Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima apiga marufuku maiti kuzuiwa Hospitalini kutokana na madeni

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.

Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini, wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.

Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.

Kistaarabu na kibeberu ni busara kusema kwa watendaji wote:

"You should ignore that order."
 
Pre paid services hospitalini ni msala. Unakuta mgonjwa anahitaji emergency medicine na hana pesa. Muhimbili Dr ulikuwa unaprescribe tuu, malipo baadae. Hii ilikuwa inapunguza stress kwa Madaktari na vifo. Hospitali za rufaa za mikoa ambako kuna pre paid services watu wanakufa Sana japo haisemwi. Anyway, mwisho wa
 
Tatizo la serikali ya Tanzania ni kwamba, hata inapotaka kufanya jambo ambalo kimsingi ni zuri, utekelezaji wake unakuwa wa kibabebabe zaidi, kulazimisha zaidi, kutoangalia kwa upeo mpana, na matokeo yake ni kutengeneza janga.

Ndiyo maana serikali inaweza kuingilia biashara ya korosho, kwa nia ya kuwapa wakulima bei nzuri, halafu ikaharibu hiyo biashara kabisa.

Waingereza wana msemo wao mmoja, wanasema "the road to hell is paved with good intentions". Barabara ya kwenda motoni imetengenezwa kwa lami ya nia njema.

Maana yake, unaweza kuwa na nia njema, na kutangaza haya maazimio kwa nia njema, halafu nia yako njema, ikaleta janga. Hususan kama unatangaza vitu kwa nia njema bila mkakati wa kufikia malengo.

Serikali ni muhimu kuweka mkakati kabla ya kushurutisha mambo.

Je, mifumo yetu ipo tayari? Watu wana hela za kujilipia gharama? Wana bima? Kama hawawezi kujilipia, na hospitali hazilipwi, hospitali zitajiendeshaje? Serikali itazipa ruzuku?

Hili wazo la kukataza kuzuia maiti kimsingi si baya (prepaying is a different matter.

Kuzuia maiti ni jambo lenye matatizo makubwa kimaadili na kifalsafa. Ni suala linaloenda kinyume na ubinadamu. Naelewa na kuunga mkono juhudi za serikali kulimaliza tatizo hili.

Lakini je, serikali inaweka mkakati gani kuhakikisha tatizo linamalizika kwa "win win situqtion" itakayowezesha hospitali zilipwe pia? Kusema tu watu walipe kabla si suluhusho, maana, kama watu hawana uwezo wa kulipa hapi unatengeneza tatizo lingine, wakataliwe huduma?

Kumkatalia mgonjwa matibabu kwa sababu hana pesa ni kinyume na maadili ya kitabibu.

Kwa sasa naona serikali kama inatoa amri tu.

Kuna mambo mengine yanahusisha uchumi, hayamalizwi kwa amri tu.
 
Kumbe Dr Gwajima ana asili ya jina la kike? duuu! hii mbaya sana ina hamasisha usagaji hayaaaa! siendi kanisani kwake tena, kumbe ni shoga? jamani mtuombee! tumebatizwaje sasa kihivi?
 
Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza.
Kwa lugha nyepesi: Pesa mbele kama tai. Hakuna kupokea mgonjwa bila cash kutangulia. Hakuna kumpa dawa bila pesa kutoka.

Zile ahadi fake za bima ya afya ya bure kwa kila mtanzania lini wataanza kutekeleza?
 
Agizo la Dr.Gwajima limezingatia uhalisia wa haki za mtu anapofariki dunia. Kuuhifadhi mwili wake mahali panapostahili na kwa wakati stahiki linapaswa kuwa jambo lenye "heshima ya lazima". Bahat mbaya hosp zilijielekeza kutafuta fedha zake tu kitu ambacho kinatia ukakasi wa jambo lenyewe.
Hata hivyo serikali bado inao mlango wa kuweka utaratibu mzuri ili hosp ziwe na hakika ya kupata fedha zake pale mgonjwa anapofariki. Kwa hili sijataka kuamini km Mh Waziri kakurupuka km baadhi ya wachangiaji humu walivyoona,ila nina hakika km kiongoz mkuu wa wizara atajihusisha pia na upande wa pili (hosp) ili kusaidia kupata fedha hizo ambazo ndizo zitatumika kutuhudumia sisi ndugu wa marehem ambao tutakuja kuhitaji huduma ya matibabu wakati mwingine.
Ninayo iman na serikal!
 
