Weekend Story! All is Fair in Love and War!

Weekend Story! All is Fair in Love and War!

Padre angeweza ku collapse baada ya kusikia hizo dhambi za king of the night...
 
EPISODE YA 10

King of the Night!

I am king of the night not literally but practically. I. Did not juts rise the ranks by luck it was by determination, ambition, and never lettinh go. Maisha yakinifilaa napaka vaseline mwendo mdundoo. Najifunza leo nako kama kwaida nachezea kiboga, napaka ky mapemaa.

Mzazi wako anaweza akamwambia somaa ukamuona firauni hujui tu ufilaji wa maisha huko mbeleee. Laiti ungejua. Boss wako anakipa kazi unadindisha kudai haki karibu kitaa ambapo haki haipatikani ila kwa ncha ya upanga. Get rich or die trying!

I am naturally a good person. A christian by birth. Nimebatizwa, nimepata sakrament zote kasoro ya ndoa tu. Na dini naijua. Basi somewhere along the road fuse zilikatika. This is the secret i am telling you msomaji. Watu wangu wakijua namjua Mungu wataitumia kama weapon. Hawatakiwi kujua kabisaaa.

I started from the ground, kama vinyoka hiviii. Small time tu. Nimekwapua power window, nimekwapua taa. Udokozi mdogo mdogo. Mara sight mirror. Napewa pesa ya bangi na bia. Umri ukatembea majukumu yakaongezekaa. Nikaamua kusaka connection ya bigger deals.

Wa kwanza kunichukua likuwa Jay, kipindi hio anaitwa Jay Sacramento sababu alikuwa mtu comitted kwa mkewe, binti zake, anaenda kanisani kila jumapili, na kikubwa kabisaa hakosii sacrament ya kitubiooo kila Ijumaa na sacrament ya ekarist jumapili. Kuna siku tumetoka kukwapua gari Arusha, jumapili ikatukuta segera, misa ilikuwa inasomwa, hamuwezi amini, alipaki gari, tukasali ile misa, na akapokea ekaristi kama sio yeye alie mlamba mtu shaba just hours before.

As any family man, Jay was a good man. Alitukonsida kama familia yake. Hakuwahi kumzulumu mtu, wala kufanya ubaya wowote. Tangu kwa Jay nilikuwa namuona Liz anakuja pale, anajigonga gonga kwa boss, it was pathetic. Jay is comitted to his wife like really comitted. Liz hakati tamaa.

Ofcourse Jay na liz kwangu ni wakubwa. Kipindi hiko na udogo wangu sijui mapenzi sijiii, nikataka tu kumstiri awe mwanamke wangu. Nikamtongoza akanopaga cha mbavu. Sikuwaza sanaa. Sikukaa sana kwa Jay nikahamia kwa mzee wa Jay. Maana mzee alinifata akanipandia dau, nako sikukaa sanaa. Nikaingia kwenye mishe za upundaa.

Nikawa na kismart, nimepiga route kadhaa fasta fasta nikapanda vyeo nikafika kuwa msaidizi wa boss. Nikausoma mchezo fasta fasta nikaawa naaminiwa kabisaa na boss. Sasa boss alikiwa slow, ashanufaika, tukimwambia tufanye hivi times have changed hataki. Nikawa sijaridhikaaa kabisaaa. Inshort nilipanga kuitaifisha ile business. Ila upinzani ukawa mkali sanaaa.

Nikaanza kuwapambanisha ma boss, wakatibuana yibuana mambo ya devide and rule. Boss akazidi kudhoofika na kufilisika kabisaa. Ila mbishiii kuachia operations. Hamna hamna siku akaniita kwenye gari lake na kuniambia kagundua mimi ndo namfitinisha na wenzie, nataka kumreplace. Kama zali tu, nilikiwa na kisu nikamchoma pigo moja maridadi cha moyo. Akafa palepale.

Nikakimbia na kisu ambacho nilienda kukifunga jiwe na kukizamisha baharini kina cha wavuvi. Hakipatikani leo wala kesho. Kesi ikakosa ushahidi. Tuliwekwa ndani, wengi wengi tukahonga tukatoka. Hamisi ambae nilimkuta hapo kwa boss akataka kuleta njaa kuji declare boss. Nae nikaenda kumchoma kisu cha moyo vile vile nacho kama kawaida baharini kina cha wavuvi.

Baada ya mauaji ya hamisi watu walikimbia kambi sanaa. Maana wakawa hawaelewi nani anamuua nani kwa nini. Territory ikawa wazi. Neglected na ma boss wengine wakawa wanasita. Huku na huku nikajichoma kisu cha juu ya moyo nilivo na roho ngumu, na kisu nikakificha kwanza nikatoka nje na kuzimia nje damu ilitoka nyingi. Nililazwa mwezi mzima. Na kusema muuaji kanikosa kosa nilimkwepa. Ndo baaaas basi tukawa tunashukiana wenyewe kwa wenyewe.

Nikaanza operations sasa kwenye hii territory. Hawakunihisi sanaa sababu na mimi si nilisha chungulia kaburi. Wakaniona na roho ngumu tu. Na roho ngumu kweli. In short baada ya mauaji hayo mawili nikagundua mimi ni natural killer. Kesi 3 ikiwemo mimi mwenyewe na zote nimetembea kiwepesi. Nika consider a career in contract killing pembeni ya powder.

Nikaanza kuwaambia tu nasikia kina muuaji wa kulipwa, kuna muuaji wa kulipwa. Ikasambaa. Ni raia wa israel. Kumpata lazima upatikane kwangu. Mpiganaji wa hisbolah! Trained Assasin. Hafanyi makosa. Mi nimemjua sababu ndo aliwaua wale wa 2 kwa zulma za nyuma huko na mhindi mmoja, akasema kaniacha nimtafutie kazi. Ujue waswahili sio watu wa contract killing ni watu wa ndumba sanaa. Unigwa jini makata wa makata fastaaa. Haina ushahidi. Kazi hazikupatikana.

Ila humo humo kwenye team yangu mtu akileta ushenzi nampoteza. Nikaanza kubadilisha silaha. Visu, bastola. Vikaniboaa. Nikaanza kuwa atumia mazingira yaliyopo kupoteza watu. Zikaanza kazi ndogo ndogo amabzo nilizifanya kwa ustadi mkubwaa sanaa, zikanijengea jina. A.k.a Israel.

Kazi ilioniweka kwenye ramani ni ya kumpoteza tajiri mmoja Arusha. Mwenyewe alichanika million 100 akasema sitaki kuwe na makosa aina yoyote. Kwa kuanzia nilienda na kisu, ila nikamkuta kasimama balconny. Nikaona hakitahitajika. Nikamsukuma tu toka gorofa ya 10. Mpaka kesho kuna debate alisukumwa au aliruka.

Uovu unaofanya una kawaida ya kujitokeza usoni hata mtu asiekujua akikutazama machoni lazima atakujua hili jitu ovu sanaaa. Ikavuma ikaeleweka mi ni mtu mbayaa sanaa! Mno mno. Hilo wanalijua kama majina yao.

I had my share of women. Some disapointed me, some i disapointed. Nishafumaniwa, nishafumania. Naweza kusema nili conclude kwamba women will always be women. Nimalala sanaa na wanawake wa kila aina. Wembamba, mi bongeee. Warabu, wahindi, waswahili, wachina, wa latina. Nimevurugaa sana. Upunda nimetembea mataifa mengi, nimekula vinhi na kuwafanya wengi.

