Waziri wa Maji ni uoga, unafiki na kujipendekeza Meatu suluhu ya maji

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,610
13,164
TBC habari saa tano usiku 19 Nov, Waziri wa maji Mbarawa ametoa tamko kwamba ameagizwa na Mh.Rais JPM visima 10 kwa dharula, kukabiliana na maji huko Mwanuzi Meatu.

Jamani mawaziri hamjiamini bila kumtaja JPM? Kwamba Rais ameridhia tuchimbe visima 10 na mtandao wa maji kwa haraka!?

Kweli hata maamuzi visima 10 mpaka ridhaa na hisani Rais!? Kwa dona katry!?
 
Huyu ndio profesa alisoma akaelewa hana blabla kama za vichwa maji wa ukawa wachumia tumbo

Kwa sasa watanzania 89% wanapata maji kabla ya 2020 nchi zima maji ni 100% hii ni ushindi dhidi ya wahaini ukawa wasiolitakia mema taifa hili

State agent
 
TBC habari saa tano usiku 19 Nov, Waziri wa maji Mbarawa ametoa tamko kwamba ameagizwa na Mh.Rais JPM visima 10 kwa dharula ,kukabiliana na maji huko Mwanuzi Meatu.
Jamani mawaziri hamjiamini bila kumtaja JPM!? Kwamba Rais ameridhia tuchimbe visima 10 na mtandao wa maji kwa haraka!?
Kweli hata maamuzi visima 10 mpaka ridhaa na hisani Rais!? Kwa dona katry!?
Hivi hii wizara ni miongoni mwa mambo ya muungano ?
 
Kuchimba visima ni matatuzi ya muda mfupi ya matatizo ya maji. Haya yanafanywa kisiasa zaidi. Matatizo ya maji yanatatuliwa kwa kuweka reservoirs za kudumu na kutandaza mabomba ya maji kuwafikia wananchi.
 
Huyu ndio profesa alisoma akaelewa hana blabla kama za vichwa maji wa ukawa wachumia tumbo

Kwa sasa watanzania 89% wanapata maji kabla ya 2020 nchi zima maji ni 100% hii ni ushindi dhidi ya wahaini ukawa wasiolitakia mema taifa hili

State agent
Mkuu wakati mwingine huwa nakubali hoja zako lakini wakati mwingine nakataa, Tanzania watu wenye uwezo wa kupata maji angalau kwa asilimia kubwa ni watu waliko mijini, huku vijiji bado tunategemea kudra za Mwenyezi Mungu, tunakunywa maji sehemu moja na mifugo, wakati mwingine hata hizo sehemu za kunywa maji sehemu moja na mifugo hatupati.

Ukitaka kutoa takwaimu sahihi unapaswa ilifahamu Taifa lako vyema, msiishie mijini tu na kuamini kuwa watu wote wako hivyo....ni vijiji/vitongoj/kaya chache zinazopata maji ya uhakika huku vijijini. Wizara ya Maji yenyewe inashughulika na maeneo muhimu tu, haitofautiana sana na Tanesco na REA.

Kuna mdau aliwahi kumuuliza Prof, Kitila kuwa wewe ni katibu mkuu wa maji kwa Taifa zima au kwa Dar es Salaam peke yake? Prof nadhani mpaka sasa hajajibu hili swali.

Sasa na wewe nakuuliza unisaidie kunielimisha, hiyo 89% ni watanzania wa mijini, wa vijijini au Watanzania wote? . Je, hiyo 100% unayokadria kufikiwa ifikapo 2020 unamaanisha nini?
 
Tunaelekea kwenye msimu mgumu sana kwa WanaSiasa..... Wakati huyu akipanga mipango ya kuuza sera kwa wananchi mwingine anapangua mipango kwa kutekeleza. Ila yote kwa yote kabla ya kumtetea mwananchi kila mmoja anaanza kwa kutetea ugali wake 😎😎😎
 
Huyu ndio profesa alisoma akaelewa hana blabla kama za vichwa maji wa ukawa wachumia tumbo

Kwa sasa watanzania 89% wanapata maji kabla ya 2020 nchi zima maji ni 100% hii ni ushindi dhidi ya wahaini ukawa wasiolitakia mema taifa hili

State agent
Maji yanayopatikana kwa asilimia 89 yako nchi gani? Mbona mnapenda kupikapika takwimu hata kwa mambo yanaoonekana wazi? Mpka vinachimbwa visima vya dharura, hapo kulikuwa na 89%?
 
