Waziri wa Elimu na Waziri wa TAMISEMI liangalieni hili ni tatizo

Big Eagle

JF-Expert Member
May 3, 2020
592
625
Baadhi ya shule za private wanawasumbua wazazi dakika za mwisho mwisho

Mtoto anasoma kidato cha kwanza - cha tatu anapoingia kidato cha nne akipata div two au three anaitwa mzazi anaambiwa amuhamishe mtoto sababu inasemekana shule inataka division one tu ili iweze kuongoza kwenye matokeo ya kidato cha nne.

Ili tatizo ni kubwa na malalamiko yapo kwa maafisa elimu wa mikoa. Mzazi anapata usumbufu wa kutafuta shule nyingine ili mtoto apate kufanya mtihani wa kidato cha nne.

Pili gharama za kuanza maandalizi mapya. Mtoto nae anaathirika kisaikolojia yaweza kumfanya akafanya vibaya kabisa katika mtihani wa kidato cha nne.

Ombi langu iwe ni marufuku kufukuza mtoto kwa sababu za ufaulu.
 
Sekta ya elimu hapa TZ ina hitaji kuangaliwa kwa umakini mkubwa sana tena sana. Watu hawapendi kusikia ukweli lakini binafsi sina namna lazima niseme ukweli tu. Wizara ya elimu ni tatizo kubwa sana pamoja na taasisi zake. Ipo haja ya serikali hii mpya kufumua hii wizara na kuleta damu mpya kabisa.

Sanjari na hilo bado TAMISEMI napo kuna shida kubwa tu tuanakalia matamko bila utekelezaji. Jafo will remain the only mistinister who performed better under this ministry. Mheshimiwa Rais ikimpendeza atizame vizuri pia hii TAMISEMI kwa kina akianzia juu hadi kwa makatibu wakuu na wakurugenzi.
 
Kabisa, kwa nini shule isiwajibike kwa huyo mtoto kupata Div 2 wakati wao wamelipwa kwa ajili ya kumfundisha apate hiyo Div 1?

On another note, hivi ni mimi tu ninayeona Ndalichako ni amepwaya kwenye hii wizara? Akiondoka ataacha legacy gani? Pengine alibanwa na maelekezo ya aliyekuwa bosi wake. Nasubiri kuona utendaji wake kipindi hiki ambacho kiongozi ni msikivu.
 
Huyu mama ni tatizo. Wizara hii inahitaji kusukwa upya kabisa
 
Kaz Sana hyo imetukuta Jana shule x huko bagamoyo yenye jina kubwa tu nilienda kumuwakilisha bro kwenye kikao nimekuta dogo kapata div 1=15 wanasema tumuhamishe Kwan wao wanahtaj kuanzia div 1=12 kurud nyuma bro kaniambia hatamwamisha atamuacha hapo dogo yupo form 3

Afanye Kama yule jamaa wa kagera anashule 2ndani ya eneo moja Kuna KEMEBOS na KAIZIREGE kwa hyo ukizingua shule ya kimkakati ambayo inampa jina KEMEBOS anakuhamishia KAIZIREGE humohumo japo nayo s haba pia inafanya vizuri
 
Ni usumbufu sana kwa wazazi na watoto
 
Sekta ya elimu hapa TZ ina hitaji kuangaliwa kwa umakini mkubwa sana tena sana. Watu hawapendi kusikia ukweli lakini binafsi sina namna lazima niseme ukweli tu. Wizara ya elimu ni tatizo kubwa sana pamoja na taasisi zake. Ipo haja ya serikali hii mpya kufumua hii wizara na kuleta damu mpya kabisa.

Sanjari na hilo bado TAMISEMI napo kuna shida kubwa tu tuanakalia matamko bila utekelezaji. Jafo will remain the only mistinister who performed better under this ministry. Mheshimiwa Rais ikimpendeza atizame vizuri pia hii TAMISEMI kwa kina akianzia juu hadi kwa makatibu wakuu na wakurugenzi.
Wewe Jaffo kashughulikie mazingira na muungano.Huiwezi TAMISEMI wewe.
 
Hata shule yangu SITAKI ujinga kabisa.
Shule binafsi tukiendekeza ufaulu wa chini tutakosa wanafunzi.
Huu ndio ukweli ndugu zangu.
 
Kabisa, kwa nini shule isiwajibike kwa huyo mtoto kupata Div 2 wakati wao wamelipwa kwa ajili ya kumfundisha apate hiyo Div 1?

On another note, hivi ni mimi tu ninayeona Ndalichako ni amepwaya kwenye hii wizara? Akiondoka ataacha legacy gani? Pengine alibanwa na maelekezo ya aliyekuwa bosi wake. Nasubiri kuona utendaji wake kipindi hiki ambacho kiongozi ni msikivu.
juzi hapa alipiga boko moja hivi matata sana; ajabu ni kuwa philipo mulugo ndiye aliyekuja kujibu na kupangua hoja zake mpaka ikaonekana mulugo yuko smarter. nilishangaa na kusikitikakweli................yaani mulugo huyu leo anamzidi maarifa ya kijanja WAZIRI?!!!!!
 
Lile katazo lake halikuwa na manufaa na watoto wanaosoma katika hali ya chini zaidi maana ukisema wawe free utaumi bure tu kwa wewe mzazi wa motto na si vinginevyo!!!! Yaani Elimu itolewe kwa moyo mmoja na sio kwa kinyongo na wazazi wawe wanahudhuria vikao vya shule na sio kulalamika tu huku hawashiriiki maanake ndio hiyo ya kuilaumu serikali!!! Na waziri hachambuagi yaani yeye akiletewa chochote anaona ni sahihi kabisa
 
Kuna hizi shule za seminary nazo sasa hiv hazitaki mtoto a some science ukipata below 60% physics na chemistry wanakuachisha unabaki na kuwa pure arts

Lengo kuu ni kurudisha heshima ya shule zao sababu watoto wengi wakisoma science ufaulu wao unakuwa sii mkubwa sana so school rank inashuka

Ila chakushangaza hawaangalii malengo ya mtoto wanawaza malengi ya kishule tu

Kunae mtoto w kaka yangu rector alimkatalia kusoma science, dogo nae akAmgomea rector,akafukuzwa akaenda shule nyingine akasoma science na akachomoka na one yake Kali tu
 
Na tatizo jingine ni kuwa mtoto unampeleka shule ya sekondari AX na ukitarajia atakapomaliza shule cheti chake kitakuwa kimeandikwa shule ya sekondari AX lakn unakuta cheti kimeandikwa amemaliza kidato cha nne shule ya sekondari BC, na wala mzazi hujawahi kuambiwa kuwa mtoto wako tunamsajiri kwenye shule ya BC, na ukiangalia mazingira ya shule unaona kuna shule 1 sasa sijui sikuizi hata darasa 1 linasajiriwa kuwa ni shule?? Na ukiuliza wanafunzi wengine wa kidato cha 1,2,3 cha shule BC hauwezi kuonyeshwa, kwa maana nyingine mtu akisha sajiri shule 1 kesho anarudi tena wizarani shule hiyohiyo inasajiriwa kwa jina lingine.
 
Back
Top Bottom