Ikafika mahala nimechokaaa, nishafanya umalaya mpaka basiiii. Laana zote nishafanyaaaa. Nimemaliza umaluuni wote wa duniani. Nataka mwanamke nitulie nae, nimuoe, niwe na familia, niwe na majukumu na mimi. Ila my no one principle ni kwamba lazima awe mwanamke exiting! Wal kuni surprise day by day.

At first nikawa nachukua wanawake wazuriii sana nikiamini ndo mpango mzima. Nikaja kugundua mwanamke mzuri akiwa si wako. Akishakuwa wako hajimaintain wala nini. Ajimaintain ili ufaidi mzigo? Thubutuuuuu yako. Akija kwako siku mbili hana tofauti na wale ilio wafurumisha. Mfurumushe week tu asharudi in shape anawakaaa. Ungese ungese kama huu ndo nikawa siutaki. Mtu inafika stage hata kunyoa tu vuzi inakiwa mpaka ligi.

Nikaamua basi sitaki tena wanawake wazurii sanaa, kwanza uzuri unaisha nataka wanawake wapole. Aaaaahh! In short mtu wa kusema sawa kila jambo anachoshaa. Nikaghairi. Nikasema sasa nitafutie wanawake walioshindikana kama Lara. Pasua kichwa kweli kweli. Wale ma kubwa la maadui. Nikapataga mmoja. Mzurii afu kichwani zimoo. Akawa ananiibia wazi wazi kimacho macho. Nikapiga chini. Mwingine nilimpata Mkurya. Huyu baunsaa. She is violent. With all my violence pale nilisalimu amri. Alikuwa ananipiga mpaka mimi. Sijui alikuwa na mapepo kwenye ngumi man to man nachapwa kipondo mpaka naomba poooh. Afu hana mwili huo wala hapigi tizi, nikajua yu huuu anabebwa na wasio onekana. Ukute wako jeshi. Kumuacha nilitumia diplomasia hatari.

Baada ya hapa nikasema hataaa! Ngoja niishi simple life. Nikimpenda mwanamke namtumia, nampa chake basi. Siku nimeenda jela kuwaona wana, namuona Liza kavurugwa kadataa. Nikamsalimu hakunikumbuka kabisaa. Akawa anaielezea sasa matatizo ya bwana wake, wakati mi najua sio bwana wake. Some how i was attracted to her, sijui i was attracted to her loyalty. Au nilimuonea imani Jay anavomguja fuja vile. I dont know.

Ikapita wiki sijamsahau. Mwezi bado kanikaa kichwani. Kumpata haikuwa shida maana siku za kutembelea wageni jela, yumooo. Nikaanza kwenda jela nimuone tu, mimi huyu huyu king of the night, msinitanie. After several attempts she showed no interest, nikawa nimedata. Namtakaa namtakaa. Nikakosa angle.
o
Baada ya Jay kutoka watu wakaniambia boss yule demu huwezi kimtaka tenaa. Nikauliza kwanini. Anavaa vijoraa bwana na kushinda vilabuni. Nikasema bora nikamuone anitumbukie nyongo tu nimsahau. Kumuona bado namtaka. Tena nikawaza nahitaji mtu kama huyuuu kuliko never before. Hata nikifungwa yupooo. Her loyalty is everything.

Nampata vipi mnazanii. Nikaona kumpata bila Jay sio rahisi. Ngoja nimuinhize kingi Jay anipe. Kweli shida mwanaharamu akajaa akanikabidhi. Nilihitaji anikabidhi kwa hiari yake. Ningempora ingenipotezea heshima kwa wafanyakazi wangu wa kiume. Kunipa Jay ashakiwa mnywa viroba haikuwa kazi. Kazi ikabakia kumfanya anipende.

Mwanzo nikaanza kumtreat vizuri tu, nikampa mda auone wema wangu. Nalala nae chumba kimoja simgusi. I wanted her to find it in her heart to love me. Naongea business yuko pembeni namuuliza Liz unasemaje. Nilimtreat vizuriii. Nikajua ananiibia pesa anampa Jay nikapotezeaa.

Kilichonitibua mavuzi mpaka nikampiga ni bangi zake. I was not in mood. Akasema you one day, me and Jay we will disapear? Nikamuuliza kwanini? Kwani nakunyanyasa mama? Unaona bora ukashinde vilabuni na Jay kuliko kukaa na mimi hapa. Am i mistreating you in any way? Akasema sikupendi tu. Nikamwambia Liz msengery wewe usiniambie hivoooo. Nitapandwa na vya kupandwa. Mi nawalisha na bwana wako dont you dare. Ashaniona junyaaa, sikupendiii wewe, nasema sikupendiii na sitokipenda, Jay nyoko nyoko.

Nilimzibuaaa kisawa sawa. Maybe i went a little over board. Ila adabu ilimuingia na sikutegemea atanichukilia poa any time soon. I felt bad realy bad. Jay akaondoka baada ya kuona nimempasua mwanamke wake. Nilimuomba msamaha sanaa. Akajibu kanisamehe not that she had a choice. To make amends i bought her new teeth, very expensive procedure.

Nikaanza kumtia wivuuu, nalala na wanawake wengine mbele zake walau ajisikie hata wivuu, wapii. Kila mtu King piga chini, piga chini. Jitu lenyewe zee kama Zari the boss lady bwanaa. Achana nalo. Mi anavonikataa ndo anazidi kunifanya nimpendee zaidii. It was exiting.

Tukaja kumponda ponda Jay. Nikamwambia usipomuacha Jay uta,sababishia kifo. He wont be this lucky twice. Baada ya lile tukio, alikaaa ndani miezi 2. Mwenywe tu, hatoki chumbani. Sijamfungia, sijamzuia. Mwenyewe tu. Ndo Jay akahisi nimemuua. Watu wengi walihisi hivoo. Baadae nikasikia Jay kaondoka nchini.

Kama baada ya siku 3 Jay kuondoka. Nikiwa chumbani kwangu maana nae ana chumba chake, na mwanamke mwengine akaja nikastukaa nikasema anataka kuniua nini. Akamfukuza yule mwanamke. Nikajua huyu ananiia kweli. Nikawa nimekaa kimachale machale. Akanitaarifu tu, ukileta mwanamke mwingine uje na jeneza kabisaa maana hatoki mzimaa. Namuua mbele zako.

Nikastukaa sanaa. Nikasema hii mbinu ya kijinga ila imefanya kazi. Nikamtuliza nilete mwanamke wa nini kama wewe umeamua kujielewa baby. Akavua nguo kwa hiari yake, ila mzigo sikulaa. Nilihisi anataka aninyofoe korodani. Nikamwambia lets just talk.

Asubuhi akaniandalia chai, maji ya kuoga. Bado simuamini kabisaa. Chai kwanza maziwa nikampa paka, hakufa, ndo nikayanywa. Yai sikuligusa. Akaja kusema unahisi nimekuwekea sumu? Akalila yeye lote. Mmmmh. Nikaenda mishe mishe ila niliwaza sanaa.

Nimerudi napikiwa chai, na kandwa, kandwa. Nikapewa na mzigo safari hii nikaula kibishiii tu hivo hivo roho ngumu kisu kiko chini ya mto just in case. Anauliza kazini vipi, namsimulia anatoa way foward. And she was smart, shule si kapita.

Nawaambia ndani ya mwezi Jay who??? Nawauliza ndugu wasomaji Jay who? Mimi na Liz, Liz na mimi. She did have me by the balls. Na cha kustaabisha nilitulia kabisaa kabisaa kama sio mimi. Mpaka kazi yangu ya contract killer nilistopisha kwanzaa. Nifaidi kwanza maisha. Nikaenda kutubu Faza alifungua kizimba anione sura kwanza sio kwa kitubio kizito vile, kama Lucifer kaja kutubu.

