Waziri Philipo Mulugo: Jina langu linatumika kutapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Philipo Mulugo: Jina langu linatumika kutapeli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Oct 24, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kumbe matapeli walishamshtukia huyu waziri long time, na kuanza kutumia jina lake kutapeli?
  NOTE: Suala la matapeli kutumia jina lake kutapeli lilitokea kabla ya kulikoroga kule Afrika ya Kusini.


  Ziara za kushtukiza zinazofanywa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, hivi karibuni zimeanza kumtokea puani baada ya watu wasiofahamika kutumia jina lake kujipatia fedha kwa njia ya utapeli.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mwanzoni mwa mwezi huu, Bw. Mulugo alisema matapeli wameanza kutumia jina lake vibaya tangu aanze ziara za kushtukiza katika taasisi mbalimbali za elimu nchini. Alisema tabia ya watu kutumia jina lake kutapeli ilianza taratibu, lakini hivi sasa imezidi kushika kasi ambapo tapeli mmoja alimpigia simu Mhasibu wa Mamlaka ya Elimu nchini (TEA) na kumweleza Bw. Mulugo amemtuma sh. milioni 1.5.

  "Ndugu zangu waandishi, naomba mnisaidie katika hili, kuna namba imepiga leo (jana), kwa Mhasibu wa TEA, kutaka sh. milioni 1.5 akitumia jina langu, tukio la aina hii pia limetokea katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaa?m na mikoani," alisema na kuongeza kuwa chanzo cha tatizo hilo ni ziara zake za kushtukiza.

  Alisema wengine wamekuwa wakipiga simu na kuomba kiasi cha fedha wakidai Bw. Mulugo anataka kukitumia kwa ajili ya mafuta ya gari lake ili aweze kufanya kazi za Serikali kwa ufanisi. "Mimi nikitaka kufanya ziara huwa simfahamishi mtu labda bosi wangu Waziri (Dkt. Shukuru Kawambwa), nawaonya Wakurugenzi, Maofisa Elimu wa mikoa, Wilaya na wadau wa elimu waache kutumia jina langu vibaya kwani wakibainika sheria itachukua mkondo wake," alisema Bw. Mulugo. Alitoa mfano kama Mhasibu wa TEA asingepita ofisi kwake kujiridhisha kama kweli anahitaji fedha hizo, fedha hizo zingeangukia mikononi mwa matapeli.

  Majira.
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Labda sababu kawa the easiest subject kuigwa, ni kuongea tu Kiingereza kilichopinda na watu wanakumini ni yeye as long as ni mwanaume.

  Na in a way inaweza kuwa strategy ya kubadili topic juu yake... Maana kwa kweli ka make headlines na hotuba yake ile. Pole zake lakini, namuonea huruma kwa kweli...
   
 3. Kertel

  Kertel JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 2,431
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Yaani kuna watu wanatumia jina la huyu tanzania imetokana na muungano wa zimbabwe na tanganyika?
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  This thread was just a flashback to show that kuna matapeli walishamshtukia long time na wakaanza kutumia jina lake kutapeli.

  Maana kama Waziri hajui Tanzania ni muungano wa nchi gani, si unaweza kumtapeli kiulaini?

  Unampa cheki yeye anasaini tuu bila hata kuangalia.
   
 5. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hahaa nimecheka sana, yaani ni rahisi sana kumuiga nikimpigia simu Mhasibu na nikatumia kiingereza kwa pronunciation mbovu tu lazima ajue mimi ni Mulugo
   
 6. T

  Tabby JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,895
  Likes Received: 5,528
  Trophy Points: 280
  Ninachojifunza hapa ni kukosa uwajibikaji na mfumo mbovu wa matumizi na udhibiti wa kodi wanazolipa maskini wa Tanzania. Sikufikiria kwamba mawaziri hawana utaratibu wa malipo ya matumizi yao hata kama wakiwa ziarani. Inaonekana ni utaratibu wa kawaida kuchotwa hela za serikali kwa njia za simu hata bila justifications. Kwenye taasisi yoyote iliyomakini hii haiwezi kuwa issue ya kuweka hadi gazetini eti ukiomba msaada. Ujinga kweli kweli!. Tayarisha circular za ku govern authorization, disbursements and expenditure ya fedha. Hii inanipa hofu kwamba wizara ya elimlu ina idle cash nyingi za watu kuchota chota bila mpangilio wakati shule hata chaki za kuandikia walimu hawana. Ujinga huu!.

