WAZIRI NAPE: Tathmini gharama huduma za mtandao kufanyika 2022

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mwaka 2022 Serikali itafanya tathmini ya gharama za huduma ya mitandao ya simu ndani ikiwa imepita miaka minne tangu kufanya hivyo.

Hayo yamesemwa leo Jummosi Agosti 20, 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kwenye kipindi cha Power Breakfast alipokuwa akizungumzia kuhusu kupanda kwa bei za vifurushi katika mitandao mbalimbali ya kampuni za simu.

Nape anayasema hayo katika kipindi ambacho wananchi wanapaza sauti kuhusu kupanda kwa bei za vifurushi na muda wa maongezi katika mitandao mbalimbali ya mawasiliano.

Amesema tathmini hiyo inakuja ikiwa imepita miaka minne tangu kufanywa hivyo kama sheria ya mawasiliano inavyoelekeza.

"Kisheria tunapaswa kufanya tathmini kubwa kila baada ya miaka minne na mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2018 licha ya kuwa katikati huwa tunafanya mabadiliko madogomadogo kutokana na sababu mbalimbali, "amesema.

Kuhusu kupanda kwa gharama za vifurushi amesema kumetokana na sababu mbalimbali ikiwemo miaka ya nyuma baadhi ya mitandao ilishusha bei zake zaidi ya bei elekezi iliyowekwa na serikali kwa lengo la kuvutia wateja.

Amesema jambo hilo liliizindua Serikali na kuingilia kati walipoona mitandao hiyo inazidiwa na wateja na huduma kuwa chini.

Nape amesema kampuni zilizokiwa zimeshusha zaidi gharama waliwapandishia japo haijafika kiwango cha bei iliyopitishwa na serikali.

Akifafanua zaidi Nape amesema wakati bei iliyopangwa kwa uniti ilikuwa ni dola 2.03 kwa bei ya chini na bei ya juu dola 9.35, wapo walioshuka na kufika dola 0.63 na waliopandisha walifika dola 40.5.

"Serikali ilipoingilia kati sasa waliokuwa chini kwa dola 0.63 tuliwapandisha na kufika dola 1.71 huku waliopandisha walishushwa kutoka dola 40.5 hadi kufika dola 9.35 kwa uniti," amesema waziri huyo.

Amesema pamoja na hayo yote, kila mtoa huduma anapaswa kutangaza pale anapopandisha au kushusha gharama kwa wateja wake na hii ni baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ambao ndio wadhibiti wakubwa kumkubalia.

Hata hivyo, aliwataka wananchi kuelewa kuwa serikali haipuuzi malalamiko yao wanayoyatoa.
 
Nilisema sana humu kuwa shida haikua mitandao ila serikali kuwabana waliouza chini ya Bei ya soko mfano Halotel, TTCL n.k watu walipovuka sana sasa sijui watasemaje baada ya hili.

Cc kimsboy njoo huku
 
... watakuambia Tz ndio nchi yenye gharama nafuu zaidi kwa ukanda huu; Kenya ni mara mbili ya hapa. So, gharama ziongezwe kidogo ili tuweze kuendana na wenzetu kwenye ushindani wa soko! Majibu wanayo mfukoni. Teh!
 
Tathmini my foot aweke Salio ajiunge atajua hayo matathminio ni porojo tu
 
Back
Top Bottom