Waziri Masauni tupunguzie Traffic Polisi barabarani

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,695
2,553
Miaka ya 2010 World Bank walitoa ripoti ya kufanya biashara nchini Tanzania na kwa viwango vya wakati ule tulishika nafasi kama ya 121 kama sijakosea. Raisi wa wakati ule Mh. Jakaya hakuridhishwa na hiyo ranking na kuchukua hatua at least tufikie 2 digits yaani tuwe chini ya 100. Majirani zetu kama Kenya na Rwanda walituacha mbali mno katika mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Mh. Raisi aliunde task force kuhakikisha hatua zinachukuliwa haraka kuhakikisha mazingira ya Biashara yanakuwa bora Zaidi. Nakumbuka TPSF walishika hatamu katika kuratibu baadhi ya Task force uhsusan zile zilizokuwa zinawagusa wafanya biashara. Maarufu ni ile ya Trade Across Border ambayo iliangazia corridor ya kusini kwa maana barabara ya Dar – Tunduma na ile ya Kati Dar – Lusumo. Kiukweli kwa wakati ule hatua zilichukuliwa na One stop Border zilianzishwa, Mizani ya kisasa ikajengwa na Mzani wa Kibaha ukahamishwa Vigwaza na Zaidi kuondosha barriers Zaidi ya 52 kuelekea Lusumo.

Kwa masikitiko makubwa kabisa Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ndio walikuwa waratibu wa task force hii na kibaya Zaidi Waziri Mh. Masauni ndio aliyekuwa Mwenyekiti wa Task Force na alikuwa Naibu Waziri wakati ule sijui kwa makusudi au kwa bahati mbaya ameachia askari polisi kuongeza vituo barabarani tena Zaidi ya mara 10 ya vilivyokuwepo wakati ule. Inawezekana kabisa askari wake hawajui lolote kuhusu mazingira na kero za kufanya biashara nchini lakini yeye Mh. Waziri arejee makablasha yake na afanye Tathmini usumbufu unaoletwa na Jeshi la Polisi barabarani.

Usumbufu wao ni ule ule unaolalamikiwa miaka yote, kwanza kupotezea watu muda wa kusafiri na kufikisha mizigo kwa wateja, Pili kushawishi na kupokea rushwa, kubambikia madereva makosa na Zaidi ni kuipaka matope nchi yetu kwa kutoonyesha weledi kazini na Rushwa. Haina maana askari wasiwepo barabarani la hasha waweke vituo vya ukaguzi vichache na vinavyoratibiwa vizuri kama wenzetu wanavyofanya. Ili muda wa maroli na mabasi kukaa barabari upungue. Chukueni mfano Morogoro Road – ukimaliza kibamba tu unaanzia Gogoni wapo, kiluvya madukani wapo, kibaha maili moja wapo, Tanita, Miomboni, Visiga, Msufini, Ruvu, Vigwaza, Chalinze na Mwidu hii ni mkoa wa Pwani tu.

Kila palipo na kituo cha polisi basi lazima wakae na barabarani kuzui magari, na hapa hatujaweka wale wa Torch, wa kukusanya maokoto na waungwana wachache wanaokaa kwenye Zebra. Hivi hakuna namna tunaweza tuka mechanise au modernize kazi za hawa jamaa wakatuacha barabarani tusafiri kwa amani. Pamoja na wingi wote huu wa askari barabarani bado wazee wa busta (pikipiki zinazobeba mkaa zinapita mbele yao) wao ni kila Fuso, Truck lazima wasimaishe na kuuliza kama unacheti ukisema hauna wakupige cheti.

Mh. Waziri wa mambo ya Ndani tunakustua tazama tena jeshi la Polisi hasa wanaosimama barabarani, na ukumbuke Rushwa ni adui wa haki tunajua Takukuru hawanaga meno na wala hawaoni lakini sie wananchi, wafanyabiashara, madereva na wakulima tunaumia sana na mapungufu ya watendaji wa Jeshi la Polisi. Tunamkumbuka Hayati mwendazake sababu wakati wake huu uzembe hakuwa na nafasi sasa umerudi kwa kasi mno sijui wamewazoea nyie viongozi wao au wanawamudu??.

Mh. Waziri ikukupendeza kadurufu tena kuhusu Doing Business Road Map 2010 na Tasks Force alizounda Mh. Jakaya Kikwete na wenyewe mjitathmini na kama wakati ule tulikuwa 121 hivi leo tumeshika namba ngapi. Tunajua Bwana Simbeye hayuko TPSF leo lakini Kaacha makablasha yoyote huko watangulizi wake waanzie watizame na wapate pa kuanzia Vipi kuhusu TCCIA, na wadau wengine au wamemuachia Mungu au na hili tumtafute Bashite.
 
