Mhe. Philip Mulugo asisitiza kiwepo Chombo huru Chenye Mamlaka ya kusimamia Elimu Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe. Philip Mulugo akichangia kwenye makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2023/2924 iliyosomwa Bungeni na Mhe. Prof Adolf Mkenda

"Awamu ya Sita toka tumepata Uhuru ukienda Vijijini tumepeleka fedha nyingi sana kwa ajili ya Shule za Msingi na Sekondari. Kata ya Udinde Jimbo la Songwe nimepewa Shilingi Milioni 600 na Serikali na wananchi wamejenga Shule inatwa Mulugo Sekondari" - Mhe. Philip Mulugo, Mbunge wa Jimbo la Songwe

"Katika mtaala mpya wa Elimu na Sera msisahau mambo ya Utawala. Mmeenda kwenye Madarasa, Sekondari, Elimu ya awali na Msingi lakini mmesahau kwenye Utawala ambako ndiko mnakosimamia Elimu maana kuna muuingiliano wa TAMISEMI na Wizara ya Elimu" - Mhe. Philip Mulugo

"Prof. Adolf Mkenda Kuna Shule za Msingi karibu 16,000 nchini. Tungekuona unafanya ziara, unatembelea Shule uone maisha ya Shule za Msingi wanavyokuwa wamekaa wale watoto pia uone majukumu yanavyoingiliwa na TAMISEMI. Wizara ya Elimu imepokonywa Mamlaka yake na TAMISEMI" - Mhe. Philip Mulugo

"Sheria inasema, Sheria namba 25 ya mwaka 1978 Mtaaluma Mkuu katika nchi hii ni Kamishna wa Elimu ambaye yupo Wizara ya Elimu. Wachukueni maafisa wa TAMISEMI muwarudishe Wizara ya Elimu maana huu ugatuaji umetuletea shida mno hasa kwenye utitiri wa mitihani" - Mhe. Philip Mulugo

"Kwenye utitiri wa mitihani, kuna mitihani ya Kata mara mbili kwa wiki, Mitihani ya Wilaya mara moja kwa mwezi, Mitihani ya Mkoa mara tatu kwa miezi minne. Sisi Shule binafsi kwanini mnatuingilia? Tuacheni na mitihani yetu maana mitihani yetu inaweza kuwa ni bora kuliko mitihani yenu mnayofanya" - Mhe. Philip Mulugo

"TAMISEMI wasimamie Shule zao kwasababu TAMISEMI ina Shule zao na sisi binafsi tuna Shule zetu, mnatupotezea muda kutuletea mitihani ambayo tunakuja kuifanya kwenye MOCK na NECTA. Afisa Mtendaji wa Kata anawaambia Shule binafsi siku fulani kuna mitihani halafu tunabaki kutoa hela tu" - Mhe. Philip Mulugo

"Tunachangia Shule za Kata Shilingi Laki moja kila wiki, Mitihani ya Wilaya kila mwezi. Wanabaki wanafaidi kwenye Kompyuta na Photocopy, kuna posho wanapata ndiyo maana wanang'ang'ania ile mitihani. Fanyeni mitihani yenu kule chini kama TAMISEMI" - Mhe. Philip Mulugo

"Tunapokwenda kufanya mabadiriko kwenye mtaala wa Elimu twendeni na jambo la kupata chombo huru cha kusimamia Elimu katika nchi hii. Wachukueni wadhibiti ubora wa Elimu Tanzania kiwe ni chombo huru kiwe na Mamlaka kama TCU kwenye Vyuo Vikuu, NACTE kwenye Vyuo vya Kati. Shule ya Awali, Msingi na Sekondari hawana msimamizi, hawana baba na mama, shule binafsi tumebaki kama yatima, unajiuliza jambo hili sijui niende TAMISEMI sijui nienda Wizara ya Elimu, lakini husikilizwi" - Mhe. Philip Mulugo

"Tunalia suala la tozo, nani wa kutusikiliza. Waziri wa Elimu huwezi kuzitoa tozo, Waziri wa TAMISEMI ndiye anayetoza tozo kule chini kwasababu mlilazimisha mkatupa leseni za biashara na mmezifanya Shule kama biashara" - Mhe. Philip Mulugo

"Afisa Baraza la Mitihani alipotoa ranking alisema ni kwasababu wanafanyia watu biashara, watoto wetu ni watanzania hawa hawa, wanapokuwa wamefanya vizuri kwenye shule binafsi ni watoto wa ndani wanaenda kuajiriwa Serikalini huko huko, wanapata uelewa mkubwa na GB kubwa kwa kufanya kazi za Serikali" - Mhe. Philip Mulugo

"Sheria Namba 25 ya mwaka 1978 inaniambia mmiliki wa Shule binafsi Nakwenda kusajili Shule yangu kwa Kamishna ananipa Kibali/Cheti lakini sikuambiwa ni biashara bila hivyo Shule zisingeanzishwa ndiyo maana sasa uwekezaji wa Shule binafsi umedolora maana tunakula hasara" - Mhe. Philip Mulugo.

WhatsApp Image 2023-05-21 at 14.59.44(1).jpeg
 
Tunataka wanafunzi wetu muwafundishe kubuni vitu na kutengeneza vitu kwa mambo wanayosomea
Sasa hizo private school zinatoa nini kama sio kukariri tu
Tunataka kuona wanatengeneza madawa vijana wetu
Wakitoka vyouni tusikie wamebuni kitu au wametengeneza kitu na kinauzika kote duniani basi sio duniani hata ndani tu

Elimu maana yake ni nini?
 
Back
Top Bottom