Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima apiga marufuku maiti kuzuiwa Hospitalini kutokana na madeni

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.

Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.

Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.
 
Sasa hapo wagonjwa watashindwa kutibiwa mpaka watoe pesa yote ya matibabu, naona kazi bado iko pale pale na wasipokuwa makini huko mahospitalini wagonjwa wengi watawafia reception kama ndugu zao hawana uwezo wa kugharamia matibabu.

Bado nawashauri hawa jamaa wa wizara ya Afya wakae vizuri waangalie namna bora ya kumaliza hii kadhia.
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.

Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini, wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.

Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.
Aisee sasa wagonjwa watatibiwaje ilikuwa unakufa unawaachia msala waliobaki wakomae walipe wazike. Kuna haja ya kutafuta utatuzi wa kudumu.
 
Sasa hapo wagonjwa watashindwa kutibiwa mpaka watoe pesa yote ya matibabu, naona kazi bado iko pale pale, na wasipokuwa makini huko mahospitalini wagonjwa wengi watawafia reception kama ndugu zao hawana uwezo wa kugaramia matibabu.

Bado nawashauri hawa jamaa wa wizara ya Afya wakae vizuri waangalie namna bora ya kumaliza hii kadhia.

Kakurupuka
 
Duuh hapa sasa anaenda kuua maelfu ya watu kwa kisingizio cha hawakulipa hela.
 
Sasa hapo wagonjwa watashindwa kutibiwa mpaka watoe pesa yote ya matibabu, naona kazi bado iko pale pale, na wasipokuwa makini huko mahospitalini wagonjwa wengi watawafia reception kama ndugu zao hawana uwezo wa kugaramia matibabu.

Bado nawashauri hawa jamaa wa wizara ya Afya wakae vizuri waangalie namna bora ya kumaliza hii kadhia.
Duh!
Maiti zikizuiwa wanaonekana hawana utu, ilhali waliacha tiba ziendelee malipo baadae.

Sasa wanasema maiti zisizuiliwe kwa sababu ya deni pia wanaonekana wamekosea, kibao kinageuka kuwa sasa wagonjwa watatakiwa kutanguliza hela kwanza.

Hebu shauri basi wewe unadhani njia sahihi ni ipi, maana tusiishie kulaumu tu na ku-speculate.
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.

Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini, wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.

Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.

Bora kuzuia maiti kuzikwa kuliko kuzuia mgonjwa kutibiwa, sio wagonjwa wote hufariki....
 
Basi Serikali iwalipie hayo madeni, kinyume na hapo ni kutafuta umaarufu tu na kujaribu kuchonganisha jamii, Serikali iweke fungu maalumu kwa ajili ya kulipia maiti ambazo zimeshindwa kulipiwa, vinginevyo mnataka kuchonganisha ninyi (Waziri) muonekane mna utu na wale wanaofwata Sheria/taratibu waonekane wakatili mbele ya jamii. Kuhifadhi hizo maiti ni huduma na huduma lazima ilipiwe ili iwe endelevu, BTW sijaisoma habari zaidi ya kichwa cha habari, ...
 
Nje ya nchi na hata hospital binafsi kubwa hapa Tanzania.. pesa kwanza ndio matibabu yanafata..

Naona waziri anataka aupeleke huo utaratibu muhimbili.. wagonjwa watafia mapokezi sana
 
Tena hapo Mloganzila huwa wanatibiwa wagonjwa wengi wenye matatizo makubwa ya Rufaa ya muda mrefu ndio maana wengi wanaofariki walikuwa wanabakisha madeni makubwa.

Kwa kauli hiyo ya waziri, Kitakachofuata ni wagonjwa kulipia kwanza matibabu kabla ya kutibiwa. Jambo ambalo litaleta usumbufu kwa wagonjwa wanaohitaji huduma ya haraka.
 
Sasa hapo wagonjwa watashindwa kutibiwa mpaka watoe pesa yote ya matibabu, naona kazi bado iko pale pale, na wasipokuwa makini huko mahospitalini wagonjwa wengi watawafia reception kama ndugu zao hawana uwezo wa kugaramia matibabu.

Bado nawashauri hawa jamaa wa wizara ya Afya wakae vizuri waangalie namna bora ya kumaliza hii kadhia.
Nilikuwa nawaza hapa itakuwaje, je tiba sasa itakuwa bure au ukifa na deni linakufa?
Ila umenitangulia kufikiri.
Lahaula
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.

Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini, wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.

Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.
Tujadili hoja hii kuhusu nini kitajiri kama si kutoendelea kupata huduma mpaka ulipe kwanza ?
 
Nadhani huyu waziri ni mjinga kabisa.
Anatoa kauli zisizokuwa na suluhisho lolote la msingi.
Sote tunajua kabisa, Hospitali huwa zinazuia maiti kuzikwa kama njia ya kushinikiza ili ndugu wajichange kulipia gharama za huduma ambazo ndugu yao alipewa wakati akiwa bado hai kwa lengo la kuokoa maisha yake kwanza.

Sasa waziri aseme sasa, nani atalipa hizo gharama za huduma alizokopeshwa mgonjwa kabla ya kufariki.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom