Waziri Sophia Simba aanza kuchunguzwa
2008-12-27 15:06:04
Na Joseph Mwendapole na Muhibu Said
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema tuhuma za rushwa zinazomkabili Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, zitafanyiwa uchunguzi na ikithibitika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Wakati CCM ikitoa kauli hiyo, Simba amegoma kutoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zinazomkabili zilizolalamikiwa na mgombea mwenzake wa nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa chama hicho, Janeth Kahama, alipotakiwa na Nipashe kufanya hivyo jana.
Kahama, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Desemba 20, mwaka huu, aliwasilisha rasmi malalamiko kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimtuhumu Waziri Simba kuwa ametoa hongo ya sh.100,000 kila mjumbe wa Mkutano Mkuu ili wampe kura.
Akizungumza na Nipashe jana, Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, alisema kwa kuwa chama hicho kinapinga vikali vitendo vya rushwa na kila mwanachama anapotuhumiwa lazima achunguzwe.
Chiligati alisema anaamini kuwa kama malalamiko hayo yamemfikia Mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete atatumia vyombo vya dola ama kamati za maadili ndani ya CCM kuchunguza.
``CCM haifumbii macho suala la rushwa hata kidogo, kila mwanachama akipata tuhuma tunachunguza na kuchukua hatua, sasa hili la Sofia Simba kama kweli limefika kwa Mwenyekiti wetu naamini yuko makini sana na anaweza kuamua kuagiza vyombo vya dola au kamati za maadili za chama kuchunguza,`` alisema Chiligati.
Uchaguzi wa UWT, unatarajiwa kufanyika Januari 7 ,2009 na wagombea watakuwa Janeth Kahama, Sofia Simba na Joyce Masunga.
Katika barua yake kwa Mwenyekiti wa chama hicho ambaye ni Rais Jakaya Kikwete, Kahama analalamika kuwa Sofia Simba na wapambe wake wamekuwa wakiitumia Ikulu kuwaomba kura wajumbe wa Mkutano Mkuu.
Kahama ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum, amewasilisha malalamiko yake kupitia barua yenye kumbukumbu namba JBK/01/08 ya Desemba 20 mwaka huu, iliyopelekwa kwa Rais Kikwete.
Nakala ya barua hiyo ambayo Nipashe inayo, imepelekwa kwa Katibu Mkuu wa UWT na Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba.
Makamba alipoulizwa na gazeti hili kama amethibitisha kupokea barua hiyo alikiri kuipokea.
Simba anadaiwa kutoa hongo hiyo kupitia kadi alizochapisha na kusambazwa na Diwani wa Kata ya Ilala, Moshi Kondo. Kadi hizo zina picha, jina na sahihi ya Waziri Simba, Kalenda ya 2009 na nembo ya CCM.
Waziri Simba alipotakiwa jana kutoa ufafanuzi kuhusu tuhuma hizo, hakukiri wala kukanusha badala yake alisema kwa ufupi: ``Sina neno.``
Alipoulizwa ni kwa nini anasema hana neno, Waziri Simba alisema kwa jazba: ``Sina neno hasa kwa (gazeti la) Nipashe, kwa sababu siku zote mmekuwa mkiniandika bila kufanya utafiti. Hivyo, sitaki kusema na mtu yoyote wa Nipashe full stop na usinipigie tena (simu)``.
SOURCE: Nipashe
Waziri Sophia Simba aanza kuchunguzwa
.................................. ``Sina neno.``
Alipoulizwa ni kwa nini anasema hana neno, Waziri Simba alisema kwa jazba: ``Sina neno hasa kwa (gazeti la) Nipashe, kwa sababu siku zote mmekuwa mkiniandika bila kufanya utafiti. Hivyo, sitaki kusema na mtu yoyote wa Nipashe full stop na usinipigie tena (simu)``. [/U][/I]
SOURCE: Nipashe
Mama Simba anaonekana anajiamini sana, kuna mahali pazito anaegemea. Kwa vile tuhuma za rushwa ni tuhuma nzito, hata CCM wakizithibitisha, sio kutamchafulia Mama Simba pekee bali chama chao na serikali ya JK. Kuliko kuchafua wataona bora wamkane Mama Kahama aonekane muongo, kwani atafanya nini zaidi ya kuishia kulia. Yaliyomkuta Nape aliyaona. Bado Mama Kahama anaamini kwenye ukweli ambao kwa CCM ni dhambi. Sophia Simba atapeta uenyekiti UWT na kansa ya rushwa itakuwa ndio inaenea mwiili mzima wa CCM tayari kwa 2010.
mna haraka.. walikuwa mapumziko ndio wanarudi mida hii kumalizia mnachosubiri..
Wakuu hakuna mwenye taarifa yoyote ya huu uchaguzi au matokeo yatatolewa kesho? Wale Kina Simba na Kahama wote wamegombea au wametolewa kwenye kugombea?