Waziri Ummy: Toto Afya Kadi haijafutwa ila sasa Watasajiliwa Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh 50,400

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,038
Waziiri wa Afya mh Ummy Mwalimu amesema Toto Afya Kadi haijafutwa ila Utaratibu ndio umebadilika sasa Watoto Watasaniliwa Shuleni kwa gharama ile ile ya tsh 50,400.
---
1694905771395.png
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Toto Afya Kadi haijafutwa ila kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili ambapo utaratibu wa sasa ni kuwa Watoto wasajiliwe Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh. 50,400 ili waingie wengi, wasio Wagonjwa na hivyo kuweza kuchangiana wachache watakaogua.

Akijibu hoja za Wadau mbalimbali kupitia mtandao wa X leo, Ummy amesema “Bima ni Sayansi, wakate wengi wachangiane wachache watakaougua, Toto Afya Kadi haijafutwa, kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili, utaratibu wa sasa ni kuwa Watoto wasajiliwe Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh. 50,400 ili waingie wengi, wasio Wagonjwa na hivyo kuweza kuchangiana wachache watakaogua”

“Kwa sasa Toto Afya Kadi wamesajiliwa Watoto laki 2 tu, tuhimizane Wazazi/Walezi kuwakatia Bima ya Afya Watoto wetu, naamini wakisajiliwa Watoto japo asilimia 10 tu (Milioni 3) kwa utaratibu huu basi tunaweza kuhakikisha ustahamilivu na uendelevu wa fao hili”

“Mwisho, Sera ya Watoto wa umri chini ya miaka mitano au Watu wasio na uwezo kupata msamaha bado haijafutwa, Hospitali zote za umma zinaendelea kuhudumia Watoto wa umri chini ya miaka mitano kupitia utaratibu wa misamaha”

“Nimeshaelekeza NHIF kutoa elimu zaidi kuhusu Watoto wanaokatiwa Bima ya Afya kwa hiari kuwa utaratibu wa sasa ni kuwa Watoto wasajiliwe kupitia Shuleni kwa gharama ile ile ya Tsh. 50,400 au kwa utaratibu wa kifurushi cha Familia, NHIF washirikiane na Kamati za Shule kutoa elimu hiii, nasi tuendelee kuhimizana na kuhamasishana kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya kwa kila Mtu, tusisubiri hadi tuwe Wagonjwa ndio tukate bima”

Source: Millard Ayo
 
Kwa hili jambo serikali imepuyanga sana, hawa watoto ambao bado hawajaanza shule itakuwaje?. Kuna watu wanajitolea kulipia watoto yatima hizi bima sasa wamefuta hawa watoto si watakufa kwa kosa matibabu?.

Serikali inapesa za kununua magari kwa zaidi ya billion 500 kwa mwaka na bado service hapo, kweli wameshindwa kuwafadhili hawa watoto wa umri chini ya miaka 5?.

Serikali inasema inataka kuzuia vifo vya watoto wadogo wakati wanafuta “Toto Afya bima” si wanakwenda kuongeza idadi ya vifo vya watoto?

Tukishindwa kuwalinda hawa watoto hapo badae tutakuwa na kizazi gani?

Mwisho, Watanzania tunalipa kodi nyingi sana ni huduma ipi ambayo serikali inatupa bure? kama bima za watoto wameshindwa lakini wanaaidhinisha malipo ya wake za vigogo wa serikali.

Serikali ya Tanzania ni moja ya incompetent govt isiyojali raia wake. Hili suala la bima limenigusa maana Bossy wangu anawalipia watoto 10 bima sasa wamefuta sijui itakuwaje sasa,

“POOR TANZANIAN LEADERS & GOVT”
 
Ma CCM ni laana
 
Hili suala linachanganya, sera ya serikali ni matibabu bure kwa under 5, wazee na wajawazito.
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema mpango wa bima ya afya kwa watoto wanaojiunga kwa hiari (Toto Afya Kadi) haujafutwa, bali kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili watoto.

Akikanusha uvumi huo kwenye mtandao wake wa X (zamani Twitter), Waziri Ummy ameeleza kuwa utaratibu wa sasa ni kwa watoto kusajiliwa shuleni kwa gharama ya shilingi 50,400 ili waingie wengi wasio wagonjwa na hivyo kuweza kuchangia wachache watakaougua.

"Bima ni sayansi. Huwezi kuwa na bima inayokusanya shilingi bilioni 5; fedha inayolipwa kwa watoa huduma, yaani matumizi, ni bilioni 40. Natamani hizo nguvu za kupotosha zingetumika kuleta ushauri ni vipi NHIF itaweza kuvutia watoto wengi zaidi ambao hawana changamoto za kiafya ili kuweza kulipia wachache watakaopata changamoto za kiafya," amesenma.

“Kwa sasa Toto Afya Kadi wamesajiliwa watoto laki 2 tu, tuhimizane wazazi/walezi kuwakatia bima ya afya watoto wetu. Naamini wakisajiliwa watoto japo asilimia 10 tu (milioni 3) kwa utaratibu huu basi tunaweza kuhakikisha ustahamilivu na uendelevu wa fao hili." Amesema

Aidha, Waziri amesema sera ya watoto wa umri chini ya miaka 5 au watu wasio na uwezo kupata msamaha bado haijafutwa, na kwamba hospitali zote za umma zinaendelea kuhudumia watoto wa umri chini ya miaka mitano kupitia utaratibu wa misamaha.

====
IMG-20230916-WA0120(1).jpg
 
IMG-20230916-WA0136.jpg
IMG-20230916-WA0135.jpg
IMG-20230916-WA0134.jpg
 
Amesema NHIF ilikuwa inapata hasara mchango bilion5 matumizi bilion40 ndiyo Mana wameondowa.haya ya kusajiliwa shule I ngoja tuone.
Waziiri wa Afya mh Ummy Mwalimu amesema Toto Afya Kadi haijafutwa ila Utaratibu ndio umebadilika sasa Watoto Watasaniliwa Shuleni kwa gharama ile ile ya tsh 50,400

Source: Ayo TV
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom