GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,551
- 108,885
Yaani Waziri Masauni umeshakiri Mwenyewe kuwa Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani kwa Makusudi wameondoa 'Spidi Gavana' katika Mabasi ya hali inayopelekea Madereva Wao kwenda Mwendo Kasi na Kusababisha Maafa (Ajali) zinazoua Watanzania na kuwapa Ulemavu wa kudumu halafu Wewe unawapa 'Ultimatum' ya miezi Sita (6) Kurejesha hizo 'Spidi Gavana' badala ya kuwapa Siku Saba (7) tu zijazo.
Kwahiyo Waziri Masauni kwa Lugha nyepesi hapa ni kama vile Umeshatoa ruhusa ya Watanzania Kuuwawa (Kuuliwa) na Madereva wa Mabasi ya Mikoani kwa Miezi Sita (6) ijayo na baada ya hapo ndipo mtawaonea Huruma kwa kuanza Kuwajali kwa Ustawi wao wawapo Safarini.
Hivi nyie Mawaziri baadhi yenu Vichwani mwenu (hasa Kiakili) mpo sawa sawa kweli au labda mnahitaji Tiba ya haraka Hospitali za Mirembe (Dodoma) na Lutindi (Tanga) kutokana na Kauli zenu na Maamuzi yenu yasiyovumilika kutokana na kuwa ni ya 'Kiudhaifu' zaidi?
Kuna Waziri Mwenzako wa Maji Jumaa Aweso nae Wiki Mbili nyuma alimsifia kweli kweli Boss Mkuu wa DAWASA Cyprian Luhemeja mbele ya Rais Samia huko Chalinze huku akimnadi kuwa ndiyo Mfanyakazi Bora wa mwaka na Jana tu katika Ripoti ya CAG Taasisi yake imekutwa na 'Madudu' ya 'Ubadhirifu' ya karibia Tsh Milioni 800 kwa Kuwadhulumu Watanzania hasa katika Usomaji Hewa wa Mita zao za Maji huko Majumbani mwao.
Waziri Masauni labda nikuambie tu Wewe pamoja na Boss wako Mkuu na Watendaji Wenzako (hasa Mawaziri) kuwa Watanzania tunajitahidi mno Kumsahau Hayati Rais Dkt. Magufuli, ila kwa huu Upuuzi wenu, Maamuzi yenu na Utendaji wenu wa hovyo hovyo ndiyo mnatufanya Watanzania (akina GENTAMYCINE) kila mara tuwe si tunamkumbuka bali pia tumlilie sana Rais Hayati Dkt. Magufuli kutokana na Utendaji wake uliokuwa ni wa Kutukuka na wa Kishujaa zaidi.
Haya Madereva wa Mabasi ya Mikoani na Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani jitahidini sasa mtuue kwa Ajali za Mwendo Kasi kwani tayari Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni ameshawapeni ruhusa ya Miezi Sita (6) na hata wale ambao bado Mabasi yenu yana Spidi Gavana mlizofunga mnaweza sasa mkazing'oa tu ili mtuue kwa Mwendo Kasi ndani ya Miezi Sita (6) ijayo na baada ya hapo (mkishashiba Damu zetu na Viungo vyetu) mtazirejesha kama mlivyoagizwa na Waziri.
Halafu akina GENTAMYCINE na Watanzania wengine baadhi wanaojua Kufikiri na Kuona mbali (kwa Kubarikiwa na Mwenyezi Mungu) wakiwakosoa kwa nia ya Kuwajenga na kuwapeni Fursa ya Kujitathmini mnatuchukia, mnatuona ni Wapinzani, tunatumwa na Mabeberu, tuna Chuki Binafsi nanyi na mpaka mnatamani tupotee tu kabisa duniani.
Kwa wale mnaopenda kujua Maamuzi haya ya 'Kipuuzi' ya Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni nimeyasikia wapi ni kwamba nimeyasikia hivi punde tu kutoka katika Kipindi kizuri cha Nipashe kutoka Radio One ambapo Mtangazaji wa Zamu leo ( Alhamisi ) alikuwa ni Mtangazaji Mahiri na Makini Maulid Kambaya.