa gwanda ili wale wadogo wakiona minyota wasiulize maswali.
Nikaona chumba ghorofani kina watu wanaongea na kwa mbalii nikaona wamevaa zile nguo za wanajeshi wa juu sana. Nikapanda juu nikikwepa Camera! Mtambo si nimeufunga mwenyewe. Kama bahati nikabana corridor, akatoka mmoja. Nikasema huyu mmoja nammudu. Nikaingia na kuzima taaa! Ijwa gizaaa!
Akapanic, rusha risasiii kadhaa hewani, nikachukua tu stuli kwa kusoma movement zake kwa hisia, nikampiga nayo kichwaniii, akaanguka kama mzoga. Nikawashaa taaa! Aliangukia sura. Nikashika pumzi shingoni kazi iliisha pale plae, nimeuaaa! Lengo nimzimishe ila nishauaaa! Nikamgeuza nimvue nguo ndo nilipopigwa na radiiii na shoti za umeme kwa mpigo.
Nimemuua Hussein ndugu msomaji! Hussein kalala pale chali, life less, just like that! Nilitetemekaaaa! Ila nikajikaza kumuangalia pumzi tenaaa! Ashaanza kuwa wa baridi kabisaa kuonesha pumziii hakunaaa. Nikaitaa Hussein, Hussein! Come on man! Come on! KIMYÀAAAAA! Nikasikia INTRUDER ALARM.
Nikaingiwa na ujasiri wa ajabu, nikavaaa nguo zake fastaaa, nikachukua documents zake kwanza kwenye wallet, ID, card za bank, simu, passport yake ya Somalia. Nikamuangalia tenaaa, na kuita Hussein? KIMYAAAAAAAA. Nikamgusaa tenaaa! Deal Done. Mimi ni askari tena Comandoo so najua kuangalia mtu alie hai na alie tangulia. Nikashuka chini fastaa, na kuunlock gari fastaa, nikaoina gari yake nikazama na kuwahi getini. Alioona tu zile rank, na ID Hussein akafungua mlango, maana ilikuwa giza, afu wametaharukiii akahisi Hussein anakimbia labda ndo jeshi lilishazamiaaa. Akakagua tu ID, akafungua geti, nikakanyaga mafutaaa.
Moyo bado uko race, ubongo uko race, mwili uko race. Nikatumia simu yake kucheki location, na kugundua siko mbali na mpaka wa Kenya. Nikakanyaga mafutaaaaaa kama nimevurugwaaa. Gari ikaisha mafuta njiani. Nikashuka na kuanza kuchanja mbuga kwa miguuu. Kama zali likaja lori la kusafirisha wasomali kwenda South. Nikasimamisha nikatoa pesa kwenye wallet ya Hussein na kulipia. Tukaachwa mpaka wa Nairobi. Tukaanza kuchanja tena mbuga kwa miguuu. Asubuhi tukavuka mpaka wa Kenya. Tukapanda Lori lingine mpaka Mombasa, tukavuka mpaka wa Tz. Bado akili inanizunguka. Njiani nilivua zile nguo za Hussein.
Nimefika Tanga, nikaenda ofisi za usalama wa Taifa kwanza ku report hata sijui nilikuwa na report nini. Nikaandika maelekezo pale. Nikaambiwa niende KIA kuna mtu atapokea vizibiti ikiwemo simu ya marehemu Hussein, card za bank na information zote. Sikuruhusiwa hata kwenda chooni mwenyewe nikawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa KIA.
Nikakabidhi vitu vyote kasoro picha moja waliopiga Hussein an Huddah. Nikaiwekaa kwenye wallet yangu. Haina siku nyingi hio picha, nadhani ndo ya mwisho. Wakaniambia sasa wewe unaingia witness protection program as of now, ticket tayari fanya kucheck in safari ianze. Nikasema hapanaa, bado Sally na Huddah! Wakaanza kuleta story za paper work zao bado, watatfutwa baadae. Nikajifanya kuongea na simu, nikasogea pembeni, waliko paki boda bodaa. Naongea na simu huku namwambia boda boda
Umewaona wale wazungu, wazungu wa unga, wanataka kunipa kesi, nikikata hii simu nadandia boda boda yako, motoooooooo ikisimama moshi mjini, kuna laki 3 hapa. Akasema poa. Nilivorukia ile boda boda hawakuaminiii kabisaaa. Tukatoka mkuku pita mashambani humooo kwa humooo uikubikia Same. Nikachukua lori mpaka Dar. Nikarudi nyumbani mfu si mfu mzima si mzimaa.
