Wazo la kijinga: Kuna dalili zote kwa serikali ya Magufuli kushindwa

Kweli hutoona cha maana kwakuwa umejiandaa kubishana tu....hivi unajua taratibu za kuajili watu katika nyazifa muhimu kama hizo ulizo zitaja, au ww unadhani ni kama kwenda sokoni unachagua matunda tu na kuweka kwenye kapu?
Hamna lolote hapo.
Wapo watumishi wa Umma WENYE WELEDI, waliolitumikia Taifa kwa UAMINIFU kwa muda mrefu ambao walitakiwa wawe promoted na kuteuliwa nyadhifa mbalimbali. Binafsi jambo hili silioni kama ni jambo sahihi.
 
well said mkuu nataman isingekua title ya huu uzi ingekua "News alert"
 
Maduka walikuwa wanayaendesha mafisadi....mirango ya kujichumia kiulaiini imefungwa.....tujifunze kuishi kiharali mkuu!
Kuna wajinga lakini wewe umezidi hivi kuishi kihalali ndio kunapeleka watu waishi kwa dhiki na kuzidi kuwa maskini
 
Msimu uliopita wa EPL nikiwa shabiki wa Manchester United,sikuwa nikipenda kuiona Man ikishinda,nilifurahi kila nikiiona inafungwa,
Ndio, ifungwe ili Van Gaal afukuzwe,

Pia hali iendelee hivi hivi. Ili watu waisomi namba na siku nyingine waitumie vizuri akili waliyopewa buuure na mola wao,na si kushabikia bila kujua unachoshabikia
 
Hakuna miradi mikubwa mpaka sasa serikali imesign zaidi ile ambayo ilikuwa imekwisha andaliwa na JK.
Unajua tatizo la madawati kwa wanafunzi limekuwepo kwa muda gani Tanzania (kuwa mkweli)?
Unadhani mradi huu wa madawati sio mkubwa, na je uliachwa na JK!
Tatizo letu mind zetu zimekuwa corrupted kiasi kwamba ukiwaza 'mradi' ni pale unapomuona mwarabu au mzungu anaongea na rais.
 
Kama hili lilimshinda sifikirii kama tuendako tutafika
 

Attachments

  • 20160430_123448[2].jpg
    20160430_123448[2].jpg
    162.6 KB · Views: 24
He still have alot of time to turn things around. But that will be possible only if he listens to others and stop the kind of politics is trying to plug In. CCM & self popularity kwanza maslahi ya wengi baadaye.
 
Kwani Ajira ni nini.
Ukikimbilia mjini kichwa kichwa lazima usomeshwe Number tu.

Hakuna Nchi yoyote Duniani ambayo wananchi wake wote wana Ajira.
USA kwenyewe njaa kali vile vile,watu hawana Ajira,itakuwa hapa.

Uwezo wa kufikiri na kujituma,ndio mtaji wako.
Vijana wa Kiume wamekuwa hovyo sana,hatimae madada ndio wajasiriamali wenye mafanikio makubwa na kwa kasi kuliko vijana wa kiume wenye kutaka maisha ya mkato na muda mfupi.Ujanja ujanja,utapeli,dili za ajabu.Huku matumizi yakiwa makubwaa

Akili kumkichwa,maisha mepesi ukiwa na akili,ukishindwa rudi kijijini,watu wa mjini wanawekeza kwenye mashamba vijijini kwa sasa na vijana mmekimbia huko mnapishana na Maisha.

Mtu akifanikiwa mnasema Freemason,sasa watu tutulieee tuendelee kusema Mkulima Masanja na Diamond ni freemason wakati vijana hao wanatumia fursa huku tukiwapiga majungu.
Blessed vijana wote wenye kujituma
Hii iwaingie wavivu wote mpaka kwenye mfupa.
 
Kweli hutoona cha maana kwakuwa umejiandaa kubishana tu....hivi unajua taratibu za kuajili watu katika nyazifa muhimu kama hizo ulizo zitaja, au ww unadhani ni kama kwenda sokoni unachagua matunda tu na kuweka kwenye kapu?
Unaweza kunionesha sehemu nilibishana mkuu ??? au wewe ni miongoni mwa hao MA-RAS na MA-DED???
 
