Websites in Tanzania, watu wa ICT mko wapi?

Mhafidhina

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
549
22
Hivi karibuni nilikua najaribu kutafuta information mbalimbali kwenye websites za mawizara na taasisi mbalimbali za Tanzania.

Kwa kweli nilichokumbana nacho huko its saddening.

Kwa mfano, Website ya UDSM iko very outdated na haina any useful information kabisa, faculties hazina information yoyote, watu walioko huku nje ya Tanzania wanahangaika sana kupata taarifa za chuko kikuu chetu, yaani information ziko so flimsy and useless na nyingi links zake hazifunguki, Professa Mkandala hebu fanyia hili suala kazi...!

Wizara ya Sheria na Katiba, Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu, Law Reform Commission of Tanzania, Msajili wa Makampuni, Hizi zote hazina Website hadi leo hii, jamani tunaishi dunia gani?

Pia baadhi ya website chache zilizopo information zake ni dhaifu, hazina msaada wowote wala hata ukiandika email kuwasiliana na Webmaster haujibiwi lolote...!

Jamani, kwa mwendo huu hii globalisation tunaizungumza kwa maneno tuu au na vitendo pia...!

Naomba serikali iamke kulifanyia hili suala kazi, website za Wizara na taaasisi zake zifanyiwe updating na ziwe na information za kutosha kwa umma.
 
ndugu mhafidhina usemalo ni noja ya weakness kubwa nyumbani TZ. Kutokuwa na updated websites kunakosesha wateja, respect na mengi.

Yaani hiyo website ya UDSM ni kama kichekesho,its so static,hata kupata specific email ya lecturer ni shida, au kupata details muhimu za course ni shida. sijui tatizo ni nini, wataalamu au pesa au vyote?
 
ndugu mhafidhina usemalo ni noja ya weakness kubwa nyumbani TZ. Kutokuwa na updated websites kunakosesha wateja, respect na mengi.

Yaani hiyo website ya UDSM ni kama kichekesho,its so static,hata kupata specific email ya lecturer ni shida, au kupata details muhimu za course ni shida. sijui tatizo ni nini, wataalamu au pesa au vyote?

Tatizo ni uzubao tulionao Tz ndio maana jirani zetu Kenya wametuacha mbali sana, na wanatucheka na kutudharau! hebu fikiria kitu kidogo kama website ambayo mtu binafsi anaweza kuwa nayo, seems like a big deal kwa sehemu kama UDSM!!! Kweli tusipoamka usingizini, future ya Tz iko so empty mpaka inatia huruma. Sasa sehemu kama MLIMANI chuo ambacho kina zaidi ya miaka 40 lakini hakuna information yoyote ya kukuongoza hata kama unatafuta nafasi ya kusoma au kazi, its a big shame, we need to wake up in this DEEP & TERRIBLE sleep. Tumeshaachwa nyuma sana na sio rahisi ku-catch up na wenzetu ila tunaweza kujaribu kama tuna nia.
 
Nakubaliana na yote mliyoyasema hapo juu; Mimi naona tatizo ni Priority tu, hakuna mtu ambye anaona kuwa na tovuti ni kitu cha maana, kuna kitengo kizima cha IT pale na wanafundisha somo hilo sasa hata sijui kwa nini kwao si muhimu. Kama tungekuwa nayo nina imani kungekuwa na mabadiliko makubwa tu. Lakini ndio hivyo bado si muhimu kwetu.
 
Kweli inasikitisha sana, manake wanafanya mabo yanakua magumu sana haswa kwa mtu anayetafuta taarifa.

Lakini kikubwa ni hii tabia ya kuendekeza usiri na kuona kila taarifa ni siri na haipaswi kutolewa kwa wanachi. Kwa mfano, hio mikataba ya madini wanayoificha huko nyumbani, ukija huku nje ya nchi ni kitu ambacho kipo waaazi na unaweza ukakipata kwenye libraries mbalimbali za vyuo vikubwa.

Hili tatizo la kuwa wasiri na kukalia taarifa litatuumiza sana sana, Zaidi ya hayo bado kuna kuzubaa sana kwa watanzania ndio maana wenzetu wakenya na waganda wanaendelea kutupita kila kukicha...!

Rai yangu ni kwamba tafadhali tujitahidi kuboresha hizo websites za institution mbalimbali...!
 
..ni tatizo la utamaduni wetu wa kulipua kazi.

..hizo websites zinahitajika kuwekwa kila vital infor. for the public. sasa, labda hii hali yetu ya kuwa wachoyo wa infor. ina-play part pia. lakini, lazima uwalipe watu ku-update kila mara.

..udsm inatia aibu, ukizingatia kwamba wao ndio walitakiwa kuwa center of excellence kwenye issues hizo kwa tanzania.
 
Jamani, mi bado nalia na websites za Serikali na Institutions zake...!
Hivi mmeshawahi kupita kwenye website ya wizara kama ya mambo ya nje au wizara ya utalii....?

Hivi kwa hali hii Mzungu akitaka kuja Tanzania atapatawapi taarifa za uhakika za serikali? Website ya BoT je mmeshawahi kuiangalia? Zaidi ya kutoa exchange rates mbona sioni kitu cha muhimu pale?

Can u imagine taasisi muhimu kama PCCB mpaka leo hainawebsite? Hivi hawa watau wanaficha siri gani? Jamani kuna haja ya kuamka, hii tabia ya kutotoa taarifa kwa umma hata kupitia website is embarassing, sasa watu watapataje taarifa kama hazitolewi?

Jamani naombeni support yenu tupige kelele mpaka walau hao watu huko maofisini wakumbuke kutengeneza na kuziupdate hizo websites....!
 