  PENGINE LENGO NI KUUFAHAMISHA NAMNA ANAVYOFANYA SAFARI ZA KUSHTUKIZA. Ili iweje? Unawashitukiza watendaji ambao hujawaandaa wala kuwawezesha katika uwajibikaji kusudi gani? Hujui ni kwa nini hawakai ofisini? Hujui kwa nini visingizio vingi? Hujui kwa nini utendaji uko chini ya kiwango? AU hujui namna ya kuunda na kusimamia mikakati endelevu itakayo leta tija ya kuborosha uwajibikaji na utendaji kazi wizarani kwako? Raisi wako anaenda nje ya nchi kila siku kutalii na wewe unaanza utalii wa ndani usiokuwa na malengo. Mligo hiyo kazi huiwezi. NI aibu kwa taifa.
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Majira wakorofi kweli habari ya mwezi uliopita ndio wanakumbushia leo lol au wanataka kukumbushia ile issue yake ya 11964 na zimbabwe?
   
 8. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Wanalitumia kutapelia sehemu ipi sasa ya tanzania ni uku bara au kule ZIMBABWE na PEMBA.
   
 9. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nimenukuu "Tanzania was formed in one nineteen sixty four by unifying the Indian ocean islands of Zimbabwe and Pemba and the mainland territory formerly known as Tanganyika" - Hon. Mulugo Philipo Augustino Deputy Minister of Education and Vocational Training.
   
 10. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Kuna majina mengine ni rahisi kuyaiga, maana inawezekana hata mwenye jina lake asijue kama ni la kwake kwa jinsi alivyo kilaza!!
   
 11. s

  swrc JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa thread hii inaonyesha dhahiri pasipo shaka kuwa waziri huyu anayomazoea ya kuomba hela
   
 12. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapa chuma kimekutana na nondo. Yeye mwenyewe waziri haoni kukubali madaraka ambayo kwa elimu na utaalamu wake hayawezi si ni utapeli pia kwa watanzania? Nchi hii matapeli mko wengi.
   
 13. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Siyo Majira bali ni mimi. Ndiyo maana nikasema inaonekana watu wengi wanamjua huyu maana wameshatumia jina lake huko nyuma kutapeli serikali.
   
 14. m

  malaka JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ameanza kujihami akijua rungu na tume zitakuja kumchunguza. Du JK ahsante kwa kutuletea vituko.
   
 15. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Huyo waziri ni kilazza sana !
  anasema Tanzania imetokana na muungano wa zimbabwe, unguja na tanganyika.
  Halafu mpaka leo anaamini hivyo
   
 16. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu inawezakana kabisa ikawa ni DECOY ya to get rid ya mapaparazi, lakini ili la Zimbabwe badala ya Zanzibar naona ilikua ni slip-up ya kawaida tu - we sema watu wakuamua kukujengea hoja utajuta kuzaliwa.
   
 17. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Napigwa na wasi wasi inawezekana ni yeye mwenyewe anataka kuibia pesa wizara yake,kwa vile ameshaburunga burunga huko south Africa anajua ya kwamba wakati wowote atapokonywa wadhifa wake ni bora achukue chake mapema.

  Kwa vile ubongo wake ni sawa na utomvu ,inawezekana anapata shida sana katika kunyakuwa fedha za serikali,hiyo ndio njia ya kujisafisha kwa wananchi kwa vile ameshtukiwa anataka kuibia fedha wizara yake.

  Hana lolote huyu Minista ofu Educationali endi Vocationali Trainingi hahahhaha
   
 18. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  nadhani nia yake ni kutaka kufunika aibu zake za ukihiyo
  tushamshtukizia la sivo aombe radhi kwa watanzania na rais wake
   
 19. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Napigwa na wasi wasi inawezekana ni yeye mwenyewe anataka kuibia pesa wizara yake,kwa vile ameshaburunga burunga huko south Africa anajua ya kwamba wakati wowote atapokonywa wadhifa wake ni bora achukue chake mapema.

  Kwa vile ubongo wake ni sawa na utomvu ,inawezekana anapata shida sana katika kunyakuwa fedha za serikali,hiyo ndio njia ya kujisafisha kwa wananchi kwa vile ameshtukiwa anataka kuibia fedha wizara yake.

  Hana lolote huyu Minista ofu Educationali endi Vocationali Trainingi hahahhaha
   
 20. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Anajaribu kupoteza upepo wa presentation yake ya kule Sauzi
   
Loading...