Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima apiga marufuku maiti kuzuiwa Hospitalini kutokana na madeni

Bima ya afya.
Wakati hili tunalisubiria, maiti anayedaiwa tuchukulie ni hasara kama vile nyanya zinaweza oza kabla hazijanunuliwa.
Kwani idadi ya wanoenda hospitali kutibiwa na kupona ni kubwa kuliko idadi ya wanaofariki.
Tusing'ang'anie sana hii hela anayodaiwa marehemu.

Biashara yoyote ina faida na hasara.
 
It’s just common sense kwani wagonjwa wote wanaoishia kudaiwa huwa wafu tu.

Lazima kuna wengine wanaingia wakiwa hawana hela na baada ya kutibiwa wanapona. Mbona awapelekwi selo za hospitali baada ya hapo mpaka walipe madeni? Si kuna namna za kudaiana.

Ndicho waziri alichosema, utengenezwe utamaduni mwingine wa kudaiana watu si wanatoa address za majumbani kwao. Kwanini sasa washindwe kufuatwa huko baadae mpaka huu utaratibu wa kuzuia maiti?

I can understand the burden cost of paying national medical treatment kwa serikali the bill might be too much, with their current income ppl need to contribute it makes sense.

However if you ask me serikali ifanye review ya ‘service costing’ za huduma ya afya na ku review charges zinazotolewa lengo liwe kukidhi gharama za uendeshaji ili watu wakawaida waweze mudu costs sio kuweka gharama kubwa.

Kwanza kwa mujibu wa katiba yetu kila mtu anastahili kupata huduma ya afya it’s agsinst the law kumkatalia mtu huduma labda wabadili katiba kwanza, wanasheria wamelala tu.

Tozo kubwa ni discrimination against marginalised groups and it’s against the law too, you can’t set criteria’s which might deprive others accessing medical services (hayo ni kwa mujibu wa katiba yetu ya kijamaa, sometimes huwa nashangaa watu wanaodai katiba mpya hivi wamesoma kweli aspects za rights zilizomo mule wakazielewa vinginevyo kungekuwa na kesi za kikatiba kila siku maana kuna sheria nyingi ni kinyume na katiba) isitoshe faida zenyewe kubwa wanaishia kutoa dividend serikalini; that’s just pathetic si bora hiyo hela iwekezwe kwenye kuboresha huduma au kununulia vifaa tiba.

Mishahara yenyewe ya nurses na madokta bado inalipwa na serikali kwa 100% kwenye government institution na dawa wananunuliwa (those are costs which you don’t include in services costing) so where is the justification.

Kwa ivyo responsibility za medical ethics zipo pale pale za kutibu mtu yoyote at the point of entry medical proffesional yoyote anayoelewa wajibu wake mgonjwa anapoingia anatakiwa ajue majukumu yake madeni ni swala la administration; na management za serikali hawana hizo sababu za kusema bila ya malipo awawezi jiendesha when they are almost funded by taxpayers.

Kama wanajua kudai sana ifike wakati na hawa mawakili kuanza kufungua kesi za medical negligence kuna wagonjwa wengi wanapoteza maisha chini ya mikono ya wataalamu au kukongoroka zaidi kuliko walivyoingia kisa uzembe tu unaofanyika kwenye medical procedures.
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.

Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.

Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.
Hawa mawaziri wao ni matamko tu lakini ukienda field hakuna utekelezaji wa wanayosema ,ni kama tanesco wanvyosema nguzo ni bure lakini kama nyumba yako inahitaji kuzo moja bei basi inabadilika inaenda hadi 520,000/= ila kama hakuna nguzo ni 320,000/= sasa hiyo laki 2 iliyoongezeka sijui ya nini.? PS Nyanya nguzo ni mali ya tanesco!! Usije kuniambia hiyo cost ni nyaya zimeongezeka.
 
Ningeshauri watoe msamaha ama tuseme wafute madai yote pindi mgonjwa akifariki,nadhani huu ndo utakuwa ufumbuzi wa kudumu wenye sura ya kibinadamu
 
Huduma za Afya ziwe bure kwa watu wote wenye kipato cha chini.
Duh!
Maiti zikizuiwa wanaonekana hawana utu, ilhali waliacha tiba ziendelee malipo baadae.

Sasa wanasema maiti zisizuiliwe kwa sababu ya deni pia wanaonekana wamekosea, kibao kinageuka kuwa sasa wagonjwa watatakiwa kutanguliza hela kwanza.

Hebu shauri basi wewe unadhani njia sahihi ni ipi, maana tusiishie kulaumu tu na ku-speculate.
 
Hawana pesa,ni maskini.
Kama ni mtoto mdogo aachiwe azikwe tu lakini mtu mzima akina ndugu walazimishwe kulipa kwanza sababu mbeleni ndio viherehere vya kutoana macho wakigombea Mirathi ya marehemu wakati alipokuwa akiumwa walikuwa hawagharimii matibabu

Kumtendea haki marehemu ndugu walipie gharama zote
 
Marehemu wengi wanakufa makapuku, hawana chochote.
Ndugu wanafiki akiumwa hawachangii matibabu akifa wanakuwa hawana huruma na marehemu kwenye kugawana mali wake

Walipe tu kabla kuchukua mwili
 
Duh!
Maiti zikizuiwa wanaonekana hawana utu, ilhali waliacha tiba ziendelee malipo baadae.

Sasa wanasema maiti zisizuiliwe kwa sababu ya deni pia wanaonekana wamekosea, kibao kinageuka kuwa sasa wagonjwa watatakiwa kutanguliza hela kwanza.

Hebu shauri basi wewe unadhani njia sahihi ni ipi, maana tusiishie kulaumu tu na ku-speculate.
Njia nyepesi kabisa ni kuacha kudai maiti ,
 
Wapo wanaoona kama waziri amekurupuka, lakini tuangalie na upande mwingine wa shilingi kuwa ina maana kuna wagonjwa wanapelekwa hospitali bila plan yoyote ya kupambana na gharama za matibabu. Sasa kipi kifanyike hapo kama suluhisho? Tunaweza kusema labda bima ya afya, bado tutasema kuwa kuna ambao hawana uwezo wa kulipia bima. Haya..suluhisho ni lipi? Kuzuia maiti? Bado kuna maiti huachwa na kupelekea kuzikwa na serikali...
Plani za kupambana na gharama zinaweza kuwepo Ila wakati mwingine mgonjwa anaweza kuhitaji vipimo au matibabu ya gharama juu ya uwezo mlionao,
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema hataki kusikia suala la watu kuzuiwa kuchukua maiti kwa madai kwamba ndugu wanatakiwa walipie gharama za matibabu.

Dkt. Gwajima ametoa ujumbe huo kwenda kwa hospitali zote nchini wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Mloganzila alipotembelea kuona namna huduma zinavyotolewa.

Amezitaka hospitali kujipanga katika suala hilo ili utaratibu uende vizuri na sio kulimbikiza bili za mgonjwa inapotokea amefariki dunia ndipo suala la kuzuia maiti linaanza na kutengeneza taswira mbaya.
Kwa kuwa serikali imekuja na tamko hilo, ni vyema ikawajibika kuilipia hizo gharama za matibabu wanazodaiwa marehemu. Nia njema za watoa huduma za afya kwa kusukumwa na sababu za kiutu isiwe fimbo tena kwao ya kuwachapia na kuishia kupata hasara.

Kama serikali imeona busara juu uamuzi huo, ije pia na majibu kuhusu ufidiaji wa gharama za matibabu hasa kwa hospitali binafsi. Kutaka kuonyesha kuwa inawajali wananchi huku haina suluhisho lolote lile juu ya ulipaji wa gharama zilizokwisha kutokea ni aina mojawapo ya ubabaishaji.


Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo hajatoa way forward.

Nathadhani atarudi kufafanua.

Bila hivo itanipa tabu sana
 
suluhisho ni kila mtanzania awe na bima ya uhakika sio hizi kajanja alafu sisi wananchi ndio tuanze msala na bima companies namna ya kulipana kama utataifishwa sawa..ila kila mtanzania hata kama kazaliwa leo anaingia kwenye mfumo wa bima madeni ya kizidi serkali inapunguza ruzuku maisha yanaendelea. tupilia mbali mambo ya nssf kila mfanyakazi apewe bima ya afya yeye na familia hata wafanyakazi wa sekta binafsi..wanaodaiwa loan bodi walipe kiasi walichokopa kama zanzibar ilivyo sio kulipa mpaka kustaafu..iyo nyingine iwekwe kwenye afya..ambae hana bima afungwe magareza ili akili ichaji yani tufanye bima ni jambo la kwanza kuliko tax.
 
Sasa hapo wagonjwa watashindwa kutibiwa mpaka watoe pesa yote ya matibabu, naona kazi bado iko pale pale na wasipokuwa makini huko mahospitalini wagonjwa wengi watawafia reception kama ndugu zao hawana uwezo wa kugharamia matibabu.

Bado nawashauri hawa jamaa wa wizara ya Afya wakae vizuri waangalie namna bora ya kumaliza hii kadhia.
Swali tumefikaje huku?
 
Back
Top Bottom