Life was a paradise mpaka siku napita hivi sebuleni nikakanyaga kitu chini ya kapeti. Kufunua hivi line ya simu. Nikaitia kwenye simu. Kumbe wanawasiliana na Jay and they were playing ,e ndugu msomaji. Meeeeeeee! THE KING OF THE NIGHT. THE CONTRACT KILLER! ISRAEL.

ITAENDELEA
Uwiiii..story tamu jamani
 
EPISODE 9

THE CRIMINAL.

Yes i am married ndugu msomaji, twice! Like anybody i though ill find the love of my life, marry her and live happily ever after. But no! Either way life facks us all. It is a pitty i have had these 2 women like all my life. And who do i love more is a question i can not answer honestly. Lets just say i love a little from each one, and most of all i love my kids.

Liz i never loved nor liked. She is not my type at all. Though she is not that bad or anything. It is just me ndugu msomaji, she is not my type. You dig. Dianne i loved this life and next life, till eternity. Only she did not love me back, or well maybe the love died mid way. She will forever have part of my heart.

Even after everything, the betrayals, the lies, breakups i still pay all her bills. For my kids ofcourse but i would still have done it even if she didnt have kids. I cant just shut her out in the cold after everything. She might be a little beastly but she is still my Diane.

Diane was girlfriend like forever. Tangu baba na mama. And she was sick, alikuwa na severe asthma, and her sister died of Asthma, so everybody thought she would not live that long anyways, and wanted me to be nice to her as long as she lives. She was also anaemic. Lets say she was a sick kid.

I treated her well God knows i did. Mpaka siku ya kutoana bikra alisema yeye. Nilimsikiliza na kumpenda kwa moyo wote. I even found her a friend Liz. We went school together, holidays together, vaccations together. We grew up together.

Then i met Liz in the middle of a family Feud. My dad was a tight man, mean and brutal. He thought Diane would die and even if she didnt alikuwa hamtakii hamtakii sabbau ni carrier wa Anaemia. Kwamba ataleta hilo gonjwa kwenye ukoo. Ad he was dead serious. Kumtibu mavuzi ndo nika stage show ya kudate na Liz chini ya uangalizi wa mama kubwa. Of course tulijua kwamba hwezi kumu approve kabisaa kabisaa because of back ground na nini.

Then i knew Liz, couldnt pretend i dont know her. Nikamshauri Diane wawe marafiki and yes she needed a friend. Wakawa marafiki wakubwa sanaa. Swala kwamba Liz ananitaka nilikuwa nalijuaa sanaa. Na nilikuwa namuona anavonitaka wazi wazi. Like i said i was comitted to Diane and even if i was not Liz was not my type.

Utu uzima ukaingia nikaanza kufanya kazi na mzee. Mzee alikuwa high life criminal. From contraband, jacked cars, money laundering, people trafficking anything that pays the bills. Nilijaribu kwenda another direction but it ment sitoweza kumudu gharama za kumuoa Diane na kumpa maisha alio zoea. Sikuwa na budi ikabidi nijiunge na mzee.

I moved fast, too fast mpaka tukagombana na mzee baada ya kugundua i did set up my own min organisation within his organisation double crossing him, he kicked me out. By then nishakuwa Mafia mwenyewe sikuhitaji refa. Unlike mzee anatanga tanga mi nikajikita kuuza gari za wizi. Zinaibiwa south mi naziuza hapa mjini kwa faida kubwa sanaa. Life was good. Dad could never be more proud of me until i made it official kwa kumuoa Dianne.

Sikuwa nimewaambia kiundani why dad hated Dianne. He was scared of Dianne cause his dad was a Police general. To be precise the IGP is Diane's uncle. Kwenye harusi alikuja kishingo upande afanyaje. Akakaa meza moja na wakuu wa nchi, IGP mwenyewe alikuwepoo waka shake hand. Alichoniambia tu ni kwamba we mngesery unachokitafuta utakipata soon. Na usinijue.

Life with Diane was like paradise. She is the best woman any man can wish for. Japo ilitakiwa asizae kwa afya yake akafosi kunizalia hivo hivo. Na ilikuwa nusra nusra almanusra nimkose, Mungu mkubwa nikawapata wote na baby.

Matatizo yalianzakama utani. Gari lili ibiwa South. Nikanunua na kuliuza. By this time nina yard. So niko legit na magendo kote kote. Bwana wee kumbe gari la ndugu yake Thabo Mbeki. Interpol wanalooo, wamelitrace trace mpaka yard kwangu. By the time wana full support ya IGP. Nikaja kubebwa nyumbani usiku usiku na kusekwa ndani.

Nimekaa ndani siku 3. Anakuja mama na Liz tu. Mzee katuma salamu nisimjue kabisaaa kabisaa. Nauliza Diane yuko wapi. Nikaomba kuonana na IGP si uncle, tunakaa nae mezani, anawabeba wanangu. Nikaambiwa kasema hakujui, wala hajawahi kukuona. Siku ya 10 Diane kaja. Nikasahahu yote na kufurahia. Ana laumu mwanzo mpaka mwisho, i played her all this time, kwanini sikuwa muwazi, nimemuharibia maisha sijui nini. Nmakubusha Dianne its me Jay, your Jay. Akaniambia ana mimba nyingine.

Nikahamishiwa segerea. Liz na Mama hawakosii kuja. Ananiletea na contraband. Upelelezi ulikuwa haujakamilika gari haikupatikanaa mpaka mda huo. Nimekaa sgerea miezi 7. Diana alikuja segerea mara 3 tu akasema mimba inanisumbua. Nikawa nampenda hivo hivo.

Anajifungua nafanya kuambiwa na mama na kuoneshwa picha. Akaja baada ya si month. Nikamwambia walete watoto niwaone akasema hamnaaa. Kwanza nawaambia uko ulaya. Siwezi kuwaambia uko jela. Niliumia sanaaa. Ila nikasema for the better ya watoto.

Nikawa nakaribia kutoka maana ushahidi hakuna, nimekaa sana ndani. Nilimwaga sana pesa. Ikiwa imebakia kidogo nipelekwe mahakamani mara ya mwisho itolewe hukumu, upande wa mashtaka ukasema umepata ushahidi mpya. Walioiba ile gari wamekamatwa south. Ni swala tu la kuletwa nchini kutoa ushahidi kwamba nilinunua ile gari kama organised crime nikijua wazi ni gari la wizi, kesi itakuwa imekwisha. Nikarudishwa segerea.

Nilichanganyikiwaaa. Miaka 40 hii hapa naichunguliaa. Mke nilietegemea atakuwa faraja kanitengaaa. Nikatuma sms Mzee aje anione chonde chonde. Nae hakuwepo mahakamani ila taarifa za ushahidi mpya alizipata. Hakuja. Akaja mama analalamika tu baba yako si mtu yulee. Si mtu yuleee.

I lost hope complately. Mpaka mda huu i only had Liz by my side ambae kasimamisha maisha yake kunipigania. Mpaka lawayer anawalipa yeye. Ananisaidiaakiona lawayer ana pwaya analeta mpya hachokiii. Kunipigania nitokeee. Alikuwa ashatolewa mahari, kaahirisha mpaka harusii. Yule bwana ashaoa mtu mwingine.

Nikamwambia Liz i am sorry you risked everything for me, ila nasikitika i will be going away 30 years. Liz anasema hapana Jay, hapanaaa, sijakubalii bado. Namwambia tutafanya nini. Liz akaenda kwaambia upande wa mashtaka ill cut a deal, nisaidie mzee na organisation yake akamatwe in return for a less sentence. Wakaniita mezani nikasema hapanaa. Siwezii kumchoma mzee. I jsut cant. We cant go away me and dad kwa wakakti mmoja Mama atakufa na pressure. Nitaenda hio miaka 30. Afterall nikajiambia sio kwamba nasingiziwa. Makosa nimetenda kweli. I refused the plea deal.

Wakaleta deal lingine niwachome mtandao mzimaa, for a lesser sentence. Nikawaza nikisha wachoma tukiwa wote huko jela si watanila kiboga kwa mtungoo. Jela yenyewe moja. Bora nikate wanipe protection. Maana hata nikitoka baada ya kuwachoma watanila shaba nje tu ya gereza shubhamit.

Tukaenda tena mahakamani, wakasema hao watuhumiwa wataletwa tarehe 27, mwezi ujao kuja kutoa ushahidi, maana wana kesi kesi zingine za Zambia, Malawi wanatoa ushahidi kwanza. Nikaona mwisho umefikaa kwelii. Dianne toka ajifungue alikuja mahakamani mara moja tu. Nilivotoka mahakamni nikagongana na Mzee after years za kukaa ndani na kwenda mahakamni ndo Mzee kaja. Akanisalimia tu. Akaniambia kuna mambo nayaweka sawa, bado kwanza ila wiki ijayo naenda South, tuombe kheriii unaweza kutoka. Stay strong son.

He is my father and i know for a fact he is a cheat and a lair. Hapo ashasikiasijamchoma ananipooza niwe jasiri mpaka nifungwe miaka 30, ahakikishe simchomi tenaa ndo akae kwa amani. Sikumfatilia sanaa. Liz alikonda kama mke wa mtuhumiwa. Aliogopa mi kufungwa kuliko mtuhumiwa mwenyewe.


Tarehe 27 nikaenda mahakamani, IGP alikuwepo, baba mkwe alikuwepo hawa watu sijawaona toka maa mwisho kabla sijabebwa ndani kwangu mzobe mzobe. Baba alikuwepo, Mama alikuwepo. Liz alikuwepo kakonda zaidii kabakia skeleton na kila saa anenda chooni. Diane hakuwepoo kama kawaida. Washkaji zangu walikuwepo.

Watuhumiwa wakaanza kutoa ushahidi mmoja mmoja. Wa kwanza mi simjui na yeye hanijui. Kwa maelezo yake msouth yeye, na ndo aliiba ile gari. Akataja ilikuwa mercedes benz ya 2013 na mambo mengi kuhusu gari alivoivusha mpaka Harare. Akasema aliambiwa mteja ashapatikana na alitajiwa jina anitwa Jayson yuko Daresalaam. Akaulizwa Jayson unamjua kwa sura? Akasema hapana. Akaulizwa unamjua kwa jina la pili akasema ndio. Anaitwa Jayson nani? Akasema anaitwa Jayson D. Kabby. Amejuaje? Alifanya wire transfer ya pesa. Upande wa mashtaka ukawasilisha copy ya pssport yangu ikithibitishapassipo shaka mimi ndie Jayson D. Kabby.

Wakili wangu akamuuliza je mlipanga wa namna yoyote na Jayson kumuuzia hii gari? Direct wewe na yeye, mliongea au kuwasiliana kwa namna yoyote na akijua fika gari la wizi hilo?Aksema hapana. Akaulizwa kwa kifupi zaidi ya wire transfer ambapo huenda mteja wangu alifanya bila kujua mchezo uliopo huna namna ingine ya kumuunganisha na kesi yako ya wizi wa hilo gari.

Akasema hapana, Jayson ni mteja wa uhakia. Sio kwamba hio gari aliuziwa kwamba ilikwapuliwa ikawa sokoni, bali alipkea special oda ya hio gari za specification hizo kutoka kwa mtuhumiwa wa pili alieagizwa na Jayson. Hawafanyi special order kwa fist time customers. Nikaona Liz anaenda chooni. Mwenyewe mshusho ulinigonga chupi. Akamuuliza maswali mengine mengine ya ilimradi.

Akaja mtuhumiwa pili, alievusha gari toka harare mpaka Lusaka. Huyu alikuwa more of the transporter and a driver . Hakuwa na mengi ya kusemaa. Alikuwa mtu wa kupewa mizigo tu ya kuvusha sio mtu wa organisation na mipango miji.

Akaja mtuhumiwa wa 3 ndo tuliefanya nae biashara. By that time mimi nimefumba tu macho. Sina hamuuu. Akajieleza kwamba yeye ndo alivusha gari toka Lusaka mpaka Daresalaam. Na yeye ndo mpango mzimaa wa operation hii. Akaulizwaje ni kweli gari lilikuwa la wizi na ni special order toka kwa mtuhumiwa Jayson D Kabby? Akasema ndio gari lilikuwa la wizi na ndio kweli ilio ya kweli likuwa la special order......" Nikaona mawakili wanakusanya ma file kazi imeishaa. Maza analia tu. IGP alitangulia kutoka nahisi kukwepa vyombo vya habari. Baba mkwe kabakia pale kajikunyata sijui henia ilisha muanza tena.

Mtuhumiwa akaendelea ......" Nikalileta mpaka kwa mtuhumiwa Jayson D Kabby kwenye yard yake Magomeni, ikalala pale siku 7 na siku ya nane nikaiuza kwa raia wa Sudan Meshack Halil. Akaambiwa tunashukuru kwa ushahidi wako. Akaendelea isichofahamu mahakama ni kwamba special order haikutoka kwa Jayson, wala Jayson hakujua kama hii gari inatoka wapi kwa minajili gani kwenda wapi. Jayson ni mushkaji yangu nauza magari hapa dar. Clean cars. hakufahamu kitutu yoyote. Meshack ambae ni general huko Dafur wa serikali ya waasi ndo alinipatia oda.

Mi naenda kwa Jayson kama rafiki, naweka gari yangu pale. Nikamuomba nimpatie $$$$ afanye transfer kwa mtuhumiwa number moja. Na mimi ndo nilimpatia mtuhumiwa number 1 oda, nikamudanganya inatoka kwa Jayson cause Jayson anauza magari clean muda yote ambayo hayako na profts muzuri. Nilimwambia hivo ajue iko risky deal nipatie kwa pesa kidogo. Ndo maana nikamtick Jayson amulipe mshkaji ili asistuke.

Jayson is a victim of circumstance and betrayal your honor. Hausikii kabisaa na hii organised crime, especially hii gari." Nikabaki heeeeeeeeee! Sihusiki kumbeeee. Thank you Lord. Ukafata mchuano mkali wa waenesha mashtaka hawakuta kukubali kirahisi. Ila huyu jamaa wa mwisho anajua mshenziii. Kawajaza mule mule kwenye ushahidi wao. Kesi ikaahirishwa mpaka mwezi ujao ndo hukumu itatolewa.

Wakati tunatoka, Mzee akanimbia nazani pale tumemaliza, nakutarajia nyumbani mwezi ujao. Jamaa kacheza kama pele. Na mimi huu mwezi ulikuwa mwepesi. Siku ya hukumu IGP nadni, baba mkwe, baba, mama, ndugu ambao siajwaona miaka na miaka si washasikia natokaa. Diane ndani na watoto wote wa 2. Roho iliniumaa mnooo.

Huku na huku Hakimu akasema upande wa mashtaka umeamua kutoendelea na kesi dhidi yangu baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha. Niko huru kwa sasa mpaka ushahidi mpya utakapowasilishwa tena kama ukijitokeza na upande wa mashtaka.

Wa kwanza kuja beside me alikuwa Diane, na watoto na baba mkwe akanipa mkono wa hongeraa, na IGP akawa anajipangusa pangusa makalio kwa aibu. Na Mzee. Tukawa tunaondoka nikamuona Liz kwa mbali ananiangalia, akiwa peke yake. Umri umeenda, aliempigania nimerudi kwa familia yangu, she could never be more alone. Nilijisikia vibaya sanaa ukizingatia yeye ndo alipambana fron miaka yote hii. Ila ningefanyaje, wakati inafahamika MALI HALALI KABISAA YA DIANE.

Nikasema nikifika tu nampigia, nikakumbuka sina simu. Kurudi kwangu kidogo nipige yoweee. Garden yangu nilio ipenda sanaa imekaukaa kau uko udongo tupu. Kwangu hakueleweki eleweki. Nikaomba statement ya ssets zangu akasema anauma snaa kichwa. Wiki likaisha sipewi msimamo. Mwisho akaniambia i sold everything, what did you expect being locked fr so long? Wanakula mawe hawa? Ada watasomea mavuzi yangu? Hapa tunamtegemea baba yangu kwa chakula fanya ukabebe hata zege tupate chakula.

Ukishafungwa ni kazi mnoo kupata commection maana unaonekana unagundu. Mpaka mzee akaniambia stay off the books kwa mda cause feds are still on you. Kuwa legit hata miaka mitano. Nilionana na Liz nae kafilisika kabisaa bora Diane, anakaa chumba kimoja hata nguo hana. I have to see women suffer. Especially not for me. Nikawa nimedata.

Naenda kunywa kilabuniii gongo, pesa ya bia sinaaa. Liz nae hana pesa, kazi alifukuzwa kutoroka kuja mahakamani na kufatilia kesi yangu. Tunakaa nae kilabuni. Hanywi anakaa tu hapo pembeni, ili nikilewa na kufanya fujo anitulizeee. I became a Liquor slave.

Nikirudi Diane kanifungia mlango nje. Mama yake akija anwambia divorce him, ashafungwa huyu akili zake bai tena. Watoto wa 2 utapata mtu mwingine wa maana, mbona si wengi. Tangu yuko jela nilikwambia mdivorce huyu. Usingetoa ile mimba ya mheshimiwa ulivosikia anatoka, sahivi muheshimiwa amechukia sanaa. Nikatokea. Mama alipaliwa na chai nahisi aliuungua ulimi yule. Nilimshika Diana kumpa kipigo. Haiwezekani mi niko jela anajiachia na waheshimiwa mpaka kashika mimba. Nilimpigaa, nilikua namuua. Bahati akaja Liz akanimbia tukimbie, baba yake akija na mali yake jeshi la polisi hutoki jela wewe. Utafungwa bila hukumu.

Nikakimbia nyubani kwangu. Nikawa naishi kwa Liz. Hana kazi, sina kazi. Tunaenda kula kwa Ticha. Ticha ansikitika, Liz mapenzi yana ku cost. Nilikwambia huyu si mwanaumeee. Ona amekuharibia maishaa. Huku na huku baba Diane akaniletea polisi wakaniweka ndani. Liz na mama yake wakawa wananiletea chakula. Maza alichokaaa. Akasema baas, mtoto si riziki.

Aliniweka ndani wiki 3, akaja siku hio kuniambia ili nitoke ni sign talaka. Nikakubali. Nikaisoma kwamba mimi ndo mkosaji, na cheat, nimefungwa, mali iliobaki nyumba yangu wanachukua wanangu kwa usimamizi wa Diane.Nikasema No sweat, wananguwatakaa. Nika sign. Wakanitoa.

Tukiwa na Liz siku barabarani tunaenda kula kwa baba yake, nilishaanza kunywa tangia asubuhi virobaa. Ikasimama gari kali sanaa. Landcruiser Mkonga. Akashuka dereva mdingi mdingi akaniambia naomba tuongee. Nikaenda akaniambia unaitiwa kazi ingia kwenye gari. Nikamwambia Liz twende. Akakataliwa hakuna wanawake kazini. Nikasema kama haji mi siji. Wakasema poa aje.

Nimefika kwa junkie tu, wanamuita King of the night. Kipindi hiko mi niko hot huyu alikuwa underground. Inaonekana nilivokuwa ndani he rose the ranks now he was hot shots. Akanichangamkia Jay the king of all jacks. I am very sorry. Nimesikia watu wamekutenga, nikasema Jay kaka angu, alini ni treat vizuri back in the days, ill take him in. Najua fed are on you.

Mi sikupeleki on filed, utakuwa training manager kuwafunza vijana hawa tricks of the trade. Nikapiga magoti kumshukuru. King of the night mara akamuona Liz! Ujue huyu mwanamke mzuriii sanaa. Sema hana matunzooo. Kama nimemuelewaa. Akaambiwa huyo mwanamke wa Jay. Liz nae anadakia mi mwanamke wa Jay. King of the night akasema Jay kafilisika ndio ila ana mke wake kisu cha hatariii Diane, mtoto nilikuwa namtamani sanaa yule. Eti Jay huyu mwanamke wako? Nikamuangalia Liz, nae ananiangalia. Nikasema HAPANA. Machozi yakanza kumtoka. Nilijisikia zaidi ya Petro kumkana Yesu. Ni dada yangu. King of the night akasema basi kamando hivo Jay wewe shemaji yangu. Serious natafuta mke, ila wanawake wa mtaani hawaaminiki, dada yako namuamini si unajua kazi zetu hizi. Juma nenda nae mjini asafishwe aje navowatakaga mimi. Sasa ole wako aje haeleweki chukua pesa kwenye buti.

Kazi niliiona chungu, najipa moyo Liz is not my type. Ila moyo unaningonga hohohoooooo nyiz iz not my type, msengery wewe. Nilijikaza sanaaa. Sikumuona Liz mpaka baada ya wiki 2, nishaanza kazi. Alipendeza sanaa. Alivoniona aksema Jay mi sitakiii kukaa na King of the Night. Mwambie ukweli nije nikae na wewe. Nikamtisha ukimwambia ukweli yule anapenda uchi balaa hakawii kuniua ili akupate. we vumilia mi nausoma mchezo. Is he treating you bad? Hapana. Unateseka hapana? Basi vumilia kidogo tu Liz trust me. Akaniambia King of the night chumbani ana mahela kibaooo hata hajui bei gani ma $$$$. Nikapata wazo nikamwambia iba, next time ukija nipe. Akawa anaiba ananipa, anaiba ananipa. Zikafika $$$ 18,000

Bwana next time namuona na King of the night kavimba jicho, hana jino moja moja. Uso umevilia damu. Anatembea kapinda pinda kama katenguliwa kiuno. Inaonekana kichapo alichopewa sio cha nchi hii. Niliumi sanaa. Akawa ananiangalia jicho la huruma mnooo. Nikashindwa kuvumilia.

Nikamface King of the night, bwana huyu mwanamke wangu, maishaa tu mi ndo maana nimekupa, sitaki uadui na wewe, you are treating her badly, unampigaaa kama jibwa, utamuua. Nipe mwanamke wangu tondoke. Akaniambia nilikuwa najua toka mwanzo kwamba mwanamke wako ila namtaka hivo hivo. Na nachompiga ni wewe. unasababisha. Mi nampa maisha ya kimalkia, hatakii anakungangania wewe kwa nini? Yuko radhi azunguke na wewe vilabuniii ila sio aishi kimalkia kama wewe.

Kwanza nimekutafuta sababu huyu mwanamke toka mahakamani namuona, alikuwa mzuri kipindi hiko, nikakuona nae vilabuni, nikakuona nae ulivowekwa ndani na baba mkwe. Hii ndo type ya mwanamke nayoitaka. Nachompiga ni kujitia anakupenda sanaa. We ondoka ila huyu mwanamke anabakia.

Nikawa napata story Liz yuko kwa King of Night kama mtumwaaa. Mda mwingine analeta wanawake Liz anafukuzwa chumbani. Anafanya mambo kumkomoa kwanini hanisahau mimi. Nikajiapiza dogo huyu bora angemtesa mama yangu mzazi sio liz. Kiboga nitachomla hatonisahau. Naandika haya moyoni. Nilijaribu kufanya mishe nyingi za kwenda kumchomoa ikashindikana.

Mara ya mwisho kwenda nilipigwa sanaaa, sanaaa, Mpaka wakajua nimekufa wakenda kumita Mzee. Kupelekwa hospital bado nikawa nadai. Nilikaa hospital miezi mi 3 kama mtu alie gongwa na train. Nikaambiwa Liz haonekani tena kwa King of the Night. Nikawaza au kamuua na kumzika nini? Nilichanganyikiwa.

ITAENDELEA.
Aisee Diane sio mke mwema..ila liz nae si kwa mahaba hayo
 
Jay noma nimemwelewa ila huyu king of the night si mtu mzuri ata kiduchu
 
Father atakua alikua anashtuka hadi anaruka mana si kwa kitubio hicho cha kuchomoana moyo na makoromeo hahahaaa Lara mtundu sana mhenga mwenzangu
 
EPISODE 11

The Fool Husband.

If loving someone is foolish, then i proudly declare myself the biggest fool in this world. I love my wife, she is the my world, my everything. You can never understand power of love till you love someone the way i love my wife. Love is dangerous.

I am old school. Ukiwa old school utaelewa kwamba mwaume ndo kila kitu. Sio mambo ya kisasa mpaka mwanamke akupende. Mwanaume ukishampenda demu inatoshaaa. Hamna haja ya kupendana. Kwanza ukomavu wa mwanaume unapimiwa na his abilities za kumtongoza msichana asiemtaka mpaka akubali kumuoa. Kama mimi hivi ni kidumee.

Unaweza kuzungumzia wanawake juu ukachanganya wanawake wenye njaa, dhiki, wasio na option ambao ni shoka moja mbuyu chini haswaa ukiwa self made kama mimi. Mke wangu habari ingineee. Yule ni GENIUS. Kumvua chupi yule inabidi uwe equal or above her. Achana na hawa wanaomvua chupi ashazeeka, amebakia botox, na surgery mimi nimemvua chupi at her peak and prime time, 23 mpaka 30s manina na kumzalisha juu. Msinichukulie poa kabisaa wasomaji.

Navosema msinichukulie poa mnaweza kusema Simba mkali mbona anazaishwaa vile vile ila mkae mkijua hazalishwi na swala hata siku moja. It takes a lion to mate a lioness. Apart from the brains and IQ mke wangu amelelewa vibaya. Kukosa mama na kulelewa na baba, it made her think she is equal or equivalent to his dad. Damn. Anaweza hata kunituma maji.

Ligi hizi za kutumana niletee maji, tumezicheza sanaaa. Ila mimi namuduuu mbona. Kuna siku wakati tuna date namwambia niletee maji jikoni. Akajibu sileti? Nikamuuliza kwanini hukufunzwa huko kwenu? Akajibu nilifunzwa kwamba na wewe una miguu na unaweza kwenda kufata maji vile vile kwa miguu yako, huna mtumwa hapa. Nikasema hunijui. Nikakumbuka simu yake anachaji jikoni. Ikaingia sms. Akakurupuka fastaaa.

Kiukweli hio sms nilimtumia mimi, " Wife i love you! Ukiwa unarudi sebuleni usisahau maji niliokuagiza basi. Mwaaaaaa! Many Kisses" Hahaaaaaa. Akawa anarudi na maji kwenye glass. Nikajiona kidumee kweli. Kumsimamisha genius akanichukulie mma sio kazi ndogo, inataka ramani ya uhakika. Akaniletea. Nikajua kakubali kushindwa.

Kunywa kidogo nizimie, maji yamejaa chumvi. Niliinuka mwenyewe kwenda kusukutua na kunywa maji mengine. It is always a league of nations sio kufua, sio kupiga deki, sio kutandika kitanda. Mpaka leo hii kuna zamu ya kutandika kitanda. Mmmmmmhhh! Aibu naona mimi. Zamu yake anafanya vizuriii tu ila zamu yangu anaisimamia zaidi ya displini master wa sekondari. Hivo it is always about equality.

Sio hasara tu ndugu wasomaji kuna faida zake kubwaa. Kuna economic equality. Sibebi zigo peke yangu. Bajei ya mwezi inapigwa, inagawanywa pasu pasu hata kama 2,575,500 Mpaka hio 250 yake ataitoa na kujustify kwa nguvu zote na mimi nitoe yangu pasu pasu. Mnaweza kuhisi sababu she has more money than me, basi nafaidiii. Wapiii. Natimiza share yangu. Mda mwengine nawaza hii sio ndoa ni business partnership and i am just a part of equilibrium equation.

Mtu anaenufaika na she having more money than me, labda dogo. Ikja swala la mwanae she doesnt compromise at all. She gives him all the best and only the best. Ila mimi mpaka niji justfy sanaa, nijidefend, nitoe logic, hamna tofauti maisha yangu ya nyumbani na darasani.

I always wanted to marry her, apart from kumpenda, pia nilijua lazima nitaishi maisha mazuriii mnooo. I always loved me some goodlife. Mi nimesoma nje, nimeishi sanaa nje, naelewa value of good living. Kuishi nyumba nzuriii, kula vizurii, mwanangu asome shule nzurii, niende vacations. Nashukuru Mungu haya yote nayatimizaa kwa raha zangu. Na uhakika hata nikitangulia kesho mbele ya haki, mwanangu huku kitonga tu, mama yake jembe moja la hatari sanaa.

Mke wangu is okay in many aspects kabisaaa. Kama ilivo kizuri hakikosi kasoro, mke wangu ana addiction ya vijana wadogo. Sijui kwanini. First i thought maybe sababu nilikuwa nipo nipo tu anapagawisha na miili ya gym, nikapiga gym mwenyewe mpaka sahivi niko Hot. Nipita mahali watu wanajingonga, wanafunzi wangu wanalowa chupi sio kidogooo. ila wapiii.

Nilikuwa najua muhuni muhuni kabla sijamuoa nikajua nikimuoa akazaa utaisha wapiiii! Kama kapakwa pili pili. Nikahisi labda simfanyi vizuriii, ila hakuna nikipiga mechi za nje naachaga kasheshe la kunganganiwa. Ofcourse nilikubali iwe open marriage sababu nilijua mda anaweka hii policy alikuwa hot and demand, lengo langu nikisha mzalisha watoto wawili wa 3 na amend policy in my advantage na hatokuwa na pakutokea. Ingekuwa tu issue ya timing.

Mtoto kazaa mmoja tu, sina hili wala lile, katengeneza matiti, tena alienda USA kufanya hio procedure kwa pesa ndefu, sababu ni pesa zake sikujali sanaa. Nikamuuliza kwanini unatengeneza matiti wakati hatujamaliza kuzaa. Ungengoja kwanza watoto wafike wa 3 ndo utengeneze moja kwa zote. Akajibu nimetafakari nimeona nisizae tenaaa! Khaaaaaaaaa! Kwanini? Sina mwili wa uzazi kama Zari the boss lady. Mtoto mmoja tu mwili kama umepigwa tsunami. Nikizaa tena who knows unaweza usifae kurepea. Hapa nimetengeneza matiti, bado kufuta michirizi na laser, kukaza tumbo nivae bikini, it costs a fortune and i am not so sure i can keep affording this. Nikajua hayuko serious, kumbe ashafunga kizazi mda sanaa.

Niliumia sanaa, nikashitaki kwenye familia. Haikusaidia kitu cause baba mtu ana muunga mkono 200% Ndugu zangu walilalamika akasemakama naona watoto dili sana basi nizae na wanawake wengine hata niktaka 10 maadamu nijua nitawalea vipi. Mxiuuuuuu! Nilisikitisha sanaa ndugu msomajiii. Baadae nikajipa moyo mbona Clinton ana mtoto mmoja pia. Kitu gani bwanaaa.

Mke wangu sio mzuri wa asili, ila kwa kujitengeneza amekuwa kituuuuu. Kagoma kuzeeka kabisaaa. Kama ana miaka 20. Most of her money inaishia kununua uzuriii. Ngozi hio treatment yake kwa mwaka mara 3, anatumia technologia za juu sana, kama laser na mambo mengine appointment moja ina cost $ 50,000. Na kwa mwaka anafanya tatu. Bado zingine zingine. Bado wardrobe, acha vacations. Asione Angelina Jollie kaenda sehemu nzuri au Kim K. Kosaaaa. My wife is Hollywood type

Matokeo yake she earns a lot and spends a lot. Hatukui kiuchumii. Input is equal to output ndugu msomaji. Ila sababu pesa ni zake mwenyewe atajijua mwenyewe. As long as she spends what she earns, who cares. Plus the sex life is good. Hollywood style. Yaani ndugu msomaji i am living the dream of many men. What other men dream is my life. And i just love it.

Hili la wanaume wadogo wadogo halikuwepo kabla. Uhuni wake wa zamani ulikuwa anatembea labdana waziri hivi, au popular star na lazimaa unakuta kuna kitu anapata in return. Hata ukisema umbananishe kunakuwa na sort of logic.

But like to years ago, aliniambia mwenywe she is having an affair, kama prenuptial agreement ilivosema the relation is open. Niliumiaa sanaaa, sanaaa. Nikaenda kushtaki kwa baba Mkwe. Akaniwahi ulikubali mwenyewe, wakati wa makubaliano yenu sikuwepo usiji victimise. Nikamuuliza unaona fair kweli, jamniiii unaona fair navofanyiwa? Akasema kiukweli aibu naona mimi mzazi, ila toto lenyewe lile unadhani nitaliambia nini. Sahivi nimestaafu namtegemea yeye anilishe, anilipie pakuishi, anilipie vaccations naanza vipi kumuingilia na kumpinga kwenye mambo yake? Cha kufanya sana sana nitashauri tuu tena juu ila sitegemei mabadiliko. We kama una la kufanya fanya.

Niliwaza sanaa. Nikawaza sijui nipige chini, nikawaza maisha mabaya mabaya nayo sitakiiii. Nishazoea mshara wangu robo 3 nautumia navojisikia, kuanza mijukumu tenaaa sitakiii. After all she is such a nice person at heart basi tu malaya malaya. Ila kwenye ubinadamu ana ubinadamu sanaaa. Mama kaumwa kamtibia ujerumani. Mwenye mama na ndugu zangu tulisanda gharamaa. And she does love me, only sex ndo inatufarakanisha. This stupid sex. Aaaaarrrggggh.

Nikaa nae chini kidiplomasiaaa kumueleza how i am heart with her decision, as a man, she should reconsider. Yule zimwi nilijualo halinili nikaisha. Akaniuliza do you prefer i do it without consulting you? Namna hio hutojua na hutoumia. Namwambia i prefer you dont do it all. Muogope Mungu hii ndoa takatifuuu. Akanza ku logically justfy it. Baby its not some one serious, useme he is threat to our marriage, he is just a boy 23 yrs. Just sex nothing more. He looks good, i like him, he likes me, thats alls. It si going no where. Nikaendelea kupinga hilo swalaa kwa nguvu zote.

Alietembea na yule kijana. Nilijua cause ni mke wangu lazima nijue. Nilikasirika nikaondoka nyumbani kama mwezi badae nikaamua tu kurudi. Like she said it was just sex, it was going no where. Why was i so mad anyway. Nikarudi. She was glad i was back. Akakaa kama mwaka, ila majuzi nimejua kaanza tena. This time hakuniambia kabisaaa. Nilijumlisha na kutoa nikajua.

This time i have to fight back aisee. Siwezi kukaa kimya namtizamaa upuuzi wake. Na mimi naretaliate. Mwenyewe sio kwamba sishawishiki kuvibutua viwanafunzi ila sio asili yangu kuwatumia wanawake kwa maslahi yangu. Wanafunzi wangu nawaona kama wanangu. I treat them the way i want my daughter to be treated.

Nikawazaaa, nikaamua huyu kumkomeshaa natoka na mtu wake wa karibuuu sanaa. Ambae kitamuuma sanaa sanaa akijua na ataelewa inauma vipi na hatorudia. My first choice nilitaka kutoka na Sandra, cause kidogooo inalandana na wife, hollywood type, mambo makubwa makubwaaa, afu mzuriii ana jielewaa, na anaelwea what good life is. Nikamtongoza mashushu niliopata si ya dunia hii. Wewe sio type yangu kabisaa. Nikakata tamaa. Sikutakaa kumbembeleza sanaa mana lengo kumtumia kama chambo.

Nikiwa bado nachuja who next mara Alice mke wa mshikaji kaanza kunishobokea. Mara i was just saying hi! Huyu nae shoga wa damuu wa wife Ila sasa nafanya vipiii ndo swalii maana kikweli sio type angu kabisaa. Kafujika fujikaa. Kachokaaa. Hata watu wakisikia ni kuruka mkojo kwenda kutua kwenye nnya. Just looking at her for once i appreciated the procedures my wife took kujirudishia usichana. Alikuwa kaishaa sio kidogo.

Pamoja na kumpa F in figure, she was still cute usoniii. Ana kasura kazuriii zuriii. Na kilichompa maxi ni ucheshi wake. Maana nilianza kuchat nae kimasihara tu, then nikanogewa na sesne of humor ya kuchat nae, then i couldnt stop chatting with her. Na mimi simu zangu zilijaa password zoteee.

And it worked, akaanza kudataa, anataka kujua natoka na nani, natoka nani? Mara ahisi lazima atakuwa mwanafunzi wangu. Au ma x zangu. Mbona mgonjwa kaanza kupona kabla sijamuandikia hata prescription ya dose? Kwangu rahaaaaaa tupuuuu safari hii. Anahaha kama kuku anataka kutaga. Nikamwambia Its just a girl, its going no where, its just sex. Wapii moja haimkai mbili haisimamii. Niambie nani niambie nani? Nikamuuliza ukishamjua itasaidia nini? Moyoni nasema tulia hivo hivo nikunyoe vuzi falasi weeee.

