Waziri Sophia Simba - Mwenyekiti Mpya UW-CCM (Taifa) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Sophia Simba - Mwenyekiti Mpya UW-CCM (Taifa)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tikerra, Sep 18, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nilishatoa wazo na wala sitachoka kusema,kwamba kuna haja ya Raisi wetu kuwa makini zaidi katika uteuzi wa wafanyakazi wa ngazi za juu serikalini.Hili sakata la Sophia Simba na Janet Kahama kutukanana hadharani kunaonyesha wazi kwamba uteuzi wa viongozi hawa haukufanywa kwa umakini. Ungefanywa kwa umakini,tabia zao zingefahamika mapema.Hii inaonyesha pia kwamba aidha Raisi hakushauriwa vizuri au alishauriwa akapuuza ushauri aliopewa.Kwa mtazamo wangu mimi, nchi haiwezi kuendeshwa hivi.Ni wazi kwamba matatizo mengi nchi yetu inayopitia sasa, yanaletwa na viongozi wa namna hii.Viongozi walioteuliwa bila uchunguzi wa kina au kwa kupendelewa pendelewa tu bila kuwa na 'qualifications' zinazotakiwa.Kwa bahati mbaya nchi yetu imetumbukia katika tatizo hili katika kiwango cha kutisha sana.Hatua za makusudi kabisa lazima zichukuliwe ili kujinasua na tatizo hili.Mwisho nashauri mamlaka zinazohusika ziwawajibishe viongozi hawa ili iwe fundisho kwa wengine.
   
  Last edited by a moderator: Jan 7, 2009
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ehh? vipi tena wakuu, kuna heri hapa? au ndio 'ukiona neno usipotia neno hutopatwa na neno?'
   
 3. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mwenzetu ana hisa kwa hawa wahusika
   
 4. africa6666

  africa6666 JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2008
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 281
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Heh yametokea wapi hayo??? hapo kibaya kilichoongelewa ni kipi??
   
 5. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2008
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ??????????
   
 6. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi nidhani waelimishwe kwamba wao ni jicho la nchi. Inawezekana walijishau na kuanza kulumbana mbele ya kundi la watu.
   
 7. M

  MROSSO Member

  #7
  Sep 18, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama anaonekana ni mlafi wa madaraka anataka sijui nini, aige busara kwa Mongella.
   
 8. N

  Nahene Member

  #8
  Sep 18, 2008
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 32
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Leta habari kamili iliyowafanya mpaka ikafikia hapo, usiegemee mlengo wa upande mmoja kwani wengine hatukuwepo wala kusikia hayo, pia ingefaa uyaeleze hayo matukano.
  Hinti, usitaraabu wa mtu haupimwi kwa qualifications- wewe Hoja habari wanJF waijambue
   
 9. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Aluu,

  Naona Wall Street tumble down na Sarah Palin vimetushika tunakosa drama za bongo.

  Imekuwaje Sophia Simba na Janet Kahama tena?
   
 10. Vica

  Vica Member

  #10
  Sep 18, 2008
  Joined: May 27, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  tupeni nyeti what exactly happened!nina nyege za kujua zaidi
   
 11. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Zzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz!!!!
   
 12. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2008
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mbona hii habari imechambuliwa sana siku karibu tatu mfululizo? nashangaa mleta mada inaamaana hajaioona thread nyingine yenye habari hii? wanaouliza nao? wanaojibu kwa jaziba lipi geni hapa? Moderator tafadhari tuunganishie hizi thereads.
   
 13. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2008
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kumbe mjadala wa mama Sophia Simba ulishafungwa nenda kwenye closed thread, utapata mambo mengi kumekuwa na Uchambuzi usio wa kawaida katika mada hii.
   
 14. m

  mwanaizaya Senior Member

  #14
  Sep 19, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kahama, Simba wakalia kuti kavu


  *Jumuiya ya Wanawake kukutana leo kuwajadili
  *Wajumbe wa kikao wajipanga kuwaweka hadharani

  Bryceson Mathias, Dodoma na Gladness Mboma, Dar


  BARAZA Kuu la Taifa la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), imejipanga kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wagombea wawili wa uenyekiti wa umoja huo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za Jumuiya hiyo kwa kukashifiana na kutumia mbinu chafu katika kampeni zao.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya Baraza Kuu la UWT kinachoendelea mjini hapa, vilieleza kwamba wajumbe wa Baraza hilo wameonesha kukasirishwa na kitendo hicho, huku baadhi yao wakiwa wamejipanga kutoa hoja ya kuchukuliwa hatua kali zaidi, ikiwamo hata kuvuliwa kugombea nafasi hiyo na uongozi wowote ndani ya Jumuiya hiyo.

  “Hatujafurahishwa na kilichotokea Dar es Salaam kwa wagombea wetu wawili kupakana matope hadharani, pia wagombea kuanza kutumia mbinu chafu za kampeni, hatuwezi kukubali hata kidogo, lazima tuchukue hatua kali...tumejipanga kutoa mapendekezo mazito, huu una ushahidi si kama ya vijana (UVCCM)," alisema mmoja wa wajumbe mwenye nguvu ndani ya UWT.

  Mjumbe huyo aliyezungumza na Majira kwa masharti ya kutotajwa jina kwa kile alichoeleza si msemaji na wakati wake wa kusema bado kwa kuwa ajenda hiyo inatarajiwa kujadiliwa leo, alisema tabia hiyo ya kuchafuana ni dalili za wazi kwamba wahusika hawafai kuongoza Jumuiya.

  Mjumbe mwingine alisema wanasikitishwa na ukimya wa uongozi wa UWT mkoa wa Dar es Salaam kutowachukulia hatua kali wagombea hao hadi sasa na kuongeza kuwa licha ya Mwenyekiti, Bibi Anna Abdallah, kulaani kitendo hicho, lakini hilo tu halitoshi.

  “Kama baba na mama nyumbani ni walevi unatarajia watoto watakuwaje? Watakuwa kama wazazi wao, sasa hatuwezi kukubali kuongozwa na watu kama hao nasi tutakuwa hivyo hivyo kuchafuana, kukafishina,” alisema mjumbe mwingine.

  Alisema wao wakiwa wajumbe hawako tayari kulea tabia hiyo ndani ya Jumuiya hiyo, hasa kwa kuzingatia kuwa walifanya kitendo hicho hadharani na kuchafua Jumuiya na chama kwa ujumla na kwamba hata kama mtu atatumia fedha zake kupita, lakini anaweza kushindwa kufanya kazi za chama ambazo hutegemea zaidi moyo wa kujituma na si fedha.

  Alipoulizwa kuhusu nafasi ya wanawake ya uwakilishi wa 50 kwa 50 ndani ya Bunge, alisema kama hali ndiyo hiyo, kuchafuana kutazidi na kueleza masikitiko yake kwamba wanawake wameanza kuonesha udhaifu wa hali ya juu hata kabla ya kufikia wanakotaka kwenda.

  Juhudi za kumpata Bibi Abdallah kutoa ufafanuzi kuhusu uamuzi na mawazo hayo ya Wajumbe iligonga ukuta kwani hadi tunakwenda mtamboni bado alikuwa akiongoza Kikao hicho na simu yake ikiwa imezimwa.


  Guninita akanusha

  Wakati huo huo, CCM Mkoa wa Dar es Salaam imekanusha Bibi Simba, kutwangana makonde na Bibi Kahama, bali walikuwa na malumbano.

  Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. John Guninita, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mtafaruku baina ya wagombea hao wa uenyekiti wa Mkoa wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT)

  Alisema Septemba 12 mwaka huu, kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa, kilikutana kujadili majina ya wagombea uongozi wa UWT ngazi ya mkoa.

  Bw. Gununita alisema kabla hawajaanza kikao, Bibi Simba aliomba nafasi baada ya kikao kumalizika azungumzie mambo kadhaa ya kuwekana sawa kama viongozi.

  "Kwa kuwa kikao hicho kilikuwa ni maalumu, ambacho hakikuwa na ajenda ya mengineyo, mimi nilimtaka Bibi Simba azungumze mara baada ya kufunga kikao," alisema Bw. Guninita

  Alisema Bibi Simba katika mazungumzo yake, alidai kusikitishwa na tabia iliyoanza kujitokeza ya kutupiana maneno yanayoashiria kupakana matope baina ya waombaji wa uongozi kwenye UWT na wapambe, wakati wagombea wote ni viongozi wanaofahamu maadili ya chama.

  Pia alisikitishwa na kitendo cha Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi Kahama kuitisha kikao cha Baraza la UWT Mkoa, bila kumpa taarifa, wakati yeye akiwa anahudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) Dodoma.

  "Hoja ya msingi katika maelezo ya Bibi Simba ilikuwa ni kusisitiza haja ya kuheshimu maadili, kutopakana matope na zaidi kusikitishwa na kuitishwa kikao bila kumshirikisha," alisema Bw. Guninita.

  Alisema wakati Bibi Kahama alipokuwa akijibu hoja hizo kwa kukana kutoa kauli za kumpaka matope, Bibi Simba ndipo kutoelewana na kujibizana kulipotokea.

  Bw. Guninita alisema alichukua nafasi ya kukemea na kutaka tatizo hilo kama lipo la msingi wazungumze katika vikao vya UWT na kama litakuwa halijapata ufumbuzi, lipelekwe kwenye chama kwa hatua zaidi.

  "Ni kweli kila mmoja alikuwa na hasira, lakini si kweli kabisa kwamba yuko kiongozi yeyote miongoni mwa hawa wawili aliyemrushia mwenziwe ngumi na kutoa lugha ya matusi kama ilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari," alisisitiza.

  Alisema wakati yanatokea hayo, tayari Bibi Simba alikuwa ameandika barua ya malalamiko kwa Katibu Mkuu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam akilalamikia kuitishwa kwa kikao cha Baraza la UWT Mkoa bila yeye kujulishwa.
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Sasa wanakanusha ili kulinda maslahi ya wakubwa wanao...back up Kimeo SS....sidhani kama JKahama...ana mkono mrefu vile hadi Guninita aambiwe awasafushe..ili malengo yao yatimie....Kama wanachama na wajumbe wa mkutanao mkuu....waaamue moja wawatose wote wa wili....wapitishe majina mengine kwani lazima wao?????????
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hivi karibuni tumeshuhudia maneno maneno meengi ndani ya UWT...na hii jumuia inaitwa Umoja wa Wanawake Tanzania.Sasa kirefu cha hii jumuia ni utata mtupu sijui hii jumuia kazi yake haswa ni nini katika kuleta mchango wa maendeleo nchini hususani kuwakomboa wanawake wa Tanzania.
  Hatuelewi ni Jumuia ya wanawake wenye uwezo ndani ya CCM?
  Kwani kazi ya hizi jumuia ni nini haswa? kama si ufisadi. kuna wamama wengi humu mjini Dar-es-salaam wanabeba zege, wanauza biashara ndogo ndogo kwenye mabeseni yani matunda,mihogo nk. wanapigwa na jua kutwa kuchwa hivi hii UWT imewasaidiaje hawa? tena kama huyo Sofia Simba na Janeth Kahama wapo hapa hapa Dar-es-salaam siku zote,kwanini wasingewakusanya hawa kupitia UWT wakawaelimisha wakawakopesha na wakawa tengea maeneo? ufala mtupu hamna lolote zaidi ya ufisadi tu.

  Hivi ni nini haswa wanacho gombea ndani ya hii UWT wanachama wake?Tunavyo jua kazi ya kukijenga chama ni ya kujitolea ...je ni kweli hawa wote wanao ng'ang'ania madaraka kwa uroho wanadhumuni hilo?

  Kwa mfano utakuta kiongozi mmoja ana madaraaka mengi sana sasa sijui atawezaje kufanya kazi kwa ufanisi ?Kwa mfano huyu mama Sofia Simba anataka kuwa;-
  Ubunge wa kuteuliwa-wewe
  Waziri-wewe
  UWT Mwenyekiti-wewe
  Mjumbe kamati kuu-wewe
  Mjumbe halmashauri kuu-wewe
  Mke wa mtu-wewe
  Mama wa watoto-wewe
  Ufisadi-wewe
  Mwanamtandao-wewe
  Kulinda mafisadi-wewe

  Sasa huyu mama vyeo vyote hivyo bado anausongo tu wa kuongoza ...humu nchini hakuna akina mama wanao weza wakagombea nyadhifa moja moja hapo?
  Tunaomba na hilo jina mnalo jinadi nalo kuwa ni Umoja wa Wanawake lifutwe maana mnawabagua wanawake wengine kwa kujipendelea wenyewe semina kwa wanawake wote hamtoi,haki za wanawake wanyonge hamtetei,mikopo kwa wanawake wote hamshughulikii ni bora mjiite tu Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWCCM kama ilivyo UVCCM.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Dec 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,203
  Trophy Points: 280
  Kahama amshitaki Waziri Simba kwa JK

  2008-12-25 18:31:26
  Na Muhibu Said

  Zikiwa zimesalia siku 14 kufika siku ya uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mambo si shwari katika mchakato wa kumpata mwenyekiti wake.

  Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mjini Dodoma Januari 7, mwakani ambapo nafasi ya uenyekiti itagombewa na Janet Kahama, Sophia Simba na Joyce Masunga.

  Hali hiyo, ambayo inazidi kuipaka matope CCM, imedhihirika baada ya mgombea wa nafasi ya Janeth Kahama kuwasilisha rasmi malalamiko kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akimtuhumu mpinzani wake, Sophia Simba kwamba amewahonga wajumbe wote wa Mkutano Mkuu rushwa ya Sh. 100,000 ili wampe kura.

  Mbali na tuhuma za rushwa, Simba, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), anatuhumiwa pia na Kahama kuwa yeye na wapambe wake wamekuwa wakiitumia Ikulu kuwaomba kura wajumbe wa Mkutano Mkuu.

  Kahama, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), amewasilisha malalamiko hayo kupitia barua yake yenye kumbukumbu Na. JBK/01/08 ya Desemba 20, mwaka huu, iliyopelekwa kwa Rais Kikwete, Ikulu, jijini Dar es Salaam.

  Nakala ya barua hiyo, ambayo Nipashe inayo, imepelekwa kwa Katibu Mkuu wa UWT Taifa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

  Makamba alipoulizwa na Nipashe juzi jioni kama amepokea nakala ya barua hiyo, alithibitisha kuipokea.
  Simba anadaiwa kutoa hongo hiyo kupitia kadi alizochapisha kwa lengo la kuwatakia heri ya Mwaka Mpya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT Taifa.

  Kadi hizo, ambazo zinadaiwa kusambazwa na Diwani wa Kata ya Ilala, Moshi Kondo, zina picha, jina na saini ya Waziri Simba, kalenda ya Mwaka Mpya wa 2009 na nembo ya CCM.

  Barua hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho: `Yah: Malalamiko dhidi ya Mhe. Sophia Simba kugawa vipeperushi mikoani`, Kahama anamueleza Mwenyekiti Kikwete kama ifuatavyo:

  ``Kwa heshima ya pekee, nakuomba uhusike na mada ya barua hii kama inavyosomeka hapo juu. Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unavyofahamu, Jumuiya yetu ya UWT hivi sasa ipo katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya taifa unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.``

  ``Mimi nikiwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Taifa wa UWT, natambua kuwa wagombea wote tulizuiwa na vikao vya UWT Taifa kutoa vipeperushi vya aina yoyote kwa minajili ya kujinadi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa UWT.``

  ``Lakini, ajabu ni kwamba, mgombea mwenzangu, Bi Sophia Simba amechapisha kalenda na kadi za `Heri ya Mwaka Mpya` zenye picha yake na nembo ya CCM na kuzisambaza kwa wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT Taifa nchi nzima, ndani zikiwa na kitita cha Sh. 100,000 (kwa kila kadi).``

  ``Mheshimiwa Mwenyekiti, nalazimika kukuandikia waraka huu ili kukupa angalizo juu ya suala hilo hasa ikizingatiwa kuwa Mheshimiwa Sophia Simba ni Waziri katika ofisi yako mwenye dhamana ya Utawala Bora.``

  ``Hivyo hatua yake na nembo ya CCM, inakwenda kinyume na kanuni za uchaguzi za CCM, kipengele cha Miiko ya Kuzingatiwa wakati wa Shughuli za Uteuzi na Uchaguzi`, ibara ya 33 kifungu kidogo cha 14 kinachosema: `Ni mwiko kutumia makaratasi ya kampeni nje ya utaratibu wa chama au kutumia vishawishi vya aina yoyote ile kwa minajili ya kupata kura.``

  ``Je, hatua hii ya Mheshimiwa Simba kuchapisha nyaraka hizo zenye picha yake na nembo ya CCM na kuzitawanya nchi nzima, si uvunjaji wa makusudi wa kanuni hizo za uchaguzi za CCM tena kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa UWT?``

  ``Je hatuoni kwamba hatua yake hiyo ambayo haijakemewa mpaka sasa ni kielelezo kingine cha ubabe na matumizi mabaya ya madaraka yake kama Waziri tena mwenye dhamana ya Utawala Bora?

  Nasisitiza hili kwa sababu Mheshimiwa Simba na wapambe wake wamekuwa wakipita mikoani na kupotosha wapigakura kuwa yeye ndiye chaguo la Ikulu.``

  ``Mheshimiwa Mwenyekiti, nawasilisha kwako waraka huu wenye malalamiko haya ili uweze kujua nini kinaendelea na kuchukua hatua kwani kama kitaachwa, kinaweza kujenga matabaka ndani ya UWT na mpasuko usio wa lazima ndani ya chama chetu, hasa pale hisia za mgombea mmoja kuandaliwa mazingira ya ushindi dhidi ya wenzake zinapoanza kujengwa.``

  ``Naambatanisha moja ya vipeperushi hivyo vya Mheshimiwa Simba vilivyosambazwa mikoani kinyume na utaratibu nilioueleza hapo juu.``

  Makamba alipoulizwa na Nipashe juzi, licha ya kukiri kupokea nakala ya barua hiyo ya Kahama, alimtaka mwandishi kama ana swali lolote kuhusiana na suala hilo, akamuulize Rais Kikwete kwa vile ndiye aliyeandikiwa barua hiyo.

  ``Mtafute Mwenyekiti wa CCM, yeye ndiye aliyeandikiwa barua, aliyeandikiwa ndiye anayejibu. Mimi nimepewa nakala, anayepewa nakala, anaarifiwa tu,`` alisema Makamba.

  Nipashe ilipowasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alisema kwa vile malalamiko ya Kahama yanahusiana na Chama, anayepaswa kujibu suala hilo ni Katibu Mkuu.

  Baada ya Makamba kuulizwa tena, alisema: ``Mimi sina cha kusema, sijaisoma (hiyo barua), sijajua maudhui.

  Nitakapoisoma na kujua maudhui, nitatoa maoni yangu.``

  Kahama alipoulizwa na Nipashe jana kama barua hiyo ndiye aliyeiandika, hakukiri wala kukanusha, badala yake alisema kwa sasa hawezi kuzungumza lolote kwa vile kipindi hiki ni cha sikukuu ya Krismasi, ambayo yeye kama Mkristo anapaswa kuitukuza.

  ``Sina comments (maoni) kabisa kabisa, mpaka nionane na Katibu Mkuu. Pia mimi ni Mkristo na kipindi hiki ni cha Krismasi,`` alisema.

  Naye Diwani wa Kata ya Ilala, Moshi Kondo, alipoulizwa juzi, alikataa kuzungumzia suala hilo, badala yake alimtaka mwandishi akamuulize Simba.

  ``Kwani Sophia Simba mimi ni nani kwake?`` alihoji Kondo, ambaye alipojibiwa na mwandishi kuwa ``Simba anadaiwa kuwa ni mtu wake wa karibu``, alisema: ``Nenda kamuulize Simba.``

  Tangu juzi hadi jana jioni Nipashe ilimtafuta Simba bila kumpata na baadaye kuelezwa na mmoja wa wanafamilia yake kuwa yuko safarini Malaysia.

  SOURCE: Nipashe
   
 18. C

  Chuma JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Duh....mi nilifikiri alishaacha kugombania huyu Sofia Simba...Kumbe bado yupo...Ikithibitika kagawa 100,000 basi hata U-WAZIRI nao afukuzwe aunganishwe na akina MRAMBA NA YONA.....
   
 19. C

  Chuma JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  nafikiri mod hii mada iunganishwe na ile ya Simba VS Kahama wakati wanagombea Mkoa wa Dar es Salaam.
   
 20. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Duh! Sasa kazi kwa kweli. Huyu Sophia juzi juzi hapa alikuwa anang'aka kuhusu Chenge na Billion yake ile, sasa na yeye kumbe ni wale wale. Hii issue wewe Bubu ataka kusema, kama nilivyokuambia awali, ni ngumu sana. Suala la UFISADI. Linakuja na clours tofauti tofauti.
   
Loading...