Waziri Dkt. Ashatu Kijaji Aipongeza Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO ) kwa Ubunifu wa Vifaa Tiba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

WAZIRI MHE. DKT. ASHATI KIJAJI AIPONGEZA TEMDO KWA UBUNIFU WA VIFAA TIBA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) ameipongeza Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO ) kwa ubunifu wa utengenezaji wa mitambo mbalimbali kwa gharama nafuu pamoja na vifaa tiba vinavookoa fedha nyingi kwa kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.

Waziri Kijaji ameyasema hayo alipotembelea Taasisi hiyo Juni 3, 2023 kuona maendeleo ya Mtambo wa Kuchakata Sukari ambao utakuwa na uwezo wa kuchakata Tani 200 za miwa ambazo zitakuwa Sawa na wastani wa Tani 10 za Sukari pamoja na mitambo mingine inayozalishwa na TEMDO

Aidha, Dkt. Kijaji ameishauri Taasisi hiyo kuendelea kutangaza na kuelimisha umma kuhusu bidhaa inazozitengeneza hususani mitambo hiyo pamoja na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali na Zahanati ambavyo vinasaidia Serikali kupunguza gharama ya kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.

Akitoa maelezo kwa Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. amesema TEMDO imebuni na kutengeneza vifaa tiba vya hospitali na zahanati nchini ikiwemo Vitanda vya Kujifungulia mama wajawazito, Vitanda vya Kulazia Wagonjwa, Makabati ya kuhifadhia vitu vya Wagonjwa, Majokofu ya kuifadhia Maiti, Kiteketezi cha Taka hatarishi zinazo zalishwa na mahosipitali na n.k.

Aidha Prof. Kahimba amesema mitambo mingine inayotengenezwa na TEMDO ni pamoja na mtambo wa kukamulia mafuta ya alizeti, mitambo ya bei nafuu ya kuchuja na kusafisha mafuta ya alizeti (sunflower oil mini-refinery plants), mtambo mdogo wa kuchakata sukari, mtambo wa kusindika zabibu pamoja na mtambo wa kuzalisha umeme wa upepo na jua kwa kutumia teknolojia rahisi na kwa gharama nafuu.

Aidha, Prof Kahimba pia alieleza kuwa TEMDO imefanikiwa kutengeneza Mtambo wakuchakata zao la muhogo wenye uwezo wa kuchakata Tani 10 za muhogo ambazo ni sawa na wastani wa Tani 3 za unga wa Muhogo, Mtambo huo una uwezo wa kuchakata muhogo kutoka shambani na kuwa unga tayari kwa mlaji siku hiyo hiyo
na mtambo wa kuchakata zao la mhogo.
 

Attachments

  • Fxv65b3XsAA3ScB.jpg
    Fxv65b3XsAA3ScB.jpg
    299.6 KB · Views: 7
  • Fxv65b_WwAgex-8.jpg
    Fxv65b_WwAgex-8.jpg
    290.5 KB · Views: 7
  • Fxv65b3X0AAJnVr.jpg
    Fxv65b3X0AAJnVr.jpg
    188.5 KB · Views: 8
  • Fxv65b-WwAAnCPZ.jpg
    Fxv65b-WwAAnCPZ.jpg
    318 KB · Views: 6
Back
Top Bottom