Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,566
- 41,085
Kila mmoja anajua kuwa Serikali, mashirika na makampuni yake, hawajawahi kuwa na ufanisi katika mambo karibia yote . Wanachoweza ni ulaghai, uwongo, kukamata watu, na mara nyingi kubambikia watu kesi. Lakini ukija kwenye utawala bora ni zero, uadilifu ni zero, ubunifu ni zero, biashara na uchumi.
Kwa sasa Serikali inachofanya ni kuwafukarisha watu kupitia TANESCO. TANESCO inafanya kazi zake kwa ulaghai mkubwa. Mara walisema mitambo inafanyiwa marekebisho, mara mvua hakuna, mara tunabadilisha nguzo, sahizi wanasema ni hitilafu!! Yaani umeme kutokuwepo kwa siku nzima ni hitilafu. Nchi nyingine, hii isingetajwa kama hitilafu bali janga. Na ni lazima Serikali nzima ingekuwa busy na suala hilo. Na vyombo vya habari vingekuwa live kufuatilia yote yanayoendelea.
Ukweli ni kwamba hawa watu ni waongo. Na kwa kutegemea hawa TANESCO, hata tungekuwa na mabwawa 1,0000 ya kuzalishia umeme, bado hatutaweza kupata umeme wa uhakika. Na kwenye hili, subirini litakapoanza kutumika bwawa la Nyerere kama kutakuwa na umeme wa uhakika. Hawa watu wameishiwa uelewa, maarifa, uafilifu, na hawana namna nyingine yoyote. Upeo na uwezo wao umegota.
Serikali ilishindwa kuendesha mabenki, viwanda mbalimbali, ATCL, simu, elimu, afya (mpaka sasa kwa kiasi kikubwa wabategemea hospitali za makanisa) n.k. Hivi tunategemea muujiza gani toka TANESCO iliyo chini ya Serikali, kwenye umeme?
Ni vema sasa, tukafanya kama ilivyofanyika kwenye simu. TANESCO inyang'anywe monopoly kwenye biashara ya umeme. Iwe ni kampuni tu ya kawaida itakayohitajika kutimiza sheria na sera ya nishati. Makampuni binafsi yaruhusiwe kuzalisha na kusambaza umeme kwenye maeneo yoyote watakayotaka na watakayoweza. Yanaweza kuanza na mikoa michache. Kwa kuanzia makampuni hayo yanaweza kutumia umeme na miundombinu ya TANESCO, huku, taratibu wakitengeneza miundombinu yao, na kujenga vyanzo vipya vya kuzalishia umeme. Huko mbeleni makampuni yatakuwa na uamuzi wa kununua umeme wa TANESCO au kununua kwa wazalishaji wengine. TANESCO watalipwa mapato ya ukodishaji miundombinu yao. Na yenyewe ikiwa mibovu, baadaye inaweza kuachwa.
Kunaweza kufanyika hata utaratibu mwingine, lakini kwa kuitegemea hii TANESCO, tusitegemee kwenda kokote. Kuna baadhi ya mataifa, umeme kukatika hata kwa saa moja, kunaweza kuiangusha Serikali lakini sisi kutokuwa na umeme inaonekana ni maisha ya kawaida.