911
Platinum Member
- Aug 22, 2008
- 852
- 499
Naam,leo ni 31/03/2011.Mwaka 2008 kulikuwa na mjadala ulikufa bila kujadiliwa kwa kina kuhusu wakurugenzi wa mfuko wa pension wa PPF waliojichotea takribani shilingi milioni 200 kila mmoja. Hali halisi ni hii hapa
1. HAO WALIOORODHESHWA MWAKA 2008 kwenye JF SIO WALIOJIGAWIA MILIONI 200. BALI NI WAKURUGENZI WA NDANI SIO BOARD MEMBERS ambao ni.Director of Finance, Chief Internal Auditor, Director of Computors, Director of Commercial Services, Director of Investiments, na Director of Pensions.
2. Mhasibu mkuu aliwagomea kulipa kwa kuwaambia sio haki yao kwa kuwa wao ni wa mkataba wanalipwa gratuity 25% ya mishahara yao kwa muda wote wa mkataba, wakamsimamisha kazi kwa vitisho vya kutaka kufukuza na kumhamisha idara. Toka June 2008 hadi March 2010 amehamishwa mara nne. Hivi sasa wamemtupa Mbeya asione madudu yao
3. Mafao waliyojilipa haikuwa stahili yao, kwani mafao hayo yapo kwa wafanyakazi wa kudumu tu pale wanapofikia umri wa kustaafu (55 years) na wawe wanaondoka kabisa PPF sio kama walivyofanya wao ambapo bado wanaendelea na kazi na karibu wote wana umri chini ya miaka 50.
4. Mwezi wa tatu 2011 wanamaliza mkataba mwingine watavuta kila mmoja karibu milioni 100 kama serikari ikiwaachia waibe tena.
5. Audit commettee ya bodi ya PPF walijua kuwa ni wizi, wakapelekwa Johanesberg kunyamazishwa.
6. Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikari alipigwa dongo la macho kusaini mahesabu ya 2008. Wakaguzi kutoka TAC walijaribu kuijia juu menejimenti ya PPF, lakini wakapewa vijisenti wakanyamaza kimya. Draft report yao tunayo ilionyesha wizi huo lakini ripoti ya mwisho haikuwekwa.
7. Mishahara kupanda kila mwaka kwa asilimia 25%.
Baada ya kuiweka bodi ya wadhamini mifukoni mwao, wamekuwa wakijiamulia mambo wenyewe. Wakurugenzi wana mishahara mikubwa, wakati walalahoi ndani ya mfuko huo huo wanasota. Kila mwaka wao hujiongezea kati shs. Milioni moja na nusu na mbili na nusu wakati wafanyakazi wadogo kuanzia mameneja kushuka wanaongezewa kati shilingi elfu kumi na elfu tisini tu. Usawa uko wapi? Waziri wa fedha anajua hili?
8. Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu aliitisha mkutano wa wafanyakazi akaruhusu maswali. Mfanyakazi mmoja alihoji kwa nini wakurugenzi wajiongezee mamilioni yote hayo wakati walalahoi wanapewa kiduchu? Aliulizia pia uizi walioufanya March 2008 wa kugawana shs.200m ambao wataurudia March 2011, kwa nini wapewe wakurugugenzi wasiostahili kabla ya umri wa kustaafu wa miaka 55? Masikini mzee wa watu, katibua hivi ninapoandika amesimamishwa kazi kwa kuhoji ufisadi wa wakurugenzi wa PPF.
9. NAOMBA PCCB, USALAMA WA TAIFA, SERIKARI-WIZARA YA FEDHA, UTUMISHI, WANAWAKE NA JINSIA WAINGIE PPF NA KUCHUNGUZA. WASIMWOGOPE DG KWA SABABU NI MTOTO WA MZEE MKAPA.
MALIPO HAYA NI NJE YA GRATUITY 25% TSHS 48M, NA PENSION 20% ZAIDI MILIONI 70
NAOMBA KUTOA HOJA