Weekend Story! Glory Be To God!

Weekend Story! Glory Be To God!

Kama umewahi kusikia bitter sweet ndo yalionikuta sikuuuu ile. Kwanza nilikuwa bitter baada ya kugundia Dee anatembea janamke la hoteli sijui li bar woman, sijui linafua mashuka huko hotelini. Halielewekiii halielewekiiii. Na halina adabu. Mwanamke mwenyewe ndo alinitafuta sijui kunirusha roho au kuni komoa sijui. Alinitumia sms whatsup.

" Taarifa rasmi za kujibinafsishia mumeo. Mimi Chiku Jumanne , mwanamke wa kizaramo nakujulisha mumeo nimechukua na ndo nammiliki na sipendi usikie kwa wapambe ila mie ndo mke mwenzio kama bado hujajua. Mimi sio mshari, nakutambua kama wewe ndo bi mkubwa, naomba na wewe unitambue mimi kama mke mdogo na tusiingiliane. Jiji kubwa hili linatutosha sote. Asipokuja kulala usiulize maswali ya kijinga jua amelala kwangu. "

Mmmmmh! Nikajua its a prank! Na Dee was pranking me. Toka lini wezi wa mabwana wakatoa taarifa rasmi. Profile picha ya Dee. Nikajifanya kuwa pranked kweli kumu ectia kwamba nimepanic na nini Dee afu baadae nimchekeeee nimwambie thubutuuuuu yakooo.

Kaja nikamuoneshaaa, nikaanza kujiliza fake tu, siaminiiii, siamiini, namuonesha ile sms. His expression was priceless. Alistukaaa kama kapigwa shoti ya umeme kama hakutarajia. Na mimi nikastukaaa kumbe kweliii naporwa bwana kwa taarifa. Kilichonimaliza he confessed kwamba ni mdada tu wa hotelini , it was a mistake, nothing serious. Khaaaaaaaa! Mazafantaaaa.

Nikawa namkamata kwenye uwongo wake, nimelala ane mara moja tu naapia. Nikamuuliza hio mara moja ndo akapata namba yangu kiaje sasa? Akatoa mijichoooo, ana la kusemaaaa? Anababaika babaika hana pa kutokeaaa. Nikamuuliza na fiona je, anajiuma umaaa na kungata maneno, I am sorry kibaooo.

Niliumia sana moyoooo, sanaaaa. Ukizingatia mi natamani kupiga japo mechi moja na msomali nashindwa, nakuwa katili namsulubishaaa ili tu kusudi nisije ingia majaribuniii, pambafffff. Ofcourse nilijua mwisho itakuwa kusameheana na kuishi happily ever after ila kabla ya kusameheana lazima na mimi nilipizee naenda kupiga game na msomaliii ili twende sawaaa. Kama ukimwi tushiriki 50 50 kila mtu kuuleta.

Najua msomali kwangu hachomoiiii miaka mia nane. Nikachomoka pale kama nimepaniccc kumbe chezooo tu. We nishaingia leba, nishashonwa nyuzi kwa bibi nije kupanikishwa na jitu zima lenye akili zake kuchepukaaa. Aaaah wapi.

Nimeenda kwa msomali, nikajilizaa pale, akaingia kingi. Baadae Dee ananitafutaaaa kwa msomali roho ikaniumaa kweli kwanini nimelala na msomali. Kama sio ujinga nini. Jitu lilinitelekezaaa. Maskini Dee japo ndo zipu nje, nje ila ni bonge moja ya mwanaumeeee.

Hussein sawa kufanya anajua ile tukiongelea being a man, Dee is a man, Hussein will never be. We nani mwanaume gani anaweza kukubali kulea mtoto wa mwanaume mwenzieee tena hafanani naeee. Labda baba Sally na Dee tu. Dee was more like my father in many things.

Watu wanaongeaaa, wanamsemaaa, ila habadilikiiii. Na upendo wake unatoka rohoniii. Msomali atakusema nywele zimefumukaaa, mara unazidi kunenepa, mara nguo haijakukaa vizuriii. Anajali watu wanasemajee, watu wataongea nini, ile kuonekana onpoint kwa watu. Ila Dee walaaa. Tena hapendi kabisaa nijinyanyase sijui nimechoka nakimbizana saluniii. Anasema kwani nani anakudai mbona unakuwa mtumwa huru. Nikinenepa tasifia, nikijipunguza atasifiaaa. Anachosema yeye if i am happy he is happy. Mwanaume kama huyu ata ukipata majaribu ya dunia sio haba atabakia na wewe sio Msomali weee.

Na ana upendo sanaaa, kama Lorranine anamnyoaga mwenyewe. Mi nilikuwa naumwa mgongo siwezi kwenda saloon, ananifumua, ananiosha nywele na kunisuka mabutuuu. Afu anasuka vizuriii sanaa si kalea wadogo zake. Kuna mda nilitaka ku retaouch, akasema kaa hapa you tube si ipo. Atakukata kuchaaa. Mambo madogo madogo kwa a busy man like Dee kuyafanya yanafariji.

Akiwa nyumbani hata sebleni atakaa kidogo atakuja kunichungulia chumbaniii mpaka raha. Even if our sex life was not that super ila our daily life was something. Dee anampenda Lorraine kama mwanae wa kumzaaa. Ndo roho yake. Ujue ukishakuwa mzazi kumpata mtu anaempenda mtoto ndo kila kituuu. Daaah hasira hasara nimemkosea sanaa Dee.

