Tujadili kama Taifa: Watoto wamefutiwa mitihani. Je Serikali iwe na plan B?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,755
Waziri wa Elimu mhe. Adolf Nkenda amesimamia maamuzi ya Baraza la Mitihani la Taifa kuhusu uamuzi wa kufuta matokeo ya baadhi ya wanafunzi ambao wamegundulika kufanya wizi wa mitihani yao ya Taifa.

Amewaomba Wabunge waunge mkono msimamo wa Baraza kwenye uamuzi huo. Na bahati mbaya sana kwa wabunhe wetu wamekosa hoja kwa umoja wao kuitaka serikali itoe plan B kwa waliofutiwa mitihani kwa sababu kuwaondoa kwenye mfumo wa elimu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa ni sawa na kuwanyima haki ya kuishi kama watanzania wengine.

Leo jamii inahangaika kwa kila familia kubeba mzigo wa watoto wao wanaoahindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufeli, utoro, mimba na hili la kuondolewa sifa ya kuelimika.
Serikali isiyojali wananchi wake huwa na kawaida ya kuwatengenezea sababu za kuwakwamisha kufikia malebgo yao. Kwa mfano, shule ambazo wanafunzi hao wanatoka zimekwepa kuadhibiwa kama vituo vya mitihani ilihali inajulikana kuwa kila shule ina serikali ya wanafunzi na ofisi za nidhamu ambazo kwa sehemu kubwa zinahusika na ulinzj na usalama wa shule, kanuni na mwenendo wa wanafunzi wawapo shuleni. Hapa mwenye akili afahamu.

Tukija kwenye hili la kufuta matokeo.
Waziri anasimama kwa kujiamini na ufahari kuutangazia umma namna serikali inavyojisikia vyema na haki kuwafutia matokeo watoto ambao wamebainika kushiriki wizi wa mitihani. Mimi binafsi ninaungana na jamii kukemea wizi na udanganyifu kwenye mitihani. Lakini kama mzazi. Kama kiongozi naangalia anguko la kesho la jamii endapo tutakuwa na wimbi kubwa la raia ambao ni illiterate. Ninapendekeza serikali iweke umuhimu wa kuangalia namna ya kushughulika na wimbi la wizi wa mitihani.

Ukiniukiza nini kifanyike ninashauri kwamba, wanafunzi wote waliofutiwa mitihani kwa sababu za wizi wanapaswa kulipia upya ada za mitihani na watarudia kufanya mtihani wa taifa unaofuata yaani wwtarudi kwenye shule zao na kufuata taratibu za kufanya mitihani lakini muda wote wa kusubiria mitihani watakuwa nyumbani au tuisheni za mitaani. Lengo ni kuwafanya wajutie na kuona aibu ya kurudia kosa walilolifanya.

Serikali pia iangalie namna ya kuwarejesha kwenye mstari wa elimu wanafunzi ambao wamekosa alama za kuendelea ngazi zinazofuata za elimu. Yaani ianzishwe mamlaka itakayosimamia mtaala maalumu wa mafunzokazi kwa wanafunzi hawa ili wakifaulu muhula wa miaka 2 waweze kukubaliwa kujiunga elimu ya diploma na hata digrii huko mbele.

Mfumo huu utassidia sana kuibua wabunifu na wanataaluma wabobezi kww sababu siyo wote waliofeli hawana uwezo darasani bali kuna memgi yanajiri kipindi cha kufanya mitihani.

Ninamshauri Prof Adolf, asiendelee kusimamia mfumo kandamizi wa elimu bali kwa taaluma yake ya uprofesa aje na ubunifu namna ya kulikabili tatizo badala ya kuishi nalo kama inavyofanyika sasa.

Ninapoona mtoto wa jirani yangu amefeli au amefukuzwa shule au amefutiwa mtihani sijisikii vizuri kama mzazi. Nawaza endapo atakosa elimu, halafu baadaye akaja kuwa kiongozi sijui itakuwaje kama taifa na jamii.

Seriaki ibebe mzigo wa hawa vijana badala ya kuwaachia wazazi na jamii kisha baadaye kuja kuwashughulikia kama wahalifu pale wanapoona hawana cha kupoteza.

Wanafunzi hawa ni wenetu. Ni wa Taifa kwa jumla.
 
Wanaruhusiwa kurudia mwaka. Wasome tena mwaka mmoja kwenye shule nyingine sio mbaya.
 
Waliokosa vigezo vya kuendelea na elimu muunganiko kutokea daraja alilopo...kuna shule za VETA zina fani zote..zipo veta nyingi, zipo nafasi za Reseaters, labda useme zitangazwe kwa nguvu na bunge ila zinatangazwa sana kwenye magazeti na TV, hivyo chances zote unazotamani,ulizotaja na ambazo hujataja zipo serikali ilishaziweka, ni namna ya walengwa kuzijua na kuzitumia..ila zipo.
 
Ninakushangaa mtoa hoja!
Waziri kaeleza kinagaubaga na nimemwelewa na maelezo yake yamejitoshekeza.

Mimi mtenda jinai yeyote huwa sisimami upande wake.

