Wazo la kuzalisha umeme kimkoa (kampuni binafsi) unalionaje?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982
Nasikia kuna magenius wetu wengine wamekuja na suluhisho jipya la tatizo la nishati ya umeme nchini; kuruhusu makampuni binafsi kuzalisha umeme kwenye mkoa na kuuzia Tanesco. Kisingizio kikubwa kinachotolewa ni kuwa kitaifa suala la kampuni binafsi kuzalisha umeme limekuwa vurugu na gumu kutekelezeka kwa hiyo wameonelea ni bora kutoa tenda ya kuzalisha umeme kimkoa. Baadhi ya makampuni tayari inadokezwa yako mbioni kuanzisha kuzalisha umeme (kama kule Mwanza).

Baadhi ya majina yanayotajwa nyuma ya makampuni haya siyo mageni masikioni mwa Watanzania - mengine tulishayataja kuanzia kwenye Dowans na Meremeta. Sasa sijui wazo hili lina ukweli kiasi gani na litatekelezwa vipi bila kusababisha hasira kwa wananchi.

Nyinyi mnalionaje? Fikiria makampuni yatakayojitokeza kuzalisha umeme kuanzia Dar, hadi Kigoma!!
 
ChiefmTz

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
2,913
898
Kama yatatanguliza masilahi ya taifa mbele yaani huduma bora, bei nafuu na uwazi. Mi naona ni poa tu. Hofu yangu ni kuwa Mikoa weak kiuchumi huenda isipate wazalishaji.
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,230
Na nimesikia Rashid Shamte ana kampuni inayohusika na uzalishaji umeme na kuuza kwa TANESCO (Kusini mwa Tanzania).......ni kweli?
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Kama maslahi ya nchi yatalindwa, hili litatukomboa kabisa, angalia.
Dodoma kuna Uranium
Singida kuna upepo
Songea kuna Uranium/maji
Iringa maji/mabwawa tele
Tanga mito/mabwawa
Kigoma kuna malagarasi
Lindi kuna Songas
Mtwara kuna Artumas
Morogoro kuna Kidatu na mito kibao
Njombe kuna Mito na Ruhuji/makaa ya mawe
Mbeya kuna mito na Kiwira
Moshi kuna nyumba ya Mungu
Kagera kuna mto kagera wenyewe
Pwani kuna Stiegler (spelling) huko Rufiji)

nk
Sasa vyanzo vyote hivi viko ndani ya mazingira yetu,hapa hakuna mafuta. Tatizo mafisadi watawahi kila kona. Any way sijui ni ndoto au kweli.
 
Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,605
1,684
Nasikia kuna magenius wetu wengine wamekuja na suluhisho jipya la tatizo la nishati ya umeme nchini; kuruhusu makampuni binafsi kuzalisha umeme kwenye mkoa na kuuzia Tanesco. Kisingizio kikubwa kinachotolewa ni kuwa kitaifa suala la kampuni binafsi kuzalisha umeme limekuwa vurugu na gumu kutekelezeka kwa hiyo wameonelea ni bora kutoa tenda ya kuzalisha umeme kimkoa. Baadhi ya makampuni tayari inadokezwa yako mbioni kuanzisha kuzalisha umeme (kama kule Mwanza).

Baadhi ya majina yanayotajwa nyuma ya makampuni haya siyo mageni masikioni mwa Watanzania - mengine tulishayataja kuanzia kwenye Dowans na Meremeta. Sasa sijui wazo hili lina ukweli kiasi gani na litatekelezwa vipi bila kusababisha hasira kwa wananchi.

Nyinyi mnalionaje? Fikiria makampuni yatakayojitokeza kuzalisha umeme kuanzia Dar, hadi Kigoma!!

Kwa kuwa tuliamua kufungua milango (ku-liberalize) uchumi badala ya kushika njia kuu za uchumi basi na tufanye tu hivyo tu yaishe - tena heri tuwe na Vodatanesco, Airtanesco, Zantanesco, Tigtanesco, Sasatanesco n.k. tuwe tunanunua vocha-cum-luku tuachane na mgawo wa umeme!
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,230
Mfumo wa kutoa umeme kimkoa upo katika nchi nyingi tu hata zilizoendelea (japo kuwa taasisi za usimamizi huwa za serikali)

Unakuta nchi moja lakini bei ya umeme inatofautiana kutoka eneo na eneo.

Kinadharia TANESCO inaweza kufanikiwa kwa kuanzisha Kampuni tanzu za kimaeneo ambazo zitajitegemea lakini kiuhalisia naona kama hapo ndo nafasi ya kuibuka kampuni hewa na kuingizwa kwenye madeni kila kona ya nchi.
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,631
8,445
Hivi ile initiative ya mwakyembe na wenzake ya kupeleka umeme wa upepo singida imeishia wapi?
 
Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,940
1,427
Kama yatatanguliza masilahi ya taifa mbele yaani huduma bora, bei nafuu na uwazi. Mi naona ni poa tu. Hofu yangu ni kuwa Mikoa weak kiuchumi huenda isipate wazalishaji.
huwezi kuwa na umeme wa bei nafuu au huduma bora kwa kampuni za vibaba.Suala la umemeni issue ya serikali kuu.

Kama ni kweli basi serikali inakwepa jukumu lake na ni upuuzi.

kama ni kampuni binasfi zinatakiwa labda zije kusambaza umeme na sio kuzalisha kuzalisha umeme inatakiwa iwe kampuni au shirika la serikali.

kweli kazi ipo
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,038
3,664
Ni wazo zuri na jema, na ikiwezekana hata lisiwe kimkoa tu. Lianze hata kwenye kata. Kama mtu anauwezo wa kuwekeza katika kuzalisha umeme japo mdogo tu, anatumia yeye na unaozidi anawauzia wasambazaji.

Merekani na Canada hata kama unazalisha umeme wa matumizi yako binafsi, unaozidi unawauzia wasambazaji.

Nadhani ianzie hata kwenye kata na si kuanzia ki mkoa tu.
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,038
3,664
Hivi ile initiative ya mwakyembe na wenzake ya kupeleka umeme wa upepo singida imeishia wapi?

Nadhani hawakuelewana na wawekezaji na au hawakupata udhamini wa kutosha na kwa sasa ana madaraka basi si hasha tukaona hilo analitimiza kwanza kabla ya majukumu aliyopewa. Hapo ndipo tutapo muuliza, kulikoni Mr. Mbwembwe?
 
ngoko

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
573
14
Nasikia kuna magenius wetu wengine wamekuja na suluhisho jipya la tatizo la nishati ya umeme nchini; kuruhusu makampuni binafsi kuzalisha umeme kwenye mkoa na kuuzia Tanesco. Kisingizio kikubwa kinachotolewa ni kuwa kitaifa suala la kampuni binafsi kuzalisha umeme limekuwa vurugu na gumu kutekelezeka kwa hiyo wameonelea ni bora kutoa tenda ya kuzalisha umeme kimkoa. Baadhi ya makampuni tayari inadokezwa yako mbioni kuanzisha kuzalisha umeme (kama kule Mwanza).

Baadhi ya majina yanayotajwa nyuma ya makampuni haya siyo mageni masikioni mwa Watanzania - mengine tulishayataja kuanzia kwenye Dowans na Meremeta. Sasa sijui wazo hili lina ukweli kiasi gani na litatekelezwa vipi bila kusababisha hasira kwa wananchi.

Nyinyi mnalionaje? Fikiria makampuni yatakayojitokeza kuzalisha umeme kuanzia Dar, hadi Kigoma!!
Hope zitaingia mikataba ambayo si ya kutegeshea kuwakamua walipa kodi wa nchi hii
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,502
3,041
katika shughuli yoyote kunakuwepo na 1st line of solving a problem, sasa kwa mazingira ya tanzania kwa sasa na hata huko mbeleni , tukizungumzia economy of scales ni vizuri kuwa na mfumo wa kitaifa katika uzalishaji umeme, kwa sababu utakuwa na watumiaji wengi hivyo cost per unit itakuwa ndogo, lakini kwa kuwa Tanzania tunafuata sera ya mafisudi ambao nia yao ni kuona kila moja anapata iwe kikabila, nk ndio maana wanataka kuja na hiyo sera yao ya kimkoa, kwa sababu ya shida yetu wao ndio kipindi cha mavuno.
Embu tu jadili hivyo vijibaba au uzalishaji wa kimkoa, ukizungumzia diesel ni njia gjali kuliko zote za uzalishaji na ndiko tunakotoka baada ya uhuru maana hatukuwa na grid ya taifa hivyo njia hii ilikuwa muafaka.
Ukija kwenye matumizi ya Gesi, sawa Ntwara/mkuranga wanayo hiyo Gesi, je wataweza kuitumia wao wenyewe hiyo yote? ndio hapo suala la economy of scale linapo kuja.
Uranium ina hitaji investment kubwa na mahitaji ya Dodoma au ruvuma ni madogo, hivyo return itachukua miaka 200 badala ya labda 10 kwa ajili ya muwekezaji kupata kifuta jasho chake.
singida na upepo wake hii naona inatakiwa kuwepo ku-complement umeme wa Gesi/Hydro/Nuklia,. na hata huu wa jua ambao mtu moja moja unaeza kuwekeza na ziada kutumika katika gridi ya Taifa kama nchi zingine wana vyo fanya ni katika ile hali ya mtu moja moja kwa mahitaji yake kuwekeza katika njia hizi za uzalishaji kwa matumizi yake binafsi, lakini katika mkakati huo akazalisha ziada ambayo gridi ya taifa ina uhitaji, na hatuwezi kuweka rohoza watu au uchumi wa nchi kwa mtu kama huyu, siku akishindwa ndio hapo tutaanza umeme wa dharura kama wa Richmondi, au wa Dowans akuwa na Vi-Artumas kila mahali.
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,631
8,445
huwezi kuwa na umeme wa bei nafuu au huduma bora kwa kampuni za vibaba.Suala la umemeni issue ya serikali kuu.

Kama ni kweli basi serikali inakwepa jukumu lake na ni upuuzi.

kama ni kampuni binasfi zinatakiwa labda zije kusambaza umeme na sio kuzalisha kuzalisha umeme inatakiwa iwe kampuni au shirika la serikali.

kweli kazi ipo
mkuu fanya research basi kwanza..... vyote vyawezekana, public au private established as long as there is effective and efficient regulations and law enforcement iko aware

going green is one of the best strategy ka kupunguza utegemezi kwa public powere divers kama tanesco

sina data zozote zaidi ya kuangalia national geopraphic na discovery channels, lakini those were enough to convince me
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,230
katika shughuli yoyote kunakuwepo na 1st line of solving a problem, sasa kwa mazingira ya tanzania kwa sasa na hata huko mbeleni , tukizungumzia economy of scales ni vizuri kuwa na mfumo wa kitaifa katika uzalishaji umeme, kwa sababu utakuwa na watumiaji wengi hivyo cost per unit itakuwa ndogo, lakini kwa kuwa Tanzania tunafuata sera ya mafisudi ambao nia yao ni kuona kila moja anapata iwe kikabila, nk ndio maana wanataka kuja na hiyo sera yao ya kimkoa, kwa sababu ya shida yetu wao ndio kipindi cha mavuno.
Embu tu jadili hivyo vijibaba au uzalishaji wa kimkoa, ukizungumzia diesel ni njia gjali kuliko zote za uzalishaji na ndiko tunakotoka baada ya uhuru maana hatukuwa na grid ya taifa hivyo njia hii ilikuwa muafaka.
Ukija kwenye matumizi ya Gesi, sawa Ntwara/mkuranga wanayo hiyo Gesi, je wataweza kuitumia wao wenyewe hiyo yote? ndio hapo suala la economy of scale linapo kuja.
Uranium ina hitaji investment kubwa na mahitaji ya Dodoma au ruvuma ni madogo, hivyo return itachukua miaka 200 badala ya labda 10 kwa ajili ya muwekezaji kupata kifuta jasho chake.
singida na upepo wake hii naona inatakiwa kuwepo ku-complement umeme wa Gesi/Hydro/Nuklia,. na hata huu wa jua ambao mtu moja moja unaeza kuwekeza na ziada kutumika katika gridi ya Taifa kama nchi zingine wana vyo fanya ni katika ile hali ya mtu moja moja kwa mahitaji yake kuwekeza katika njia hizi za uzalishaji kwa matumizi yake binafsi, lakini katika mkakati huo akazalisha ziada ambayo gridi ya taifa ina uhitaji, na hatuwezi kuweka rohoza watu au uchumi wa nchi kwa mtu kama huyu, siku akishindwa ndio hapo tutaanza umeme wa dharura kama wa Richmondi, au wa Dowans akuwa na Vi-Artumas kila mahali.

Kwanza sidhani kama inaposemwa mkoa inamaanisha kila mkoa uwe na shirika lake linalojitegemea, rather nafikiri inaleta maana zaidi kama ni mashirika ya kimaeneo ambayo yatatoa huduma kwa zaidi ya Mkoa mmoja.

Na linapokuja suala la economy of scale ningetarajia kama serikali itachukua hatua za kuzalisha umeme kimaeneo basi itumie mfumo wa smart grid ambao grid zote ndogo ndogo zinaungana ili kuleta ufanisi kwenye uzalishaji na usambazaji wa umeme.

