CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 4,984
- 4,083
Huyu Mama afikiriwe nafasi za Juu hapo baadae,===
Waziri wa TAMISEMI, Mhe Ummy Mwalimu amekemea utozaji wa michango mbalimbali kwa Wanafunzi Shuleni sanjari na vitendo vya baadhi ya Walimu kuwazuia Wanafunzi kuingia Shuleni kwa kukosa sare na mahitaji mengine yanayohitajika Shuleni hapo.
Amesema vitendo hivyo havikubaliki na kwamba Walimu hao wanapaswa kuwa na huruma kwa Wazazi na Walezi wa Watoto hao na kwamba wanapaswa kuhakikisha wanaepuka kuwakwamisha Watoto hao kusoma.
"Walimu wasiweke vikwazo kwa Watoto wanaoanza darasa la kwanza, Katibu Mkuu hakikisha unaandika waraka wa utaratibu, tunataka Shulr zinapofunguliwa January Watoto 90007 wa kidato cha kwanza waanze Shule"
Katika kulisisitiza hilo Waziri Ummy amesema anatafuta Shule mbili au tatu za kutolea mfano endapo zitabainika kutenda kosa hilo na kusisitiza kuwa Wazazi hawapaswi kubebeshwa mzigo kwa kuwa Serikali ilishaweka utaratibu wa elimu bila ada.
"Sitaki kuona Mwanafunzi amerudishwa kwasababu ya michango na kwa hawa wanaonza kidato cha kwanza hata kama hawana sare ya Shule aliyochaguliwa asirudishwe bali apewe muda”Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akihutubia kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na Binafsi leo Dar es salaam
View attachment 2045856