Nikarudi nyumbani akafurahiii sanaa, sanaaaa. Anajieleza nimekutafuta kote koteeee sijakupata. Utaniuaaa Sally. Mimi nipo kimyaaa. Anauliza yameishaaa. Namwambia yameishaaa. Tukaanza kuongea kawaidaaa kabisaaa. Usiku mda wa kulala akatoa simu yake kampigia yule jidada na kumuweka loud speaker na kumwambia its overrrrrrrr!

Akataka mchezooo kuhakikisha yameishaaa kweli. Mi nikamwambia na mimi ninalo la kusemaaa. Akaganda kwanzaaa. Akasema please yasianze upyaaaa! Nikamwambia nahitimishaa tu. Akakaa mkao wa kusikiliza. Nikamwambia bwana nimeuzaa mechi hii jioni. Akastukaaa! Akatoka kabisaa kitandani kama sio yeye aliefumaniwa dakika 10 zilizopita. Akase, please dont tell me ni Msomali. Pleaseeee! Nikakaa kimya. Akasema ni Msomali kwa hio? Nikatikisa kichwa. Ukapita ukimyaaa.

Akauliza kwa hio navompigia mlikiwa wote. Nikatikisa kichwa. Umeanza leo aumuendelezo? Nikajibu leo. Ukapita ukimya. Akauliza why are you telling me now abt it? I mean you could have kept it silent and i would never have guessed! Nikamwambia cause i dont want it to happen again. I am hopping if you know i wont repeat it again. Akavaa suruali na shati akatoka nje. Nilikaa macho mpaka asubuhi hajarudi.

Msomali anatuma sms na delete tu, not now kwa kweli not now. Ikapita wiki hajarudiii. Sitoki nawaza labda atakuja anikose walaaa. Nikampigia akapokea. Nambembeleza rudi nyumbani baby familia yako tumekumisss mnooo. Anazuga zuga hasemi kama atarudi au harudiii. Naomba msamaha upyaaa na kuchomekea wewe mbona umemla mtu pia. Anasema tofautiiiii, ningelala na mtu mpya inhekiwa stress ila msomali tunapendana sanaaa. Sio sawa. I broke his trust. Hawezi kurudi cause he will never trust me again. Nambembelezaaa nambembelezaa kagomaaa.

Ukapita mwezi hajaja. Tukikutana tunaongea kabisaaa ila kama watu wa kawaidaaa. Baadae nikazoeaaa. Nikaamua kuchukua likizo kwanza kukimbiwa na mabwama wa 2 sio mchezooo. Nikachukua likizo ya mabwana nifanye kwanza maisha mengine kidogooo.

Msomali akawa anakuja kuona mtoto na kutuhudumiaa. Kweli kila mtoto anakuja na riziki yake. Toka huyu Huda aje sifanyi kazi nafugwaa na mabwanaaa. Hatariii. Akija ni salamu na kuheshimiana, afu kwangu kuna Malliq madada wa 2 na wote wanajua baba yao ni Dee. Anakuja kumcheki mwanae na nini, mara kumchukua baasi. Mi na yeye tunaheshimiana kama wazazi.

Anataka mambo mengine namkataliaaa kwamba watu watatuonajee si wataona aliosema dee kweli. Mi nipo likizo kwanza napumzisha kipapa kwa mda. We lea mwanao baas. Yangu niachie mwenyewe. Dee akaenda kupanga nyumba akamchukua na mwanae wanaishi wote.

Basi na mimi nampeleka Lorraine akiwa kwa Dee Lorraine, msomali akileta pesa ni Hudda, wakacheze na kaka ake, mradi tu nimkute Dee nimseduce seduce huenda i may pull a msomali on him. Wapii. Nikienda tu, anamuita na winni na mwanae na tumbo lake picha inakuwa imeunguaaa.

Nikaka kitako na Winni na kumuomba ushauriii mbona kama nimelogwaaa? Nikiwa na Dee namtaka Msomaliii mpaka naumwaa. Dee kasepa namtakaa Dee mpaka naumwaaa. Mchezo gani huu nachezaaa jamaniii. Sio pepo hiliiii?

Winni anasema alietuloga shoga angu kafa. Mi mpaka nazaa mtoto wa zinaa. Napanga kuondokaa nashindwaaa nampenda mume wanguuu kufaa. Na kaka ako nae nampendaaa kufa. Kweli shoga angu tumelogwaaa sio bureee. Neema ikizidiii inakuwa kama laana.

Jana nimemwambia baba wa 3 huyu mtoto sio wako, nishajiandaa hata kuchinjwaaa but i had to tell hime the truth. Akanibadilikia, huyo mtoto sio wangu vipi? We mke wa nani? Nani katoa mahari? Nani anakupeleka clinic? Nani ana deki matapishiii? Hayo maongezi mtoto sio wangu sitaki kuyasikia kabisaaa. Ukitaka kujua ubaya wangu nisikie tena hio kauliii. Shoga nilinyamza kimyaaaa.

Nikabaki na mimi Sally natoa mijichooo. Niseme nini sasa. Nikaamua kumpandia dau Dee. Nikampigia simu we need to talk. Akakubali, hakatai mkutano. Akaja nikamwambia Msomali ameniomba anioe na mimi nina mpango wa kumkubaliaaa.

ITAENDELEA KESHO USIKU.
 
Back
Top Bottom