BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,150
Wazito PPF wachota 'vijisenti'
Mwandishi Wetu Mei 7, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
Walipwa kama wastaafu, kisha warudi kazini
WAKURUGENZI kadhaa wa Mfuko wa Pesheni ya Mashirika ya Umma (PPF), wamejilipa mamilioni ya fedha, ikiwa ni mafao yao ya kustaafu kazi, lakini imebainika kuwa wanaendelea na nyadhifa zao licha ya kujilipa.
Habari ambazo Raia Mwema imezipata wiki hii zinasema kuwa mafao ya wakurugenzi hao yanafikia kati ya Sh. milioni 130 na 220 kwa kila mmoja, kiwango ambacho kinafikia jumla ya Sh. bilioni 1.2, kilichotolewa na PPF kwa 'wastaafu' hao.
Raia Mwema imearifiwa kuwa malipo hayo yamefanyika kwa kufuata utaratibu uitwao Group Endowment Scheme, ambao unahusu mafao ya wafanyakazi yanayopaswa kutolewa kwa mtumishi anapostaafu kazi katika PPF.
Kwa mujibu wa habari hizo, chini ya mpango wa Group Endowment Scheme, wafanyakazi hukubaliana na mwajiri kabla ya kuanza kazi, ambapo shirika linakuwa linachangia kiasi fulani cha fedha kama akiba ya mfanyakazi, ambayo hupewa mara anapostaafu.
"Mnakubaliana wewe mfanyakazi na mwajiri. Ni kama mkataba wa aina fulani. Shirika linatoa fungu, linakuchangia…Unapoondoka kazini wakati unastaafu, unapewa fedha zako ili zikusaidie kwenye maisha yako mengine.
"Ukipewa fedha chini ya utaratibu wa Group Endowment Scheme, hatutarajii kuona mhusika anabaki kazini. Kama kuna watu wanafanya hivyo, basi wanauhujumu utaratibu huu," alisema Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa PPF, Naftali Nsemwa, ambaye aliombwa na Raia Mwema kutoa ufafanuzi wa jinsi mpango huo unavyofanya kazi.
Lakini Raia Mwema imeambiwa kwamba katika jambo ambalo linashangaza, wakurugenzi hao sita wa PPF wamejilipa mafao hayo ya Sh. bilioni 1.2, kwa maana ya kustaafu, lakini hadi jana Jumanne walikuwa wakiendelea na kazi, wakiwa tayari wameweka mafao yao vibindoni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Badru Msangi, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alikiri kuwapo kwa utaratibu wa Group Endowment Scheme, lakini akakataa kuzungumza zaidi kwa maelezo kuwa yeye si msemaji wa PPF, bali Mkurugenzi Mkuu mwenyewe, William Erio ambaye yuko safarini Afrika Kusini.
Hata baada ya kumsihi azungumze, Msangi alisema: "Msubiri Msemaji wa Shirika, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu. Atakuwepo ofisini wiki ijayo. Unapotaka sisi ndio tuzungumze, hututakii mema, unataka tufukuzwe kazi."
Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Gray Mgonja hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, na hata pale Raia Mwema ilipojaribu kuwasiliana naye, simu yake ilikuwa ikiita mfululizo na baadaye ikafungwa.
Raia Mwema ina majina ya wakurugenzi hao lakini kwa kuwa haikufanikiwa kuzungumza nao kuoata maelezo ya upande wao kwa sasa hawatatajwa.
Habari zaidi zilizopatikana zinasema kulipana huko kumehojiwa na mmoja wa wajumbe wa Bodi ya PPF, Monica Mbega akitaka kujua ni nani aliyeyaidhinisha.
Mbega alihoji suala hilo katika mkutano wa Jumamosi iliyopita wa timu ya ukaguzi ya Bodi ya PPF ambayo yeye ndiye Mwenyekiti wake. Yeye na Erio, na baadhi ya wakurugenzi ambao ni wajumbe wa timu hiyo, wako safarini Afrika Kusini.
Mikataba ya Group Endowment Scheme katika PPF imekuwa ikifanyika kila baada ya miaka mitatu, na mwenye kufaidika na mpango huo anapaswa kuwa awe anastaafu na kuondoka kabisa katika ajira ya PPF.