Wazo la kijinga: Kuna dalili zote kwa serikali ya Magufuli kushindwa

Pesa zipo cha msingi ni kuzitafuta kwa kufanya kazi halali, hata ajira zikitoka sidhan kama ugumu wa maisha utapungua kwa watanzania, watu wanaotarajia kuajiriwa ni wachache kuliko wasio kuwa na kazi.
 
Kama hali ni ngumu na unaendelea kukaa jamiii forums unalalama kama upo kwenye menopause basi we ni wa kufwaa tu dead maza fanta huna faida kwa taifa
 
Unaweza kunionesha sehemu nilibishana mkuu ??? au wewe ni miongoni mwa hao MA-RAS na MA-DED???

Mkuuu hii ni Tanzania yetu wote....kama serikali ikikosea tunaikosoa wote na kama ikifanya jambo zuri tunaipongeza wote......ushabiki wa vyama hauna tija
 
Acheni upotoshaji wa hali halisi.
hakuna cha hali halisi mkuu....raisi wetu sio mtu wa matumizi mabaya ya madaraka....baraza lake la mawaziri nalo kama yeye....sasa unadhani kwann khali ya uchumi, ukata utokee kwa muda mfupi hivi?
 
Kuna wajinga lakini wewe umezidi hivi kuishi kihalali ndio kunapeleka watu waishi kwa dhiki na kuzidi kuwa maskini

Mkuu namanisha kuishi kwa kufata utaratibu unaotakiwa na serikali.....hao wanaowatuma kuandika matusi humu ndo wanaowacheka na kuwafanya maisha kuwa aghali.
 
Hamna lolote hapo.
Wapo watumishi wa Umma WENYE WELEDI, waliolitumikia Taifa kwa UAMINIFU kwa muda mrefu ambao walitakiwa wawe promoted na kuteuliwa nyadhifa mbalimbali. Binafsi jambo hili silioni kama ni jambo sahihi.

Serikali ya ccm kuanzuia mwinyi mpaka kikwete pale tulichagua koloma.....ata hao unaowasema walikuwa na weledi ni wa kudonoa tu.
 
Wala sio uchama mkuu....haya maisha ya kijinga jinga tunayaeendekeza sisi....sasa kama magufuri anadai kuna watu wameficha pesa na wanatakiwa wazirudishe nyie mnashabikia waeendeleee kuficha na zisizunguke mitaani,mnategemea hayo maduka mtayaendesha kivipi?....Wambie hao mafisadi wafichue hizo pesa na sisi walala hoi tupate ujira wetu ,tukanunue bidhaa huko kariakoo na mwanza uone maduka kama yatafungwa kwa kukosa wateja!!
we jamaa umeandika nini hapa, acha mihemuko!
 
mkuu kwanini kitu kikikosekana inaonekana kimefichwa??!sukari ilisemekana imefichwa sasahivi pesa imefichwa dont you think hakuna alternative ya kusolve haya matatizo tofauti na kuomba walioficha warudishe na badala yake kuacha maisha yakiwa magumu mtaani?

Hii ni kwakuwa Waafrika tulio wengi hatupendani....hakuna kumjali aliyekuweka madarakani, wakishafika walipopataka hawana tena huruma....wanaoficha sukari na pesa hawana mapenzi na watanzania wa hali ya chini.....hii ni vita ya mafisadi na serikali,mafisadi wanamua kuturudushia sisi maumivu.
 
Urahisi wake ulikuja tu kwa mpango wa shetani wala haikutarajiwa
 
Kinachonisikitisha ni kutotoa ajira kwa vijana ambao wengi wanatoka familia maskini mno halafu nae anajinadi kutetea maskini wa nchi hii ingekuwa kweli kabla ya kuwateua hao MARAS 2 NA MADED 13 angetoa kwanza ajira kwa vijana ambao baba zao na mama zao ni maskini anaowatetea, kwa kutofanya hili kwangu kapoteza mvuto kwa 100% hakuna atakachoongea eti kikawa cha maana kwangu.
Ndugu yangu ccm ni ileile na wana ccm ni walewale............
 
Matatizo yanakufanya mtu uwaze sana kwa usahihi ama kimakosa! Sometimes huwa nafikiria kungekuwa na uwezekano wa kunywa dawa (iwe hospitalini ama kwa dr. JJ ) iwe ni ya kuleta uzalendo ingekuwa poa tu, ili jambo baya likifanywa na mtu au kikundi cha watu tulikatae wote na likifanywa jambo zuri kwa ajili ya taifa letu tulikubali wote.
 
Serikali ya ccm kuanzuia mwinyi mpaka kikwete pale tulichagua koloma.....ata hao unaowasema walikuwa na weledi ni wa kudonoa tu.
mkuu unaongea ukiwa na akili timamu au umelewa kwa hiyo yale maisha ya zama za Nyerere za bidhaa adimu uliyafurahia sana
 
Kuna kitu nadhani hautambui....hivi kipind cha kikwete maisha ya kambale kila mtu anandevu,unaweza yalinganisha na maisha ya kipindi hiki cha bro Magu....cha sheria bila shuriti?

hamna lolote...

ni sawa na kusafisha chupa nje pasipo kusafisha na ndani penye uvundo.

Ameshatuangusha kabla ya Safari kuanza.

Ameshashindwa vibaya mno..yupo hoi now


Utawala wa matamko na maagizo una karaha yake na raha zake...
 
Back
Top Bottom