Waziri wa Mambo ya Nje hajafanya jambo jipya, anafanya majukumu yaleyale. Tunahitaji ubunifu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kwa wale ambao wamekuwa wakitembelea Balozi zetu nje watabaini wazi kwamba muundo wa kiutumishi kwenye balozi zetu zote Duniani umejengwa kidiplomasia na tafsiri ya watendaji wa Wizara ni kwamba ukihudumu Wizara ya Mambo ya Nje basi wewe ni mwanadiplomasia na hivyo unaweza kuisaidia nchi kama mwakilishi ubalozini.

Kwa ngazi ya kiuchumi ya nchi yetu hatupaswi kujikita kupeleka timu ya wanaohitwa wanadiplomasia kwenye Balozi zetu bali tunapaswa kupeleka wataalamu wa fani mbalimbali walioelekezwa namna ya kuishi huko Ughaibuni.

Ni kawaida kwenda kwenye balozi zetu kuomba Huduma ukajibiwa Huduma hiyo haitolewi na ubalozi rudi nyumbani wakakusaidie.

Ni mara kadhaa unakutana na watu wasio na uwezo wakuchambua mambo ndio wamewekwa mapokezi ubalozini hasa nchi za Ulaya; unakosa ile ladha ya uwakilishi wa Kimataifa kwenye balozi.

Misingi hii yakuweka watu kwa sababu tu wapo wizarani au wamesoma chuo cha diplomasia ni kosa kubwa kiufundi na linaiguarimu nchi kiuchumi na kimahusiano.

Kwa maoni yangu, Mama Mulamula anayo exposure kubwa na tulitegemea kusikia amefanya reform zifuatazo.

1. Utoaji wa visa Kwa wageni pamoja taratibu nzima za wageni kuja Tanzania; Kama hakuna maafisa wenye dhamana nchini Katika kutoa visa na vibali kwenye balozi zetu tukamchukua mtu wa wizarani wakati kazi hii haifanywi na maafisa wa Wizara ya mambo ya nje tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu for years. Watendaji wengi wanaonekana wababaishaji hasa pale wageni wanapotaka kuja Tanzania Kwa utalii, matembezi au kufanya kazi. Maafisa waliopo kwenye balozi zetu wanapaswa kuwa watu waliosomea na wanaojua kiundani taratibu za kuishi na kufanya kazi nchini zipoje?

2. Diplomasia ya uchumi: Wapo watumishi Wizara ya fedha waliobobea kwenye masuala ya uchumi,wapo watu waliobobea kwenye masuala ya utalii , wapo watu waliobobea kwenye biashara siyo Kwa kufanya Bali Kwa kuzichambua sera na Sheria za nchi. Mama Mulamula tunategemea Kwa umaskini wetu Balozi zetu ziwe na wataalamu wa masuala ya kiuchumi wenye network ya Moja Kwa Moja na Wizara husika Ili wamsaidie Balozi kutafsir sera na mipango yetu ya uchumi huko ugenini na anapokutana na wadau au wawekezaji basi mtaalam atoe lecture sahihi kuwashawishi wajekuwekeza. Hii tabia ya kuwa na mabalozi ambao badala ya kushawishi watu waje KUTALII na kuwekeza tunamobilize watu wazungumze na mkuu wa nchi au Kiongozi wa kisiasa sidhani kama Ina tija. Wekeni Dawati Balozini linalozungumza lugha Moja na Wizara au Idara za Ndani.

3. Pasipoti na Uraia wa Watanzania: Wanadiaspora wengi wamekosa msaada Kwa sababu Balozi zetu hazina watu wa Idara ya Uhamiaji. Unafika ubalozini kuomba Huduma unapewa namba za afisa Uhamiaji huko nchini akupe ufafanuzi au akuelekeze kuhusu pasipoti au uraia. Kwanini tusipeleke maafisa Uhamiaji wawe na Dawati maalumu Kila Balozi watuhumie bila kututaka turejee nchini kufuatilia pasipoti au uraia pale tunapojaliwa watoto nje?

Je, tumewahi kujiuliza ni Watanzania wangapi wanateseka Ughaibuni Kwa kuogopa kurudi nchini Kwa sababu awana pasipoti na wanaogopa kukamatwa? Kwanini Mhe. Waziri usije na kampeni ya kuwashawishi Watanzania wajitokeze Balozini na wale waliopo detention center wakapatiwa Huduma tuwatoe vifungoni? If the challenge is staff, hao maafisa waliopo ubalozini wasio na taaluma za Huduma wanafanya kazi gani kama siyo kuipa gharama nchi?