(japokuwa kwa Tanzania vitu vyengine kufikiri vitafanywa ni kujidanganya)
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982
Sasa yule anayeuza kwa mkoa tujue si kwamba anachimba hydropower station.. au kuanzisha kituo cha umeme wa nyuklia yeye ataleta majenereta tu makubwa - yale ya Industrial halafu ndio anafunga na kuanza kuuza umeme.
 
Lakini zaidi ya hiyo ya kanda kuna kitu kinachoitwa bahati ambayo Mwenyezi Mungu ametupatia nayo ni hiyo Gesi/Uranium/Hydro/Upepo/Jua mawimbi baharini nk nk na Diesel ya huko inakotoka.
Sasa unaposema nataka kuchukua njai hii au ile unatakiwa ufanye tathimi, sasa tathimi endelevu mara nyingi ni zile za muda mrefu na tija zaidi, ukitilia maanani mambo ya teke linalo kujia, environment na mtaji, sasa kwa hali ilivyo bahati mbaya mimi si mtaalamu wa mambo ya umeme au sija jikita saana ili kujua ni umeme upi nafu na tekelinalo kujia ipi ndio bora zaidi na hayo mambo ya elimu uhai wa viumbe na uoto.
sasa ukichukua hiyo concept ya shirika fulani kutoa huduma maeneo fulani, litakuwa gumu kidogo maana concept ya muwekezaji ni kujaribu kupata soko kubwa kadri inavyo wezekana, sasa leo hii huwezi mwambia artumas na gesi yake baki Ntwara tu au njoo mpaka Dar, Tanga nk atataka arusha, Mwanza na hata ikiwezekana Rukwa, na Yule wa Kidatu vile vile, Malagarasi naye atataka soko kubwa zaidi.
Sasa hitimisho ni kwamba muwekezaji yoyote ataangalia maslahi yake leo na miaka kumi ijayo na ikiwezekana zaidi ya hapo, kuna mwingine kama Richmonduli uwezo wake mdogo yeye atakwambia nitazalisha 100mw unipe advance, mwingine Rowans ataanza kutafuta LC benki zote zenye viongozi hafifu kisa kaona soko la siki mbili tatu, kuna mwingine hatumjui yeye kaona chanzo na umeme wa miaka kadha wa kadha, ndipo hapo serikali kama msimamizi mkuu wa shughuli anapotakiwa kuangalia ampe leseni yupi. Virichie richie, vi-Rowans nk.
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,502
3,041
Sasa yule anayeuza kwa mkoa tujue si kwamba anachimba hydropower station.. au kuanzisha kituo cha umeme wa nyuklia yeye ataleta majenereta tu makubwa - yale ya Industrial halafu ndio anafunga na kuanza kuuza umeme.
Tekelinalokujia la uranium huwezi kuwa na vinu vingi vya uranium kila kanda au sembesu mkoa, kwa sababu za kiusalama na za kiuchumi, na kitaalamu, ukitilia maanani nchi yetu matumizi yetu bado ni madogo, na ki-afrika bado hatuna mashirikiano ya kutosha ya kiuchumi ndio hapo suala la economy of scales linapo kuja. Sasa ili umtumie ipasavyo huyo mtaalamu wa Nuklia ni vizuri uwaweke wengi pamoja, maana hata shift moja hawezi kuka saa 24 au ikitokea dharura atoke huko aliko akatatue tatizo.
Ukija Hydro inategemea na vyanzo vilivyopo na uwezo wa hivyo vyanzo, na pia kuwa na hao wataalamu, tukirudi kwenye economy of scale katika kuwa tumia wataalamu hawa ni vizuri wawe sehemu moja wengi kuliko kuwa tapanya sema ,unao wanne moja Ntwara, mwingine Dodoma, Mwingine Malagarasi, mwingine Kagera, sasa wakagera aikugua au kikiwa na dharura wa mtwara ndio aende huko?
Ndio maana Pale Kidatu palijengwa na chuo kikawekwa ili kutibu tatizo la economy of scales.
Kwa hiyo Solution ya hao Majini wa Wizara/tanesco nk ni huo wa majenereta. wao wanafikiria jinsi ya kupata 5 to 10 years wakati tuna waya waya umeme tutapata kutoka wapi, baada ya hapo wanamuuzie huyo huyo tanesco majenereta yao, na wao kuingia ubiya kwa uranium/Gesi/Hydro kwa hela watakayo pata katika kipindi cha mpito.
 
babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
78
Mkuu MM wazo hilo linawezekana iwapo tu kutakuwa na sheria na kanuni imara zitakazotoa muongozo mzima wa namna ya kuendesha shughuli hii. Nimekaa Finland, wale wanatumia mfumo huu. Kila mji (Mkoa??) unashirika lake la uzalishaji na usambazaji wa umeme. Ukienda Turku, utaikuta TURKU ENERGY, Helsinki Nao wana shirika au kampuni yao. Bei ya umeme inatofautiana toka mji mmoja hadi mwingine kulingana na gharama za uzalishaji. So hata hapa kwetu tukiamua inawezekana. Mi nafikiri moja ya tatizo linaloikabili Tanesco ni ukubwa wa nchi na unapokuwa unategemea maamuzi yote mazito yatoke makao makuu, basi inakuwa ni mzigo mzito. Kama nchi nafikiri tunaweza kuteua baadhi ya mikoa au wilaya na tukazifanya kama pilot study ili kuona zitafanyaje. Naamini tukijipanga tutaweza.
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,038
3,664
Sasa yule anayeuza kwa mkoa tujue si kwamba anachimba hydropower station.. au kuanzisha kituo cha umeme wa nyuklia yeye ataleta majenereta tu makubwa - yale ya Industrial halafu ndio anafunga na kuanza kuuza umeme.

Si lazima iwe hivyo. Kuna hydropower zs kuzalisha hata kikata tu. Na hili limeshafanyika Tanzania. Kuna wazungu fulani niliwahi kusoma habari zao, wamefunga kamtambo kadogo kwenye moja ya vijiji vya Tanzania na kanazalisha umeme safi na salama kimazingira.

Inawekana ikatumika wind power vilevile au masalio ya miti, yaani branches za miti na majani yanayoanguka yenyewe na sio kukata miti yenyewe. Hii ni Teknologia mpya ambayo imeshanza kutumika Canada. Kuna kampuni tayari inazalisha huko Canada na wameonyesha interest Tanzania.

Kuna teknologia nyingi za kuzalisha umeme wa kiwango kidogo, ambao ukipewa kipaumbele matatuzi ya umeme yatakuwa things of the past.
Tuanze kutambaa wakati tunajitayarisha kukimbia.

Kwanza la kufanya naona ingekuwa kuibinafsisha Tanesco au tu sheria ya kuruhusu wasambazaji wengine ianzishwe haraka haraka (imeahidiwa na Kikwete).

Nna uhakika kuwa resources za kuzalisha umeme mdogo na mkubwa tunazo nyingi sana. Visheria vilivyopitwa na wakati ndio vinatubana bana.
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,038
3,664
Sasa yule anayeuza kwa mkoa tujue si kwamba anachimba hydropower station.. au kuanzisha kituo cha umeme wa nyuklia yeye ataleta majenereta tu makubwa - yale ya Industrial halafu ndio anafunga na kuanza kuuza umeme.

Si lazima iwe hivyo. Kuna hydropower za kuzalisha hata kikata tu. Na hili limeshafanyika Tanzania. Kuna wazungu fulani niliwahi kusoma habari zao, wamefunga kamtambo kadogo kwenye moja ya vijiji vya Tanzania na kanazalisha umeme safi na salama kimazingira.

Inawekana ikatumika wind power vilevile au masalio ya miti, yaani branches za miti na majani yanayoanguka yenyewe na sio kukata miti yenyewe. Hii ni Teknologia mpya ambayo imeshaanza kutumika Canada. Kuna kampuni tayari inazalisha huko Canada na wameonyesha interest Tanzania.

Kuna teknologia nyingi za kuzalisha umeme wa kiwango kidogo, ambao ukipewa kipaumbele matatizo ya umeme yatakuwa things of the past.
Tuanze kutambaa wakati tunajitayarisha kukimbia.

Kwanza la kufanya naona ingekuwa kuibinafsisha Tanesco au tu sheria ya kuruhusu wasambazaji wengine ianzishwe haraka haraka (imeahidiwa na Kikwete).

Nna uhakika kuwa resources za kuzalisha umeme mdogo na mkubwa tunazo nyingi sana. Visheria vilivyopitwa na wakati ndio vinatubana bana.

Pia kungoja Serikali itufanyie kila kitu, hii pia inachangia kuturudisha nyuma. Its time tuanze kuifanyia Serikali na si kungoja itufanyie.

Sidhani leo, kama mtu anaweza kuwekeza kwenye kuzalisha umeme japo kwa kiwango kidogo kama atakataliwa. Si tunaona majenereta binafsi ya kila saizi yalivyojazana na pia kwa sasa tunaona umeme jua unaingia kwa kasi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom