Weekend Story! Glory Be To God!

Weekend Story! Glory Be To God!

NAONA UTABIRI MSHAUMALIZAAAA ILA NASIKITIKA BUKU KUMI YANI 10,000 NITABAKIA NAYO MWENYEWEEEEEEEEEEEEEEE NAENDA KU RETOUCH NYWELE YAANI MMESHINDWA KABISAAA KABISAAAA KUTABIRIIII MXIUUUUU. INASIKITISHA SANA. AMA KWELI MMENIANGUSHA.

MI SIPENDI UJUE KUTOTOA 10,000 KWA WASOMAJI. JANA SIJAANDIKA KUSUDIIII KUONGEZA MUDA LABDAAAA KUNA MTU ATAPATIAAA WALAAAAA. TATIZO YOU DONT PAY ATTENTION.

NATOA HINT: 1. PAY ATTENTION TO DETAILS. DETAILS. 2. MOST ROMANTIC ENDING EVER.

HAYA NAONGEZA DAKIKA ZA NIONGEZAAA. JIMALIZENIII. BUKU KUMI KWA UCHIMI WA MAGU SIO DOGOOOO. OOOOOOH! MSINIANGUSHE. Labda @Moneypenny anaweza kupatia.
 
NAONA UTABIRI MSHAUMALIZAAAA ILA NASIKITIKA BUKU KUMI YANI 10,000 NITABAKIA NAYO MWENYEWEEEEEEEEEEEEEEE NAENDA KU RETOUCH NYWELE YAANI MMESHINDWA KABISAAA KABISAAAA KUTABIRIIII MXIUUUUU. INASIKITISHA SANA. AMA KWELI MMENIANGUSHA.

MI SIPENDI UJUE KUTOTOA 10,000 KWA WASOMAJI. JANA SIJAANDIKA KUSUDIIII KUONGEZA MUDA LABDAAAA KUNA MTU ATAPATIAAA WALAAAAA. TATIZO YOU DONT PAY ATTENTION.

NATOA HINT: 1. PAY ATTENTION TO DETAILS. DETAILS. 2. MOST ROMANTIC ENDING EVER.

HAYA NAONGEZA DAKIKA ZA NIONGEZAAA. JIMALIZENIII. BUKU KUMI KWA UCHIMI WA MAGU SIO DOGOOOO. OOOOOOH! MSINIANGUSHE. Labda @Moneypenny anaweza kupatia.
Tumechemka endelea kutushushia story Lara 1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I was at the top of my game in my career, nina projects za kutoshaaa, boss mwenyewe alikubali. Ananiambia interview ulifeli ila Mungu tu aliniambia nikuchukue. Na mimi naitikia Amina. My respect for money was next to none. Nishajifunza zinaishagaaa hizi. Kwa hio this time nikawa very careful na matumizi, na nikaamua kumalizia mjengo wangu huko salasala na kumpa maisha mwanangu na wazazi wangu.

Nikaenda tour France na mzee, maana kitambo ndo alitokaa, tukapita Monacco kote, na mjukuu wake, basi anamsimuliaa pale ilikuwa hivi, pale vile anamuonesha na picha. Mama aliona tunamchoshaa tu, yeye misosiiii tu. Bibi kwa misosiii hajambooo. Mda mwingine anashinda hotelini kalala na kula misosiii. Hobby yake kujaribu misosi mipyaaa.

Bibi akaanza tafuta mumeee. Pamoja na yote yote bado msichana mbona, usisuseee, tafuta mume, pesa unayooo, kama hutaki kuendeshwa, oa wewe basi, tafuta kijana umfugeee. Sio kwamba una dhiki, inaongeza heshimaaa na kupunguza ugaidiii mwanangu. Akioza mmoja sio wote wameozaaa. Sawa Dee hakuwa riziki na Msomali nilikwambia siku ya kwanza sio riziki pia. Mtume mwenyewe alijua kupata mume kazi isio ndogo ndo maana akaruhusu vyuo kumi na mbili. Uolewe na kuachika mara kumi na mbili. Sasa wewe mara 2 ndugu yangu ushakata tamaa! Mimi harusi naitakaaa, kila siku naoa mimi tu kwa kaka zako, naitaka kitchen party na sendoff.

Bibi anaboaaa sanaaa. Mpaka akaanza kuniboa sasa. Akija nyumbani utasikia kungekuwa na mwanaume hapa angefaidiii. Hahahaaaaaa! Mxiuuuuuuuuuu. Enzi nataabika si angewaambia wanaume waje waniokoe. Nyoooo. Anawaambia kaka zangu jamani hamna marafiki huko mumuunganishe dada yenu, atakaa peke yake mpaka lini bwanaaa. Huu mda wa kuongeza mtoto mwingine jamani. Mi nahitaji wajukuuu. Mxiuuuuuuuuu. Mpaka nikawa namkwepaaa kelele zake.


Kweli baada ya maisha kuachia kidogo nikaanza kuona gape ya upwekeeee na u lonely. Mtoto alikuwa hanisumbi sanaa, sababu hawa watoto wa digitali anajua kwamba baba yake tume divorce and she was fine with it. Ila mwenyewe tu kutokana na kuwa kila kituuuu kawaida ya sisi binadamu unaanza kutafuta hata kwa touch kilicho miss maishani mwako. Ni dalili za Neema kufurika.

Enzi nimeyumba hapo kati kati huo mda wa kumuwaza mwanaume ninao? Sijui sina mwanaume, nimepungukiwaaa! Huo mdaaa haukuwepo kabisaaa. Sana sana labda niwaze nipate bonge la bwanaaaa linipe mihelaaaa niwakomesheee kina msomali na Dee. Ndo akili zangu zilivokuwa zinanitumaaa. Ila sikuwa naona gap yoyote, luxury hio nilikuwa sinaa kabisaaa, maisha yalinibana kwenye konaaa.

Yaani hakuna mwanaume nilie muamini kama Dee, ishu wanaume wabayaa, wanaume sio watu nilikuwa nasikia kwa watu tu, ila wanaume zangu woote walijua kunipendaa na kunienz. Ila Dee ndo nimekaa nae mda mrefuuu, afu nilikuwa namuamini kuliko baba yangu mzazi. Kunifanyia vile, hata kaka zangu wala baba yangu mzazi nikaacha kuwaamini kabisaa, achilia wanaume wa kukutana nao njiani. Yaani ndo niliwajua wanaume ni sumu hawajaribiwi kwa kulambwaa. Mmmmmmmmmmh!

Watu kibao wananitaka, wananihitaji kwa mahusiano lakini ile imaniii ya sasa kuingia nae chumbani kumpa mambo ndo ilinitokaaa kabisaa. Nawaza wasije kunifanyia yale alionifanyia Dee na zaidiii. Akhaaaaaaaaaaaaaa! Nilikomaaa. Ukisikia kiranga komooo ndo hii. Nawatamani wasichan wenzangu anakutana na mtu, anaenda kulala nae bila wasi wasi, mimi kwa kweli nilipatwa na Phobia ya wanaume. Mechi ya mwisho kupiga ilikuwa ya Dee. Miaka karibuni mi 3 na.

Ila of recent nikaanza kutamani kuwa na mtu, tatizo nani? Na challange ingine mwanangu mkubwa siku hizi, sikutaka leo ajue baba ni huyu, kesho kazinguaaa hatusemeshani. Sikutakaa kabisaa. Na nilitaka most of all mtu atakaempenda mwanangu kwa dhati na kuwa tayari ku settle down kuwa baba. Sio mtu ambae bado yupo on the move, anajaribisha jaribisha wanawake, hajaamua kutulia. Sikutaka kumdisapoint mwanangu tenaaa. Na sahivi mkubwaa, she asks questions, na anajielewa.

Kama yangekuwa mapenzi yangu mtu nimchunguze pembeni weee, nikimuelewa ndo nimpeleke kwa mwanangu na hapo awe kafikaaa, hana mahangaiko mengineee, mengineee. Na awe karidhia kukaa na sisi, sio mtu maisha ymembana atufanye sisi tiketi ya maishaaa. Achume afu akale na wengine. Mwenyewe Mafia vile vileee.