Jamani, mi mwaka huu nimeamua kutoa nguvu na jitihadaa zangu kupiga debe hadi hizi website za mawizara na Taasisi za Seriakali ya Tanzania ziboreshwe...! Jamani hebu angalieni kwa macho yenu wenyewe website ya Wizara yetu nyeti ya Nishati na Madini....!

http://www.mem.go.tz/about_us/about_moem.php

Angalieni ilivyo shallow, sasa hapo kwa mtu aliye nje ya nchi anaweza kupata taarifa gani ya maana? Yaani inasikitisha sana...!

Jamani noambeni hawa wanaohusika na hizi website za serikali wajaribu kuziboresha hizi website...!
 
Hiyo website ya ministry of energy and minerals inachekesha. Nimejaribu ku-search "tanzanite", "diamonds", "gold", hata "tanesco" results zero. Nothing in the entire website inaongelea mambo hayo. What a waste of time. Hawa wanaona fashion kuwa na website lakini hawako makini na hawako serious kwamba waweke nini. Sidhani kama wanakaa na kujadili haya mambo.
 
Jamani natafuta website ya Jeshi la polisi...! Hivi kuna mtu anaifahamu?
 
website ya wizara ya Viwanda na Biashara inatia kichefuchefu....! Hivi hawa hawana webmaster au?
 
Kweli tutaendelea kuwa wasindikizaji hiyo website ya UDSM imechoka utafikiri ya mwaka 60
Hapo UDSM kuna wanafunzi wanasoma Computer Science na IT kwa nini wasipewe deal ya kudesign website mpya ?
 
Mfano mzuri wa ubovu wa tovuti zilizosukwa na Wataalam wa Kitanzania ni hii hapa ambayo nimekuta kibahati leo:

http://www.ewura.com/news.html

Angalia jinsi database password na User ID vilivyo nje nje! Huyu anaonekana ni programmer amateur tu, lakini utakuta kalipwa milioni 20 au zaidi kutengeneza mdubwasha hovyo kama huu!
 
Mhafidhina,

Unadhani wataalam wa ICT hatupo? Mbona tupo?

Wanaopata hizo tenda ni wale wenye uwezo wa kutembeza brown envelopes.

Mie sina uwezo huo kaka. So, nitapewa na NANI?

./Mwana wa Haki

P.S. Usidhani mahala kama UDSM hakuna grand corruption. IPO! Ndio maana unaona hizo websites zao zimekaa kiholela.

Kaangalie za Open University pia, ambazo zilitolewa tenda, na watu wamekwenda na hela yao! Mis simo!
 
Udsm wana webmaster wao na watu wao wengine walioajiriwa kwa ajili ya kazi hizo kwahiyo tusikimbilie kusema watu wamepewa tenda huo ni uzushi na ni kudhalilisha taasisi kama udsm .

Pia kila makala kuna utaratibu wake wa kufanya kazi na ratiba za kazi kwahiyo tusilazimishe kufanyike vitu ambavyo haviko katika mikataba na mikakati ya kikazi
 
Udsm wana webmaster wao na watu wao wengine walioajiriwa kwa ajili ya kazi hizo kwahiyo tusikimbilie kusema watu wamepewa tenda huo ni uzushi na ni kudhalilisha taasisi kama udsm .

Pia kila makala kuna utaratibu wake wa kufanya kazi na ratiba za kazi kwahiyo tusilazimishe kufanyike vitu ambavyo haviko katika mikataba na mikakati ya kikazi
Hakuna website inayonikera kama hiyo ya Udsm......ukienda pale computing center unakutana na walimu wake wamening'niza flash disc kifuani na mavitabu yao makubwaaa kama vile wanafanya mambo.....

taasisi kama ile haitakiwi kuwa na site mbaya na mfu kama ile.....imagine kama kuna mtu yuko abroad anataka kusoma udsm atapataje information? nimesahau site moja ya shule ya msingi inaeleweka kuliko ile ya udsm
 
hakuna website inayonikera kama hiyo ya udsm......ukienda pale computing center unakutana na walimu wake wamening'niza flash disc kifuani na mavitabu yao makubwaaa kama vile wanafanya mambo.....

Taasisi kama ile haitakiwi kuwa na site mbaya na mfu kama ile.....imagine kama kuna mtu yuko abroad anataka kusoma udsm atapataje information? Nimesahau site moja ya shule ya msingi inaeleweka kuliko ile ya udsm

yoyo wanafunzi wa udsm wanaweza kusoma na tovuti hiyo hiyo katika elimu yao ya mtandao na hakuna tatizo lolote , sasa ungekuwa mwanafunzi pale kwa sasa ungeuliza zalongwa wamefanya nini katika kuunganisha tovuti hiyo na shuguli zingine za wanafunzi na walimu tunapoangalia tovuti tunaangalia mambo mengi haswa utendaji na ulinzi sio mauwa tu au picha za vikatuni kama wewe unavyotaka iwe , nafikiri ungefurahi sana ungeona picha ya mbowe amevaa gwanda za mgambo si ndio ??

Kuhusu wanafunzi wa nje kuna link za admini na link zingine za contacts mtu anaweza kuwasiliana moja kwa moja yoyo wacha kupotosha uma wa watanzania

halafu pia ujue ucc na udsm ni vitu tofauti ucc ni taasisi inayojitegemea ina wafanyakazi wake na ina mipango yake ya kazi

habari ndio hiyo
 
Leo nimepitia pitia website za kule nyumbani, Walau Website y TANROADS inajitahidi, lakini website ya Wizara ya Miundombinu na ya BoT zinatia kinyaa....! Hazina Ubunifu wowote wala taarifa za kumsaidia mtu...!
 
Back
Top Bottom