Tatizo la serikali ya Tanzania ni kwamba, hata inapotaka kufanya jambo ambalo kimsingi ni zuri, utekelezaji wake unakuwa wa kibabebabe zaidi, kulazimisha zaidi, kutoangalia kwa upeo mpana, na matokeo yake ni kutengeneza janga.

Ndiyo maana serikali inaweza kuingilia biashara ya korosho, kwa nia ya kuwapa wakulima bei nzuri, halafu ikaharibu hiyo biashara kabisa.

Waingereza wana msemo wao mmoja, wanasema "the road to hell is paved with good intentions". Barabara ya kwenda motoni imetengenezwa kwa lami ya nia njema.

Maana yake, unaweza kuwa na nia njema, na kutangaza haya maazimio kwa nia njema, halafu nia yako njema, ikaleta janga. Hususan kama unatangaza vitu kwa nia njema bila mkakati wa kufikia malengo.

Serikali ni muhimu kuweka mkakati kabla ya kushurutisha mambo.

Je, mifumo yetu ipo tayari? Watu wana hela za kujilipia gharama? Wana bima? Kama hawawezi kujilipia, na hospitali hazilipwi, hospitali zitajiendeshaje? Serikali itazipa ruzuku?

Hili wazo la kukataza kuzuia maiti kimsingi si baya (prepaying is a different matter.

Kuzuia maiti ni jambo lenye matatizo makubwa kimaadili na kifalsafa. Ni suala linaloenda kinyume na ubinadamu. Naelewa na kuunga mkono juhudi za serikali kulimaliza tatizo hili.

Lakini je, serikali inaweka mkakati gani kuhakikisha tatizo linamalizika kwa "win win situqtion" itakayowezesha hospitali zilipwe pia? Kusema tu watu walipe kabla si suluhusho, maana, kama watu hawana uwezo wa kulipa hapi unatengeneza tatizo lingine, wakataliwe huduma?

Kumkatalia mgonjwa matibabu kwa sababu hana pesa ni kinyume na maadili ya kitabibu.

Kwa sasa naona serikali kama inatoa amri tu.

Kuna mambo mengine yanahusisha uchumi, hayamalizwi kwa amri tu.
Waziri kwenye hotuba yake ametoa mwongozo kwa hospitali. Anasema kuna Social Welfare Office kwenye hospitali ambao ndiyo wana hukumu la kutathmini uwezo wa mgonjwa na kumpa msamaha wa gharama za matibabu. Wanachokosea watendaji wanakaa na bills bila kuwaonyesha ndugu au mgonjwa akiwa mzima, wanakuja kuzitoa mwishoni pale mortuary na ndipo drama zinaanza. Hicho ndicho Waziri anakikemea
 
Hizo hospitali zinatoa wapi madawa ya kutibu?

Siasa nsio zinarudisha nyuma hizi nchi masikini.

Tutaendelea kua masikini hadi mwisho wa ulimwengu.
Kweli siasa zetu mbovu zinachanhia kuvuruga mambo. Mbunge anatuambia akina mama waende kujifungua bila kununua vifaa. Wanaambiwa watapewa hukohuko hospitali Hospitali hakuna panadol Wala bendeji,sembuse vifaa vya kujifungulia? Tunadanganywa jamani bajeti yenyewe finyu na pesa haijaletwa miezi na miezi. Bado tuna safari ndefu Sana kwenye afya na sekta zingine.
 
