Waziri wa Michezo: Soka la Tanzania haliwezi kuendelea kama hatupingi rushwa

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe.Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania haiwezi kupiga hatua kwenye sekta ya michezo, iwapo itashindikana kuboresha miundombinu ya michezo, ujenzi wa viwanja vya kisasa, ujenzi wa academy pamoja na ujenzi wa vituo muhimu vya michezo.

"Rais wetu wa Awamu ya Sita yeye anaamini kwamba michezo ni ajira, na kwa namna ya kipekee kila Mtanzania anatambua kwamba.

“Eneo hili la michezo Watanzania walitamani waone tunapiga hatua na tunakwenda mbali.

"Anguko la soka hapa nchini litategemeana na wadau wa soka wenyewe mentality zao, tunaamini kila mmoja wetu akiwa mwadilifu kujituma na kupiga vita rushwa katika michezo, basi tunaweza kupiga hatua,"- Mohamed Mchengerwa.

Waziri wa Michezo.jpg

Source: East Afrika Radio
 
Soka halina pesa ndefu. wafenye kuwekeza badala ya kuwageuza vitenga uchumi
 
Na rushwa ilivyotamu sasa ukipinga wewe mwenzio hapingi..!
Nchi ngumu hii anaepinga anatembelea baby walker,asiepinga anatembelea range!.. hapo ndipo Bible husema amani ya bwana na iamue ndani yako..😂
 
Back
Top Bottom