The Return of TROY!
Najua mpaka sasa ndugu wasomaji you consider me a Villain of the highest order katika hii story, second only to THE SNITCH. Mna haki ya kuniona hivo cause you dont know me yet, watu tu wana exaggerate, wanakuza mambo sanaa. By the time you get to know me, the real me you will love me to the fullest, even more than Freddy perharps. Muache unafiki wasomaji, we AVERAGE JOES should stick together. Hahahaaaa.
Kweli what did to Zai was not justifiable, it was wrong and inhuman. To repay someone who did nothing but love you with that kind of hate and evil was dispeakable of me. And karma have already payed me back, and fried my balls out in the openning. Thubutu kukutwa na Mwarabu, anaacha doa kabisaa la udongo wa Dubai. Aiseee.
Honestly i didnt love either sio Zai wala Mama Kijacho, Wote walinipenda wao wakanihitaji kimapenzi na mimi nikaona kitongaaa basi nikakubali nifanyaje sasa. Ila tatizo la kutongozwa ni moja, you just settle and try so hard to be nice to the people waliokutongoza. Ndo maana wanwake wengi sanaa duniani ni unhappily married, wame settle tu cause mtu anawafanyia wema kidogo, na maisha bongo yanabanaa wanakubalii hivo hivo. Sasa na mimi ndo kilinikutaaa hiko.
Why i moved from Zai to mama Kija, because mama Kija said she was preggo and i wanted a baby by that time, nilitaka tu kuwa na mtoto na mimi. Napenda watoto sanaa. Afu Zai aligoma kunizali mpaka nimuoe. Na mimi namuoa vipi bila kujua kama atazaa au vipi? Ugomvi wetu mkubwa ulikuwa hapo kwanye kunizaliaa. Hawa watoto wa kishua wagumu kama nini kukuzalia sio kidogo.
Zai anangangania nimuoe kwa maisha gani niliokuwa nayo back then? Nikamwambia tuzae kwanza, tuishi mambo yakiwa mazuri nitakuoa kwa harusi. Hataki. Ndo nikajua all she wanted was wedding sio ndoa. She loved the idea of me and the white dress na sio ndoa as kuwa pamoja despite anything. Nikaona yule mwingine sababu maskini kuliko mimi maybe atakuwa na right values kumbe hamna kitu.
Now i was all alone and moving slowly. Sasa mwenzenu mimi sio Malaya hata kidogo, nikiwa na mwanamke mmoja ndo huyo huyo, ndo maana nilikaa na Z miaka 5. I have nothing to hide, simu yangu kagua, ratiba zangu fata utakuta kama nilivokwambia, i dont fancy using women for my own pleasures. I am a one woman type of guy always. Baada ya lile purukushani i took a break. Na hivi nilikuwa nishaharishaa kijiweni pale ikabidi nianze ku avoid watu, and peeps didnt like me anymore any ways. I was alone i guess. And life was good untill on day.
One day i met Anna, not that she cut me out complately baada ya sagga lile but i was avaoiding her. Katika watu woteee kijiweni the only person ambae hakuni judge na kunihukumu ni Anna peke yake. She was always understanding and never rude to me during the all fiasco. Kuna watu kama Marriane nikimsemesha hajibu utadhani Zai mdogo wake wa damu. Tina Mkinga ndo tulikutana China, nikata kumu waoh wee alinikata jicho likanipeleka kuzimuuu wakati zamani she was my mentor kwenye business na ndo alinipeleka China mwanzo na kunionesha chimbo zote. Mkinga ananiambia hakuna kupanda tax, tunapanda daladala kwenda Gwandaa nenda canaan pale panda bus, soko flani panda metro, soko la pochi nenda canaan kula boda mpaka leather market tax za nini? Kamtaji kenyewe hako upande na tax we kijana wewe. Namwambia nataka kuweka loose cargo kwenye maji. Unasikia we Kijana, hivo vi CBM ndo upakie kwenye maji utamuuzia nani? Hivo ngoja nikuombee kwa wakinga wenzangu na wapemba wanaofata spea za magari na piki piki wakupe kila zoa, wale wote wapo Gold huko Emirates wana kilo za kutoshaaa. Anachukua simu, Mapembelooo, Ndauliiii, hapa na pale napata watu wa kunibebea mizigo yangu. Tina alinibeba nyie acheni tuuu. Baada ya Kukinukisha kama hanijuiiiiiii. Tena kuna siku kanitukana kikinga kabisaa namsiki ananisema mimi "Limdondooo linyokooo, mngunuuuuh!, chakufurafura na matusi kibaooo anamwambia mwenzie jinsi ambavo sifaiii hata kwa mboleeaaaa. Halima mzaramo ndo kabisaa akiniona ananyesha gharikaaa ya mitusiiii, ananichamba wimaa wimaaaa. Nyie wazaramo sio watu, hakupigi ila anaweza kukusema mpaka roho ikatoka. Kama kunichamba basi ananichamba na steelwire.
Fine nilikoseaaa, na nishajua makosaa, sasa kuniandama, na kuniwekea uhasama vikawa havinijengi. Nikaanza kuwakimbia, nikiwaona wale navuka barabara au naingia dukani. Kasoro Anna ndo ataniuliza unaendeleaje, vipi, za masiku, are you okay na mambo kama hayo. Ila wengine nahisi walitaka wasikie nimekufaaaa. Siku hio nimemkuta ubalazini basi tu akanivutiaaa sanaaa. Kiukweli nikawa namtakaaa. Na nilimtaka nikamtongoze China maana hapa bongo jau tu. Wanga wengi. Basi tunatoka hapa naonesha ma care hatari. Tumefika Dubai mimi Silver so ningeeda kulala hotel sasa kumuacha yeye airport Jau, ikabidi nizame kwenye dollari za mtajii tuchukue hotel, na kila mtu chumba chake maana hapo bado najipanga najipa moyo nitafidia hizi dollari. Kutua china mjinga Freddy huyu hapaaa, kama Vampireee.
Afu mtumziima yule alivyo hovyooo kampeleka Anna downtown Guanzhou kwa wachina wale mambo byeee chumba tu unakuata hotel kwa siku RMB 6000. Daah ikabidi ninawe niende pale Shushanlo walau RMB120 kwa siku sio kesi. Kamzuia mtoto huko huko. Siku ya siku kunitandika bakoraaaa za macho tena sio bakora mijeledi ya macho kaniita ili anissuze mbele ya yule demu. Daaah! The man is savage as fack! Kampiga finger mbele yangu. Savage piece of shit. An throw cash kama uchafuuu na Anna nae analogeka kabisaaa na zile cash. Daaah. I was in a bad position.
Ila sababu na mimi mbishi yeye si anajitia Jihad John sasa na mimi ndo Singanga Amir Ghabar Singh. Nikaona kumface front sitomuwezaa atanisagasaga kama bulldozer na kupoteza kabisaaa. Nikaamua nimfatilie in shadows, nanyemelea kama fisi nikingoja that one timeee, afanye makosa ni make a killing. Inaitwa kosa defence bao. As a man Freddy was good as a striker, fowrd kule kumpata demu kwake sio kazi kabisaaa, kama Messi lazima atapata badoooo tuuu. So kushindana kumpata demu huwezi sababu atakushinda iwe isiwe. Lakini he was worse as a defence. Hajui kumlinda demu baada ya kumpataaa na kumuenzi ili abaki nae. Akishawinda basi kamalizaaa, defence was one of his weaknesss ya wazi kabisaa, ndo maana he was abusing Anna. Not that he didnt love her enough, but hajui kumuenzi na kumlea demu, akishampata demu anamchukulia for granted and his savage nature kwa demu wake anaiendeleza. Hapo sasa ndo palikuwa pa kunipa mimi ushindi. Na kwa angle hii mende ndo nilikua naenda kupindua kabati
China sawa alinigaragaza vibayaa vibayaaa, point zote 3 alichukua yeye. Ila kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongeziii. Tumerudi Dar, wao walikuja na Emirates mi na Turkish nilipitia Uturuki kwanza. Nimerudi nikamcheki kwanza. Akaniambia naenda kwa Marriane na ambavo hanipendiii, nikajikaza nakusindikizaaa. Tumefika kule nina mashaka Marriane atanila nyamaaa. Kumbe walaa, she was not even mean to me, hata kidogo kinirushia shades, hamnaaaaa. Tuko vizuri tuuu. Nikamuona yule mtoto mwarabu, alinikumbusha mbalii hatariii. Wa kiume.
Kumbe Brother K aliamua sioe tenaaa, awe analea wanae wote wa 3 na kale ka nje basi. Marriane kaolewa huku, ka slimu, anashinda na madreaaa na hijabu utamjua sasa Shehat. Ila huyu mwarabu hana hela kabisaaa ukimlinganisha na K. Sasa Anna alivoenda jikoni nikamuuliza Mariane humkumbuki K hata kidogo? Akasema namkumbuka sanaa. almost 10 years naanzaje sasa kumsahau. Hata Feisal saa zingine namuita K na anaitika tu.