Unapoamua kutumia milioni ya fedha katika uwekezaji au kuanzisha kampuni ni jambo la msingi uangalie soko utalimudu vipi, katika hali yoyote ile, iwe ya neema au dhiki. Ninaamini kwa aliyepata mtaji kwa jasho lake, hawezi kukurupuka katika uwekezaji. Sasa hawa wanaofunga biashara sasa au kupunguza watendaji wao, kuna mushkeli sehemu fulani ambayo kwa sisi watazamaji hatutaweza kuing'amua, bali tutaendelea kulaumu serikali. Si siri wizi wa kutisha ulikuwa ukiendelea serikali iliyotangulia, pengine hata huo uwekezaji waliofanya ulitokana na wizi wa fedha za umma. Pengine biashara ilikuwa si nzuri tangu wakati huo lakini kwakuwa kulikuwa na sehemu ya kuiba basi hawakujali hasara ya vitega uchumi vyao. Sasa mambo yanabanwa na ukweli unawekwa wazi, lawama zinatupwa kwa serikali. Maisha yanaonekana dhahiri ni magumu kwa wananchi, ila tuipe muda serikali wa mwaka au mwaka na nusu, kama mpaka wakati huo mambo yatakuwa hayaeleweki, hapo ndio tuhitimishe kuwa imeshindwa.
 
Serikalii inafanikiwa, itaendeleakufanikiwa na mwisho Panapo Uhai Watanzania wataomba Magu aongeze kipindi cga tatu. Sababu za kufanikiwa Magu aendeshi serikali kishkaji na kama alikuteua na hukuonyesha tija anakutumbua. Miradi mipya inakuja lakin iiliyopo ndio iyo mnayo lalamika kwamba deni la Taifa linaongezeka. yaani Maendeleo mnataka lakini deni hamlitaki!! Anachokifanya Magu ndiokinachotakiwa kufanywa. Ameanza na msingi anapanda taratibu na kwa baadhi ya watu kulalamika haikuanza leo . Kipindi cha Mwinyi walilalamika, Mkapa wakalalamika, Kikwete wakalalamika waka mtukana. Nasasa wanalalamika ila huyu huwezi kumtukana maana utafundishwa adabu. Naatakaye kuja watalalamika.
sawa itafanikiwa, mwambie basi aachie ajira za watoto wa maskini anao watetea jukwaani.
 
jamii01: hakika mada yako ni "wazo la kijinga" ikidhirishwa na mifano uliyotoa ambayo haiendani kabisa na wazo lako kuu "kuna dalili zote serikali ya Magufuli kushindwa".

Dhana mbili kuu zinahitaji ufafanuzi wako ili ueleweke:
1) Nilitegemea ungefafanua maana yako ya serikali ya Magufuli kushindwa!

2) Ni dalili zipi za kushindwa kwa Serikali!
Nimesoma mada yako sijaona "dalili" hata moja ya inayoonesha/thibitisha au kutoa mwanga kuna mwelekeo wa kushindwa kwa Serikali ya Magufuli. Yawezekana unazo takwimu, kwa kila dalili za Serikali kushindwa, basi tuwekee hapa tuzijadili.
 
Kuna pepoo watu wabadilike

IV
Watu wanapinga hoja inamaana hawaoni kama life taafu??!
Tuache ushabiki tubadilike

Hahahahhahahahha
 
jamii01: hakika mada yako ni "wazo la kijinga" ikidhirishwa na mifano uliyotoa ambayo haiendani kabisa na wazo lako kuu "kuna dalili zote serikali ya Magufuli kushindwa".

Dhana mbili kuu zinahitaji ufafanuzi wako ili ueleweke:
1) Nilitegemea ungefafanua maana yako ya serikali ya Magufuli kushindwa!

2) Ni dalili zipi za kushindwa kwa Serikali!
Nimesoma mada yako sijaona "dalili" hata moja ya inayoonesha/thibitisha au kutoa mwanga kuna mwelekeo wa kushindwa kwa Serikali ya Magufuli. Yawezekana unazo takwimu, kwa kila dalili za Serikali kushindwa, basi tuwekee hapa tuzijadili.
Achien kwanza hizo ajira za watoto maskini na mrudishe fao la kujitoa kwanza,
halafu tuanze kurumbana kwa hoja
 
Back
Top Bottom