Huyu ndio profesa alisoma akaelewa hana blabla kama za vichwa maji wa ukawa wachumia tumbo

Kwa sasa watanzania 89% wanapata maji kabla ya 2020 nchi zima maji ni 100% hii ni ushindi dhidi ya wahaini ukawa wasiolitakia mema taifa hili

State agent
Labda kama mtahesabu hata mikojo ni maji
 
Black Mirror,
Hoja yako naikubali.

Na hapa nitamke waziwazi kuwa Prof. Makame Mbarawa ni mtu sahihi kwa Wizara hii ambayo 'Watanganyika' wasomi wa Uhandisi wa Maji waliigeuza kichaka cha kuibia pesa badala ya kujenga miundobinu ya maji.

Hoja ya maji kupatikana kwa asilimia 89, ni hoja potofu.

Vijiji vyenye miundombimu ya maji ya bomba havifiki asilimia 50, na ndani ya hivyo vyenye mabomba, upatikanaji wa maji ni chini ya asilimia 30!

Prof. Mbarawa aendeleze juhudi zake ili Watanganyika tupate maji.

Prof. Mbarawa is a top performer.
 
Kuchimba visima ni matatuzi ya muda mfululizo ya matatizo ya maji. Haya yanafanywa kisiasa zaidi. Matatizo ya maji yanatatuliwa kwa kuweka reservoirs za kudumu na kutandaza mabomba ya maji kuwafikia wananchi.
Hill linafanyika sasa, lakini mambo yanakwenda hatua kwa hatua.
 
Miongoni mwa maprofesor wachache sana wenye kufanya kazi kwa weledi na kuskiza watu(Rejea mkutano na wanachi wa mikumi na mbunge wao Prof J)

Wizara hii ni ngumu maana inagusa na kuhakisi maisha ya kila siku ya binadamu.

Maji ni uhai,pambana maprofesor kwa mipango ya muda mrefu huku ukiwezesha ya mud mfupi ili watu wapate maji maana miradi mikubwa huchukua muda mrefu kidogo so huku tukisubiri basi lazima ziatikane jitihada kama hizi za uwezeshaji wa visima n.k
 
TBC habari saa tano usiku 19 Nov, Waziri wa maji Mbarawa ametoa tamko kwamba ameagizwa na Mh.Rais JPM visima 10 kwa dharula ,kukabiliana na maji huko Mwanuzi Meatu.
Jamani mawaziri hamjiamini bila kumtaja JPM!? Kwamba Rais ameridhia tuchimbe visima 10 na mtandao wa maji kwa haraka!?
Kweli hata maamuzi visima 10 mpaka ridhaa na hisani Rais!? Kwa dona katry!?
Hujafuatilia hili swala. Kati ya jumamosi au jumapili ilirushwa Taarifa ya ukosefu wa maji kiasi cha kuwa wanasambaziwa na maboza.
Jana waziri kaagizwa kudhukuwa hatua za Dharura. Hili si mpango wa wizara hivyo anakila sababu ya kumtaja aliyeasisi wazo hilo ndio uungwana.
 
Miongoni mwa maprofesor wachache sana wenye kufanya kazi kwa weledi na kuskiza watu(Rejea mkutano na wanachi wa mikumi na mbunge wao Prof J)
Wizara hii ni ngumu maana inagusa na kuhakisi maisha ya kila siku ya binadamu.
Maji ni uhai,pambana maprofesor kwa mipango ya muda mrefu huku ukiwezesha ya mud mfupi ili watu wapate maji maana miradi mikubwa huchukua muda mrefu kidogo so huku tukisubiri basi lazima ziatikane jitihada kama hizi za uwezeshaji wa visima n.k
Usimpake mafuta kwa mgongo wa chupa.

Wizara imemshinda hii.

Fedha za miradi zinaliwa na watendaji wa Wizara na fedha hazifiki kwenye miradi.
Katikati ya wizara vile vile kuna katibu mkuu profesa asiyejua maji yanatokaje kwenye bomba.

Kampeni yake ya kusimamia makandarasi moja kwa moja toka ofisini mwake imebuma maana inaelekea hata princioles za project management hana idea nazo.

Pengine nayo wizara iendeshe miradi ya maji kwa Force Account.
 
Back
Top Bottom