Then i wanted to move things next level. Nikamualika gym kwengu. Mi na wife tunaenda gym tofauti. Akawa anakuja na mimi ndo trainer wake. Training her kidogo nighairi maana ndo nikaona mwili ulivozidi kuharibika. Bora uuone kwenye nguo. Nyonyo sasa for once nikaona every penny aliolipa wife Carina kwenye plastic surgery was worth it. Tena ningemjua surgeon ningeenda kumfuta jasho walau hata tudola 2000. Sio kwa kazi nzuri alionifanyia. Alice ana malapaaa, afu yamenywa sanaa hamna kilichobakia. I pitied her.

Katika story story nikamchomekea wife, yule Alice si shoga akoo yulee. Akasema sanaa. Vibaya mnoo. Nikamchomekea wewe na Sandra mmefanya boobs job, kwanini msimlipie na shoga yenu hata happy womens day au mothers day mka mtreat na yeye kwa procedure hata cheap cheap tu. Akastukaa! Told you she was genius. We maziwa ya mke wa mtu yanakuhusu nini? Na uligunduaje kama hayafai? Ofcoure hata mimi naliyaona mara ya kwanza nikasema Jesus ila wewe umejuajeee?

Nikamwambia wife na wewe, naangalia picha zenu huku Insta naona havai bikini, anajificha ficha, namna hio anaharibu pichaaa. I love looking at your pics. Akauliza hujaona tako la Sandra lilivokuwa kubwaaa? Mbona huja coment juu ya hilo? Au ndo unazugia namalapa ya Alice. Hahahaaaaa! Tukaishia kucheka tu. Ila hakustukia issue.

Sikutaka mwenyewe kumwambia Alice afanye procedure ingempa low esteem sanaa. Nikata itoke from her girls. Ikapita pita mda wife akiendelea na jitihada za kuhack password yangu, akasahau hata kuendelea kuchepuka akawa obssesed kunifatilia mimi Kubwa la Maadui, akaja kuniambia finally kakubali kurekebisha ile milapa . Ila bwana yule mwili shauharibuu watoto wa 3 genes zenyewe mbaya vileee, hio procedure tunatupa tu pesa, she wont be able to bounce back to a bikini body ever. Itasaidia kidogo. Kama mtumbo ulee sijuii. Cellulite imemlaa sanaa, stretch marks. Yule ashaharibu mwili. Basi tenaaa. Si tunamwambia aweke D cups, kitu kama hiki anangangania C cup. Atajua mwenyewe. Kujifuja fuja vile kisa mwanaume hakupendi mi siweziii.

Kweli hakuja gym mda, akaniambia anaenda Thailand kutibiwa. Sikumuuliza nini. Akaja kurudi kaweka hizo boobs. Ni kitu kidogo ila kikawa na matokeao chanya. Atleast. Basi anatamani hata apige gym uchiii, chezea kurudishiwa dodo saa 6 zako uzeeni. Basi ananizuga mazoezi siachi yamefanya nido zangu zimekaa poa sanaa. Like wife said it was too late for her, mwili usha haribika sanaa. Yale usipoziba ufa utajenga ukuta.

Nikataka kupiga chinii offcial nifanye issue zangu zingine, ila nikawaza wife namna hii ashaka kwenye mstariii. Nikijirudi yeye atatoka nje ya mstariii. Kwanza ukiacha matatizo ya mwonekano she sucha a nice person, and i enjoy her company. A lot. Ana upendo sanaa Alice. Maybe nimvumilie tu hivo hivo.

Unajua watu wazima sisi, nilivobonyeza tu imoooo. Kama kumsukuma mleviii. raha ya kuchepuka we uwe na mke, na yeye ana mume. Usiku kila mtu yuko recall. Asubuhi mnaanza kubebishana. Ila design yeye alianza ku fall sanaa sasa kwangu. Maana hapo nyuma aliniomba nimnunulie Morrano. Moyoni nikasema kwa Uchi gani labda? Labda Rav 4 tu itakutosha. Akisema wanae wana pata shida kwenye school bus hasa huyu mdogo analala wanampitisha.

Sikuwa na nia ya kumpa wala nini ila kama kawaida yetu wanumee nikamuahidi ili nimle mle basi. Then baadae nikaamua nisipompakabisaa sio vizuri, nimpe hata used third hand ya hapa hapa bongo. Nataka kuja kumpa kashakolea mapenzini anasema haina haja, nisihangaikeee ashazoea dala dala. Nikaamua kumpa anyways. After everything i started to like her a little bit na wanae nikawajua, anawaambia rafiki wa mama. Nikawaza hata mwanangu akioneshwa viserengeti anaambiwa hivo hivo rafiki wa mama. Potelea pote. Nikaingiwa imani nikaamua nimpe Harrier mpya kidogo direct from Japan. Ila nikamuuliza mumeo hatokusumbua? Akaniambia huyo niachie mimi.

Kweli akawa anaitembelea, sikuwahi kumuona mumewe anaiendesha ile gari hata siku moja. Gari kwa mtu kama Carina mke wangu is so nothing, achia Mereceds na Vogue anazonunua edition mbaya sanaa imepita 2 yrs. Ila kwa Alice gari ilikuwa kila kituu, alini consider kama baba yake mzaziii. Unajua mwanamke akishukuru sanaa, design anakuloga umpe zaidii na zaidiii. Mwenyewe tu kwa hiari yangu nikaamua kumfungulia bakery, sio bakery ya kitoto. Bakery ya kimataifa. Latest equipemnts na kila kitu. Niimpa kama mkopo auendeshe hio bakery anilipe kwa installments investment cost yangu asikae tu nyumbani. Na aliniambia she likes cooking nikaona itamfaa. Mbona ujana ulianza kumrudiaaa.

Huku kwangu kukawa stable kabisaa, kabisaa. Heshima imerudiii mpaka basi. Nikiomba maji naletewa. Zamu ya kutandika kitanda nikatolewa. Napikiwa, naulizwa unajisikia kula nini? I really wished Carrina angenifanyia haya mapemaaa kabla mambo hayajawa complicated kama hivi. Maana anafanya haya mi tayari moyo wangu usha gawanyika mafungu mafungu.

Ukitaka kujua akili za wanawake ni mbaya mwenzenu sina hili wala lile Alice asiniambie ana mimba yangu! Haaaaaaaaaaaaaaa! Tobaaaaaaaaaaaaaaaa! Nikamuuliza tu una uhakika mimba yangu sio ya mumeo? Akasema nauhakikaaa! Nilidata sanaaa! Kwanza kweli nataka mtoto mwingine leo jana kesho. Nafanyaje sasa wakati yule mke wa mtu. Afu mke wa mtu sumuuu. Niliumiza kichwa sanaa, nampataje yule mtoto bila kutibua kwa wife na kwa mume wa yulee. Yaani i wanted my cake and i wanted to eat it at the same time. Nilisitisha vipindi nikarudi nyumbani.

Kufika home nikakuta pregnancy test iko postive kama ilitaka kutupwa kwenye dude lake la pedi fasta fasta ila ikaanguka pembeni. Kama sikufa na pressure siku hii sifi tenaa. Nikaichukua na kuiweka kitandani. Niliwazaa mengi. Labda wife kumtia jamba jamba kamua kunizalia. Au yeye kama Alice mimba ya nje. Maana ndnai tunapiga show ukute na yeye nje tunapiga show. Whatever the case nafanyaje bado kwangu ni loose loose situation. Nikashinda chooni naharisha tu
 
Back
Top Bottom