Waziri Sophia Simba - Mwenyekiti Mpya UW-CCM (Taifa)

Waziri Sophia Simba - Mwenyekiti Mpya UW-CCM (Taifa)

Nafikiri mmoja wao kwa hili lazima aondoke haraka yaani
- Kama ni Simba basi aondolewe kwa kutoa HONGO ya laki moja.
- Kama ni Kahama basi aondolewe kwa kusema uongo.
Kama wataendelea kuwepo wote basi uchaguzi ujao CCM wenyewe kwa wenyewe watakuwa wanatoana macho. Itakuwa kama mechi Uingereza ambayo Refa karuhusu rafu zote RUKSA.
 
Sheria ifuate mkondo wake na iwe mapema kabla ya uchaguzi ili UWT wapate viongozi safi na walio bora
 
Haishangazi kwani Wazungu walisema "Birds of the same feathers ....." na hata Waswahili nao msemo wao " Waarabu wa Pemba............"
Viongozi wengi wa Siasa hapa kwetu wapo kwa ajili ya manufaa yao tu na sio kwa ajili ya Taifa. Mimi huwa nashangazwa na wale wanaowateta na kuwakejeli wanaokwenda upande wa upinzani, ukweli ni kwamba Si CCM si wengine, huwa wanaongozwa na ubinafsi na kutumikia wananchi inakuwa ni kujikomba kwao tu. Kama tuna siasa za uadilifu mambo ya kuhonga, kutukanana na kupakana matope kwa nini na hasa chama tunachoambiwa kuwa kina maadili. Niaminivyo mimi kuwa kiongozi mzuri huchaguliwa na wananchi kwa ridhaa yao na sio kwa hongo. La kutia aibu na kuogopesha ni kuwa Taifa linajipanga kutowa nafasi zaidi kwa wanawake na tunachokiona sasa ni matusi ya nguoni na kuanika nguo za ndani. Labda hatujawa tayari, sijui!!!!
 
Makamba alipoulizwa na Nipashe juzi, licha ya kukiri kupokea nakala ya barua hiyo ya Kahama, alimtaka mwandishi kama ana swali lolote kuhusiana na suala hilo, akamuulize Rais Kikwete kwa vile ndiye aliyeandikiwa barua hiyo.

``Mtafute Mwenyekiti wa CCM, yeye ndiye aliyeandikiwa barua, aliyeandikiwa ndiye anayejibu. Mimi nimepewa nakala, anayepewa nakala, anaarifiwa tu,`` alisema Makamba.

Nipashe ilipowasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alisema kwa vile malalamiko ya Kahama yanahusiana na Chama, anayepaswa kujibu suala hilo ni Katibu Mkuu.

Baada ya Makamba kuulizwa tena, alisema: ``Mimi sina cha kusema, sijaisoma (hiyo barua), sijajua maudhui.

Nitakapoisoma na kujua maudhui, nitatoa maoni yangu.``

Kahama alipoulizwa na Nipashe jana kama barua hiyo ndiye aliyeiandika, hakukiri wala kukanusha, badala yake alisema kwa sasa hawezi kuzungumza lolote kwa vile kipindi hiki ni cha sikukuu ya Krismasi, ambayo yeye kama Mkristo anapaswa kuitukuza.

``Sina comments (maoni) kabisa kabisa, mpaka nionane na Katibu Mkuu. Pia mimi ni Mkristo na kipindi hiki ni cha Krismasi,`` alisema.

Naye Diwani wa Kata ya Ilala, Moshi Kondo, alipoulizwa juzi, alikataa kuzungumzia suala hilo, badala yake alimtaka mwandishi akamuulize Simba.

``Kwani Sophia Simba mimi ni nani kwake?`` alihoji Kondo, ambaye alipojibiwa na mwandishi kuwa ``Simba anadaiwa kuwa ni mtu wake wa karibu``, alisema: ``Nenda kamuulize Simba.``

Tangu juzi hadi jana jioni Nipashe ilimtafuta Simba bila kumpata na baadaye kuelezwa na mmoja wa wanafamilia yake kuwa yuko safarini Malaysia.

SOURCE: Nipashe

Hawa jamaa wote kwenye huu mtiririko wa hizi 'one touch' nasuggest Maximo awaite kwenye timu ya Taifa, yani wanapasiana mpira kama Brazil!
On the other hand, kapeperushi alikofowadi Kahama kwa JK kangenoga zaidi kama kangekuwa na kilo yake ndani! tehe, tehe,tehe!
 
Nimepoteza imani na wote wawili hao toka walipotwangana makonde kwenye kikao. Wamethibitisha wote hawana maadili. Hapo ni kuwapiga chini wote na apewe huyo Kasunga
 
Nimepoteza imani na wote wawili hao toka walipotwangana makonde kwenye kikao. Wamethibitisha wote hawana maadili. Hapo ni kuwapiga chini wote na apewe huyo Kasunga

Masatu angalau umerudi bwana. Tulikukosa sana (tuli-mis) kwenye Tusker Cup!
 
Hivi kwa nini kila uchaguziw a CCM au jumuiya zake uwe na mizengwe ya aina hii (rushwa na kushutumiana?)
Ni matarajio ya wengi kuw Mwenyekiti atareact haraka kuhusiana na madai haya ili kuweka mambo sawa kabla ya uchaguzi
 
Tatizo la wajumbe wa vikao vya CCM wamejiweka kuhongwahongwa; hawasikilizi chochote zaidi ya pesa maana wengi wao hizo nafasi walizipata kwa utaratibu huohuo. Hili tatizo la ufisadi ni donda sugu ndani ya CCM. Solution pekee ni kuwaweka pembeni wawe chama cha upinzani wajifunze kuwa siasa ni utashi, passion na utumishi badala ya kufikiri ni mtaji wa pesa na cheo.
 
Mama Janet Kahama katoka mbali na UWT anaamini hii sasa ni zamu yake. Mama Sophia Simba yeye ni mtu wa kuja. Ni mwanamtandao wa JK hivyo mbinu zote safi na chafu lazima zitumike kuhakikisha Mtandao unashika jumuiya zote za chama. Pamoja na kelele zote za Mama Kahama, hiyo barua itamtoke puani. Kuliko CCM kukubali waziri wake wa utawala bora ametoa rushwa, hii itakichafua sana chama na serikali, hivyo ni bora kumkana Mama Kahama kuwa ni muongo na hivyo hafai. Sophia Simba atapeta kwenye uenyekiti, mtandao utafurahi, Mama Kahama atamwaga chozi kwani anaamini kwenye haki.

Kama Umoja wa Vijana wa CCM umeweza kuaford kumtosa kijana shupavu kama Nape, leo itakuwa issue kumtosa Mama Kahama, after all yeye 'hagawi', anabaniabania wakati wenzake wanagawa kama pipi!. Bado Mama Kahama ananafasi hapo?.
CCM ya Nyerere sio CCM ya JK. Ya Nyerere ilikuwa ya Uadilifu, hii ya JK ni ya 'mwenenacho' huongezewa na asiye nacho ananyang'anywa hata kidogo alichonacho. Debe tupu hupiga kelele na mkono mtupu haulambwi.
 
Sijui lini mtandao wangu utakuwa kwenye chat kama huu! Subira yavuta kheri
 
Sasa mtu kama Mama kahama anasubiri nini ndani ya chama kama hicho?
 
Mtandao wako Mwanjelwa, mbona uko kwenye chat tayari!. Chat gani zaidi unayoitaka wewe?.

Duh! Mkuu, angalia sana. Takes a minimum of a decade to have a sound Mtandao. Kama hivi sasa, kuna wapumzishaji, wapumzikaji, wapiga debe, watu wa issue za hovyo hovyo na,,,, mwisho Mkuu wao. Siyo rahisi kuwapanga wote hao na akili zije elewana! Just imagaine, katika mazingira ya kawaida, suala la kumchinja Nape halikuwa rahisi kama linavyoonekana. Lakini alichinjwa huku anaangalia. Sasa subiri mbuzi kibao wa kafara mwaka 2010 July.
 
Duh, ama kweli kuna kazi ktk kuondoa Ufisadi nchini.. Hivi hao wajumbe wa kamati wako wangapi ukizidisha na 100,000 kwa kila mmoja wao. Huyu Mama hizo fedha za ziada kazipata wapi na zililipiwa kodi!..
 
Kama Umoja wa Vijana wa CCM umeweza kuaford kumtosa kijana shupavu kama Nape, leo itakuwa issue kumtosa Mama Kahama, after all yeye 'hagawi', anabaniabania wakati wenzake wanagawa kama pipi!.

Tafsiri, tafadhali, tafsiri! Hagawi nini?
 
Mtu anahonga mamilioni ya fedha just kuwa mwenyekiti wa jumuiya ccm,kunani jumuiya??
 
hagawa njuruku! tehe tehe tehe!!

Asante, Mkuu. Sasa nimeelewa. Hasambazi vibahasha kama inavyoelekea wengine wanafanya! Lakini si tamaduni kuwa wakati huu watu wanapeana kadi na vijizawadi? Tatizo liko wapi?
 
Back
Top Bottom