Mara Dee akaja ofisini kuniambia wameachana na Jolline, nikampa pole, kama mjuavyo ndugu wasomaji either way life fack us all, yasipokula kiboga lazima yakupige chuma mchicha, yakikuonea huruma utaukalia huku ukikatikaaa. Sasa Dee naona yaliamua kumpiga style ya Popo kanyea mbingu. Hahahaaaaa! Si ya kucheka. Sikushangaaa sababu Jolline alishaniambia story nzima akivutia upande wake. Mi kiufupi niliona hayanihusuuu. Zilipendwaaaa.

Basi baada ya hapo Dee akaanza design kujirudisha taratibu ile ki silencer. Hahahahaaa! Nyoko kweliii. Ataniita dinner, nakuuula sijibaniii. Naagiza most expensive food kwenye menu. Namsikilizaaa anavojikoshaaa. Namuitikia ndiooo, kabisaaa kabisaaa. Sawa sawa. Haswaaaa haswaaaaa. Ndiooooo. Sanaaaaaaa. Mnooo mnooo. Kama nilivokuwa namfanyia msomaliii kumdhihaki tu. Anakuwa frustrated hatariii sema atanifanya nini. Ikifika saa 3 naaga naenda kufanya home work.

Akaanza oooh maybe its time, i come home, nianze kubond na Lorraine again, so she gets to know me. Mxiuuuuuuuuuu! Hana hayaaaaaa. Nikaamua kumtolea uvivuuu. Nikaamwambia Dee, kwa ulichonifanyia mimi do you honestly think i will ever like EVER let you near my daughter? Like seriously? Hahahaaaa! Umle kiboga? Au umuwekee deep throat? Weeeeeeeeeeeeeeeeeee! Acha hizo mambo kabisaaa. Sitakiiii, ni sitakiii kabisaaa usoge hata Kilomita moja jirani na alipo mwanangu. Yaani Uncle Dee anakula mikwajuuu sio ya nchi hii. Namsisitiza kama sala DEE IS NOT YOUR UNCLE AND YOU SHOULD BE VERY CAREFUL WITH PEOPLE LIKE DEE. Analijua hilooo kama ishara ya msalaba.

Mi nakujua wewe kuliko mtu yoyote, and i am sorry you will never get near me, ili uni abuse tenaaa? Thubutuuuuu! Mwangu ndo kabisaa hata kama hakuna wa kuachia bore niende nae nakoenda ila sio kukupa wewe, nakujua vizuriii. We niite nije nikunywee bia zako nikusapoti ujinga wako sababu ni binadamu at a point in life ulikuwa mtu, at apoint umegeuka mnyama, i dont judge you and i dont blame you either cause either way life facks us all, lakiniii I DONT TRUST YOU hata kwa kukutaniaaa. Ndo stage tuliopo mimi na wewe.

Alijaribu kuongea maneno hayatokiii, yamekwamiaaa kooni. Dakika anajaribu kuongea kitu maneno hayatokiii kama kapigwa shoti ya umeme. Nikachukua funguo zangu za gari huyooo nikaondokaaa nikamuacha hapo amebungaaa pumbu zimemlegeaaa. Haaaaaaaaaaaa! Hivi alijua nimesahahu au ni mjinga au alijua nini sijuiii. Nyoko kweli kweliii huyu mwanaume. Shubhamiiiit, shenzi wahid.

Msomali akawa anatumia ujanja wa kizamani wa kumfanya mtoto ndo kuwadi wake. Anamlisha maneno ya kuja kuniulizaa. Why cant dad come to live with us here? Mmmmmmh! Na mimi nunda wasinitanie na mwanae. Namwambia because he has a house and a wife, your other mother who used to beat you, do you want her and dad to come to live with us ? Macho yanamtokaaa. Anasema Noooo. Nasema shubhamiiit kama baba yako. Sasa msomali anamuuliza kasemaje anamwambiaaa, msomali anampa maneno menginee. Nikija tu ananidaka, daddy said my other mommy is not my other mommy they are divorced, can daddy come to live with us? Please mom, pleaseeeee. Mmmmmhhh!

Na mimi namwambia, remember when we used to saty in that old house with no pool, and daddy was living in his now house with a view and pool with the other mommy and he never let me even once to sleep in his house, even sit in his sitting room well i got news for you both, you and your sorry a.ss dad, he is not welcome in my house not now and not ever. And if you keep asking me about when dad is comming to live with us, you will find yourself living with your dad, or babu or who ever. Sawa sawaaaa! Mambo ya daddy daddy sitakiiiii nyumbani kwangu. Kama daddy alivokuwa hataki kujua nakula nini nalala wapi na hivo hivo sitakiii.