Nimefika namwambia Sally chukua mtoto twende. Anauliza wapi namwambia huu sio mda wa maswali. Polisi wanakuja. Akaanza kuchonga umeibaaa tenaaaa? Jambazi jambazi tu. Nikamwambia sijaiba Sally trust me. Nitakwambia ila for now just trust me. Wnakuja sasa hivi. Akaamua kunifata kwa wasi wasi, nikakodi gari rental mpaka Bagamoyo kujificha kwanza.
Sally anatukana tu, kama umefanya tukio huko haki mi nitakuwa upande wa mashitaka dhidi yako. Nikamwambia Hussein alikuwa gaidi, wa Alshabab! Akasema NOOOOOO! NO WAY! Nikamuonesha proof kwenye computer yangu, ndo kuanza kunikaanga kwamba kumbe nilimfata Hussein and i used her. She cant believe it was all a lie. Nimemla bureee. Ashasahu mambo ya ugaidi kabisaa anawaza papa kuliwa.
Nikamwambia now is not the time Sally. Akaanza kusema huwezi kumfunga Hussein, anataka kunikimbia na mtoto nishageuka adui. Damu nzitoo. Nikamwambia Mogadishu kulikuwa na tukio na sina uhakika kama Hussein anaendeleaje kama atakuja au vipi. Ila Hussein anatafutwa, na hata asiposhikwa, mimi pia natafutwa na wote interpol na Alshabab. Nikamsimulia kwa umakini mkubwaaa sana ilivokuwa kasoro sehemu ya kumuua Hussein tu. Akachanganyikiwa na yeye.
Nikamwambia i am going back to the US, you can come with me, na Huddah, i can protect you. Msomali na ndugu zake wote magaidiii, they will come for Huddah if Msomali hayupo hata akiwepo are those people the people you want your daughter to grow arround? They kill innocent people just to prove points, just to take ransom. I can protect Huddah! Alivvurugwa kuliko mimi. Akauliza how sasa tuatenda huko marekani,how, nikamwambia there is something Interpol will need from me soon. Ill bargain nyie mpewe makaratasi in exchange.
Siku 2 tulikaa Bagamoyo, ya 3 interpol wakapiga wanataka maongezi. Nikasema siongei chochote na yoyote mpaka mimi na Sally na Huddah tupelekwe marekani na kupewa uraia wa ukimbizi. Only then nitawapa password kwenye simu ya msomali na kutoa codes nilizoweka. Wakakubali. Tukaletewa ticket, business class. Hatukuaga mtu, ile kupotea tu vaaaaap. Tuakenda nchi kama 5 kwanza tukibadilishiwa identity na passport incase Alshabab wakitu track, na finally tukaingia new york.
Lile tukio bado likawa kichwani mwangu, nikapangwa ofisini na kumuona shrink. Nilikuwa silali, nikilalaa naotaa mambo ya kutishaaa. Kichwa kikaanza kuwa kinapata moto. Kuna siku nililala na Sally, nikaota Hussein kaja ananiambi "You killed me, you took my woman, and now you are raising my daughter, i come for revange" Nikastukaa Sally ananiamshaaa. Vipiiiii? Najikausha hamna kituuuu. Akaniuliza Mogadishu kilitokea nini? Najikaza hamnaaaa! Akasema mbona kwenye ndoto, unasema "No Hussein man! I didnt know it was you, come on man"?????? What wente down B? Najikausha tu nothing Sally! Ilikuwa vuruguuu sanaaa. Ni ndoto tu, nimetesekaaaa sanaa Sally, ningekufa mimi, nikaanza kulia. Akanibembelezaaa. Nikaamua silali tenaaa nisije kuharibu.
Nikaenda kwa mtaalamu wa ki Jamaica, na kumwambia kuna mtu ananisumbua snaaa ndotoni na mchanaaa, kuna tukio lilitokea sasa nataka ufanye manuvaaa, na juju asinitokeee tena. Akasema itategemea, kama mzimu wenyewe una hasiraaa, itabdi sasa umalizane nao kwanza, kama hauna umekusamehe itakuwa kazi rahisi. Akafanya fanya mambo paleee. Akasema inatakiwa kitu chake chochote, nikaenda kuifukua ile picha niliko ifichaga na kumpa. Akaichoma, na kufanya ndumba ndumbaa. Akaniambia tayari hatokuja tenaaa. Amekusamehee.