4. Wataalamu wa Sheria na saikologia ; Leo kwenye balozi nyingi nchini Kuna kitengo Cha masuala ya saikologia na uokoaji wa watu kwenye utumikishwaji. Lini Serikali yetu itapeleka wataalum wa aina hii kwenye balozi zetu na kufungua milango ya Watanzania kuhudumiwa hasa wale wanaotumikishwa kwenye madanguro na kufanyishwa kazi ngumu bila kupewa haki zake stahiki na waajiri? Mtanzania akiwa Ulaya akafika ubalozini hakuna Cha ziada atakachosaidiwa Zaidi ya masimango na kejeli Kisha kuambiwa anaitia nchi aibu; Lakini tujiulize wazungu wangapi wanaranda mitaani na tunawasaidia na wakifika kwenye balozi zao wanapewa misaada? Changamoto hapa nadhani ni kupeleka Watanzania ubalozini wasiojua jukumu lao la msingi kwamba nikuwatetea Watanzania.

Uhuru wa Watanzania utapatikana pale ambapo Balozi zetu zitapambana kusimamia haki za Watanzania waliopo nje bila kujali Wana makosa au la. Kama Wana makosa basi tusimamie Sheria na wakishamaliza kutumikia adhabu tusimamie wapewe haki zao. Watanzania wanachuma huko nje mwisho kupitia majungu na fitna wanatengenezewa Kesi na kutiwa hatiani Kisha ubalozi bila kusimamia haki zao unasimamia repatriation. It's not fea at all, tujiulize wageni wanaokamatwa hapa nchini wakahukumiwa tunawafukuza wakaacha vitu walivyochuma? Kama tunawapa nafasi ya kuuza au kuandikishana na mtu Mali zao kwanini Watanzania waliopo nje wasipewe Huduma kama hizi? Tunahitaji msimamizi wa haki za wananchi wetu nje. Bora tutumie gharama Lakini tuwafanye watanzaia wajisikie wana watetezi wawapo nje.

Mhe. Mulamula dada yangu, hoja hizi nilizozitoa zikusaidie kufikiri upya namna ya kutengeneza muundo wa kiutumishi kwenye balozi zetu. Shirikiana na mabalozi wetu utalisaidia Taifa Zaidi ya unavyodhani. Diaspora wanatamani Balozi ziwe sehemu ya kukimbilia tuwasaidie.

Na nikuakikishie kwamba Watanzania wengi nje awahitaji msaada kama wanavyochukuliwa na maafisa ubalozi, na hata pale wanapohitaji msaada siyo lazima Serikali itoe pesa watu sahihi wakiwepo ubalozini watatenga muda kutembelea holding center na maeneo ya magereza kuwatoa Watanzania Kwa gharama za ndugu zao.

Mnapokwenda kwenye sensa natamani tujue Watanzania wangapi wapo nje Kwa mujibu wa sheria,wangapi wapo magerezani na makosa Yao,wangapi wanazuiliwa na kwanini wanazuiliwa,wangapi wanamitaji ya uwekezaji,wangapi wanataalumu ambazo nchini zinahitajika zaidi,wangapi wamepoteza Utanzania na wanatamani kuurudia, wangapi wamezaa watoto na awajui watoto wao ni raia au Wana haki Gani za Tanzania nk

Haya matakwimu yatakusaidia kuandaa bajeti nakuwasiadi wale wanaohitaji msaada. Amka Sasa ukaangaze, ubobezi wako usiwe tu kwenye networking na wageni Bali uwe chachu ya kushughulikia matatizo yetu wenye nchi tunaotafuta riziki nje.

Nimekuchokoza sista usimind chukua point niache pumba........umofia kwenu.
 
Yapo mengi mpya, Jana tarehe 22/03/2022 mida ya saa tatu Usiku Mh. Waziri Liberetha Mulamula ameyasema Mambo mengi kuhusu maendeleo ya Wizara ya Mambo ya nje, Majukumu ya wizara, fursa zilizopo kwenye wizara, mipango ya wizara, Uzalendo, misimamo mbali mbali ya wizara pamoja na Diplomasia.
Tatizo lilipo ni kwamba wananchi wengi hatuna elimu na wagumu kujifunza mambo mapya yanayohusu Nchi yetu. tembelea tovuti ya wizara ili kujifunza na kua updated kiachoendelea katika wizara husika.
asante sana.
 
Back
Top Bottom