Wazo la kijinga: Kuna dalili zote kwa serikali ya Magufuli kushindwa

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,969
1,393
Naomba kusema mie sio mwanauchumi ila mpaka sasa naona dalili zote za serikali ya awamu ya tano kushidwa..
Tulikuwa tukitegemea unafuu wa maisha lakini hari imekuwa mbaya kuliko awali.
Kwa sasa mzunguko wa biashara hakuna kwa mfano.Kariakoo kwa sasa watu wanachia milango kwa sababu hakuna faida anayopata ukiachilia kodi kuwa juu..mtu anamua kwenda kupanga mtaani.
Tatizo la ajira linaendelea kuwa kubwa hakuna ajira mpya kama alivyohaidi baada ya miezi 2 ajira zitatoka mpya hakuna mpango mahususi wa kuwawezesha vijana kupata mikopo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha
Teuzi sasa zimekuwa za kumsifia JPM anakupa teuzi.mfano.nafasi za makatibu wa kuu na manaibu wake hawa walikuwa wajiriliwa kutoka serikalini kama ilivyo kwa wakurugenzi ..motisha kwa wafanyakazi wa huma imekwisha hawezi mtu kutoka kutangaza TV.leo anakuja kuwa boss wako.
Uhuru wa vyombo vya habari na watu kujieleza umebinywa sana ..kila kitu lazima usifie serikali hata kama ni jambo baya ..
Hakuna miradi mikubwa mpaka sasa serikali imesign zaidi ile ambayo ilikuwa imekwisha andaliwa na JK.
Kazi anayoifanya kwa sasa ni kuteua na kufukuza..
Watanzania tunahitaji kuona maisha yakiboreshwa na uhuru wa kujieleza..
Ongeza mengine unayoyajua wewe...
 
hali imekua ngumu sana ajira ngumu,makampuni yanapunguza watu mahoteli yanafungwa,mengine yanageuzwa hostel au kuuzwa,watalii wamepungua sana,wale waliokuwa wanafanya shughuli za kusafirisha magari na mizigo nchi jirani wengi wao wako nyumbani tuu ,mafao ya kujitoa bado ni ishu
 
Maduka walikuwa wanayaendesha mafisadi....mirango ya kujichumia kiulaiini imefungwa.....tujifunze kuishi kiharali mkuu!
Kuwa na hofu na Mwenyezi Mungu kwa hii post ulioutoa.hali inajulikana kuwa ngumu wewe unaleta uchama wako.
 
Kwani Ajira ni nini.
Ukikimbilia mjini kichwa kichwa lazima usomeshwe Number tu.

Hakuna Nchi yoyote Duniani ambayo wananchi wake wote wana Ajira.
USA kwenyewe njaa kali vile vile,watu hawana Ajira,itakuwa hapa.

Uwezo wa kufikiri na kujituma,ndio mtaji wako.
Vijana wa Kiume wamekuwa hovyo sana,hatimae madada ndio wajasiriamali wenye mafanikio makubwa na kwa kasi kuliko vijana wa kiume wenye kutaka maisha ya mkato na muda mfupi.Ujanja ujanja,utapeli,dili za ajabu.Huku matumizi yakiwa makubwaa

Akili kumkichwa,maisha mepesi ukiwa na akili,ukishindwa rudi kijijini,watu wa mjini wanawekeza kwenye mashamba vijijini kwa sasa na vijana mmekimbia huko mnapishana na Maisha.

Mtu akifanikiwa mnasema Freemason,sasa watu tutulieee tuendelee kusema Mkulima Masanja na Diamond ni freemason wakati vijana hao wanatumia fursa huku tukiwapiga majungu.
Blessed vijana wote wenye kujituma
 
Ukweli ni mmoja tu, Taifa la Tanzania limepoteza mwelekeo wote wa Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. Kwa sasa Kiuchumi hali ni mbaya(Mpaka Rais mwenyewe anakiri kuwa Pesa hakuna tena mtaani), Kisiasa hakuna tena Demokrasia(Mpaka rais anapiga marufuku shughuli za Kisiasa) na Kijamii hali ni mbaya sana (Mpaka Rais anawaita watoto wa maskini waliofaulu vizuri kuwa ni Vi.la.za!).

Yote hayo ni matokeo ya makosa ya Mtu mmoja tu, ambaye anaamini yeye hakosei, hapaswi kukosolewa na kushauriwa na hapaswi kufuata sheria za nchi.
 
Sasa kama mafisadi wameficha pesa hizo boxer utanunua na sindiria utanunua na nini?.....lazima wafunge tu.
kwani hizo pesa zimeanza kufichwa serikali ya awamu ya 5?? mbona enzi za kikwete hali haikuwa hivi!! unaweza fikiria zaidi ya hapo
 
Ila hili la kuteua hovyo hovyo tutegemee utendaji wa hovyo hovyo...... Tunawasubiri huku Halmashauri ili tuwanyooshe
 
Kinachonisikitisha ni kutotoa ajira kwa vijana ambao wengi wanatoka familia maskini mno halafu nae anajinadi kutetea maskini wa nchi hii ingekuwa kweli kabla ya kuwateua hao MARAS 2 NA MADED 13 angetoa kwanza ajira kwa vijana ambao baba zao na mama zao ni maskini anaowatetea, kwa kutofanya hili kwangu kapoteza mvuto kwa 100% hakuna atakachoongea eti kikawa cha maana kwangu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom