Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima apiga marufuku maiti kuzuiwa Hospitalini kutokana na madeni

Kitakachofuata sasa.

1. Hospitali zitachelewesha kumpa mgonjwa huduma husika mpaka alipe kiasi fulani cha pesa kwanza kama dhamana.

2. Kuna baadhi ya huduma muhimu za gharama kubwa hospitali zitasita kumpa mgonjwa aliyezidiwa kwa hofu kuwa ikiwa atafariki hawataweza kulipwa.

3. Hospitali hazitapoteza muda kuzihifadhi vizuri maiti za watu maskini wenye kudaiwa pesa na hospitali.
 
Duh!
Maiti zikizuiwa wanaonekana hawana utu, ilhali waliacha tiba ziendelee malipo baadae.

Sasa wanasema maiti zisizuiliwe kwa sababu ya deni pia wanaonekana wamekosea, kibao kinageuka kuwa sasa wagonjwa watatakiwa kutanguliza hela kwanza.

Hebu shauri basi wewe unadhani njia sahihi ni ipi, maana tusiishie kulaumu tu na ku-speculate.
Nionavyo, kabla ya hilo tamko waziri angetakiwa kukaa na watendaji wake wizarani wafikirie namna bora ya kumaliza hilo tatizo bila kuathiri sana upande wowote (mgonjwa na hospitali), tatizo la waziri namuona kama mtu anaependa sana one man show, mfano mwingine wa Magufuli, ndio maana mambo anayoamua yanaonekana hayatekelezeki badala yake yanaacha maswali zaidi.
 
serikali ipo watalipa gharama
Duh!
Maiti zikizuiwa wanaonekana hawana utu, ilhali waliacha tiba ziendelee malipo baadae.

Sasa wanasema maiti zisizuiliwe kwa sababu ya deni pia wanaonekana wamekosea, kibao kinageuka kuwa sasa wagonjwa watatakiwa kutanguliza hela kwanza.

Hebu shauri basi wewe unadhani njia sahihi ni ipi, maana tusiishie kulaumu tu na ku-speculate.
 
Nilishasema walioapishwa ngoja chaji ijae.sasa iko 100% majibu tunayaona now
 
Duh!
Maiti zikizuiwa wanaonekana hawana utu, ilhali waliacha tiba ziendelee malipo baadae.

Sasa wanasema maiti zisizuiliwe kwa sababu ya deni pia wanaonekana wamekosea, kibao kinageuka kuwa sasa wagonjwa watatakiwa kutanguliza hela kwanza.

Hebu shauri basi wewe unadhani njia sahihi ni ipi, maana tusiishie kulaumu tu na ku-speculate.
Ushauri wangu ni kwamba Mhe Waziri asiishie kupiga marufuku hospitali kutoza malipo ya mochwali. Swali la msingi hapa ni kwanini hospitali zinatoza malipo haya. Mimi nahisi hizi ni tozo zilizoidhinishwa na wizara husika na kama wizara inazipiga marufuku basi utolewe waraka kwa nchi nzima kuhusu katazo hili na serikali itoe ruzuku ya hii garama kwa hospitali zote. Hii ni kwa sababu tozo hizi usaidia kuboresha na kuendeleza huduma za mochwali zenyewe.
 
Duh!
Maiti zikizuiwa wanaonekana hawana utu, ilhali waliacha tiba ziendelee malipo baadae.

Sasa wanasema maiti zisizuiliwe kwa sababu ya deni pia wanaonekana wamekosea, kibao kinageuka kuwa sasa wagonjwa watatakiwa kutanguliza hela kwanza.

Hebu shauri basi wewe unadhani njia sahihi ni ipi, maana tusiishie kulaumu tu na ku-speculate.
Huyu mama ndo mnamuona kama super women eti kichwa cha madaktsri sasa nataka watu waondoke Bilal, kulipia huduma
 
Nadhani huyu waziri ni mjinga kabisa.
Anatoa kauli zisizokuwa na suluhisho lolote la msingi.
Sote tunajua kabisa, Hospitali huwa zinazuia maiti kuzikwa kama njia ya kushinikiza ili ndugu wajichange kulipia gharama za huduma ambazo ndugu yao alipewa wakati akiwa bado hai kwa lengo la kuokoa maisha yake kwanza.

