Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
WAZIRI PROF. KITILA MKUMBO - TUKIONGEZA UFANISI TUTAFAIDIKA ZAIDI NA BANDARI ZETU
"Wenzetu wamepeleka sumu nyingi kwa watu na hawataki tuiondoe, tulikuwa tunawaangalia wakadhani CCM haipo, CCM ipo, serikali ipo na watu wake tupo tutafanya kazi hii (ya kutoa elimu kuhusu uwekezaji wa bandari) hadi kieleweke" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji
"Miaka 30 iliyopita nchi yetu ilikuwa na uchumi uliohodhiwa na serikali, kila shughuli za uchumi zilikuwa zinafanywa na serikali. Baada ya miaka 30 ya uhuru tukaamua tubadilishe mwelekeo wa kisera na kwenda kwenye uchumi wa soko, na uchumi wa soko unagawanya majukumu katika maeneo mawili moja ni kwa serikali na jingine kw sekta binafsi" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji
"Duniani imeonekana njia nzuri ya kuleta maendeleo sio kutegemea misaada bali ni uwekezaji" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji
"Ili nchi yetu ikuze uchumi ni lazima shughuli za uchumi ziongezeke, na huko duniani kuna mitaji mingi na teknolojia, na ile tuendelee ni lazima tuvute mitaji hiyo mikubwa pamoja na teknolojia ije kwetu" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji
"Wataalam wameanisha na kueleza kwamba tukiongeza ufanisi tutafaidika zaidi na hizi bandari zetu katikati bandari zetu. Kufuatia hilo, ndipo serikali kwa niaba yetu ikatoa fursa kwa wawekezaji wenye uwezo waje kuwekeza katika bandari" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji