field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 1,171
- 2,730
Binafsi sina chama cha siasa na sijawahi kuwa mshabiki wa chama chochote cha siasa katika maisha yangu yote.
Naomba niseme yafuatayo, kwanza sina chuki na kiongozi wowote wa aidha CCM au CHADEMA au chama chochote cha siasa.
Nimefuatilia ziara na ufanyaji kazi wa waziri wa Afya Dr. Dorothy Gwajima, ndiyo anakosea kwenye uongeaji wake hasa akichamba zaidi au akiongea sana kumsifu Magufuli sana kupita kiasi lakini huyu Waziri anaongea mambo yalio uozo kwenye serikali na anajaribu kufuatilia kila kitu na kuweka wazi.
Huyu mama anajitahidi mno na nina imani uchapaji wake wa kazi utaleta matunda mazuri kwenye wizara hii iliyoharibiwa vibaya na waziri aliyepita.
Ninapenda kumpongeza na kumwambia asikate tamaa, kuna uozo mwingi kwenye wizara ya Afya kwa kiasi kikubwa na kuna uzembe mkubwa, wizi mwingi wa madawa, fedha na miradi hewa inayoibiwa pesa kila siku.
Waziri Gwajima endeleza uzi huo huo, uzembe na wizi uondoe hapo wizarani.