beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.
Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.
Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.