Websites in Tanzania, watu wa ICT mko wapi?

sasa ungekuwa mwanafunzi pale kwa sasa ungeuliza zalongwa wamefanya nini katika kuunganisha tovuti hiyo na shuguli zingine za wanafunzi na walimu tunapoangalia tovuti tunaangalia mambo mengi haswa utendaji na ulinzi sio mauwa tu au picha za vikatuni kama wewe unavyotaka iwe , nafikiri ungefurahi sana ungeona picha ya mbowe amevaa gwanda za mgambo si ndio ??

halafu pia ujue ucc na udsm ni vitu tofauti ucc ni taasisi inayojitegemea ina wafanyakazi wake na ina mipango yake ya kazi

habari ndio hiyo

Just kuongezea tu kama msisitizo kuwa watu wa ict tanzania wapo, zalongwa software imekuwa miongozi mwa Top ICT Youth Innovation in Africa for 2008. Hii imetangazwa mjini Johannesburg wakati wa maadhimisho ya African ICT Achievers Awards for 2008.

hata hivyo wakati zalongwa software imekubalika kuwa is a serious innovation, pale udsm sijui wana mkakati gani kuiendeleza software hii ili iendelee kusaidia vyuo vingine. maana chimbuko lake ni udsm
 
Nijuavyo ni kuwa UDSM kuna watu wa IT wenye uwezo wa kurekebisha muonekano wa tovuti yao, tatizo ni mazoea na priority.

Mazoea kwa maana kwamba nimewahi kushuhudia e-debate kati ya wanataaluma wakipinga kubadili tovuti ya UDSM kwa kigezo kwamba wameizoea na hawaoni umuhimu wa kuibadilisha. Mwisho wa debati ikaonekana hakuna haja ya kubadili na wale waliokuwa wamependekeza wakaambiwa kuna sehemu nyingi zinahitaji huduma yao kuziboresha na si tovuti hiyo pekee.

Kuhusu Priority nachelea kusema kwamba wanajumuiya hao hawaoni kama tovuti ni suala la kulipa kipaumbele kama masuala mengine ya upatikanaji wa vitendea kazi vya kufundishia na kusomea. Kumbuka, tangu limekuja suala la kuchangia gharama, Serikali kuu imepunguza sana mgawo wa fedha kwa UDSM kiasi kwamba wakati mwingine chuo kinashindwa kutimiza hata mahitaji muhimu kabisa kwa walimu na wafanyakazi wengine.

Labda tujadiliri namna ya kumaliza matatizo ya kifenda kwa chuo hiki kikongwe kabla ya kuangalia issue ya tovuti. Walimu pale wana matatizo kama vifaa vya kufundishia, vyumba vya madarasa vyenye ukubwa ambao hauendani na wingi wa wanafunzi, vitabu vya kiada na ziada, vyumba vya ofisi za walimu, na mengine mengi. Tukimaliza hili ndio tunaweza kuangalia hili la tovuti!!
 
Mara nyingi tunafanya makosa ya kiufundi tunapo husisha matatizo ya content za websites na wataalamu wa IT. Ni makosa kama haya ndo husababisha katika Taasisi nyingi website kuwekwa chini ya vitengo vya IT.

Website ina sehemu kuu mbili Content na Technology. Wataalam wa IT hawajasoma kudevelop contents, bali wanasoma technolojia za kupresent contents kwenye browser yako. Kama kuna tatizo la muonekano au mpangilio wa contents kwenye website hapo shutuma ziende moja kwa moja kwa watu wa IT. Lakini kama maelezo kwenye website hayajitoshelezi basi hilo siyo tatizo la watu wa IT.

Owners wa website kwenye organization ni watu wanaohusika na Public relationships, publicity, ambao mara nyingi ndo wasemaji wa Taasisi. Kitu ambacho wengi hawajui kuwa website ni tool moja wapo ya kuwasaidia hawa jamaa kufikisha ujumbe wao kwa jamii na dunia kwa ujumla. Sasa hawa ma public relationship officers wetu ndo wanatakiwa walaumiwe. Wengi wao hawajui majukumu yao katika swala la website. Kazi yao ni kuhakikisha contents zilizopo kwenye website zinajitosheleza na ziko up to date. Wizara na taasisi zote za umma zina watu hawa wa mawasiliano/information, kazi yao mara nyingi ni kuongea na vyombo vya habari tu.

Pia kitu kingine ambacho kinakosekana ni ni kutokuwa na malengo mahususi ya kuanzisha tovuti. wengi wanafanya kama mkumbo tu, bila kujiwekea malengo mahususi ya website yao na kuandaa website policies ambazo zitatoa responsibility kwa wahusika katika kuhakikisha malengo ya website yanafikiwa.
 
Jamani hebu angalieni kwa macho yenu wenyewe website ya Wizara yetu nyeti ya Nishati na Madini....!

MEM - About the Ministry - Energy and Mineral Sectors in Tanzania

Angalieni ilivyo shallow, sasa hapo kwa mtu aliye nje ya nchi anaweza kupata taarifa gani ya maana? Yaani inasikitisha sana...!

Jamani noambeni hawa wanaohusika na hizi website za serikali wajaribu kuziboresha hizi website...!
Dongo hilo hapo juu lilikuwa la tarehe 4 Sept.

Ukiitembelea mem.go.tz utakutana na ujumbe huu:

mem.go.tz

This site is temporarily unavailable as from 27th November, 2008.

Please contact the undersigned for assistance.
amujuni@uccmail.co.tz, 0784 717 342 or 022 2410645.
 
Back
Top Bottom