Police karibu wote hata mimi naona sijui wako barabrani, hivi barabarani ndio ulinzi mkubwa wa usalama wa raia na mali zao ulipo? Kwa hili la traffic police kujaa barabarani linahitaji kabisa Mh. Rais aingilie kati, maana kuna tatizo kubwa, haiwezekani mtu aendeshe gari kilometa 5 au 10 high way unakutana na police, sasa hiyo ni high way au Police way?

Tukisema ukweli, traffic police wamekuwa wengi mno mno, hili suala hata Mkuu wa nchi kipindi fulani alilisemea nakumbuka, kiuhalisia Traffic police tena barabarani wangekuwa wachache sana hasa highway, eg, mfano njia kuu ya Dar Moro, labda wawe Mbezi ya Magufuli, Kibaha, Mlandizi, Chalinze, Bwawani, Mikese na Morogoro tu..!! Ila hali ilivyo inatisha, kila kilometa 5 au 10 highway traffic unakutana nao..!! Sasa hiyo sio kabisa highway, biashara zitadumaa sana hasa za malori, maana ni kusimamisha magari kila kona..!!
 
Naunga mkono hoja. Askari wa usalama barabarani ikiwezekana waondolewe kabisa barabarani, na badala yake zibakie check points chache kwa ajili ya masuala ya kiusalama, na pia kuwepo na askari wachache wa doria kwa ajili ya tahadhari.

Mbadala wa askari wa barabarani ziwe ni camera za CCTV ambazo zitafungwa kwenye yale maeneo muhimu tu. Na hizo CCTV Camera zitarekodi matukio yote yanayotekea kwenye hayo maeneo husika.

Na ikitokea dereva amefanya makosa kwa kukiuka sheria za usalama barabarani, atasimamishwa kwenye check point, na utatatibu mwingine utafuatwa.

Kwa sasa kweli hali ni mbaya. Kila baada ya hatua chache unakutana na askari wa barabarani wakisimamisha magari, huku wakiulizia vitu vile vile! Na lengo hapo ni kutaka tu wapewe rushwa!

Wale wa tochi nao muda wote wanajificha vichakani ili kuvizia magari wayapige tochi, na baada ya hapo mazungumzo yafuate!! Yaani uchague kuwapa rushwa ya kuanzia elfu 5-10, au wakuandikie faini ya elfu 30!!
 
Police karibu wote hata mimi naona sijui wako barabrani, hivi barabarani ndio ulinzi mkubwa wa usalama wa raia na mali zao ulipo? Kwa hili la traffic police kujaa barabarani linahitaji kabisa Mh. Rais aingilie kati, maana kuna tatizo kubwa, haiwezekani mtu aendeshe gari kilometa 5 au 10 high way unakutana na police, sasa hiyo ni high way au Police way?

Tukisema ukweli, traffic police wamekuwa wengi mno mno, hili suala hata Mkuu wa nchi kipindi fulani alilisemea nakumbuka, kiuhalisia Traffic police tena barabarani wangekuwa wachache sana hasa highway, eg, mfano njia kuu ya Dar Moro, labda wawe Mbezi ya Magufuli, Kibaha, Mlandizi, Chalinze, Bwawani, Mikese na Morogoro tu..!! Ila hali ilivyo inatisha, kila kilometa 5 au 10 highway traffic unakutana nao..!! Sasa hiyo sio kabisa highway, biashara zitadumaa sana hasa za malori, maana ni kusimamisha magari kila kona..!!
Idadi ya traffic polisi inatakiwa kuongezeka ili wananchi waache ukondoo
 
Kuna wakati mwaka jana mzee Kinana alisema hili, baada ya hapo wakapungua.

Hata sticker za usalama barabarani ziondolowe, zinatolewa bila gari kukaguliwa. Alafu sticker 5,000 traffic police akikuta huna faini 30K
 
Nashauri wapewe baadhi ya garage leseni ya kufanya ukaguzi wa magari kwa ufanisi bila hongo
Na certificate zitolewe kwa wenye magari yaliyopasi kuangaliwa kama hayana dosari yoyote

Kila miezi 6 zikakaguliwe na garage ziwepo mikoa na wilaya zote kwa dhamana ya serikali
Kama tairi mbovu hakuna kuendesha mpaka litengenezwe na cheti hapati

Hii itapunguza sana rushwa za barabarani kwani hao wapo kula tu na sio kuangalia usalama wa magari
Magari yanauwa kila leo na sababu ni zile zile kutoka kwa Polisi ooh imekata brake
Sasa gari halina mafuta ya breki unategemea nini?
Mara ooh gari limeacha njia kwanini? Matairi yameisha kabisa na unakuta mwenye mali anajua ila anasema watoe kidogo ntakupa ukija
Akiuwa watu kumi mnasema matajiri wanatoa kafara kumbe dereva kaachiwa kajaza watu na matairi yameisha kabisa

