Joshua justine
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 792
- 1,007
Anataka kuchomwa kisu na form two huyoKumbe walimu wa nidhamu bado wapo zama hizi?
Anataka kuchomwa kisu na form two huyoKumbe walimu wa nidhamu bado wapo zama hizi?
Nakumbuka form one headmaster alisema hatambui uniform nje ya shule lazima tutoe hela tupimishwe shuleni,tulitoa hela baadaye wanaume tumeletewa suruali nyeusi za mtumba
Unadhani leo kwenye hizi shule hiyo maana ya uniform bado ni ile ile ya miaka hiyo?Lengo la uniform ni mwanafunzi anapotoroka au akipata matatizo mtaani watu wanajua waanzie wapi; ni utambulisho wa mwanafunzi.
Ndio maana kwa wale waliosoma boarding ilikuwa tukitoroka shule kitu cha kwanza ni kuvua mashati yatakayo tutambulisha tumetoka shule gani au kutovaa uniform kabisa.
Huyu mama mweupe sijapata kuona halafu sijui kwanini wanapenda kumpa wizara kubwa na ngumu; it’s beyond me.
Hata wengine, kama imechakaa kichaka cha kujificha ndo hicho hapoNi kwa form One tu mkuu
Halafu juzi wamewaruhusu kupata mimba, za kuambiwa changanya na zako mbayuwayu....Huo uhuru wakianza kuutumia vizuri ndipo itafahamika kama wamesaidia au wameharibu.
Walau uniform zinasaidia hususan upande wa nidham wanapokuwa nje ya viunga vya shule.
Logic nadhani ipo kwenye nembo ndio utapata shule.Unadhani leo kwenye hizi shule hiyo maana ya uniform bado ni ile ile ya miaka hiyo?
Leo lengo kubwa ni pesa tu, mfano mzazi unaweza kupata uniform kwa gharama kidogo huku mtaani, lakini shule inataka ikuuzie yenyewe tena bei kubwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kwa form One tu mkuu
Tuna lea ujinga kesho watasema hawana madaftari, haya mambo ndiyo yanayo shusha hadhi ya elimu haya .Ikiwa wewe una uwezo kumbuka wapo wasio na uwezo.Ikifika mwisho wa mwaka,kuna kulipia kodi ya pango la nyumba,watoto wakuwanunulia uniform sio mmoja,wapo wa ndugu na jamaa waliofiwa na wazazi wao.Sikukuu za mwisho wa mwaka.Wapo wenye wagonjwa,nk,wengine wanamsubiria michango ya ndugu na jamaa.
Kifupi tuna lea ujinga sare za shule zinasababu waache kingiza siasa kesho watasema hawana viatu na madaftari wazazi wanafunzwa uzembeUwelewa mbaya,ukiangalia shule za private mwanafunzi anafika shuleni Hana uniform anaenda darasani mpaka itakapokuwa tayari Sasa ubaya upo wapi wa wazazi kupewa muda huku mtoto akiendelea na masomo?
Tuache kufikiria negative kila kijacho
Huyu Mama afikiriwe nafasi za Juu hapo baadae,
HahahaAnataka kuchomwa kisu na form two huyo
Kaziiendelee dada Ummy,===
Waziri wa TAMISEMI, Mhe Ummy Mwalimu amekemea utozaji wa michango mbalimbali kwa Wanafunzi Shuleni sanjari na vitendo vya baadhi ya Walimu kuwazuia Wanafunzi kuingia Shuleni kwa kukosa sare na mahitaji mengine yanayohitajika Shuleni hapo.
Amesema vitendo hivyo havikubaliki na kwamba Walimu hao wanapaswa kuwa na huruma kwa Wazazi na Walezi wa Watoto hao na kwamba wanapaswa kuhakikisha wanaepuka kuwakwamisha Watoto hao kusoma.
"Walimu wasiweke vikwazo kwa Watoto wanaoanza darasa la kwanza, Katibu Mkuu hakikisha unaandika waraka wa utaratibu, tunataka Shulr zinapofunguliwa January Watoto 90007 wa kidato cha kwanza waanze Shule"
Katika kulisisitiza hilo Waziri Ummy amesema anatafuta Shule mbili au tatu za kutolea mfano endapo zitabainika kutenda kosa hilo na kusisitiza kuwa Wazazi hawapaswi kubebeshwa mzigo kwa kuwa Serikali ilishaweka utaratibu wa elimu bila ada.
"Sitaki kuona Mwanafunzi amerudishwa kwasababu ya michango na kwa hawa wanaonza kidato cha kwanza hata kama hawana sare ya Shule aliyochaguliwa asirudishwe bali apewe muda”Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akihutubia kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na Binafsi leo Dar es salaam
View attachment 2045856
Daaaah khaaaaSasa tutajuaje kama ni miaka 30 au ni hawa wa mtaani kina Mwajuma ndala ndefu?
mkuu upo?Itapendeza sana kama yatasimamiwa...
Kaziiendelee===