Nikamuuliza hujutiii kuacha mijumba ile, fleet ya magari unabadilisha tu, siku hizi una kaa ndani tu, nyumba yenyewe ya kawaidaaa sanaa, mwarabu sio kivileee. Akaniambia "Upendooo tu Troy! Sometimes tunakuwa watumwa wa pesaaa, sawa kule nilikuwa na pesaa ila i was void, upendo hamnaa, acting nyingiiii, ndo maana kila siku nafanya shughuli ili wawepo kupunguza void in my heart. Sina amani, kila nawaza lini nitakufa na ukimwi mwanaume malayaaa mbwa, hana muda na mimi kabisaa. Unaweza hata muhitaji na asikupe tendo wala nini mpaka ajisikie.
Sahivi Feisal hana hela nyingi ila ana utu, ana niheshimuuu na kila siku ananifanya nijisikie wa thamani zaidiii. Kwanza mi nimempita miaka sijui mi 3 na haoni shidaaa, na hivo sikumlazimisha anioe, kanioaa kwa idhini yake, dini hakunilazimisha nibadilishe, mwenywe kwa upendo wake, na kujali nikaona anashindwa kuswali nikamwambia nitabadilishaaa. Kwa jinsi hali ya wanaume wa kawaida mimi na mke wake yule mkubwa wa zamani angeegemea kule maana yule mtoto modogo, mzuri, mwarabu pia kama yeye, mi mzee, afu nishazaa watoto wa 2, ndugu zake hawanipendii hatari, ila yeye akaweka msimamo kwamba it is me he wants kwa dunia ya leo sio kitu kidogo kabisaaa. Basi nikaamua kubadilisha kumfata.
Na watoto wa 2 nimelea mwenyewe, K hayupooo hana mdaaa. Ila huyu niliezaa na Feisal sijatesekaaaa kabisaaa, nalala usiku anamuangalia mwanae na kesho anawahi kazini, saa 10 yuko ndaniii na hatoki tenaaa mpaka kesho anamuangalia mwanae, mnaongeaaa, mnaishiii. Huna haja ya kujiuliza yuko wapi. Yule mkewe akaomba talaka, akampa, mtoto wake namlea mimi sahivi. Na haniingilii kusema sijui nini namlea vibaya au namtesaa walaa. Mtoto alikuja na tabia chafu huyuu, ana matusi matusi, na mama yake na bibi zake washamtia sumuuu, ila kaka na mimi mwenyewe kaona nampenda, sahivi ananiheshimu hatari, na ananipenda kuliko mama yake. Na wale lkina Lorraine Feissal ananisaidia kuwapata, maana bado tupo kwenye mazungumzo ya mda mrefu na K, anipe wanangu japo kagomaaa gomoooo, katu katuuu madai he failed as a husband but he cant fail as a father. Sasa yeye he is not a father ni baba la mjini, out of guilty sahivi kila wanachotaka anawakubaliaaa sasa ndo malezi hayo. Ki Lorraine kimeshaanza kunichukiaaa. Na yeye mda hanaa, kukalala na watoto nyumba moja sio kuwalea, maana mda hana, wanalelewa na dada wa kazi, afu watoto wa kike ataweza kuwaleaaa, ndo namuombaaa anipe wanangu waje waungane na hawaaaa. Bado hatujafikia muafaka. Now i am not rich but i am happy"
Moyoni nikasema huyu ndo wa kumfanya mshirika wangu katika campaign. Nikamchomekea. "Ujue Freddy anamfuja fuja Anna." Akasema "Najuaa ila mwache Anna atajifunza the hard way kama mimi, i cant balme her, it took me 30yrs kujua kipi sahihi nae ukifika mda wake wa kujua atajua. for now ni sawa unampigia mbuzi gitaa acheze." Nikachomeka "Ujue mimi namhitaji nimuoe, but she is not giving me a chance and i dont have forever" Marriane akatikisa kichwa tu "Anna sio mjinga na wewe Troy humuweziii, Freddy tu ndo atamuweza, labda. Mdogo wangu yule sio wife material, hii kazi ya kukaa ndnai kufua michupi ya wanaume haiwezi, nae lifeyst yule hatariii. K wanaiva mpaka kesho kumlipia starehe zakeee, na mambo kama hayo. leo ataamka anataka kufanya hiki, kesho kimemboa antaka kufanya kile, wa mjini sanaa. Na Feisal hawaivi cause Feisal anamwambia olewa uzae watoto si unajua Feisal mwarabu so anaona Anna pale anatupa maisha hatari hahaaaaaa! Hawapikiki chungu kimojaaa. Anna anasema Feisal Alshabab!"
Hakunikatisha tamaa, mimi ndo Troy i always get what i want, sina haraka. Nikaanzia nyuma kuwa bestfriend wa Anna kwanza, ili mwanya ukitokea tu nasababisha ya kwangu. Nazengea kama fisi. Always in shadows, waiting for that one time and all i need is one time and one time only to change the game. I have forever to wait, and i will wait.
ITAENDELEA SAA 10 JIONI.