Sasa waziri aseme sasa, nani atalipa hizo gharama za huduma alizokopeshwa mgonjwa kabla ya kufariki.
Natofautiana na wewe. Hakuna kitu kibaya kama kutoizika maiti inayostahili kuzikwa kwa sababu peyote Ile. Wenzetu Waisalamu wanalitekeleza sana hili. Hata sisi Wakristu tunasubiria kidogo kama ndugu wa marehemu wako mbali.

Kitendo cha maiti kuendelea kushikiliwa hospitali kwa sababu ya gharama za matibabu hazijalipwa siyo utamaduni wa Ki-Afrika. Iko siku itakuwa ni MAITI yako wewe au MIMI

Nampongeza Mh Waziri kwa tamko hili kwani litatunza hadhi ya mtu hata kama ameshakufa.

Watanzania tubadilike, tunapenda kuchanga hela ya msiba lakini ya matibabu hatuchangi. Tunapenda kuchanga hela ya harusi lakini ya kusomesha asiye na uwezo hatujihusishi. Hapo ndiyo Wakenya wametuzidi. Wanachanga sana hela ya matibabu na simu kuliko maharusi.
 
Tujadili hoja hii kuhusu nini kitajiri kama si kutoendelea kupata huduma mpaka ulipe kwanza ?
Wanandugu wanaosubiri kuchanga fedha ya maiti baada ya Hospitali kukataa, wachange sasa mgonjwa anapoingia hospitali kutibiwa. Very simple, tofauti ni muda wa kuchanga tu
 
.......kutoza malipo ya mochwali... .....Swali la msingi hapa ni kwanini hospitali zinatoza malipo haya.
...huduma za mochwali zenyewe.
Issue sio tozo za gharama za mortuary.

Issue ni deni la huduma toka siku ya kwanza ulipotumia mashine ya kupimwa uzito na muda wa afisa masijala aliyekufungulia faili la mgonjwa kwenye dirisha la kwanza pembeni ya mlango wa mbele mpaka umeme wa jokofu la maiti
 
Aisee sasa wagonjwa watatibiwaje ilikuwa unakufa unawaachia msala waliobaki wakomae walipe wazike . Kuna
Kama ni mtoto mdogo aachiwe azikwe tu lakini mtu mzima akina ndugu walazimishwe kulipa kwanza sababu mbeleni ndio viherehere vya kutoana macho wakigombea Mirathi ya marehemu wakati alipokuwa akiumwa walikuwa hawagharimii matibabu

Kumtendea haki marehemu ndugu walipie gharama zote
 
huyu ndo humu nilikuwa nasoma eti ana akili kubwa mbona uwezo wake mdg tu

bora kuzuia maiti kuliko kuzuia matibabu
 
Ndugu wanafiki akiumwa hawachangii matibabu akifa wanakuwa hawana huruma na marehemu kwenye kugawana mali wake

Walipe tu kabla kuchukua mwili
 
Mgonjwa ajidhamini kwa mali zake na za ndugu zake na ndugu wamdhamini kuwa wasipolipa mali zao zitwaliwe
 
Wapo wanaoona kama waziri amekurupuka, lakini tuangalie na upande mwingine wa shilingi kuwa ina maana kuna wagonjwa wanapelekwa hospitali bila plan yoyote ya kupambana na gharama za matibabu. Sasa kipi kifanyike hapo kama suluhisho? Tunaweza kusema labda bima ya afya, bado tutasema kuwa kuna ambao hawana uwezo wa kulipia bima. Haya..suluhisho ni lipi? Kuzuia maiti? Bado kuna maiti huachwa na kupelekea kuzikwa na serikali...
 
Sasa hapo wagonjwa watashindwa kutibiwa mpaka watoe pesa yote ya matibabu, naona kazi bado iko pale pale, na wasipokuwa makini huko mahospitalini wagonjwa wengi watawafia reception kama ndugu zao hawana uwezo wa kugaramia matibabu.

Bado nawashauri hawa jamaa wa wizara ya Afya wakae vizuri waangalie namna bora ya kumaliza hii kadhia.
Mkuu umeongea bonge la pointi aisee!!
 
Back
Top Bottom