Sikuelewa kama kweli au nimetapeliwa pesa. Ila nikapata amani na kurudi nyumbani. Hata nyumba niliisahau kabisaa, na mwanamke nilikuwa namugopa. Nikamwambia tu Sally nimepona kabisaa kabisaa leo. Akauliza huoni vitu? Nikamwambia sioni tena. Nimesamehewa. Akauliza nani? Nikajibu na dunia.
Nikarudi kazini ila upande wa paper work! Field tena basi. Sally kila baada ya mda anamuulizia Msomali, sijui atakuwa wapi, anaendeleaje, na nini. Mi nasikia utumbo unanikataa. Nikikumbuka amenisamehe basi napata amani ghafla tu. Nampa moyo, maybe one day mtakutana tena. Anahangika kupiga simu bongo kwa namba tofauti kuulizia kama Msomali kaonekana au vipi au wamesikia kitu, anaambiwa hamnaaa.
Mi najitahidi kuishi nae kwa upendo mkubwaaa, amani, na hivi nchi ya watu, hana shoga, na kwanza tunaishi under fake identity, tunasema wakimbizi wa Congo, we only have each other. Haturuhusiwi social life kabisaaa. Nawahi nyumbani, nashinda nao, naonesha upendo wa hajaaaa. Untill i won her love back.
Mungu akatubariki na kimimba, nikamwambia tuoane kwanza. Ilikuwa ndoa ya watu wa 2 tu. Na siku ya harusi akaniambia B i am becoming more and more convised Hussein is dead. Mbona hakuna anaesikia kitu. Lazima angenipataaa. He is gone for good. Nampa moyo kwamba he is jsut hiding. Ana theory nyingi sanaa labda Alshaba wamemuua baada ya mimi kutoroka. Au yuko Guantanamo. Au yuko huko kwenye mahandaki ana teka meli. Kila siku anaamka na theory mpya. Moyoni nawaza angejua ukweliii!
Tukabarikiwa mtoto wa kiume, mimi nikampa jina la Hussein. Ilileta mzozo sanaa kwanini jina hilo? Nikamdanganya aliniokoa na wale wanajeshi kwa kunipa nguo zake, alijitokea kubakia nafasi yangu. I owe him mylife. Akaelewa somo. Moyoni najaribu kufanya malipizi tu nilichofanya Mungu pekee ndo anakijua.
Siku iso na jina Sally akiwa na Huddah na Hussein Jr. na mimi tukakutana na mdada wa kisomali mall. Akamjua Sally. Sally akakomaa kafananishwa sio yeye. Akamjua na Huddah. Katika maongezi akamuuliza hutaki kujua Hussein alipo? Sally nilimungalia pleaseeee usiniangushee jikaushe wewe sio Sally na humjui Hussein, akashindwa kabisaaa. Akauliza where is he? Yule dada akjibu tu kwa masikitiko HE DIED in Mogadishu. Nikaona Sally amekaa chini. Akaendela kusema they found him dead in the room, undressed. Murdered, brutally murdered. He was such a nice soul! Although we live in difficult times, we chose the difficult path but my brother was such a nice harmless soul, full of love and full of life.
Nikafanya sasa kumbeba kinguvuuu na Huddah, na Jr. Ikabidi twende ofisini kuomba kuhamishwa nchi mambo yashaharibika. Tukapewa karatasi za Germany. Na kuhama wiki hio hio. Nilimuonea huruma Huddah ashaanza kuzoea new york na kupata mashosti. Baada ya kutuli sasa ndo wife kujadili kuhusu Hussein.
"B roho imeniuma sanaaa, sanaaa kuhusu baba Huddah!Who on earth could do that to him? How could he? How? Hanaga ubaya na mtu masikini. Si alikupa nguo zake uondokeee, na una deni kwake? sasa PROMISE ME YOU WILL LOOK IN ALL THE INTERPOL FILES, GO TO FIELD IF NECESSARY, NOT LEAVE A SINGLE STOME UNTOUCHED UNTILL YOU FIND OUT WHO MURDERED HUSSEIN AND BRING THEM TO JUSTICE! PROMISE ME B! PROMISE ME1???????
NIKAJIBU TU "I PROMISE" MOYONI NIKAMALIZIA "TO LOVE YOU FOREVER"
**********************THE END************************************
NAKIMBIA MAPEMAAAAA KABLA HAMJAANZA KUNINYOSOAAA NA VILAINISHI MLIVOKUJA NAVO!!!!!!!!!1 NITARUDI BAANA YA MIEZI 10.