Dawa ni kuwapa baadhi ya garage nguvu ya kutokuwapa vyeti

Hii wataondoka wenyewe barabarani au kupunguzwa sana
 
Miaka ya 2010 World Bank walitoa ripoti ya kufanya biashara nchini Tanzania na kwa viwango vya wakati ule tulishika nafasi kama ya 121 kama sijakosea. Raisi wa wakati ule Mh. Jakaya hakuridhishwa na hiyo ranking na kuchukua hatua at least tufikie 2 digits yaani tuwe chini ya 100. Majirani zetu kama Kenya na Rwanda walituacha mbali mno katika mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Mh. Raisi aliunde task force kuhakikisha hatua zinachukuliwa haraka kuhakikisha mazingira ya Biashara yanakuwa bora Zaidi. Nakumbuka TPSF walishika hatamu katika kuratibu baadhi ya Task force uhsusan zile zilizokuwa zinawagusa wafanya biashara. Maarufu ni ile ya Trade Across Border ambayo iliangazia corridor ya kusini kwa maana barabara ya Dar – Tunduma na ile ya Kati Dar – Lusumo. Kiukweli kwa wakati ule hatua zilichukuliwa na One stop Border zilianzishwa, Mizani ya kisasa ikajengwa na Mzani wa Kibaha ukahamishwa Vigwaza na Zaidi kuondosha barriers Zaidi ya 52 kuelekea Lusumo.

Kwa masikitiko makubwa kabisa Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ndio walikuwa waratibu wa task force hii na kibaya Zaidi Waziri Mh. Masauni ndio aliyekuwa Mwenyekiti wa Task Force na alikuwa Naibu Waziri wakati ule sijui kwa makusudi au kwa bahati mbaya ameachia askari polisi kuongeza vituo barabarani tena Zaidi ya mara 10 ya vilivyokuwepo wakati ule. Inawezekana kabisa askari wake hawajui lolote kuhusu mazingira na kero za kufanya biashara nchini lakini yeye Mh. Waziri arejee makablasha yake na afanye Tathmini usumbufu unaoletwa na Jeshi la Polisi barabarani.

Usumbufu wao ni ule ule unaolalamikiwa miaka yote, kwanza kupotezea watu muda wa kusafiri na kufikisha mizigo kwa wateja, Pili kushawishi na kupokea rushwa, kubambikia madereva makosa na Zaidi ni kuipaka matope nchi yetu kwa kutoonyesha weledi kazini na Rushwa. Haina maana askari wasiwepo barabarani la hasha waweke vituo vya ukaguzi vichache na vinavyoratibiwa vizuri kama wenzetu wanavyofanya. Ili muda wa maroli na mabasi kukaa barabari upungue. Chukueni mfano Morogoro Road – ukimaliza kibamba tu unaanzia Gogoni wapo, kiluvya madukani wapo, kibaha maili moja wapo, Tanita, Miomboni, Visiga, Msufini, Ruvu, Vigwaza, Chalinze na Mwidu hii ni mkoa wa Pwani tu.

Kila palipo na kituo cha polisi basi lazima wakae na barabarani kuzui magari, na hapa hatujaweka wale wa Torch, wa kukusanya maokoto na waungwana wachache wanaokaa kwenye Zebra. Hivi hakuna namna tunaweza tuka mechanise au modernize kazi za hawa jamaa wakatuacha barabarani tusafiri kwa amani. Pamoja na wingi wote huu wa askari barabarani bado wazee wa busta (pikipiki zinazobeba mkaa zinapita mbele yao) wao ni kila Fuso, Truck lazima wasimaishe na kuuliza kama unacheti ukisema hauna wakupige cheti.

Mh. Waziri wa mambo ya Ndani tunakustua tazama tena jeshi la Polisi hasa wanaosimama barabarani, na ukumbuke Rushwa ni adui wa haki tunajua Takukuru hawanaga meno na wala hawaoni lakini sie wananchi, wafanyabiashara, madereva na wakulima tunaumia sana na mapungufu ya watendaji wa Jeshi la Polisi. Tunamkumbuka Hayati mwendazake sababu wakati wake huu uzembe hakuwa na nafasi sasa umerudi kwa kasi mno sijui wamewazoea nyie viongozi wao au wanawamudu??.

Mh. Waziri ikukupendeza kadurufu tena kuhusu Doing Business Road Map 2010 na Tasks Force alizounda Mh. Jakaya Kikwete na wenyewe mjitathmini na kama wakati ule tulikuwa 121 hivi leo tumeshika namba ngapi. Tunajua Bwana Simbeye hayuko TPSF leo lakini Kaacha makablasha yoyote huko watangulizi wake waanzie watizame na wapate pa kuanzia Vipi kuhusu TCCIA, na wadau wengine au wamemuachia Mungu au na hili tumtafute Bashite.
We utakuwa ni muhalifu tu.
 
Back
Top Bottom