May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,818
Hizi kauli mbona si mpya, tatizo liko wapi?.
Miezi kadhaa nyuma mapema asubuhi nilikutana na Kijana mdogo akiwa amevaa sare za shule ambazo zilikuwa zinasadifu tosha hali ya kiuchumi ya familia anayotokea.
Mtoto yule alikuwa anakwenda kama hataki huku usoni akionekana analia hivyo nikavutika kumuhoji kujua kulikoni...akasema Mama yake amempiga kwa sababu alikuwa anakataa kuondoka nyumbani bila kupewa mia tano ya mchango shuleni ambako nako akifika bila ya hiyo hela Mwalimu husika anamchapa.
Nilimpa mia tano na kumwambia akimbie awahi shuleni, walau akabadilika na kuonesha matumaini.
Hapa unaweza kuona Mtihani anaoupata Mtoto kama huyu wa darasa la kwanza tu ambaye hata kwa kumuangalia inaonesha kabisa kama hata amepata kifungua kinywa ni bahati....hivi kwa nini huyo Mwalimu asivae viatu vya huyu Mtoto?. Mwalimu anapata wapi msukumo wa kumshinikiza Mtoto alete hiyo mia tano kwa kumpiga yeye Mtoto anayepaswa kusubiri apewe pesa na Mzazi?.
Hapo huwa najiuliza Mwalimu anapoamua kumuadhibu Mtoto hivi ni kwamba hatumii akili kumbebesha Mtoto matatizo yasiyomuhusu? tena bila hata kujali hali ya huyo Mtoto mwenyewe.
Je kwa kauli hii ya Waziri itabadilisha nini ambacho hakijawahi kutamkwa kabla?.