Weekend Story! Glory Be To God!

Weekend Story! Glory Be To God!

Baada ya kutoka pale kwa Dee, na mwanangu kwanza nilikuwa nachekaaaa kama mazuri. Nilipanic mpaka nikawa nachekaaa kwa masikitiko. Nimefika nyumbani nikamkuta Malliq, nikaamua kuongea ongea nae tu kupunguza stress kwanza. Basi nikawa namchagiza tu ana mpango gani na maisha yake? Angependa fanye nini au anawaza nini. Akaniambia i wish to be a hotelier, ni supervise hiviiii, nihakikishe standards. Sikushangaa cause Maleeq kukaa nae kunataka moyo. Kufanya Hotel Rome kulimuharibuuu. Anaweza kwenda kwa mtu akasema Kunanukaaa, au kuko rough. He just cant stand uchafuuu. Anapata shida utamuonea huruma. Kaninyooshea kina dada hatari.

Nikamwmbia sawa we nipe Cv zako sasa hivi twende tukamuone mtu namjua yupo kule Ramadar Encore. Akakubali, tukaibuka Ramadar. Shida nisikae peke yangu kutafakari. Nikaenda nikamwambia kaa nje kwanza. Nikaingia mimi kuongea nae, akasema nafasi hakunaaa. Namwambia huyuuu kafanya Rome, hotel kubwaaa, he is highly experienced. Anagoma. Nikamwambia basi talk him for 3 minutes mdanganye hata, tumetoka mbaliii, it is cold kumtoa kavu kama mbwa, mwanaume mwenzio yule ujueee. Kishkwambiiii mjazeee afu mchinjie baharini.

Akakubali nikamwambia ingia, tukaingia nae, akaona little details kama globe ilikuwa imekaa vibaya kidogooo, akaiweka mahala pake, pazia ilikuwa haijawekwa vizuri, akaliweka vizuriii, na door mat ilikuwa imesogea kidogo akaiweka mahala pake, little little details akazirekebisha ambazo honestly siku notice, afu ndo akakaa sasa. I could tell the boss was impressed au sijui ndo interview yenyewe. Nikasikia tu what type of figure are we looking at kuku hire. Akaropoka tu $3000. Akaulizwa negotiable? Akasema Yes. Tukaambia jiandae kwa official interview soon, haitaisha week, akamuachia Cv na details zingine.

Tumetoka like hatujafika mbali kapigiwa na Hr simu interview kesho. Nikaona ana raha nikaamua kumuuliza kwanini huongei na Hussein na dada yako? Na kwanini ulijificha Rome miaka yote hio. Akanisimulia, kumbe bwana alikuwa na mwanamke Muitalia, alimtoa SA, akamtumia documents aende Rome holiday. Kufika kule akamshawishi ajifanye mkimbizii, atamsaidia kupata karatasi za uraia. Na baba wa demu wana pesa ndefu sanaaa huko Rome. Na hata hio hotel aliokuwa receptionist, baadae manager baba mkwe ana hisa, ni ya familia yao. Tatizo baba mkwe alikuwa hamtakiii hamtakiii sababu msomali. Ila bintie ndo roho yake. Akiwa bintie arround he is very cool, asipokuwepo wanamnyanyasa ni balaaa. Baba mkwe ndo akamwambia akate mawasiliano na ndugu wooote. Wasijue kama yupo hai au vipi maana migration wana mkono mrefu ndo apewe karatasi za ukimbizi. Ndo kukubali.

Sasa kaaratasi hawajamtafutia, wala nini, baadae yule dada akabadilika na kupata mzungu mwenzie akaolewa, yeye karatasi hanaa, akabakia kunyenyekea tu pale hotelini cause ni the only place ambayo angeweza kufanya kazi na wanajua hana karatasi. Alivumilia saanaaa. Of recent yule dada akawa ashaanza kutibuana na mumewe anamfata hotelini warudiane na harusi ilishafungwaaa. Ana uhakika baba mkwe alimchomaaa migration cause walikuja direct kumbebaaa, hakuchukua hata hankerchief. Ndo hivo kamuachia Mungu. Nilimhurumiaaa.

Nikashangaaa kama Hussein hajamfanyia kitu mbona haongei nae. Nilijua sijui kuna nini beef kati yao. Nikamuuliza akasema bwana iko hiviii, naanzaje, sijaongea nao miaka bila sababu. Amehangaika sanaaa sabbau yangu. I am ashamed. Nikikutana nae sio kwamba napanga kumkalia kimya maneno hayatoki. Na akijua sinalolote it will break his heart. Bora asijue nini kinaendelea maishani mwangu. Nikamwambia hapana make effort. Nenda kwake kaa kimya siku 2 au 3, ye 4 maneno yatatoka. Make effort. Tukarudi nyumbani.

Usiku nikawa natafakari mambo alionifanyia Dee. Niliumiaaa sanaaaa, sanaaaa. Sikukasirika ila niliumiaaa. Nikawaza si ajabu angenila hata kibogaa. Nilisikitikaa kwamba Dee mda wote nilioishi nae nilikuwa sijamjua bado. Na kilichoniuma sanaaa ni kwamba nilijishushaaa, nilifanya kila kitu nilichoambulia ni kunusurika na kifilo tu, maana nimekojolewa mdomoniii, nilipigwa mabaooo, nimefanywaaa hovyooo hovyooo jamaniii.

Kilichonipa nguvu ya kumsamehe ni sababu he was nice to me and my girl at a point. Basi tukio moja ndo unasahauuuu miaka ya kufugwa na Dee. Sikuwa na uhakika kama ni yeye au pepo lilimkumbaaa jini Kiboga labda. Na nilisikitika urafiki wetu unaenda kufa rasmiiii siku ya leo. Kweli hekalu linajengwa miaka 40 na uvunjwa siku 3. Udugu wetu ulikuwa na miaka na miaka umezimw na tukio la masaa tu.

Nikiwa natafakari kwa kina hili tukio, ikaingia whatsup ya msomaliii, nikaifungua na kukuta chupi yangu iliobakia kwa Dee, na hio chupi alininunulia msomali. Sikutaka maneno mengiii nikaa tu kimya. Na kutafakari mbona sina baharti mimi jamani. Mtaka yote kwa pupaaa hukosa yote.

Kesho msomali akaja kanunaaa, kafuraaaa, kavimbaaa, ananipita kama hanioni kwenda kumuangalia mwanae chumbani. Pesa anampa dada wakati mimi nimekaa kwenye kochi. Sikusema chochote. Nishajichokea namuangalia tu. Ikawa ndo tabiaa.

Siku kukawa na party ya mtoto wa Dee, sikutaka Dee aji murder, hakunialikaaa ila aliwaalika kina Maleeq na dada. Mi nikaenda na mwaanangu nikawa nime chill tu sina neno na mtu. Anahaha kama anataka kutaga. Akajizoa zoa kuja kunisalimia. Nmachekea kama si mimi, nimekua siku hizi. Anajisemesha it means a lot kwangu, wewe kujaaa sijui nini namuitikia tu. Party ikaisha tukasepaaa.

Kuna siku nikawa namsikia msomali anaongea alikuwa hajaniona na kina Chriss, nimemuacha yule mwanamke Malayaaa sanaa, kwanza nasikia Dee kamla kibogaaa akamtimua uchi uchi, yule msichana wa kazi wa Dee ndo kasimuliaaa, sasa mimi mwanake asie na marinda wa nini. Nikakohoa akageuka ili ajue tu nimesikia. If you think he was sorry think again. Nikamwambia tu, mimi mzazi mwenzio kama huwezi kuniheshimu kama mwanamke basi niheshimu kama mzazi mwenzio. Akasonyaaaa. Nikaondoka zangu. Mi si mnyonge bwanaaa, acha waninyongeee.

Dee akawa kamvisha pete Jolline, baada ya Jolline kuachana na Tonny kwa sababu zisizo eleweka. Winni alizaa mtoto wa kike, ila kwa jinsi Mungu alivotulaani au kumuokoa Winni toto jeusiii kama mumewe, wakati kaka yangu na sisi wote weupeee. She doujed a bullet. Kila mtu alifurahi sanaaa, except my brother. Na wakaachana for good. Baada ya mumewe kumkubalia hata kama mwana ni haramu atamkubali hivo hivo it meant the world to her. Ndo alipojua kweli yule mwanaume anampenda kweli na yeye akaamua sasa rasmi hapa mpaka kifo kiwatenganishe. She was so happy. Things worked out for her amaizing mpaka nikapata nguvu na mimi ya kuyasuluhisha na msomali, maybe nijishue you know, start over.

Siku hio msomali kaja kumuona Huddah, nikamkaribisha chai, akakubali maana of lately kama maadui. Nikampigia magoti binadamu mwenzanguuu, i am sorry zisizo na idadi. Nisamehe tumlee mwanetu. Nimejifunzaa maishaaa, nimejua maishaaa, ill be the best wife ever. Tumlee mwanetu. Mbona ulinitelekeza nikakusamehe kwa moyo mmoja.

Akanitazamaaa, akasema umeechelewaaa Sally, nishatoa mahari kwa mdada Msomali, nimeona nioe mtu wa kabila langu, anaejua mila za kwetu, aliefundwaa, wahi kumuomba msamaha Dee huenda asimuoe Jolline, dakika za mwisho akakuoa wewe. You never know! Mmetoka mbali sanaa, mimi msomali nimewakutia kati kati, penzi la kweli halifiiii na penzi lenu ni la kweli, mi nitalea tu mwanangu. I failed as a your man but i wont fail as a father. Niliumia rohoooo ndugu msomaji. Kweli mimi Sally wa kukataliwa na kila mtu ama kweli dunia duara.

Alianza kuoa Dee, kama masiharaaaa, kila mtu akajua sitoenda kwenye hio harusiii. Ilikuwa beach wedding, guess best man alikuwa nani? Msomaliii Hussein. Kila mtu alinihurumiaaa, ila niliendaaa sijui hata kwanini nilienda. Kama kuolewa aliolewa Pendo nikampinduaaa, ila anyway sijui kwanini nilienda, na nilikaa mpaka mwisho, nilikuwa na Maleeq, hapo ashaanza kuongea na kaka yake, na kwangu kahama he has his own place.

Hussein alienda kuoa Nairobiii, huyo dada wa Kisomali. Mi picha niliona tu Instagram. Maleeq hakwenda kwenye harusi, nikamwambia yule kaka yako, akasema siwezi, we ni kama mama yangu, siweziii, washanizoea huwaga sipo kwenye kila kitu. Siku Hessina anaoa nilishinda nasafisha nyumba kila sehemu, nilitoa vyombo vyote kabatini nikavisuguaa, nilidekiii, nilidataaaa. Sikuamini kama ndo nishakuwa Single mother rasmiiii. Sikuaminiiiii. Ila it was what it was.

Honey moon anapost picha za mkewe kwa fujooo, mtoto mdogooo, mzuriiii ni balaaaa. Nilishindwa ndugu msomaji nika mu unfollow Insta. Huku Jolline kapata ndoa ya uzeeni ananichapaje bakoraaa sasa. Anajifanya Dee kamzaa yeye. Ananifanyia kusudiii. Wanajitia wako apologetically Happy. Mapicha pichaaa ya fujoooo. Kila unapoenda wapooo. Kama walitunaaa mjiniiii. Nikaanza kumwambia baba kama vipi mi nataka nizamie ulaya, anipe ramani. Mzee anagomaaa ulaya sio kwa mwanamke, na isitoshe ulaya inataka miaka 21 ukichelewa sanaa walau hamna hamna 25. Sally una miaka 32 na mtoto mmoja komaa tu hapa hapa. Bongo haikaliki, huku Dee, hukuu Msomali na mkewe wa Kisomali. Kunikomesha wanakuja nao kwenye maeneo yetu. Nikafanya mchakato nihamie hata kenya wapiii. Michongo inabumaaa. Biashara sio baba yako, sio mama yako useme upumzike miaka 4 afu uje urudi ikubaliii kama ulipoachia thubutuuuu. Nilikata mitaji mi 4, kaka zangu wakasema baaaaaaaasss. Sally utatufilisi, kama vipi tafuta bwana uoleweee, biashara huna nyota tenaaa, nyota umempa Msomali.

Niliishi miaka mi 2 katika hali hio. Mpaka nikaanza kuona Mungu hanipendiii, kabisaaa ananichukia sio bureee. Mtaji sinaaa, mume, sinaaa, maishaaa sinaaaa. Umri tu hazina nilio nayo, na uzee ulivo nuksiii sasa. Nilikondaaa, nikazeeka kabisaaa. Mtoto sina hamu nae, basi nilimpata kwa shida shida inabidi nikomae nae. Na ndo mtu pekee duniani ambae hatokuja kuniachaaa. Nikitizama mwanangu anaishi maisha ambayo siayelewiiii yaani siyaelewiiii wala sikubaliani nayo. Maisha ya kuomba kuomba kwa wajombaaa. Hataaaaaaaaa. Mi niko haiiii.

Nikamfata Hussein, tena mkewe alikuwepo siku hio, akanikaribisha vizuriii, Hussein sio yule maskini kapuku wa kariakoo anajiona ni balaa. Kakaaa kochi la 4 kama nanuka vileee. Nikamwambia naomba nisaidie pesa nifanye business. Akanijibu simple tu Sinaaa. Labda Dee anaweza kukusaidia mmetoka mbali sanaa. Nikamjibu sijazaa na Dee ndo maana sijamuomba. Anajibu kuzaa sio sababu, mi pea sina Sally nikupe nini anafokaaa kabisaaa. Kama mimi sikuwahi kumsaidia maishani mwake.

Zikaanza dharau anamchukua mtoto hata siku 3. Mtoto ananiambia nimechapwa na mama, namuuliza baba yako alikuwepo? Anasema ndio, akafanyaje anasema Dady yelled at me. Nikamuuliza kwenye simu inakuwajeee sasa? Mtoto anaumaa wasitake kunifanyia dharau. Akasema naona mimi sio baba yake, maneno maneno yakamtoka, na mimi nikamtukanaa alizaliwa haupo unaweza kusepa vile vile. Anawaambia watu Sally kanitukanaa, toto lake silisomeshiii, atakula jeuri yake.

Nikakaaa nikawazaaaa, nikawazaaaa, hivi kweli ndo mwisho wangu huu? Kweli? Is there nothing absolutely nothing, i can do kujiokoa? Likanijia wazo, mi si nilisoma mimi mpaka masters, kwanini natesekaaaa? Nikaend akufanya clerance na kuchukua vyeti vyangu. 33 years of age, 0 experience. GPA lower second. Ama kweli academics were not for me. Nikaanza kuwaambia watu, natafta kazi huko kwenu hata PA, customer service, HR, kufagia mradi mkono uende kinywani. Wnanizingua tu. Mpaka Lidya alininyima kazi. Ana kazi ya kusema msichague sanaaa, there was a point in life Sally alikuwa anagombaniwa na Dee shemeji yangu official na Msomali, that was long time ago, both men are married. Yeye kabakia single mom. Mmmmmmmhhhh! Nika anza ku apply mitandaoniii.

Nmuomba tu Mungu wangu for second chance. Hamad siku hio nikaitwa kwenye interview kampuni tu hata siielewi elewi. Kwanza kumwambia sina experience akaanza kuvuta mdomo. Maswali sijui, najibu najiaibishaa tu. Mwisho akauliza una lolote la kusema? Nikasema hapa hapa. Nikasema sikia mdogo wangu sijui kaka yangu, mimi dada sijui mdogo wako, hapa unavoniona maishaaa yamenifiraaaaa kila idaraaa, wanaume wamenizalishaaa wamenikimbiaaa, mimi nilikuwa mtu na maisha yanguuu, mi sio mtu wa hivi ndo maana sina experience ila maishaa yamenila kibogaa yamenimalizaa, i have a daughter she is 6 years old, baba hamtakiiii, mama kavurugwa, not the best way to grow up, nisaidie hii kazi, najua hamna cha maana nilichojibu, ila mimi maisha nayajuaaa. Sitolalamikia mshaharaaa, nitawahi kazini kama sina akili nzuri, kazi zote wewe nipe tu nitafanya, sitoenda likizo, sitoomba ruhuaa, wala sitohama kazi nipo hapa kufanya hii kazi mpaka nizeke basi sina dreams, wala ambitions zaidi ya kuamka kuja hapa asubuhi na kutoka saa 11.

Akasema sawaaa nimekusikia. Nikaondokaa zangu natikisa tu kichwaaa. Nikajua nishakosa ile kazi. Nikaamua niuze kiwanja changu kilikuwa na boma. Hiko kiwanja nilikiandika Hussein akili zilivokuwa ndogooo sasa siwezi kukiuzaa bila Hussein kukubali kunibadilishia jina aukukiuza on my behalf. Nikamfata japo kumfata Hussein au kuingia period mwezi mzima ningechagua kuingia period. Nikamfata anyway na kumwambia kile kiwanja nahitaji kukiuza mambo yangu mabaya sanaaa. Nisamehe kwa yote ila kiwanja inabidi nikiuze. Akagomaa kunipa ushirikiano. Nikamuuliza swali moja tu Hivi Hussein nilikukosea nini kikubwa namna hio mpaka umeninyanyasa maisha yangu yote? Najuuta na nailaani ile siku niliokuona Kariakooo. Ilaaniwe ile siku imeniharibia maishaaa. Akauliza na siku ulionizalia mtoto je? Nikaondoka kimya kimya.

Nikaanza upya mipango ya kwenda nje. Kila nachojaribu kinabumaaa. Pesa sinaa na pesa ndo kila kitu. Mawazo sijui ninywe sumu tu, yakaanza kunijiaaa. Kwanza mwanangu kaka zangu watamlea fresh tu, bibi na babu. Kama vipi nikajaribu maisha upande mwingine wa shilingi. Haya mawazo yakawa yananijia mara kwa mara. Jolline akabeba mimba ya Dee. Hali ikazidi kuwa mbayaaaaa sanaa kwangu.

Siku hio nimekaa sina hili wala lile mara ikaingia simu, jumatatu nianze kazi. Sikkuaminiii. Nilisali usiku mzima nashukuru. Japo sijui naenda kulipwa bei gani. Nikasema Mungu ndo anajuaaa kila kitu. Jumatatu nimemuandaa mwanagu awahi shule, nikatoka kwenda kazini. Nikamkuta Boss yule yule anaefanyisha interview. Akaniambia nakuajiri kama Marketing Manager, hii kampuni mpya, kwa hio utalipwa mshahara million 2 take home kwa kuanziana comission 20% ya kila kazi utakayoiletaaa. Navoshukuru mtanijua ndugu wasomajii. Ofisi ina watu wengi tu, wadada mabinti, wakaka vijana, wahenga kama mimi. Tuko full.

Dhiki mbayaaa, nikimuona boss ambae ndo MD sasa, nambebea bag, namkorogea chai bila kuombwaa. Njaa mbaya sanaa. Najitoa tu ufahamu. Hapo vidada ninakwambia hapa sikai sanaa, hapa mi napitaaa tu. Umri si wanao mkononiii. Wnatamba industry nzimaa. Muhenga bibi naenda wapi na 0 experience yangu. Kazi nafundishwa na wadogo zangu. Ukute boss aliona aibu uzee huu aniajiri officer si aibu hizo akaona bora aniajiri manager. Navojifunza kwa makini sasa. Jioni namkagua mwanangu home work anendelea na kazi. Saa 1 niko ofisini. Boss mtu mzuriii sanaa sanaaa.

Watu wakawa wanasema boss nae kaajiriwa, kwanza sio boss mkubwa wala nini. Dharau. Mi namuona kimungu chagu kidogo kunipa hii kazi mwenzenuuu sijui nimshukuru vipiii. Sasa walikuwa hawajapata kazi kubwa. Kwa hio kampuni ina run na investor coasts. Nikaamua kwenda kwa shoga angu wa kampuni ya simu. Nikapiga jaramba weeee, namkumbusha enzi zangu namletea mavitu China, namkumbushaaa, namwambia niokoe nitafukuzwa kazi. Akasema atajaribuu. Namwambia marketing director bwana wako mnyonye hata pumb ikibidi anipe hio kazi, nakutegemea. Akasema nitajitahidi. Usicheze na ngu za uchi, wakatuita mezani bwana. Boss yuko vizurii akawa convise sijui uchi wa shoga angu ndo uli wa convise zaidiii, ile kazi tukapewa kidogooo tuka break even. Msifanye mchezo na 20% nililo lipwaaa. Oooooooohhhhh!

Kwanza mwanangu kutokana na uhanisi wa baba mtu nilimtoa IST, nikamrudishaa kwa fujo kubwaa, na madonation mengi mengi. Nikahamia Masaki, mtaa mmoja na Hussein awe ananiona kila asubuhiii kumkomoaaa tu. Nilipanga kufanya matusi sio ya nchi hiii. Nikaagiza Mercedes Benz convertible Ebooooooo. When the Gods sees, si ya hela kidogo. Nilienda weekend Dubai shopping kwanza. I AM BACK NDUGU MSOMAJI, KWA KAZI MOJA TU YA KUWANYOOOSHA WALE FUNZA WAWILI, DEE NA MSOMALI. Kama waliona wamenimalizaaa basi mimi ndo nimerudi kivingineeee. Natishaa kama radi. Na nilikuwa na kazi kama 4 kwenye hatua za fainali hizo ni 20% nnee. Remmy ongalaa alivoimba Wemaaaaa, Wemaaa KM/Nyokooooo sasa itakuwa Sally, Sally KM/Nyokooooooooooooo.

ITAENDELEA KESHO.
 
Woyoooo woyooooo I'm team toney twanyakua mtoto mbwa wote watajuuuiita amna msomali wala mzaramooooo
 
Sally wewe kidogo unitoe machozi nijua maisha yamekukula kiboga sally sally woyoooooo

sent from paradise
 
Dee alimfanya vibaya bana

Msomali abaki tu Tz, ili azishuhudie vizuri bakora za Sally. Atakumbuka tu k/koo alipookotwa

Mi bado sioni kosa la Dee, ndo maana hata Sally hana hasira nae kama ilivo kwa msomali.

Al-shabab lenu limeshindwa hata kutunza mwanae! Limesahau lilivo okotwa kariakoo!

Sally amchomeshe uhamiaji shubamit.

- KANA -
 
Ulivyomkataa msomali


Kam sio wewe vile uliekua unashangilia full picture!

- KANA -
Haha me nakuwa honest bana, siwezi kumtetea pa kumtelekeza mtoto wake, ni mpumbavu sana. Sally anamuomba mtaji anamnyima while ndiye aliyemtoa k/koo, bado mtaji huo huo ungetumika kuendeshea maisha ya mwanae. Kuna kitu nilitaka kusema ila lara atageuza gear angani teh
 
Back
Top Bottom