Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,161
- 1,493
Waziri WyEST, yawezekana kanuni, taratibu na mifumo ya mitihani yetu ya Kitaifa haiwezi kufanya mtu aliyepata matatizo akapa namna nyingine ya kufanya kwa wakati hayupo sawa kuifanya mitihani hiyo.
Kuna mtoto anaitwa Careen Mathew Metili anayesoma Shule ya Secondary Mwika mkoani Kilimanjaro amefiwa na ndugu zake Wanne kwa ajali ya gari akiwepo mama yake mzazi.
Huyu mtoto amezika ndugu zake jana , leo amerudi Shule kwa ajili ya kesho tarehe 02.05.2023 kuanza mitihani yake ya kumaliza kidato cha sita.
Mheshimiwa Waziri WyEST, Huyu mtoto lwa sasa anahitaji msaada wa kisaikolojia ili aweze kuwa sawa, didhani kama anatakiwa kwenda kufanya mitihani, kwa namna yeyote huyu mtoto hayuko sawa na hatakuwa sawa ndani ya siku mbili hizi.
Pengine kupitia tukio la mtoto huyu tuangalie namna ya kurekebisha Kanuni za mitihani ya Kitaifa ili kumpa mtu Uhuru anapopitia mamabo magumu kama ya huyu mtoto.
Mh Waziri, huwezi kuzika ndugu wa nne na kesho ukaendelee na majukumu ya kawaida. Tumsaidie huyu mtoto kumpa watu watakao msaidia badala ya kumpa mitihani.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu Mbariki Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.