BabaDesi, Pole sana; hizo ndio sheria za mafao ya PPF kama zinavyoelezwa ktk PPF Act, No. 14 ya 1978 na marekebisho yake ya 2001.
Lakini, scenario kama yako ilisababisha kurekebishwa kwa kifungu cha 26 na 44 cha sheria ya 1978 hapo mwaka 2001. Kama unadhani huitaji kusubiri kama inavyosema sheria ya PPF basi unalazimika kujitoa kwenye mfuko huo ambapo utarudishiwa michango yako yote na ile ya Mwajiri wako:
"44.-(1) Where a member ceases to be benefits employed in circumstances in which he is not eligible for any pension, gratuity or any other benefit under the provisions of this Act, he shall be refunded the amount of his own contributions and that of his employer to the Fund."
Kumbuka, kifungu kinacholazimisha mafao kutolipwa mpaka ufikishe miaka 55 kiliwekwa strategically kumfanya mhusika ambaye atakuwa amehacha/kuhachishwa kazi kabla ya retirement aendelee na mfuko huo pale anapoajiriwa sehemu nyingine. Kwahiyo inabidi uwathibitishie kwamba hujaajiriwa sehemu nyingine na wala hupokei mafao ya aina yoyote kama ilivyoelezwa kwenye marekebisho ya 2001 [9.(d)(b)] ya kifungu cha 26 cha sheria mama ya 1978.
Niishie hapa, wengine pia waweza kukupa ushauri mzuri zaidi na wenye manufaa. Dukuduku muhimu ambalo tunapaswa kuliangalia ni ufinyu wa fao la PPF. Jamani kwa wenye uzoefu tunaomba tusaidiane, fao analopata mstaafu wa PPF ni dogo sana, kuna umuhimu wa kujipanga ili kuomba mabadiliko kwenye hesabu zinazofanywa maana kuna walakini ukilinganisha na fao walipatalo wastaafu wa mifuko mingine.
Weekend njema!