BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
MAWASILIANO: Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema Kampuni ya Starlink inayotoa Huduma za Intaneti kwa kutumia 'Satelaiti' inakamilisha hatua za mwisho ili kupata vibali vya kutoa huduma nchini.
Ametoa kauli hiyo baada ya kuulizwa na Mdau kupitia X (zamani Twitter) kuhusu uwezekano wa Starlink kutoa huduma kwasababu Watoa Huduma waliopo Intaneti zao zinasuasua.
Nape ameongeza kuwa Starlink ikishatimiza taratibu zote itaanza kutoa huduma na kwamba Serikali inasubiri wakamilishe tu taratibu hizo. Ikumbukwe, moja kati ya Matakwa ilielezwa kuwa Starlink inatakiwa kuwa na Ofisi zake Tanzania.