DOKEZO Mazingira ya kazi kwa Vibarua wa Magazeti ya Serikali si mazuri, mamlaka ziangalie malipo wanayopata

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa Wafanyakazi katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN) inayojihusisha na uchapaji wa magazeti ya Habari Leo, Daily News na Spoti Leo, bila kuzunguka sana utaratibu ulivyo Rais wa Nchi ndiye Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Serikali, hiyo pekee inaonesha heshima ya magazeti hayo.

Pamoja na hivyo kwa uhalisia si rahisi kushuhudia Rais akishughulika na utendaji wa magazeti hayo kwa kuwa Wasaidizi wake wapo na wanatakiwa kumsaidia majukumu hayo.

Kuna changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikijitokeza hasa kwa ndugu zetu ambao wanafanya kazi kama vibarua (correspondent), mazingira yao kwa kweli si rafiki japo kama taasisi kwa jumla kuna changamoto za hapa na pale, nitazitaja:

Malipo mdogo kwa Vibarua
Waandishi ambao hawajaajiriwa wanalipwa Shilingi 4,000 kwa stori moja ambayo inayoka gazetini au mtandaoni, makala ni Shilingi 7,000, hii ni kwa upande wa Habari Leo, upande wa Daily News wanalipwa Shilingi 7,000 kwa stori moja na Shilingi 20,000 kwa makala.

Asilimia kubwa ninakaa nao na ninaona uhalisia ulivyo mgumu hasa kwa wale wa machapisho ya Kiswahili, unamlipa mtu buku 4, tena katika mazingira ambayo stori zinakuwa na ushindani kwa kuwa wapo wengi na wote wanahitaji kiwango hicho.

Ukifuatilia baadhi ya magazeti, kiwango kama hicho walikuwa wanakilipa miaka zaidi ya 7 au 10 iliyopita. Uongozi unatakiwa kulizingatia hili kwa kweli ndugu zetu wana hali mbaya.

Waziri amewasahau vibarua
Waziri Nape Nnauye anafanya kazi nzuri na ameshafika mara kadhaa kwenye ofisi za magazeti lakini mara zote anazokuja hapati nafasi ya kuzungumza na vibarua, anazungumza ama na sisi waajiriwa au wakuu wa vitendo, hiyo inamaanisha vibarua hawana nafasi kabisa ya kutambulika wakati wanafanya kazi kubwa.

Mikataba hewa

Kuna wafanyakazi wengi waliokuwa katika ajira ya kudumu na wengine ajira ya mkataba, walisitishiwa ajira zao na baadhi wakabaki kama vibarua, huu ni zaidi ya mwaka wa tatu sasa hawana mikataba licha ya kuwa wapo hapohapo.

Kila mara tunapata darasa kuhusu elimu ya ajira na mikataba, Sheria za kazi kwani zinasemaje, mtu afanye kazi kwako muda gani kabla ya kupewa mkataba?

Tena hii ni taasisi ya Serikali lakini hilo halizingatiwi, wakiona kuna dalili ya kelele nyingi, wanachofanya ni kuwapa mikataba ambayo wanaambiwa wasaini lakini sehemu ya malipo inaachwa wazi kwa kuwa hawawalipi kulingana na mikataba.

Hali hiyo inasababisha vibarua hao wanaishi “Mungu Saidia”, kwani hakuna huduma muhimu kama za bima na nyinginezo.

Wanatengwa katika shughuli za kiofisi
Kuna shughuli kadhaa za kiofisi zinafanyika lakini vibarua wamekuwa wakitengwa, ni kitu kidogo lakini kinaweza kuwa na maana kubwa katika utendaji kazi.

Rais hajatembelea chombo chake cha habari
Inawezekana lisiwe jambo la muhimu sana lakini as long as Rais ni Mhariri Mkuu wa magazeti ya Serikali, watendaji wake walitakiwa kuhakikisha inatokea hata mara moja Mhariri Mkuu anatutembelea, hilo halijafanyika, tunamuona Mheshimiwa akitembelea Media nyingine lakini hapa ‘nyumbani’ kwake hafiki.

Nashauri ujumbe huu umfikie Rais kuwa hizi changamoto kadhaa nilizozitaja zinaathiri utendaji wa kazi wa watumishi hasa wa ngazi ya chini.

Naomba kuwasilisha.
 
Hatari hatari 4,000/=anaishi vipi huyo mtu?bora wale wa commercial news Kuna mshiko sasa hawa wa hard news hatari sana
 
Doh, Mara Mia kuwa chawa kama kina mwafulani, kuliko kujitumikisha kwa ujira wa elf 4
 
Si aje kua galagaja tu wa mbuzi sasa ,hakosi msapu wa 20k per day siku vikichanganya mpk 100k
 
Back
Top Bottom