Wana JF, kwa kuwa wenzenu tuko huku Bongo, pengine tunafahamu mambo mengi ya huku kuliko ninyi huko. Taratibu za kuteua, kuapisha mabalozi wateule zinakuwa kama ifuatavyo.
1.Balozi mtarajiwa mteule huwa kwanza anachunguzwa kuanzia tabia,uhusiano,mwenendo,utendaji kazi wake,security issues,maswala ya familia yake, yaani historia yake yote ya maisha kwa ujumla.
2.Baada ya wahusika kuridhika kuwa mtu huyo yuko safi na ana uwezo wa kuwakilisha Taifa, Mtarajiwa Balozi mteule anaulizwa kama jina lake likipendekezwa kwa Mhe. Rais atakubali? au la
3.Akikubali, ndio jina linapelekwa kwa Mhe. Rais kwa idhini yake na kupangiwa Kituo.
4.Baada ya kupangiwa Kituo, taarifa zinapelekwa kule nchi ambayo anatarajiwa kwenda kuliwakilisha Taifa kwa ajili ya nchi hiyo kumkubali au kumkataa. Wakimkataa, huwa hawatoi sababu yoyote wanasema tu mtu huyo hatufai basi. Wakimkubali, taarifa inarudi kusema wamemkubali mteule huyo. Sasa, mlolongo huo wa kutuma jina na kusubiri majibu huwa unachukuwa muda mrefu sana maana huwezi kuwaharakisha watendaji wa nchi nyingine maana na wao huwa wanafanya uchunguzi wao kuhusu huyo mteule. Ndio maana utasikia mtu kapendekezwa kuwa Balozi wa nchi fulani, lakini inachukuwa muda mrefu kuapishwa.
5.Baada ya jina kukubaliwa na nchi anayotarajiwa kwenda huyo Balozi, ndio Mhe.Rais anamuapisha Balozi mteule.
6.Baada ya Balozi mteule kuapishwa, anaenda na mwenza wake Chuo cha Diplomasia kupata mafunzo ya Udiplomasia, na wakihitimu, wanapewa vyeti na kusubiri mpaka wapate taarifa kuwa Balozi aliyekuwa hiyo nchi anayotarajia kwenda ameshaondoka, maana nchi haiwezi kuwa na Mabalozi wawili kwa wakati mmoja.
7.Baada ya kuwa Balozi wa zamani ameshaondoka huko anakotarajiwa kwenda, sasa ndio anakwenda rasmi huko alikopangiwa. HUO NDIO UTARATIBU WA MAMBO YALIVYO. ...Darasa hilo.
Kama kuna maswali uliza!