Waziri mwingine aihujumu CHADEMA

Waziri mwingine aihujumu CHADEMA

Aluta continua makamanda pamoja na cdm,ukombozi uko karibu.
 
BAADA ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira kutajwa kuwa nyuma ya mkakati wa kukihujumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), waziri mwingine ametajwa kufadhili kundi la vijana wasaliti wa chama hicho.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumamosi, umebaini kuwa kigogo huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayeni naibu waziri wa wizara moja nyeti, juzi alifadhili kikao cha kutathimini athari za tamko la aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa wa Baraza la Vijana la CHADEMA Taifa (BAVICHA) aliyefukuzwa,Juliana Shonza.
Naibu huyo pia anadaiwa kutumia siasa za ukanda na ukabila kuwarubuni vijana waliofukuzwa uanachama wa BAVICHA.

Baadhi ya vijana hao waliofukuzwa uanachama na kuungwa mkono na naibu waziri huyo, ni Shonza, MtellaMwampamba aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki 2010 na Habib Mchange aliyegombea Kibaha Mjini.
Vijana hao walivuliwa uanachama baada ya BAVICHA kujiridhisha kuwa walikuwa wakitumiwa na CCM pamoja na baadhi ya viongozi wawili ndani ya CHADEMA ili kutoa matusi kwa viongozi waandamizi wa chama na kuwazushia uongo.

BAVICHA pia iliwataja Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigella na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mwigulu Nchemba, kuwa nyuma ya mkakati huo.
Mmoja wa wajumbe walioshiriki kikao hicho juzi usiku, alisema kuwa watatathmini kazi aliyokuwa amepewa Shonza.
Alisema kuwa Shonza alipewakazi ya kutoa tamko la kuwatukana viongozi wakuu wa CHADEMA, kukishambulia chama na kuwashambulia baadhi ya viongozi wa BAVICHA, hasa mwenyekiti wake, John Heche.

“Tulikutana pale Mikocheni kwenye nyumba moja, tukajadili kwa mapana mkutano wa Shonza na waandishi wa habari baada yakufukuzwa. Sikujua nyumba ni ya nani, lakini aliyekuwa mwenyeji zaidi ni Shigela,” alisema.
Aliwataja wengine waliohudhuria kikao hicho kuwa ni Mwampamba, Tambwe Hiza, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Salumu Hapi pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, Wareni Kamnyoge.

“Katika mkutano ule, Shigella alimuuliza Shonza anaendeleaje baada ya kutoa tamko na athari zake kwa jamii. Shonza alijieleza na baadaye wajumbe wakamsifu kwa kusema CHADEMA ni chama cha Wachaga na cha ukanda,” aliongeza.
Aliongeza kuwa Shigella alisema kuwa; “Hapa kwenye ukanda na ukabila, nakwambia Juliana umetufurahisha. Maana sasa,tutakuwa tumefanikiwa sana. Tutatembea na agenda hii hadi mwaka 2015.”

Shigela hakupatikana kuthibitisha madai hayo, lakini Tambwe aliliambia gazeti hili kwa ufupi kuwa; “Mikakati ya kuwatumia vijana wa CHADEMA inaendelea vizuri.”
Akizungumza kwa kujiamini, Tambwe alisema juzi hakwenda Kinondoni hasa Mikocheni, lakini akathibitisha kuwa; “unachokisema cha kuwatumia vijana wa CHADEMA ni kweli maana mikakati ni ushindi katika uchaguzi mkuu 2015.”

Kuhusu kuwapokea CCM vijana hao, Tambwe alisema hayo mengine ya kutumika au kupokelewa waulizwe viongozi maana hao ndiyo wasemaji.
Shonza hakupatikana ili kuzungumzia madai hayo, ingawa kuna taarifa kuwa wameahidiwa kazi kulingana na elimu zao. Shonza inadaiwa kuwa ataajiriwa kwenye kazi za ustawi wa jamii, Mwampamba ameahidiwa ualimu.
Chanzo hicho kinaongeza kuwa, kwa mujibu wa mkakatihuo, Shonza na kundi lake, wamepanga kufanya ziara mikoani, wakianzia Mbeya, Iringa na baaye Mwanza.
Naibu waziri anayedaiwa kuwafadhili inasemekana anatumia ukabila na ukanda akisema kuwa waliofukuzwa ni vijana wa Mbeya, na hivyo anataka kuwatumia kuivuruga CHADEMA mkoani humo hasa Jimbo la Mbeya Mjini analojitapa kutaka kulirejesha CCM.

Chanzo: Tanzaniadaima 19 Jan 2013.
 
Kabla ujaandika pumba za Tanzania Daima soma kwanza nyuzi.

Huu upupuu tayari humu humu.
 
fanyeni uhunu wote tunajua kuwa ni uhuni na sisi tutasimama imara kuitetea cdm, hao vijana wanajimalizaaaaaaaaa kisiasa wanasahau cdm iliwapa umaarufu sasa wanajiona wao maarufu kuliko cdm, wanapotoka
 
Mungu yuko nyuma yetu hata wafanyeje CDM itasonga mbele tu maana hatukumbatii magamba.
 
Mkuu chama,

Naona huyo kabwela analazimisha kujuana na watu aame kwanza Kimara kwa shemeji.

Akina mama hushauriwa kuhudhuria clinic kipindi chote cha ujauzito ili kuzuia kuzaa watoto wenye akili kama zako Ritz. Una kila dalili ya athari ya kifaduro na pepopunda kwenye ubongo wako...
 
Last edited by a moderator:
Kama hiyo ndiyo silaha yao ya kuchukuwa jimbo la Mbeya thru Shonza....mmh I don't know about that. Ila wawe waangalifu na huko Mbeya wakienda jimboni kwa Sugu akiwa na Shonza itakuwa vyema wakahubiria siasa zao za ukanda wakiwa kwenye gari ambalo ni STONE-PROOF, seriously maana ujira wa USALITI uko mbioni kulipwa. Mark my word.
 
Nadhani niache kukujibu dada yangu kwa sababu ulichobakiza ni kuokota makopo maana stage zote umefuzu. Nampa pole mumeo. Alamsiki!

Majibu kama haya siyo ya ajabu kwa mtu mwenye akili za kiazi ambaye hata chupi anategemea fadhila za CDM achilia mbali pango la kuishi.

Chezea uso wa watu wengine, not me. Keep on being a loo of CDM machinery. Huu ndiyo ujira wako unaokufanya kuishi.

There's nothing I can do with your inferiority complex, I wish, you could afford to buy intellect

Keep on spitting filthy nonsense cos it makes your life
 
mkuu taratibu uchunguzi bado unaendelea stay tuned

Ndiyo maana nikasema kuna tatizo katika uandishi wa habari Tanzania. Kama uchunguzi bado unaendelea, kulikuwa na haraka ya nini kuleta habari badala ya kusubiri uchunguzi umalizike ili habari ikamilike. Hizi ni habari za kufikilika. Hakuna cha uchunguzi zidi ya kuamusha hisia katika jamii na kuuza gazeti.
 
Nafikiri utakuwa ni upuuzi tu kuogopa kuanzisha gazeti la chadema ambalo litaandika habari za kiuchunguzi kama za Mwanahalisi, kwani Mwanahali na Raia mwema yapo na yanaandika habari zenye mlengo wa CHADEMA na bado Tanzania daima linauza? At a time Mwananchi pia lilikuwa linaandika kwa mlengo wa CHADEMA kabla halijarubuniwa, yet gazeti la Tanzania daima liliendelea kuuza. Utakuwa ni wehu, na ubinafsi usio na maana iwapo Mbowe ataendelea kuweka kigingi uanzishwaji wa media za chama. Kwa kawaida, uwepo wa media za chadema ungesaidia sana kuongeza mapato pia, ukiachilia mbali utoaji wa taarifa. Why cant they do so?
CC. John Mnyika, Zitto, Mwita Maranya, Crashwise

Wazo lako ni zuri lakini dalili hazioneshi kama linaweza kuwa acceptable and implimented kama hata wazo la kujenga au kununua office kuu ya chama bado halijawa channeled katika chama kitu ambacho ni muhimu kwa chama.
 
Majibu kama haya siyo ya ajabu kwa mtu mwenye akili za kiazi ambaye hata chupi anategemea fadhila za CDM achilia mbali pango la kuishi.

Chezea uso wa watu wengine, not me. Keep on being a loo of CDM machinery. Huu ndiyo ujira wako unaokufanya kuishi.

There's nothing I can do with your inferiority complex, I wish, you could afford to buy intellect

Keep on spitting filthy nonsense cos it makes your life

Sawa dada msalimie shemeji
 
Ndiyo maana nikasema kuna tatizo katika uandishi wa habari Tanzania. Kama uchunguzi bado unaendelea, kulikuwa na haraka ya nini kuleta habari badala ya kusubiri uchunguzi umalizike ili habari ikamilike. Hizi ni habari za kufikilika. Hakuna cha uchunguzi zidi ya kuamusha hisia katika jamii na kuuza gazeti.

Unajua tena miezi hii ada za watoto zinatakiwa kwa udi na uvumba
 
soma mtiririko hapo juu, umegusia waandishi mi ndo nimekujibu critically waandishi wengi njaa anaandika ili apone njaa

Ok.
Mkuu, aliandika kwa kufupi sana kiasi kwamba iliniwia vigumu kuuelewa ujumbe wako.

Waandishi wetu wanachofanya ni bora habari halafu cha kusikitisha, unaweza ukakuta karibu magazeti yote yana habari moja na inakuwa kama wame copy& paste.

Polepole ndiyo mwendo. Naamini tutafika.
Thanks
 
Back
Top Bottom