Waziri kwenye hotuba yake ametoa mwongozo kwa hospitali. Anasema kuna Social Welfare Office kwenye hospitali ambao ndiyo wana hukumu la kutathmini uwezo wa mgonjwa na kumpa msamaha wa gharama za matibabu. Wanachokosea watendaji wanakaa na bills bila kuwaonyesha ndugu au mgonjwa akiwa mzima, wanakuja kuzitoa mwishoni pale mortuary na ndipo drama zinaanza. Hicho ndicho Waziri anakikemea
Tatizo la watu wenye kipato kidogo wengi wasioweza kumudu bills realistic haliwezi kumalizwa na Social Welfare Office.

Kwa sababu huyo Social Welfare Officer akikwambia kwamba, 25% ya Watanzania hawana bima ya afya na hawatamudu kujilipia gharama, hiyo gap atalipa nani?

Solution si kuwa na Officer wa kutuambia nani hawezi kulipa, solution pia ni kujua huyo asiyeweza kulipa pengo lake litazibwa vipi?

Watu wanahangaika kulipa ada za shule na kodi za nyumba kila January. Na haya ni mambo ambayo yanajulikana yanakuja nanwatu wanaweza kuyapqngia bajeti.

Huko kwenye ugonjwa ambako magonjwa yanakuja bila ratiba maalum tutamalizaje tatizo kwa kumwachia Social Welfare Officer atuambie nani anaweza na nani hawezi kulipa tu?
 
Basi Serikali iwalipie hayo madeni, kinyume na hapo ni kutafuta umaarufu tu na kujaribu kuchonganisha jamii, Serikali iweke fungu maalumu kwa ajili ya kulipia maiti ambazo zimeshindwa kulipiwa, vinginevyo mnataka kuchonganisha ninyi (Waziri) muonekane mna utu na wale wanaofwata Sheria/taratibu waonekane wakatili mbele ya jamii. Kuhifadhi hizo maiti ni huduma na huduma lazima ilipiwe ili iwe endelevu, BTW sijaisoma habari zaidi ya kichwa cha habari, ...
Hebu kwanza tueleweshane,huduma za afya kiserikali ni huduma au biashara? Kama ni biashara basi bora hiyo wizara yake ijumuishwe kwenye wizara inayohusika na mambo ya biashara na uchumi,maana huko kuna sera na taratibu za kushughulika na WATEJA korofi wasiolipa madeni kisheria,ila sasa huwa napata mfadhaiko pale ninapofika kwenye hospitali yetu ya mount meru na kukuta wamama wa kimaasai wamemleta mgonjwa wao aliye hoi bin taabani,wanatarajia kuwa wakishamfikisha tu pale basi kazi yao imeisha,ni kusubiri tu madokta wafanye yao ili warudi nyumbani na mtu wao,sasa mara mtu wao anafariki,wanasema Ok,mara tena wanaitwa mezani na kupigiwa hesabu ambazo hawaelewi mbele wala nyuma,unaona wanaitana,wanaongeaongea kidogo,kisha wanayeyuka eneo la hospitali,wanapotelea pasipojulikana!!! Huko wanapoenda wanakutana na kauli za kodi kwa maendeleo ya taifa,wakiuliza maendeleo hayo ni yapi wanaambiwa ni kununua dawa za hospitali,kununua vitanda na majokofu ya kuhifadhia miili ya wapendwa wao,kujenga barabara nk,wakati huko kwao olelenovos hakuna barabara iliyojengwa na serikali zaidi ya miguu ya ngombe na ya kwao wenyewe kufanikisha shughuli hiyo,wanaona tu wanaonewa!! Wanasema serikali imewapora fedha zao kwa kodi then inawapora hadi miili ya wafu wao!! Hujawahi kukutana na familia duni ya kimasai iliyopatwa na msiba halafu usikie na hospitali wanadaiwa! Huwa wanahama hadi boma,wanahamia machakani huko!! Sijui tufanyeje sasa
 