Mwanzo tulidhani watoto wameonelewa, kumbe walikwiba mtihani!

Hili jambo lina mnyororo wake mrefu unaogusa mpaka wazazi.

WaTz tumezoea sana rushwa na ufisadi kuanzia umri wa chekechea!

Eti kufutiwa mtihani ni kunyimwa haki ambayo ni sawa na haki ya kuishi!

Kauli hizi zimenikera mpaka nimeshindwa kuendelea kusoma!

Upo serious kweli wee baba!

Yaani ufisadi tunaoupigia kelele ukomeshwe na watu waishi kwa staha, wewe unaunga mkono na kutukuza vitendo hivyo viovu!

Panga lililofyeka vyeti feki, ndiyo lililofyeka na hao wanafunzi vihiyo.

Serikali imetimiza wajibu wake na imetenda haki.

Viva waziri wa elimu!
 
Ninakushangaa mtoa hoja!
Waziri kaeleza kinagaubaga na nimemwelewa na maelezo yake yamejitoshekeza.

Mimi mtenda jinai yeyote huwa sisimami upande wake.

Mwanzo tulidhani watoto wameonelewa, kumbe walikwiba mtihani!

Hili jambo lina mnyororo wake mrefu unaogusa mpaka wazazi.

WaTz tumezoea sana rushwa na ufisadi kuanzia umri wa chekechea!

Eti kufutiwa mtihani ni kunyimwa haki ambayo ni sawa na haki ya kuishi!

Kauli hizi zimenikera mpaka nimeshindwa kuendelea kusoma!

Upo serious kweli wee baba!

Yaani ufisadi tunaoupigia kelele ukomeshwe na watu waishi kwa staha, wewe unaunga mkono na kutukuza vitendo hivyo viovu!

Panga lililofyeka vyeti feki, ndiyo lililofyeka na hao wanafunzi vihiyo.

Serikali imetimiza wajibu wake na imetenda haki.

Viva waziri wa elimu!
Mtihani kuibiwa ni organized crime.
Unapomuadhibu mtoto ambaye hajaweza kuvunja na kuiba mtihani huku wahusika wengine wakiachwa ni namna ya kuonesha how biased watoa maamuzi walivyo.

Hqpakuwepo na tukio la kuvunja na kuiba bali walifanikiwa kuiba mtihani

Pia ukiangalia sana masuala ya kisheria kuna eneo linapaswa kutumia reasonable thinking.

Wewe unachokisimamia sijapingana nacho bali nasema kesho hawa watoto wanapogeuka kuwa panyaroad ujue msingi wake umeanzia kwenye misimamo yenu ambao mnajivika uungu dhidi ya wengine ilihali kila mara mnatubu madhambi yenu mkimuomba Mungu awasamehe bila nyie kuwasamehe wengine
 
Sheria ichukue mkondo wake

Lakini shule husika zipewe adhabu...

Mfano wa adhabu ambazo ni Bora kuwapa baada ya matokeo kufutwa ni hizi.....

1. Watoto wasome shule ile ile Bure mwaka ambao wanarudia mtihani.

2. Gharama za mitihani ya Taifa Kwa shule zinazotakiwa kulipa, iwe ni gharama ya shule husika.

Kwa mtindo huu adhabu itakuwa pande zote mbili, watoto watapoteza mwaka mwingine kurudia darasa na shule itaingia gharama kubwa ya kubeba majukumu ambayo wazazi walishamalizana nayo.

Kutokana na Hilo, watoto wakipewa majibu siku nyingine watajua kitachofuata ni kupoteza mwaka, shule nayo itafahamu kuwa wakigundulika wanajiingiza kwenye gharama kubwa Kwa upumbavu wao. Hivyo pande zote zitasimama kwenye mstari hata kama udanganyifu utakuwepo basi ni Kwa kiasi.
 
Nilidhani ungeshauri hatua zisiishie kwa watoto ila zipande zaidi kwa wahusika wote.

Haujisikii vibaya kutetea wizi wa mitihani mkuu? Najua umejidai kusema kuwa huungi mkono wizi huu ila kweli anaekamatwa kuiba unataka apewe plan B? Seriously?

Hebu Watanzania tujifunze kuwa accountable na matendo yetu. Au wewe unahisi Hao watoto hawana mchango katika huo wizi? Hawa watoto lazima jamii isimame kuwajenga wawe wakweli na waaminifu. Mtoto anaposhiriki kuiba mtihani na unamkamata unampa eti plan B unategemea akiwa mkubwa utamwambia wizi wa mtihani ni mbaya? Unategemea utamwambia rushwa ni mbaya? Unategemea utamwambia ufisadi ni mbaya?

Wacha hatua zichukuliwe tujengee jamii yenye maadili. Hawa watoto walikuwa na mchango wa kuripoti walipopewa majibu kabla ya mtihani, walifanya hivyo?

Pendekeza hatua zaidi. Hao watoto waulizwe walipewa na Nani mitihani Kisha hatua kali zichukuliwe. Jamii lazima iwe na Woga juu ya matendo mabaya.
 
Back
Top Bottom