Wazo la kuzalisha umeme kimkoa (kampuni binafsi) unalionaje?

Labda Tanesco ijitokea kabisa kwenye kuzalisha ibakie kama jina lake linavyosema "Tanzanie electricity "supply" corporation" Wabakie kwenye ugavi. Yaani, wazalishaji wakodishe njia za tanesco kusambaza umeme; badala ya tanesco kuwalipa kununua umeme, tanesco ilipwe kusambaza umeme unaozalishwa na hao IPPs.. Hapo mtaona watakavyokimbia watu!
 
Inahitajika TANESCO ivunjwe vipande vitatu. Kuwe na (1) Kampuni inayojihusisha usambazaji (transmission) na hii inahitajika kwa kiwango kikubwa iwe chini ya serikali for stategic reasons, (2) kuwe na makampuni mbalimbali ya kibinafsi na serikali kwa ajili ya kuzalisha umeme (power generation/production) ambo utasambazwa na kampuni namba moja; na (3) Kuwe na kampuni nyingi zitakazopatikana kwa mfumo wa tendering kwa ajili ya usambazaji (distribution) wa umeme za kikanda, kazi kubwa ya kampuni hizi itakuwa ni sales and marketing of the product produced by in companies in (2) and transmitted by (1). The companies in (3) are the one that will be dealing directly with consumers (connecting new customers and sales in general). For this proposal to work does not need rocket mathematics, just a political will.
 
Kampuni za watu binafsi zitauza kwa serikali ya mkoa au mkoa utatakiwa kuanzisha vyanzo vyake vya umeme halafu waiuzie TANESCO? Kama jibu la pili ndilo, pesa zitakazopatikana mkoani kwa kuizuia TANESCO zitabaki mkoani au zitaenda Hazina halafu mkoa uziombe tena? Maana mikoa yetu haina mamlaka kamili.... lakini itahitaji tena pesa za kuendeshea/kuzalishia vyanzo hivyo...
 
Sasa yule anayeuza kwa mkoa tujue si kwamba anachimba hydropower station.. au kuanzisha kituo cha umeme wa nyuklia yeye ataleta majenereta tu makubwa - yale ya Industrial halafu ndio anafunga na kuanza kuuza umeme.

Nafikiri cha msingi ni kuweka kanuni za aina ya umeme unaoruhusika kuuzwa kwa grid ya taifa na za kusimamia bei za ununuzi wa umeme.

Kiuhalisia katika nchi zinazojua kuweka kanuni na kuzifata, hakuna kampuni inayotaka kuzalisha umeme kwa jenereta na kuuza kwa sababu umeme unaozalishwa kwa mafuta ni ghali mno per unit kulinganisha na umeme wa vyanzo vyengine kama makaa ya mawe au nguvu za maji.
 
Sio kwamba hili swala Halipo.......TPC pale Moshi walikuwa wateja wa TANESCO na walikuwa wanalipa monthly 400M then wakaanza kuzalisha umeme wao under TANESCO infrastructure, walianza na 10MW then 15MW na mpaka mimi natoka Moshi tayari walikuwa na 15MW ila target yao ilikua ni 30MW sijui kwa sasa wameshafikisha au la.....Ilipofika kipindi cha Mgao wa mwaka 2008/2009 wao wakasema waanze kuiuzia Tanesco Umeme koz Load yao ni 8MW so wataweza kuinject 7MW kwenye grid lakini ukiritimba uliojitokeza hapo hauelezeki wala hauandikiki.

Yapo makampuni ambayo yanaweza kuzalisha umeme tatizo lanakuja katika utaratibu wa mauziano ambao Serikali kupitia Tanesco umejiwekea ambao ni kandamizi kwa Umeme Endelevu. TANESCO yenyewe kama ingeweza kujitenga kuwa na makampuni matatu yanayojitegemea ingekuwa na ufanisi mkubwa katika usimamizi hapa namaanisha GENERATION, TRANSMISSION and DISTRIBUTION yafanye kazi independently then tungeweza kuona mafanikio wala hakutakua na kutupiana mipira pale zinapotokea faults kubwa.

Ni wazo zuri kuanzisha Power generations Kimkoa lakini viwepo vyanzo yakinifu na Stable ambavyo vinaweza tengenezewa a Ring Network na Mkoa usitegemee source moja ili kuepuka Black outs pale chanzo kinapopata Hitilafu.....
 
Labda Tanesco ijitokea kabisa kwenye kuzalisha ibakie kama jina lake linavyosema "Tanzanie electricity "supply" corporation" Wabakie kwenye ugavi. Yaani, wazalishaji wakodishe njia za tanesco kusambaza umeme; badala ya tanesco kuwalipa kununua umeme, tanesco ilipwe kusambaza umeme unaozalishwa na hao IPPs.. Hapo mtaona watakavyokimbia watu!

sasa hapa MM bado hujaelezea vile vyanzo ambavyo kwa sasa vipo chini ya Tanesco vitakuwa chini ya nani??? au navyo wavikodishe???? koz hapa tunazungumzia Hydro Power plants zote za TANESCO na 100MW Gas PP ya Ubungo......Mi nadhani kama Tanesco inaweza Kugawanywa kuwa makampuni matatu tofauti.....ili kila anaweza anaweza akajiingiza katika aina 3 ya makapuni hayo (GENERATION, TRANSMISSION and DISTRIBUTION) though kwa jinsi nijuavyo Transmission itabidi ibaki kuwa hii iliyopo japo inatakiwa kufanyiwa Upgrades kutoka 220KV to 400kV. Ila kama huu mradi wa kutoka Mtwara mpaka Singida utakamilika then atleast utaboost upatikanaji wa Nishati hii ambayo kwa sasa naweza iita Nishati "adimu"
 
Kanuni za kitaalam za uzalishaji wa umeme zinaonesha kuwa kadri mtambo unapokuwa mkubwa na kuzalisha umeme mwingi zaidi ndivyo na ufanisi wake unavyoongezeka. Kwa hiyo, mtambo wa kuzalisha Megawatt 200 unaweza kuendeshwa kwa ufanisi zaidi kuliko mtambo wa Megawatt 100 na kuendelea. Kanuni hiyo ni kanuni muhimu sana katika uendeshaji wa mitambo ya kuzalisha umeme.

Matatizo yanayotufanya tushindwe kuendesha Tanesco hayana uhusiano na kanuni za uzalishaji wa umeme. Tunashindwa kwa sababu somewhere inaonekana hatuna uwezo kabisa wa kuendesha vitu vikubwa. Kwa hiyo tunafikiri kuwa dawa ya kutibu Tanesco ni kuwa na mashirika madogo madogo ya kimkoa ambayo tunaamini yataendeshwa kwa ufanisi zaidi kwa sababu ya udogo wake!! Hili si la kweli hata kidogo. Mashirika haya madogo madogo ya kimkoa yatahamishia gharama kubwa za kuzalisha umeme kidogo kidogo (ufanisi ni kidogo kwa uzalishaji mdogo mdogo) kwa walaji na matokeo yake yanaweza kuwa mabaya zaidi.

Jambo zuri hapa linalozungumzwa ni kwa makampuni binafsi. Tunajua matatizo yetu yameanza kuwa makubwa zaidi toka tulipoanza kuingiza hicho tunachoita makampuni binafsi. Ni nani anaweza kuthibitisha kuwa ikiwa tumeshindwa kuingia mikataba ya maana na wazalishaji wakubwa wa kitaifa (ambao huzalisha umeme mwingi kwa ufanisi zaidi) tutaweza kuingia mikataba mizuri na wazalishaji wadogo wadogo wa kimkoa ambao watazalisha umeme kwa gharama kubwa?

Hapa itakuwa ni Mbuni kujificha kwa kuzika kichwa kwenye mchanga. Tatizo letu la msingi la kuendesha uongozi kwa kufuata kanuni za kiuchumi litaendelea kututafuna. Ukiongezea na ufanisi mdogo wa kuzalisha umeme kwa viwango vidogo vidogo tutarajie bei ya unit moja ya umeme kufikia Shilingi 500 hadi 1,000; ambayo manake ni kuwa umeme utakuwa ni anasa ya watu wachache tu. Kitu kingine tutarajie miji mikubwa yenye viwanda vingi kupata umeme wa bei nafuu na miji midogo isiyo na viwanda kukosa kabisa umeme.

Kusema kuwa kuwa na makampuni madogo madogo ya kimikoa kutatatua tatizo la umeme ni sawa na kusema serikali za mitaa huko mawilayani zina ufanisi kuliko serikali kuu. Tunajua mfumo wetu wa utendaji, unazuia walioko huko low level kufanya kazi zao bila kuingiliwa na wale walioko high level. Tunajaribu kusema kuwa haya makampuni yataingia mikataba na mikoa, mikoa ipi? Watendaji wa serikalini mikoani huko wote ni watu wa kuteuliwa na serikali kuu. Ni watu ambao wapo kwa sababu wamewekwa pale na waliowaweka, si watu wa kuwajibika kwa wananchi. Sasa utaniambia kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kwa mfano ataingia mkataba wa kuzalisha umeme kwa ajili ya mkoa wa kilimanjaro? ..... Halafu tutarajie huu ufisadi tunaouona kwenye level ya kitaifa kule mkoani usiwepo???? We are lost!

Tuna tatizo kubwa la kimfumo, mfumo ambao unaifanya serikali kuu kuingilia kila mahali kwa mkono wa nyuma (kupitia uteuzi wa watendaji). Uteuzi wa watendaji tumeona mara nyingi ndo imekuwa donda ndugu kwani wangi huteuliwa kwa kufuata patronage na si uwezo na record ya utendaji uliotukuka. Wenye record za utendaji wengi wameishia kwenye middle level management na mara nyingi mawazo yao huishia kwenye trash. Ni lazima tufumue kabisa huu mfumo wa kijamaa ambao haufanyi kazi (dysfunctional), tuweke mfumo ambao unawawezesha watu kufanya kazi na kuwajibishwa kwa kazi zao. Vinginevyo tunarudi kule kule kwenye mfumo wa mashirika ya umma. Ingawa tunasema wazalishaji watakuwa binafsi, serikali ile ile itaingia mikataba na wazalishaji hao. Serikali ile ile iliyoshindwa kufanya mikataba na wazalishaji wakubwa, itaingia mikataba na wazalishaji wadogo, halafu tutarajie matokeo tofauti!!
 
Nasikia kuna magenius wetu wengine wamekuja na suluhisho jipya la tatizo la nishati ya umeme nchini; kuruhusu makampuni binafsi kuzalisha umeme kwenye mkoa na kuuzia Tanesco. Kisingizio kikubwa kinachotolewa ni kuwa kitaifa suala la kampuni binafsi kuzalisha umeme limekuwa vurugu na gumu kutekelezeka kwa hiyo wameonelea ni bora kutoa tenda ya kuzalisha umeme kimkoa. Baadhi ya makampuni tayari inadokezwa yako mbioni kuanzisha kuzalisha umeme (kama kule Mwanza).

Baadhi ya majina yanayotajwa nyuma ya makampuni haya siyo mageni masikioni mwa Watanzania - mengine tulishayataja kuanzia kwenye Dowans na Meremeta. Sasa sijui wazo hili lina ukweli kiasi gani na litatekelezwa vipi bila kusababisha hasira kwa wananchi.

Nyinyi mnalionaje? Fikiria makampuni yatakayojitokeza kuzalisha umeme kuanzia Dar, hadi Kigoma!!
Kumbe ulishalianzishia hili suala mjadala humu?

Ndo wanasema Muhongo anataka kufanya hivyo.Watatoa taratibu na taarifa siku ya june 30th.

Binafsi nadhani ni hatua nzuri endapo Itasimamiwa na kutekelezwa vyema!
 
Mkuu MM wazo hilo linawezekana iwapo tu kutakuwa na sheria na kanuni imara zitakazotoa muongozo mzima wa namna ya kuendesha shughuli hii. Nimekaa Finland, wale wanatumia mfumo huu. Kila mji (Mkoa??) unashirika lake la uzalishaji na usambazaji wa umeme. Ukienda Turku, utaikuta TURKU ENERGY, Helsinki Nao wana shirika au kampuni yao. Bei ya umeme inatofautiana toka mji mmoja hadi mwingine kulingana na gharama za uzalishaji. So hata hapa kwetu tukiamua inawezekana. Mi nafikiri moja ya tatizo linaloikabili Tanesco ni ukubwa wa nchi na unapokuwa unategemea maamuzi yote mazito yatoke makao makuu, basi inakuwa ni mzigo mzito. Kama nchi nafikiri tunaweza kuteua baadhi ya mikoa au wilaya na tukazifanya kama pilot study ili kuona zitafanyaje. Naamini tukijipanga tutaweza.
Very well said!
 
Back
Top Bottom