Nilikuwa nawaza hapa itakuwaje, je tiba sasa itakuwa bure au ukifa na deni linakufa?
Ila umenitangulia kufikiri.
Lahaula
Tiba haijawahi kuwa bure nchi hii wala nchi yoyote ile,hata enzi za nyerere tulikuwa hatudaiwi kwa kuwa kodi zetu ziligharimia huduma hizo,sasa hivi kodi ni za kujengea fly over za daresalam na madaraja ya daresalam tu,huku umasaini kwetu hakuna pesa inayobaki,hivyo tunalazimika kudaiwa kila kwa kila neno linalotoka mdomoni mwa daktari,bado hapa naona bango kuwa jengo la hospitali limejengwa kwa msaada kutoka denmak,ambulance ni msaada kutoka kwa mbunge,kitanda kimeandikwa "donated by Saibaba community" vibanda vya kupumzikia nje vimeandikwa donated by asas,kuna vya cocacola,kuna misaada imetoka sijui nmb bank,acha hao akina bush&melinda gates,kuna vya who,mosquito net ni za mradi wa roll back malaria kutoka UN,nini cha bure hapo? Ukinipa hospitali moja ya serikali leo,nakuwa milionea ndani ya mwezi tu,na kila mtu atafurahia huduma!!
 
Wapo wanaoona kama waziri amekurupuka, lakini tuangalie na upande mwingine wa shilingi kuwa ina maana kuna wagonjwa wanapelekwa hospitali bila plan yoyote ya kupambana na gharama za matibabu. Sasa kipi kifanyike hapo kama suluhisho? Tunaweza kusema labda bima ya afya, bado tutasema kuwa kuna ambao hawana uwezo wa kulipia bima. Haya..suluhisho ni lipi? Kuzuia maiti? Bado kuna maiti huachwa na kupelekea kuzikwa na serikali...
Kwa hili mimi nadhani basi serikali iweke tu utaratibu mzuri wa kuwaruhusu ndugu wa marehemu kushiriki maziko ya ndugu yao aliyeshindwa kujilipia gharama za matibabu na za maziko yake,sawa tu,kama serikali itaona ina haki ya kuzika ndugu zetu kwa kuwa tu hatuna uwezo wa kuilipa bill basi na tuipe haki hiyo,ila nayo itupe haki yetu ya kushiriki msiba,tuwaachie tu,acha wazike!!
 
Hivi Singida kuna jimbo linaloongozwa na upinzani? Ama kuna mtu anawindwa kupokonywa jimbo
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.

Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.

Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.
Universal Health Insurance (U.H.I) ndiyo suluhisho.
 
Duh!
Maiti zikizuiwa wanaonekana hawana utu, ilhali waliacha tiba ziendelee malipo baadae.

Sasa wanasema maiti zisizuiliwe kwa sababu ya deni pia wanaonekana wamekosea, kibao kinageuka kuwa sasa wagonjwa watatakiwa kutanguliza hela kwanza.

Hebu shauri basi wewe unadhani njia sahihi ni ipi, maana tusiishie kulaumu tu na ku-speculate.
Middle ground itakuwa ni negotiations kati ya ndugu wa mgonjwa na serikali kupitia utaratibu rasmi wa kiserikali.

Kama wanasema ndugu hawana uwezo, na baada ya kuleta vithibitisho, serikali iweke utaratibu wa wao kufanya kazi za jamii kufidia deni au uwepo utaratibu wa kiserikali wa kutudisha deni kwa installment kadri ya uwezo kupitia TRA au Wizara, au chombo chochote cha kiserikali, baada ya kulipa kiwango ambacho wana uwezo.

Naona ndiyo njia iliyokaa kiTanzania zaidi
 
Duh!
Maiti zikizuiwa wanaonekana hawana utu, ilhali waliacha tiba ziendelee malipo baadae.

Sasa wanasema maiti zisizuiliwe kwa sababu ya deni pia wanaonekana wamekosea, kibao kinageuka kuwa sasa wagonjwa watatakiwa kutanguliza hela kwanza.

Hebu shauri basi wewe unadhani njia sahihi ni ipi, maana tusiishie kulaumu tu na ku-speculate.
Ondoa elimu Bure kwani imefeli jaribu tiba Bure
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.

Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.

Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.
Lugola mwingine!
 
Kwa hiyo bila hela hutibiwi na mochwari huwekwi ili ndugu wasidaiwe???
Wangeboresha bima ya bei nafuu kwa wananchi wote.
 
Back
Top Bottom