Web Designers needed!

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu habari zenu?

Tunahitaji web designers 10 walio ndani na nje ya Tanzania. Unaweza kuwa mtanzania ama si mtanzania, haijalishi!

Ili ku-qualify ni vema ukatutumia yafuatayo:

1. Website(s) ulizowahi kutengeneza au unazotengeneza na uzoefu wako katika soko hili

2. Unaposhindwa katika designs zako (be frank) ili itusaidie kujua tutashirikiana nawe vipi kusuluhisha tatizo lenyewe. Siamini kama kuna mtu anaweza kujigamba anajua kila kitu!

Tunahitaji mawili hayo juu kwani kwangu ndiyo muhimu.

Kutakuwa na mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi pamoja na kila kazi italipwa kulingana na ugumu wake na kwa maelewano baina yetu.

Tumepata kazi kadhaa na tusingependa kula peke yetu, tunapenda kuwashirikisha na tunaamini kwa pamoja tunaweza!

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa kupitia:
Code:
info@jamiimedia.com
 
Thanks invisible sasa hii kazi lazima ianze imediately au hata baada ya mwezi hivi.
 
Thanks invisible sasa hii kazi lazima ianze imediately au hata baada ya mwezi hivi.
Tunachohitaji ni kuwa na makubaliano na crew ya watu 10 hivi.

Halafu, tunahitaji Server Administrators wanne. Watapangwa in levels. Ngoja niangalie possibility ya kutuma matangazo ya nafasi za kazi via local papers Tanzania ili kuwathibitishia tuko serious. Nilitaka kuwashirikisha hapahapa ili tunapo-deal na mtu awe ni mtu anayeifahamu JF na anafahamu 'Tumedhamiria'!

Kwa wale wanao-deal na System Security pia wanaweza kutuma maelezo yao. Unaweza kufanya kazi ukiwa kazini kwako (kama mazingira yanaruhusu) au hata ukiwa nyumbani kwako. Muhimu ni kuwa tutapangiana majukumu na earnings zitakuwa wazi kwa kila mmoja.

Ahsante Kinyau
 
Kuna jamaa hapA Haidery Plaza wanajishughulisha na mambo hayo unayoyahitaji.......mpigie jamaa mmoja, Mkurugenzi anaitwa Octavian, namba yake ni 0713 817081
 
sasa edwinito inv ndio ampigie au yeye ndio apige, si umpelekee tangazo kama ana haja ya web design atapiga
 
nipo ktk mstari mmoja hapo
ngoja nikafungue sanduku langu nikaangalie vyeti nilisomea nini maana kama ujuavyo naweza nikawa nimesomea udaktari ila kazi nikapangiwa uhakimu (bongo kiboko)
Mkuu invisible nimehamasika
 
Kuna jamaa hapA Haidery Plaza wanajishughulisha na mambo hayo unayoyahitaji.......mpigie jamaa mmoja, Mkurugenzi anaitwa Octavian, namba yake ni 0713 817081
Dah,

Watu wananipa namba za makampuni etc, ninachoangalia sanasana si CV ya kampuni...

  • Kazi walizokwishafanya
  • Kitu gani hawawezi... (Mtu asiyesema hawezi nini nitakosa imani naye mapema tu!)
Simply vitu viwili hivyo. Nimefurahi kuna wawili wameonesha wapi hawawezi na kote huko wasikoweza nakuwezea haswaa, nina uhakika watafaa kwa nyanja wanazoweza kiasi design ikifikia hatua ambapo tunahitaji input toka kwangu nitaiweka.

Hapa target yangu ni kuhakikisha tunafanya kazi as a team... Design period ikiisha, hosting tunafanya sisi na webmaster anakuwa partner ambaye tumeshirikiana naye katika design maana ndiye anajua kila kitu katika website husika.

Nimefurahi JF kuna vichwa wakali, websites kadhaa nilizopewa wamefanya kazi nzuri sana.

Kudos wakuu... United we stand!
 
Namimi naomba kazi kama mshauri maana kwa sasa sina website ya kuonesha!
 
Nadhani kwa sasa hamhitaji tena webdesigners sivyo. Mwaweza kutumia template manager ziko aina kwa aina.
 
Mkuu Invisible, unajua TZ ukitangaza kwenye gazeti siku hizi watu wanacheka tu?Siyo kwamba ndio umeonyesha seriousness,maana kwa kawaida hizo kazi zinakuwa tayari kishapewa mtu hapo inakuwa kujiosha?Umefanya vizuri kuangalia CV za mtu na sio za kampuni.Umemsoma SteveD?Maana tuko wengi tungetamani lakini hatuna website za kuonyesha inakuwaje hapo?
Kt
 
kudadadeki siku hizi wabongo tunapenda kamisheni hata kwa kumuongoza njia kipofu aliyepotea.
 
Dah,

  • Kazi walizokwishafanya
  • Kitu gani hawawezi... (Mtu asiyesema hawezi nini nitakosa imani naye mapema tu!)

Mimi sina website nyingi practical nilizotengeneza ziko kama 4 hivi with no complicated features kama db connectivity with the webpage, verification and validation, infomation capturing etc, as you IT Tz imekamatwa na wahindi. Ila ili kugain experience naweza ni play part as a silent team member to assist you on fef tasks as a volunteer for 6 months and then we will evaluate my contribution on the team. I have a knowledge of advance html, php, asp and mysql db, I have started working with pearl on linux I haven't master it yet. I am eager to learn. Count me in if you think I can add something to your team.
 
Wakuu habari zenu?

Tunahitaji web designers 10 walio ndani na nje ya Tanzania. Unaweza kuwa mtanzania ama si mtanzania, haijalishi!

Ili ku-qualify ni vema ukatutumia yafuatayo:

1. Website(s) ulizowahi kutengeneza au unazotengeneza na uzoefu wako katika soko hili

2. Unaposhindwa katika designs zako (be frank) ili itusaidie kujua tutashirikiana nawe vipi kusuluhisha tatizo lenyewe. Siamini kama kuna mtu anaweza kujigamba anajua kila kitu!

Tunahitaji mawili hayo juu kwani kwangu ndiyo muhimu.

Kutakuwa na mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi pamoja na kila kazi italipwa kulingana na ugumu wake na kwa maelewano baina yetu.

Tumepata kazi kadhaa na tusingependa kula peke yetu, tunapenda kuwashirikisha na tunaamini kwa pamoja tunaweza!

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa kupitia:
Code:
info@jamiimedia.com

Invisible:

Naomba hiyo kazi, my expertise yapo kwenye 2-tiers, 3-tiers web architecture.
 
Invisible,

I will PM you for about the position and thank you for sharing the opportunity.

As you said, as a team we can do more accomplish more than depending on one person.
 
Back
Top Bottom