But Mom we should forgive, you should forgive dad! Huddaaaa ill ground you a year if you say Daddy one more time. Seriously! Anakaa tu kimyaaa. Damu nzito kama maji, ashajazwaa na baba mtu anataka kunijaza mimi thubutuuuuu. Wajipange upyaaaa. Siku ya birthday yake ndo walinichoshaaa sio kidogo. Party ilifanyika shule, sasa tukaend akwa bibi alikuwa kamuandalia ki party kidogo tu tuko wazee tu mule ndani.

Akizima mishumaaa, ku make a wish, asiseme, "I wish for my mom to forgive my daddy and let daddy come to live with us" Haaaaaaaaaaaa! Tobaaaaaaaaa! Mxiuuuuuuuuuuu. Kila mtu alibakia mdomo wazi na kumalizia kusonyaaa tu. Sikuongeaaa kitu, sikusema kitu nilijua nitachokifanyaaa. Nilikuwa na firaha yooote iliisha. Nimewapeleka nyumbani na dada, nikatoka kwanza kwenda kuwa huyo shubhamit zeee lilikosa hayaaa. Nikamkutaaa.

Sikumbakizaa na kumuuliza why in the heel is he turning my daughter against me?Nikamwambia Hussein unanijuaaa vizuri sanaa, haya mambo ya kumnyanyasa mtoto kisaikolojia kwamba asali na kuamini tunaweza kurudiana ni usengery wa hali ya juu. Tena akiniuzi hio kazi naiweza kuliko yeye kumfanya mwanae asimsalimie hata barabarani na sitoifanya mimi nitawaruhusu kina bibi na kila mtu wamwambie ukweli kwamba he has always been a deadbaet daddy, alimkataa na makila kitu aone kama atapata hug wala chochote. The only reason hawamwambii ni sababu sitaki akukumbuke vibaya na ufirauni wako wote.

Be a man na mwambie mtoto ukweli kwamba you are nothing but a piece of shit, sababu ni damu yako atakupenda hivo hivo. Ila kujifanya mwema kwenye macho ya mtoto afu mi ndo mbaya haitaishia vizuriii kabisaaa. Mbona mi sikuja kwenye harusi yako na mtoto kuji victmiseee, jamani nimezaa na Huseein nisaidieniii, asioe. Si uliamua unaoa nikakutakia maisha memaa? Why cant you let me be happy? Kuna mda sina hela ya daladala natembea na mguu nisogee sogee ili nipande bus moja, wewe na mkeo mnapita na big engines, akinipungia na mimi nampungiaaa, akinipa lift na mimi napanda sina ubaya na mtu mie. Nalala njaa nampeleka mwangu akale kwa kaka zangu we chakula unamwagaaa, mbona sikumtuma mtoto aje akwambie mbele za watu mama kalala na njaa siku 3. Na kama kukulaani nakulaani moyoni not even once nimekulaani mbele za mtoto.

Mimi na wewe kuzaa sio sababu. Kama kuzaa niliamua mwenywe sio bahati mbaya au vipi, kwa hio usinijaribuuu kabisaa. Mimi ni yule yule Sally nimeliwa kiboga na Dee, sina marindaa utampeleka wapi mwanamke asie na marindaa, mimi sio msomaliii, wala sio Muislam. Sina ubaya na mtu, sina ubaya na wewe, Let me live my life in peace. Majaribu sipendiiii. Umeninyanyasa sanaaa, sanaaa, katika maisha yangu, na umemnyanyasa sanaa sanaa mwanangu utoto wake, sahivi sitokaa nikutizame utunyanyase mimi na mwannagu. Patachimbikaaaa. Unanijuaaaa lakini.

Akabakia pale mijicho imemtokaaa tu kama mjusi kabanwa na mlango. Nikaondoka zangu. Na tangu siku hio sikusikia my daddy tenaaa. Nyama wakubwa. Heshima ilirudi na mwannagu tukawa tunaelewana sasa yule pepo mchafuuu tulimdhibitiiii. Siku mwanangu akaniambia Daady has another aunty, she is very beautiful, nikamwambia we should be happ for daddy. Na story hio sikuisikia tenaaa.

Nikiwa naendelea na maisha mengine siku hio nikapokea simu ya mtu ambae sijamsikiaaa kitambooo sanaaaaa. Kitambo kweli kweliii. Nikahisi nimesikia vibaya labda. Nikamuuliza nani mwenzangu nipate uhakikaaa! Akauliza Sally hunijui serious au unafanya masiharaaa? Nikashangaaaa! Nikasema jamani nitatafutwa mpaka na mashetani. Nilikuwa na drive, nikasema nitakupigia maana naona kama ndivo sivo.

Nimefika ofisini sikumpigia ila nika mblock kwanzaaa. Nikampigia mama simu, na kumuuliza kuna mtu yoyote amempa namba yangu karibuni. Akasema yeye hajampa mtu ila baba yetu ndo alimpa mtu hio namba, na mtu mwenyewe yeye hamjui ila baba anavosema anaitwa sijui Baunsa!!!!!!!!!!!! Hilo jina Baunsaaaa likanipiga shoti ya umeme. Mama anajimimina tu, baba yako mwenyewe anavodai alikuwaga bwana wako zamani, ndo alikuja kukutafuta, sasa baba yako alijua jinsi nilivo na ugwadu wa harusi yako asingetoa namba ningetoa mimi mwenyewe hata kwa kumkimbizia huko mbele. Mxiuuuuuuuuuuuu bibi jamaniiii.

Nikamuuliza kwa hio ulimwambia napo ishi? Mama akakaa kimya inaoneka alimuelekeza mpaka chumba nacholala dirisha lake liko upande gani. Mxiuuuuuuuuuu! Mbona majangaaaaa. Nikamuuliza hivi mama unamjua huyu baunsaaa vizuriii wewe? Unajua anchofanya mjini? Bibi akapanic, kwani anafanya nini? Mbona unanichanganya? Nikamwambia mwenzio baunsa JAMBAZI LA KUTUMIA SILAHA afu umemuelekeza kwangu, na nina mtoto. Bibi yupo Yesuuuuuuuu wangu! Nimefanya nini mimi. Sasa itakuwaje? Basi labda nimpigie yule rafiki yangu mke wa boss wa brigedia labda atatusaidia. Nikamwambia mama umuite polisi wakati nishakwambia jambaziiii, we acha usifanye chochote niachie mimi nita solve.

Nikawa nimebanwa na kazi nikasahahu kumtoa kwenye block, ikapita wiki nzima. Siku hio Msomali akanipigia simu nikawa sipokei. Sikujisikia. Aakapiga mara 7 sikupokea. Akapiga na namba mpya sikupokea cause tangu ni mblock baunsa namba mpya sipokei. Akatuma meseji kuna hatari pokea simu acha mambo ya kimaku. Akapiga nikapokeaaa. Akaniuliza hivi una akili timamu. Nikataka kukata simu. Akaniambia naona siku hizi una wanaume majambaziii yana tatooo mwili mzimaa afu unamuacha akae na mwangu, akimbakaaaa mtoto yule, nasemaje nitawabaka wewe huyo bwana ako, wazazi wako na ukoo wenu wote. Nikakata simu na kutoka nakimbiaaa.

Break ya kwanza nyumbani. Naingia kama mwizi, namkuta Baunsa katulia sebleni, na mwangu kashika simu ya baunsaa anaichezeaaa, na uhakika ina porn za kutoshaaa. Dada simuoniii. Nikasema tu Hi! Aka smile Hello beautiful. Mwanangu akanisalimia Hello mom! Akarudi kwenye simu nikasema leo leo, nawakogesha mikwajuuuu sio Hudda, sio Dada mikwaju sio ya nchi hii. Wataikogaaa kweli kweli. Tena na mkandaaa.

Nikaingia jikoni, na kuita dadaaaa ile ya danger. Dada akaja, nikamuuliza yule nani sebleni? Unamjua yulee? Nafokaa sijali kama anasikia au hasikii. Dada akasema kaja na babu mimi sikujuaaa, nisingeweza kumfukuza babu. Akaita babuuu. Baba akaitikia toka chumbani na kuuliza kaondoka? Dada akajibu ndio. Nikamuuliza kaondoka nani? Akasema baba Huddah! Babu alikuw anamkimbia baba Huddah akajificha chumbani. Nikajua dada hana kosa.

Nikamfata baba chumbani, na kumuweka mtu kati kwanini kamleta baunsa nyumbani kwangu bila ridhaa yangu. Babu anazeeka vibaya. Kubwa alilosema sikulielewa kiukweliii. Sana sana ni kwamba baunsa ni kama ndugu yetu. Mmmmh! Kama simtaki nitumie siasa za hali ya juu, sio kumfukuza live live. Ananikumbusha mambo ya mwak arobaini na saba alikuwa kapigika baunsa alimsaidia elf 50. Sijui akamsaidia na nini tena, akamsaidia na nini. Hata tulipoochana alipokuwa jela alikuwa akipata simu anamsalimia. Hata alipoenda nje kutafuta maisha sikuu ya mwaka mpya lazima amsalimie na kumtakia sikukuuu njema. Kabla hajarudi alimwambia anataka kurudi, karudi na ndege ya saa 8, saa 11 kaja kumsabahi, sasa ndugu huyo. Tangu na hapo ulaya alikuwa anamtumia tumia western union $300, $500 anamwambia siku hizi wanangu wana hela, hizo fanya mambo yako baba, anamwambia sikupi sababu huna au una shida ila nakupa kama mzazi wangu ili unibariki.

Ama kweli pesa ilimuuza Yesu, basi hizo $300 babu haskii chochote, ananganganaa Baunsa ni ndugu yetu wa damuuu, bado kidogo angesema kamzaa yeye. Nmawambia ashafungwa huyu, anasema ni maisha tuuu, sio kila mtu alibahatika kupata wazazi wa kumuongoza, amekuwa amebadilika, anajitambuaaa. Nikachoka tu kuongeaaa. Nikaamua tu liwalo na liwe, hili baunsa napambana nalo mwenyeweee.

Nikarudi sebleni, kukaa, nimekunja suraaa, niko serious, sichekiii, sura ya mbuziii.

ITAENDELEA USIKU.


MLISHINDWA KUTABIRIIII WAHUSIKAAA, SASA ILE BUKU 10, BADO IPO, OBVIOUSLY BAUNSA ATAISHIA NA SALLY HUO SIO UTABIRI.

TABIRINI PLOT, ATAMPATAJE PATAJE SALLY! ITS GONNA BE HOOOOOOOOOOOOT TONIGHT! ATAEPATIA PLOT YANI SEQUENCE YA MATUKIO, AU CHEZO ZIMA LITAKALO FANYWA NA BAUNSA ATAJICHUKULI HUYU MWEKUNDU WA MSIMBAZI.

LET YOUR IMAGINATIONS GO WILD. MWEKUNDU WA MSIMBAZI KUKOSA WA KUMNYAKUA ITANIUMAAA.
 
Kama nawaona nilivowala Kiboga cha mawazo yenu na kuwapiga akili zenu kifo cha mende, hahahaaaaaa. FANANI NI FANANI TUUUU NA HADHIRAAA NI HADIRAAA TU. HAHAHAAAAAAA! YOU DIDNT SEE IT COMMING. HAHAHAAAAA!

Najua mtasema nimebadilisha Engine angani, na seat za gari, na board zimaaa. Mi nilikuwa nawachora tu mnavojimalizaa. Na hint juu wapiiii. Kweli 10,000 haikuwa riziki yenu.
 
Weeee km Maji ya bahari yanaporudi hayana taarifa, ss Fanya yako uwanja umewekwa nyasi bandia mwaga radhi.
 
Naona timu zooote mmeingia mitini. Jmani 10,000 nimeiwekea ushindi wa mezani. Msipotabiri tuonane kesho jioniii
Hapo baunsa anachukua point tatu kwa Huddah. Dawa ya single mother ni moja tu, mpende mwanae!

Sema itabidi aonyeshe kua amechange.

Lazima utokee ugomvi kati ya Sally na Msomali kuhusu baunsa. Hapa ndo baunsa anamaliza mchezo like a pro!

- KANA -
 
Back
Top Bottom