Waziri Prof Kitila Mkumbo ameongea nini leo?

Kakumamoto

JF-Expert Member
May 6, 2015
965
1,267
Habari wanajamvi, leo nimeona mahali Waziri wa Nchi (Mipango na Uwekezaji) Mh Prof K. Mkumbo kaita waandishi wa habari anazungumza jambo. Amezungumza juu ya nini?! Au alikua anatetea Dissertation yake? Au alikua anatabaisha mafanikio ya wizara yake? Aliyepata muda wa kumsikiliza atujuze.
 
Atakuwa alikuwa anatetesa dissertation yake. Maana kama jambo lingekuwa kubwa linge trend
 
LINI SERIKALI ITAACHA KUWATIMUA WANANCHI

Badala yake ardhi ya mtu au kijiji iwe ndiyo mtaji wake wa kufanya biashara ya ubia na mwekezaji.

Anaongelea wekezaji mdogo, lakini hataki mchimbaji mdogo au kijiji kuingia ubia na wawekezaji wakubwa wa nje.

Serikali ya CCM kazi yake ni kuwatimua mchimbaji mdogo au wanakijiji wenye ardhi iliyo na madini au Vito

Toka Maktaba :

Na mgawanyo uwe vitofali vya dhahabu, karai la Vito n.k au makubaliano baina ya mwananchi mnyonge mwenye kumiliki ardhi au baina ya kijiji kinachomiliki ardhi na mwekezaji.

1 July 2023

Under the new deal announced on Friday, Botswana gets a bigger share of rough stones from their joint venture, Debswana.

Botswana and mining company De Beers have announced a new diamond sales deal.
1704994164069.png

The new deal, concluded on Friday, gives Botswana a bigger share of rough stones from their joint venture.

Debswana, a joint venture between Anglo American unit De Beers and Botswana's government, sells 75% of its output to De Beers, with the balance taken up by state-owned Okavango Diamond Co.

The new agreement covers a 10-year sales deal for Debswana rough diamond production through to 2033 and 25-year Debswana mining licences.

In the run-up to Friday's deal, Botswana President Mokgweetsi Masisi, who is expected to seek re-election next year, had pushed De Beers for a bigger share of Debswana's output.

In March, Botswana announced it would take a 24% stake in Belgian gem processing firm HB Antwerp in a move seen as designed to loosen De Beers' grip on the country's gems.

Botswana supplies 70% of De Beers' rough diamonds
 
Waziri Prof. Kitila Mkumbo anasema mtaji siyo lazima uwe tajiri wa fedha, Lakini wamewanyima wananchi umiliki wa ardhi !

Swali kuu kwanini hamtaki kuwapa umiliki wa ardhi raia au vijiji ili watumie ardhi hiyo kama mtaji wao kwa kuwa ardhi yao ina dhahabu, vito, gypsum n.k badala yake mnawatimua kwa kudai ardhi ni mali ya umma iliyo chini ya udhamini wa rais pia kwa sababu hiyo serikali inaweza kuwaondoa au kuinyakua ardhi wakati ardhi iliyo juu ya madini ndiyo mtaji wa asili ya wananchi wanyoge ?

View: https://m.youtube.com/watch?v=UJd5yCq3yyQ
 
JIBU LA KUWEZESHA NCHI NA RAIA KUWA TAJIRI NA AKIBA YA DHAHABU, MADINI NA VITO LAPATIKANA

1 July 2023
Gaborone, Botswana

View attachment 2748460

Nchi ya Botswana imepata jibu kuwa mfano Tanzania mkataba wa mgodi na mwekezaji wagawane vitofali vya dhahabu na serikali badala ya kusubiri faida ya kwenye balance sheet.

Mgawanyo wa vitofali au almasi au tanzanite inaipa uhuru Tanzania kuhifadhi kitu halisi na kukiuza kwa thamani ya uhakika bila makando kando ya kusubiri mwekezaji asafirishe madini yote nje na mwisho wa siku akuambie faida ni ndogo kama ripoti yake ya katika mahesabu ya mwaka yanavyoonesha .

1 July 2023
Gaborone, Botswana,

Botswana na De Beers Zasaini Mkataba wa Kuendeleza Ushirikiano Tajiri wa Almasi

Chini ya makubaliano mapya ya uchimbaji madini, Botswana itapata mara moja asilimia 30 ya mawe machafu (almasi ambayo bado kuchongwa) yaliyochimbwa, kutoka asilimia 25, na itapanda hadi asilimia 50 ndani ya muongo mmoja, De Beers na maafisa wa serikali walisema.

Afisa wa serikali ya Botswana na mtendaji mkuu wa De Beers, muungano wa kimataifa wa almasi, walitia saini mikataba ya muda siku ya Jumamosi ili kuendeleza ubia wenye faida, wa miongo kadhaa wa uchimbaji madini ya almasi ambao ulionekana kuvunjika katika miezi ya hivi karibuni.

Dakika chache kabla ya tarehe ya mwisho ya usiku wa manane siku ya Ijumaa, pande zote zilitangaza kwamba baada ya mazungumzo ya miaka mingi, walikuwa wamekubaliana kimsingi juu ya mpango wa kuunda upya ushirikiano ambao unaipatia De Beers sehemu kubwa ya almasi yake na serikali ya Botswana sehemu kubwa zaidi ya mapato yake.

Maelezo ya mpango huo bado yanashughulikiwa, maafisa wa serikali na De Beers walisema. Lakini inashughulikia moja ya matatizo makubwa ya serikali ya Botswana, kuhusu mgao wa almasi ambayo inapokea katika ubia wake wa uchimbaji madini na De Beers.

Chini ya makubaliano ya zamani, Botswana ilipokea asilimia 25 ya mawe machafu yaliyochimbwa, huku De Beers ilichukua mengine. Sasa, Botswana itapata mgao wa asilimia 30 mara moja, na hiyo itapanda hadi asilimia 50 ndani ya muongo mmoja, De Beers na maafisa wa serikali walisema.

De Beers alisema katika taarifa yake kwamba imekubali kuwekeza kiasi cha dola milioni 825 katika kipindi cha miaka 10 ijayo kusaidia kuendeleza uchumi wa Botswana. Makubaliano hayo pia yanajumuisha kuanzisha chuo nchini Botswana ambacho kitafundisha wenyeji ujuzi katika biashara ya almasi, maafisa wa serikali walisema

Source : The New York Times
 
11 January 2024

Kamati ya Kudumu ya Bunge, Uwekezaji ya Mitaji ya Umma (PIC) yaja na muswada wa uwekezaji ili kuleta mageuzi makubwa

View: https://m.youtube.com/watch?v=BmtHCk3PDlk

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Uwekezaji ya Mitaji ya Umma (PIC) afunguka kuelezea faida za muswada wa sheria ya Uwekezaji wa Umma wa mwaka 2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Uwekezaji ya Mitaji ya Umma (PIC), Deus Clement Sangu ( Mbunge CCM) amesema ikiwa Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma wa mwaka 2023 utapitishwa na Bunge kuwa sheria utakwenda kufanya mabadiliko makubwa kwenye ofisi ya msajili wa hazina na kuunda mamlaka ya uwekezaji wa uma, pamoja na kuanzishwa kwa mfuko wa uwekezaji.

Mheshimiwa Deus Clement Sangu ameyasema hayo jijini Dodoma Jumatano, Januari 10, 2023 ambapo ameeleza kuwa sheria hiyo itatatua changamoto ya muda mrefu ya mitaji kwenye mashirika ya kimkakati ya umma.

Mbunge wa Jimbo la Kwela kupitia CCM kkoani Rukwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge mheshimiwa Deus Clement Sangu inayoshughulikia uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Deus Sangu, amesema historia imeandikwa kutokana na watu wengi kutoa maoni ya muswada wa Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.

Akizungumza Jijini Dodoma, Sangu amesema kwa mara ya kwanza Novemba 10, 2023 Serikali kupitia Bunge walipeleka muswaada huo ili kuleta mabadiliko na mageuzi kwenye sekta ya uchumi na kufanya marekebisho hasa kwenye Ofisi ya Msajili Mkuu wa Hazina.

“Ofisi ya msajili wa hazina kwa majukumu yake pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kama ofisi ambayo inasimamia mashirika ya umma, lakini kwa muda mrefu sana tangia kuanzishwa kwa ofisi ya msajili wa hazina kumekuwa na gepu kubwa kwenye huendeshaji wa mashirika ya umma.” alisema.

Sangu aliongeza kuwa, “tuna mashirika mengi ambayo kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na msajili wa hazina mpaka kufikia June mwaka jana yalikuwa 304, mwanzo yalikuwa 298 lakini kutokana na uwekezaji ambao serikali imekuwa ikiendelea kufanya yameongezeka mpaka kufikia hapo.”

Hata hivyo, amesema takwimu za mwezi Juni 3023 zinaonesha uwekezaji katika Mashirika hayo bado upo chini na Serikali imewekeza zaidi ya Tirioni 76.73 na kukua hadi Tirioni 80 na wanakisudia kufikia Trilioni 100.
 
LINI SERIKALI ITAACHA KUWATIMUA WANANCHI

Badala yake ardhi ya mtu au kijiji iwe ndiyo mtaji wake wa kufanya biashara ya ubia na mwekezaji.

Anaongelea wekezaji mdogo, lakini hataki mchimbaji mdogo au kijiji kuingia ubia na wawekezaji wakubwa wa nje.

Serikali ya CCM kazi yake ni kuwatimua mchimbaji mdogo au wanakijiji wenye ardhi iliyo na madini au Vito

Toka Maktaba :

Na mgawanyo uwe vitofali vya dhahabu, karai la Vito n.k au makubaliano baina ya mwananchi mnyonge mwenye kumiliki ardhi au baina ya kijiji kinachomiliki ardhi na mwekezaji.

1 July 2023

Under the new deal announced on Friday, Botswana gets a bigger share of rough stones from their joint venture, Debswana.

Botswana and mining company De Beers have announced a new diamond sales deal.
View attachment 2868849

The new deal, concluded on Friday, gives Botswana a bigger share of rough stones from their joint venture.

Debswana, a joint venture between Anglo American unit De Beers and Botswana's government, sells 75% of its output to De Beers, with the balance taken up by state-owned Okavango Diamond Co.

The new agreement covers a 10-year sales deal for Debswana rough diamond production through to 2033 and 25-year Debswana mining licences.

In the run-up to Friday's deal, Botswana President Mokgweetsi Masisi, who is expected to seek re-election next year, had pushed De Beers for a bigger share of Debswana's output.

In March, Botswana announced it would take a 24% stake in Belgian gem processing firm HB Antwerp in a move seen as designed to loosen De Beers' grip on the country's gems.

Botswana supplies 70% of De Beers' rough diamonds
Mtanzania ni marufuku kumiliki Ardhi ya Madini,ila ukikutwa na bangi kwenye Ardhi ni Yako!
 
Mtanzania ni marufuku kumiliki Ardhi ya Madini,ila ukikutwa na bangi kwenye Ardhi ni Yako!

Nchi ya ajabu sana, haitaki raia wake wafaidi madini yaliyo katika kiwanja, shamba au eneo lake.

Serikali itanyakua na kumkabidhi mwekezaji huku pengine raia au kijiji kilichohamishwa kitapewa kifuta jasho cha fidia moja badala ya kupata mgao hadi mwisho wa uvunaji madini.
 
Agosti 2023

Ardhi yote ya Tanzania ni ardhi ya umma iliyokabidhiwa kwa Rais kama Mdhamini kwa niaba ya wananchi wote.

View: https://m.youtube.com/watch?v=f-vsNoV8gKM
Video Mkurugenzi mkuu NHC Bw. Hamad Abdallah akizungumzia uwekezaji
Akizungumza katika kikao na wahariri, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linalomilikiwa na Serikali, Bw. Hamad Abdallah, alisema Tanzania inakosa mapato mengi kwa kuwanyima tu wageni haki ya kumiliki ardhi nchini.Anasema kuwa nchi nyingine, kama vile Rwanda, Kenya, na Afrika Kusini, na nchi zenye uchumi wa juu kama vile Dubai, zinaruhusu wageni kumiliki nyumba bila malipo.

Alisema Bill Gates, ambaye anapenda kutembelea Tanzania, anaweza kumiliki nyumba hapa; hata hivyo, kutokana na vikwazo vyetu vya kisheria, hawezi kumiliki nyumba ya likizo nchini. "Bill Gates akija Tanzania tunamuuzia nini zaidi ya uchoraji wa picha?" alihoji. "Bill Gates anaweza kumudu kununua nyumba ya likizo ya dola milioni 2 huko Arusha. Hii itatupa fursa ya kumshawishi kuifanya Tanzania kuwa mahali anapopendelea zaidi."

Tofauti na nchi nyingine ambazo zina haki ya kumiliki ardhi bila malipo, Tanzania inaruhusu tu umiliki wa ardhi, ambapo mtu hairuhusiwi kumiliki ardhi kwa kudumu isipokuwa kwa kukodisha kwa muda usiozidi miaka 99.
 
🤣🤣 Kumbe ana dissertation?nikajua sikuhizi ukifanikiwa kupenya kwenye uongozi kimagumashi,utapewa ma PhD ya bure y mchongo hadi ya Israel 🤣🤣kama hukusoma hukusoma tu🤣🤣
 
Back
Top Bottom